Home
Unlabelled
nuksi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
huo ni ukosefu wa elimu tu kaka michuzi.tumejaa ujinga kiasi ya kwamba mambo mengine tunayofanya ni aibu tupu.sasa hawamuoni ana kitambulisho na pia kama hawakuta hhao waandishi wa habari warushe sherehe hizo kwenye tv au kurekodi chochote kwanini waliwaruhusu kuingia uwanjani? kama nilivyosema huu ni ujinga tu wa kukosa elimu.
ReplyDeleteDuh! hii kweli noma! unajua hii serikali ndo hiyo iliyo wapiga hata wale waandishi hasa hapo kulikuwa na sababu gani ye kupiga zake picha? huu si mpango!
ReplyDeleteUshamba mtaumaliza lini na kuwekana kindugu huku katika nyeti bila qualification uelewa na hekima ndio maana mambo ya aibu kama haya yanatokea kwani hana beji to show kwamba yeye ni press na anatoka wapi na hao jamaa hawajui kusoma nini mnaweka ndugu zenu mno ndio maana. Sasa ingekuwa ni press kama 100 hivi kama kwa obama ingekuwa vipi kumbukeni this is 2008 punk!
ReplyDeleteMMhh! Democracy, Still long way to go ?
ReplyDeleteI wonder is anything to hide, within the government of Zanzibar, in regarding the public ceremony such as Sherehe za Mapinduzi.
I suspect, may be the TV crews did not have a permit to do a video shoot??? I wonder is there such a thing.
Or may be the officer was totally confused, wondering how to execute the orders given by his supreme. "usiachie mtu yoyote kuchukua video!".
Or may be, just may be, we zanzibaris/Tanzaians among the few tend to be boosting and pride while in UNIFORMS, which in somehow go over the top, when we are given a mandate to protect our dignitaries and members of the high office, ie. President, Army generals and other people of high office.
Who knows ????
By Mchangiaji
Imekaa vibaya huyo jamaa hana TV nini au bado ni-MSTONE AGE.hajuwi umuhim wa vyombo vya habari,apelekwe class afundishwe somo la umhimu wa habari.hapa siyo kwa kibaki alaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.kwanza yeye nani hapa bongo?
ReplyDeleteKwa neno la lugha ya kichagga (In facy la Ki-Kibosho, mijitu kama hiyo inayomgasi huyo mpiga picha tunaiita 'MATONDO'. Neno hili halina literal translation kwenda kiswahili lakini maana yake ingeweza kuwa mpumbavu asiyejua wajibu wake na kuheshimu kazi za wenzao.
ReplyDeleteIn fact kuna wengi usalama wa taifa wenye tatizo hili. unaonaje wakapewa orientation?????????
Tukio kama hili linalomhusisha mkuu wa nchi, ni laziima itifaki ya ulinzi na usalama ifuatwe.
ReplyDeleteMimi napongeza hao walinzi kwa kuhakikisha taratibu za kiulinzi/usalama zinafuatwa. Nadhani huyo askari anatii 'order' kutoka kwa wakuu wake wa kazi.
Waandishi wa habari acheni kulalamika; huyo askari yuko kazini kama nyie!
Hawa wazanzibari hawajatulia kabisa! Tatizo wamezoea ubinafsi sana na kukataa umoja (Muungano) kweli wameshindwa kuielewa TVT!! Tatizo hawa wandugu ni wabinafsi sanaaaaa kitu nje ya Zanzibar wanaona sio nchi yao, wamesahau maana ya muungano kabisa!
ReplyDeleteichunguzwe sababu na hatua kali zichukuliwe kama fundisho kwa wengine!
