Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. kasi ya gari ilimzidi dereva, konda akaamua kudrop,lakini yaelekea dereva kalimudu anarudi barabarani.nashauri atumie vioo vyake kuwacheki konda na matingo wake.maana mbele kuna uchaguzi bridge giri lisijejikuta mtoni.

    ReplyDelete
  2. Konda alikua anadhulumu abiria,

    sometimes anadai hela mara mbili na pia wakat mwingine anakataa kurudisha chenji.

    Abiria kuja juu ndipo gari likaanza kuchukua uelekeo mwingine lakin hatimae limerudi barabarani, konda ashapatikana mwemngine kwan mbele kuna trafiki aitwae Uchaguzi, wenye gari wameogopa

    ReplyDelete
  3. hats off for KP.niko short of words.keep up the good work

    ReplyDelete
  4. My God! Kipanya una kipaji cha ajabu kabisa. Kwa ubunifu huu unastahili sifa kem kem Bro. manake dah! sijui niseme nini zaidi.....

    Ila Be Blessed and keep it up.

    ReplyDelete
  5. Kipanya nimekukubali, wewe ni funika bovu, hata sijui uwa unawaza nini kutoka hizo katuni zako. huna mpinzani bongo..... angalia husije kumalizia nguvu kwenye fani za kudandia (eg. mitindo) fani yako ndo hii, ungekua nchi zilizoendelea kwa kazi hii hii ungeendesha VOGUE, Big up masoud

    ReplyDelete
  6. " Mbwembwe za bwana duleva zilikuwa nzuri kweli ... kalamba kona then shwwwwwwwwwwwwwaaap karudi katika lane" ha ha ha..

    KP huwaga unanichoshaga mie! kila siku skosi kupita mtaa huu ili ncheke nawe... Tumia kipaji mtoto tuelimishe, tufurahishe na tuhekimishe.. keep up Kijana.

    Bangusilo Bint Kilongola

    ReplyDelete
  7. We Misupu usituzevenze na KP wako! Kitu hata hakijaeleweka mnasema tumerudi kwenye mstari. Kwanza tuhakikishiwe watuhumiwa watashitakiwa, pili tuelezwe fedha za uma zilizopotea zitarudije. Vinginevyo ni kiini macho tu.

    ReplyDelete
  8. Unajua sikuhizi gari za viongozi zimefungwa VITU huko chini, hii ni katika harakati za 'Ku-Control' spidi za magari,'Ku-Ditect' milipuko, basi alimradi tu kuwalinda Viongozi wetu.Na nnaelekea kufikiri hapa dereva wa gari hilo la viongozi alikuwa anakwepa mlingoti uliojitokeza ghafla katikati ya Barabara,Mhh!cha ajabu hata KP mwenyewe hakuuona!!
    **Haya tena Mambo ya Mlingotini hayo jamani**

    ReplyDelete
  9. Acheni kumpa huyo kipanya sifa zisizo zake hana ubunifu wowote zaidi ya kuchora.Kwa akili yenu finyu mnadhani sikuzote hiyo critic inakuwa ya kipanya!!?? Huyu bwana analetewa mawazo na wachambuzi wa mambo na kisha anaambiwa achore.anachofanya huyu bwana ni ku-translate katika picha.Msivamie fani kisha mkaanza kutoa sifa bila kujua undani wake.Mchoraji yeyote anaweza kuhamisha mawazo yoyote kuwa picha.

    ReplyDelete
  10. Asiyependa sifa hapo juu samahani kwa kukukera kumsifia Kipanya.. Ila swali langu kwako, ingekuwa ni wewe umeletewa mawazo na hao unaowaita wachambuzi wa mambo utaweza fanya alichokifanya huyu jamaa? Kama jibu ni ndiyo, basi nakushauri utudhihirishie kuwa Kipanya si lolote kwa kubuni idea yako mwenyewe then uipresent tuione otherwise jitahidi kupunguza wivu usio na maana.

    ReplyDelete
  11. bwana usiyependa sifa, masoud kipanya mkali, tusisubiri afe ndo tumsifie.

    roho inakuuma kuona mwafrika tena mtanzania akifanya mambo kama haya, we unaamini haiwezekani tu. na utakufa hivyohivyo ukiamini watanzania hawawezi

    ReplyDelete
  12. mimi naona bado hatujarudi barabarani.

    Yaani ndio story imeisha hivyo jamani . Na hela na walioiba nini ni kitawakuta au ndio hivyo ukiiba unajiuzulu then siku inaisha...badoo tuambiwe nini...kam ani hivyo basi hata mimi nataka niwe kiongozi nijitajirishe kesho nijiuzulu...Bado bwana kipnya bado hatujarudi barabarani kabisa.....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...