Bwana MICHUZI,
habari ya siku nyingi.
Mimi ni Kiongozi, na mwanzilishi wa huduma nzuri ya Western Union Money Transfer, Tanzania. Tuna zaidi ya Miaka 10 kwenye huduma hii hapa Tanzania. Habari hii ni ya KUSIKITISHA NA IMELENGA KUPOTOSHA ukweli kwa wanaotajia kutumia huduma hii baadae.
Wale waliokwisha itumia, IKIWA NI PAMOJA NA BWANA MICHUZI, watakubaliana na Mimi kuwa MPOKEAJI HATA SIKU MOJA haombwi KITAMBULISHO cha Mtumaji.
Mpokeaji huhitajika kufanya MAMBO MATANO yafuatayo ili apokee hela.
1)Awe na kitambulisho halishi chenye picha,
2)Ajue jina la mtumaji,
3) Ajue kiasi kilichotumwa angalau +/-10%ya kiasi alichotumiwa,
4)Ajue hela zimetoka nchi gani, na
5) Ajue jibu la swali ambalo mtumaji amemtungia.
Haya yote Bwana Mwakidila naamini aliambiwa na Ofisi alipoenda kutuma hela afanye nini ili Mama apokee hela baada ya kutuma, na nakala yake anayo. Hata kama alipata taizo, alipaswa aende alipotumia hela ili kujua ukweli wake muda ule ule.
Hata hivyo, anaweza kupata uhakika kupitia kituo chochote che Western Union au website hii www.westernunion.com .angalia taratibu za kutuma au kupokea hela "Tanzania".
Kila nchi imetoa taratibu zake, ambazo hazifanani kwa nchi moja na nyingine...hasa ukilinganisha nchi za mabara mengine na Africa...CHUNGUZA.
USHINDANI. Bwn Michuzi dunia ya sasa ni ya ushindani, isije ikawa inalenga kitu kingine zaidi.Huduma ya KUTUMA na KUPOKEA hela Kupitia Western Union na MoneyGram kwa Tanzania MASHARTI na TARATIBU ni zile zile, kimsingi.
Wote ni MABENKI na tunaongozwa ni SHERIA za fedha chini ya Benki Kuu ya Tanzania. Hivyo,alichokieleza Bwana Mwakidila hakipo katika taratibu za kupokea hela kupitia huduma hii.
OMBI: Namuomba Bwana Mwakidila atusaidie kujua undani wa jambo hili kwa kuwasiliana nasi moja kwa moja, au atupe namba ya simu ya Mama hapa Dar es salaam, ilituweze kulifanyia kazi kwa manufaa yetu wote. Labda ni kitu kingine kimejificha hapa!!!!!
Kisha atueleze kama Mama alilipwa au nini kilifuata baada ya hapo.
HITIMISHO: Namuomba Bwana Mwakidila awasiliane nasi kupitia namba za ofisi alikotumia hela, ziko nyuma ya fomu aliyopewa, au kwetu (Tanzania) moja kwa moja.
Nawaomba WA-TZ wote mtume hela nyumbani, tusaidie ndugu, jamaa, rafiki na familia zetu, na Taifa letu changa la TANZANIA, KUPITIA HUDUMA NZURI YA WESTERN UNION.
TAWA,
KPR
PS: GLOBU YENU HII YA JAMII INAKARIBISHA VIMEO KAMA HIVI ILI TUSAIDIANE KUTOA YALIYO MOYONI NA IKIWEZEKANA KUPATA UFAFANUZI WA KINA KAMA ALIVYOTUSAIDIA MDAU HUYU WA WESTERN UNION AMBAEO NAMPA ZAWADI YA MWAKA MPYA KWA TANGAZO HILI LA UBWETE


Hizi habari za Western Union ni za ukiukaji wa haki za binadamu. Naelewa muelekeo wa mratibu wa Western Union wa Tanzania, lakini hata hivyo kasumba na ukiritimba kama huu haujamtokea bwana Mwakidila peke yake, imewatokea wengi mimi ikiwa mmoja wapo.
ReplyDeleteNa yote hayo maamuzi ya ajabu ajabu, kuwatopatia pesa wapokeaji au kusumbuliwa kwa kutuma pesa watumaji, yanasababishwa na Western Union Marekani, kwenyewe.
Je unajua kama ukituma US Dollar 1000 au Euro 1000, unatakiwa kutoa copy ya passport, ambayo jina lako linakwenda disclosed to FBI, na government agency za Marekani, kabla ya kuweza kupewa go ahead kwa Western Union, kurelease pesa zako, kwa mpokeaji au kupata refund back.
Na hii yote, inatokana na Western Union, kujaribu kuaccomadate hizi sheria za ajabu ajabu, ijapokuwa wewe si raia wa Marekani, unakuwa subjected to this stupid behaviour by Western Union, Tanzania Western Union, they cannot do anything about this. the only way foward ni kuboycot services zao.
Kama watadeny haya, basi Western Union wa Tanzania watoe statement kupinga hili kama haya ninayoongea ni ya uongo.
Yote haya ni kuhusiana na vita dhidi ya Ugaidi, aambiwa. Uhuru, haki ya mtu unadhalilishwa bila kujali.
hizi habari za western union kuzuia kutoa pesa mpaka mtumaji atoe kitambulisho ni za uhakika 100% nikiwa mimi mmoja wapo washanidhulumu
ReplyDeleteMiezi miwili ilopita nlimtumia mdogo wangu school wakamwambia mimi mtumaji niwasiliane nao kuwapigia simu wakataka passport na mimi niko mitini sina passport ikabidi niisamehe hela yenyewe
ya kubeba box iliniuma sana
sasa hivi natumia jamaa zetu wa kibemba au money gram.na sio mimi pekee yangu jamaa kibao nawajua waliochukuliwa pesa zao na western union na jina lako likiwa Mohamed au Rahman Hapondio noma kabisa