ReplyDeleteTv huwa zina nembo, cnn wananembo kwahio hata ukiona unachukuliwa unajua kwamba ni cnn, na ni vituo vingi vya tv vina nembo, kama tvt walikwenda kibububu jamaaa hawatawaelewa
ReplyDeletenani kasema mwandishi wa habari anapaswa kufanya kazi kwa starehe???? shurba shurba tu hadi kieleweke!! Mimi siwaonei huruma kwani ni sehemu ya kazi yao. acheni kulalamika, aliye somalia sudan na ethiopia asema nini???? acheni kulemaa lemaa na kazi zenu. wajibikeni ipasavyo. hamkufundishwa mbinu za kazi??? hebu angalia alivyonenepeana ovyo hajui kabisa maadili ya kazi yake huyo wacha apelekeshwe kisawasawa.
ReplyDeletekuitoa ishu kwenye blog anataka apewe picha ya matukio yaliyopita??? mwambie asubiri kumbukumbu za mapinduzi mwaka 2009. kwasasa akishe akiomba na kusali afike salama!!!
Yakhe Mdebwedo huo wataka tuseme nini tena siye? si swadakta kabisaaaa!!
ReplyDeleteKaka Michuzi, hii sio ajabu, bali mpiga picha anaelezwa kwa vitendo kuwa ZNZ ni taifa lingine. TVT ni ya bara tu, kule kuna TVZ. Au Bwana Habibu GUnze Hajui hiloooooo
ReplyDeleteImekaa sawa tu. Na serikali yenyewe ionje joto ya jiwe. Hao askari labda waliambiwa wasiruhusu vyombo vya habari sasa kwanini kama chombo cha habari kiwe cha serikali tuje juu? Safi sana askari
ReplyDeleteHuyo jamaa anaemzuia huyu mpiga picha wa TVT ni askari wa vikosi vya serikali ya Zanzibar. Hao jamaa wako juu ya sheria yoyote ya Zanzibar.Hakuna anaethubutu kuwagusa hao. Majeshi na polisi walioko Zanzibar wote huufyata mbele ya hao. Kama unakumbuka kuna wakati askari hao walikuwa wanakwenda kukata magogo katka maeneo ambayo ni ya hifadhi na watu walikuwa hawaruhusiwi. Wakayapakia kwenye gari lao na walipofika mahali panapoitwa Fuoni walisimamishwa na Polisi ambao waliwataka watoe kibali cha magogo hayo. Basi jamaa walishuka kwenye gari lao na walimpa kisago(kipigo) askari huyo mpaka akalazwa hospitali. HAKUNA LOLOTE LILILOKUWA. Sasa huyo jamaa wa TVT angeonesha ukaidi kidogo tu basi angepigwa hapo hapo na baadae akenda kupanda boti kurudi Bara bila YA LOLOTE KUTOKEA. Hiyo ndio Zanzibar Bwana Michu kama huujui. Hao jamaa wako juu ya sheria. Na wenyewe wanajua kuwa hawagusiki.Mifano iko mingi mpaka ya kuuwa.Lakini huu mmoja unatosha.
ReplyDeleteKaribuni Zanzibar.
Ni aibu kwa kweli,kama ni vyombo vya habari vya taifa wana expect kupiga picha bila vizuizi ukizingatia ni sherehe za mapinduzi. kama vyombo vya taifa haviruhusiwi wa binafsi inakuaje?na je,hakuna ID ambazo waandishi wa habari wote wanatakiwa kubeba ili wapewe access kwenye sherehe mbalimbali?
ReplyDeleteTatizo la hao jamaa ni shule tu.Yaani wakiambiwa kitu ni lazima kiwe hivyo! Mbona wenzao wa Mareakni wakiambiwa shoot, wanasita kwanza, licha ya kwamba amri ni amri! Huwezi ukaambiwa shoot na unayem-shoot ni dada yako au mama yako, nawe uka-shoot! NI lazima common sense iwemo! Hilo ndo jeshi la kisasa duniani. Lakini hao wabongo, mhhh! Ndo maana huyo haelewi maana ya TVT na live shootings!
ReplyDeleteUnanikumbusha mbali sana Michu. Enzi hizo Jeshini. Hao jamaa wenye tepe nyekundu kwa kweli wananiuma sana hao, licha ya kwamba nilii-enjoy sana jeshini.
inasikitisha.. Lakini ngoja nikuulize swali wewe Michuzi (ambaye pia ni mtu wa mambo ya habari) JE WEWE UNAONA HII IMEKAAJE??????!!!!!! Maybe it's time you commented on something....
