Ndugu Michuzi,
katika kuchambua chambua kwangu mtandaoni kwa bahati mbaya au nzuri nilidondokea katika mtandao wa
www.kongoi.com nikawakuta wazee kongoi huko Oslo,Norway, wamemweka javini mwanamziki nyota mwimbaji na kiongozi wa The Ngoma Africa band, Bwana Ebrahim Makunja aka Ras Makunja. huyu nyota alipewa kibano cha maswali juu ya kwa nini mziki wa dansi ulichelewa kufika katika masoko na majukwaa ya kimataifa, na maswali mengi mengine, ambapo wazee wa kongoi walitaka piga ua lazima wapate majibutena yenye kuwalidhisha wazee wa baraza waliokuwa JAMVINI

Pasitoshe baadhi ya maswali ilikuwa ni kama kumuhadhibu nyota huyo kwa kumbebesha msalaba kwa niaba ya wanamziki wenziwe wa mtindo wa dansi!
Lakini Ras Makunja alikuwa hana ujanja ila ni kutoa majibu tuu

Wazee hao wa kongoi
huko Norway walitaka kujua kwa nini bendi kama msondo hawaji Ulaya? majibu soma www.kongoi.com

Siwezi kusema kuwa Ras makunja alionewa kubamizwa maswali haya! ah! mwanamziki huyu ana sifa za malumbano ya kimataifa na haiwezekani aulizwe maswali ya kitoto ila huu mzigo wa mswali ni SIZE YAKE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hii!!!te!!te!teh!!!!
    Mahojiano babu kubwa labda tuseme ni wito kwa kila mtanzania,naona
    hapa ras makunja kahamua kutema cheche za moto!uwoga ndio unaofanya
    mziki wa tanzania kutofikia masoko ya kimataifa
    kweli kichaa wetu ras makunja
    kaza buti

    ReplyDelete
  2. ndiyo mchokozi wetu Ras Makunja!!!
    Pasua!Pasua! wamekuwita wenyewe javini !huo ni ukweli!Lakini kaka nawewe umezidi kuporomosha mawe!
    punguza kidogo

    ReplyDelete
  3. Pasua!Pasua!Ras Makunja
    heti badala ya kukupa zawadi ya mwaka mpya wanakuweka kiti moto!
    Hivi?wanategemea nini?kutoka mdomoni mwa Bwana Kichwa ngumu,pasua wameyataka wenyewe

    ReplyDelete
  4. Chizi!kaokota rungu halafu kakimbilia sokoni mnategemea nini?
    ni mawe!tu na kushambulia hizo
    ndizo zake

    ReplyDelete
  5. Jamaa huyu mimi namzimia sana sana
    kwa ushujaa wake wakuutangaza mziki wa bongo na kufanikiwa kimataifa,sio kazi ndogo hata kidogo,tena bila ya support ya nyumbani!kaza buti.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...