ReplyDeleteIn a bigger picture,hii ina-underline baadhi ya kero za Muungano wetu.Sitaki kuamini kwamba hao askari walikuwa wanawabughudhi wanahabari kwa utashi wao (askari) wenyewe bali walikuwa wakitekeleza maagizo ya wakubwa zao.Ndugu zetu wa visiwani ni wepesi sana wa kulalamika,na laiti mtu wa TVZ angetendewa hivyo,basi pangekuwa hapatoshi hapo.Unyanyasaji dhidi ya wanahabari unapaswa kulaaniwa kwa nguvu zote.
ReplyDeleteHawawataki huko eti TV ya taifa??? taifa la wapi? hawawajui nyie...rudini bara
ReplyDeleteKimsingi haijakaa vizuri kuona kwamba mpiga picha tena zinazorushwa moja kwa moja kwa watazamaji kubugudhiwa akiwa anatekeleza majukumu yake.Maana kwa kufanya hivyo sio tu kulimletea usumbufu mpiga picha huyo,bali hata kuwakosesha wananchi matukio na habari zilizokuwa zikitokea mahali hapo.Lakini mimi binafsi kabla zijaendelea kuwatupia lawama wanausalama hawa,ningependa kwanza nijue sababu.Maana katika hali ya kawaida sio rahisi wapiga picha wa TV kutingwa kiasi hicho wanapokuwa kazini.Sasa naomba unisaidie kujua walitoa sababu zipi za kumzuia bwana huyu.Maana isijekuwa tunawalaumu wanausalama kumbe mpiga picha mweyewe ndiye alikiuka taratibu zilizowekwa.Tunakuwa hatuwatendei haki hawa maafande.Kila jambo naamnini lina taratibu zake na ni lazima zifuatwe.
ReplyDeleteTumsifu,BGSU,Ohio-USA
Michuzi! Kaka Tatizo linalosababisha yote hayo ni tatizo la kutokujiamini. Jamaa hawajiamini kwa kuwa wanajua kuna uchafu mwingi umefichika serikalini na wananchi hawatakiwi kuuona. Katokeo yake wanajihami kuliko kawaida kwenye kila kona ili mradi kulinda maslahi yao! Ni upuuzi mtupu hata mahusiano ya viongozi na wananchi we huoni yalivyo tofauti! Kiongozi anajiweka mballi sana na wananchi wa kawaida kwa sababu anaogopa wat wakimkaribia watagundua siri ya mlo wake. We angalia hata maeneo ya ikulu, ukionekana unapita pita tu pale jirani jamaa wanakumaindi! Hapa USA mtu unakatiza white house kama vile ni eneo jingine tu wanalkaa binadamu!!! Ila Bwana haya yote yaa Mwishoipo siku nchi yetu itasafika tu!! NAamini ipo !!!
ReplyDeleteMi naona kila kitu kiko wazi na hawa jamaa waliomzuia picha zipo, kilichobaki wachukuliwe hatua za nidhamu. na kama walitumwa basi aliyewatuma awajibishwe. Hawa ni sawa na wale waliomwagia mwandishi/mhariri tindikali. hii ni aibu na ubabe wa kishamba
ReplyDeleteHiyo imekaa vibaya...kwanini tusidai maelezo kutoka kwa wahusika?? Gunze atueleze alidaiwa kukosa/kukosea nini na hao mabwana watueleze ni kwa nini walishindwa kumvumilia mpiga picha huyo!!SIMPLE!!
ReplyDeletemimi binafsi naikiri huyo mwanhabari hana skills za kiandishi kama communication skills kazi ya uhandishi ni ngumu sana kama huna skills za public relations habri hazipatikani kirahisi yote hayo ndio sehemy ya kazi na ni kipimo kizuri sasa cha kutumia skills zako za uwana habari ambapo moja ya skills hizo ni public relationsmichuzi acha kulalama tumieni ubunifu na mbinu za kitaalauma kama kweli ninyi ni waandishi wa haberi profesional
ReplyDeletemi nahisi hao maafande ni wafuatiliaji wazuri wa blog hii, NA WAMEONA ILE POST NIKO VEKESHENI ZANZIBAR...
ReplyDeleteHivyo ni sahihi kabisa kuwazuia watu wanaoenda vekeshen kwenye sherehe za wenziwao na mikamera mikubwa mikubwa!
Najionea huruma muda wangu niliopoteza kuandika comments hizi, kwani michuzi hawezi post hizi...
Yahe huyo ameenda uwanjani hajavaa vizuri, muone hapo katinga lijinzi lakee na tisheti hata haina hadhi, liwapi lile jikoti likizibau la khakhi ati. Ndio nimemfukuza aende akavae vizuri bwanaa anadharau shughuli ya watu kwa kuvaa vibaya! Akavae suruali na koti au akavae kile kijizibau cha khaki kuficha hivyo vesti yake ya kijivu. Lazma shuguli za kiserakali ziheshimiwe ntu anakuja mbele za wakubwa kavaa kana kwamba anaenda sokoni tutalubali wapi yakhee!!
ReplyDeleteIngalikuwa hii shughuli infanyika bara angalionyesha zarau ya wazi wazi hivyoo? Hebu nyie muoneni jamanii!!
kwa nini hukumtetea badala yake unampiga picha mwenzio?au we ndo uliwashtua ili upige picha peke yako?tanzania hiyo mzee kila mtu na sheria yake ilimradi yuko kwenye himaya yake.
ReplyDeleteTVT imeonyesha hizi sherehe live. Vibali vinatolewa kwa waandishi wote, lakini ijulikane kuwa kila kituo kina vibali vyake kadhaa. Kama huyo muandishi hakuwa na kibali basi alikuwa ON THE WRONG PLACE AT THE WRONG TIME. Sio mnamlaumu tu askari, yeye anafanya kazi yake na inaonyesha kuwa huyo muandishi hakutakiwa kuwa kwenye hiyo sehemu aliyokuwepo.
ReplyDeleteWAANDISHI WA TANZANIA MSIJIFANYE NANYI NI NGUZO MOJA YA DOLA KAMA MNAVYOJIITA, MUENDAPO KWENYE SHUGHURI YOYOTE NI LAZIMA KUTOA TAARIFA YA MAANDISHI KWA WAHUSIKA IWAPO JAMBO LOLOTE LITATOKEA WAWEZE KUWASAIDIA PIA MVAE VITAMBULISHO VYA MWAJIRI WENU PAMOJA NA CHA PRESS KWA USALAMA ZAIDI, MSITEGEMEE ZAIDI KULALAMIKA KWA WATU ILI MUUNGWE MKONO KWA KUTOKUJUA KWENU.
ReplyDeleteAnon 12 7:33 we mzee TIBAIGANA nini maana hizo ndo sentensi zako mzee.
ReplyDeleteAnon 13 12:51 huyo jamaa mwenye utepe mwekundu ni MP military Police hata mimi aloo hapana mijamaa inahusudu valangati kama nini hiyo ila hapo anaonekana ana mapenzi mema.
kaka michuzi,stori za sherehe za mapinduzi ya zanzibar ni miaka arobaini na nne sasa,kurusha live ndio nini? alfu lela u lela hiyo haimalizi toka mwaka 64,stori ndo hizohizo~~~ naona jambo la msingi kwa nyie wanahabari kwa sasa si masuala ya mapinduzi wala muungano!issue ni kukazania katika suala la upotevu wa mabilioni ya mahela yaliyo fisidiwa NA BANK OF TANZANIA,hiyo mipesa ingeweza kufanya mambo mengi tu kwetu sisi watanzania~~~hii imekaje wadau,mabillioni si mchezo~~~
ReplyDeleteMDAU SEOUL~~