Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Hapa Kipanya hongera lakini rekebisha lile kosa la beast uliteleza. Na ukiomba msamaha basi mambo yatakuwa mswano.

    Vinginevyo,

    Hatusikilizi kipindi chako redioni
    Hatuji dukani kwako
    Hatunywi Serengeti

    ReplyDelete
  2. Yes KP mpe vitu hivo anataka kuzuga ili akupige changa la macho.Kuwa mwangalifu.Senyandumi

    ReplyDelete
  3. Hivi karibuni kumekua na watu au mtu fulani anajaribu kumkandia sana MAsoud kila inapokuapo katuni ya KP,wanasema mengi ikiwa ni pamoja na kutokua na shule.Lakini mimi sidhani kama madigree ndiyo uleta busara "wisdom" kwa maana ya shule ambayo huyu/hao watu wamekua wakidai Masoud hana.Katika fani yake ni ukweli usiopingika kwamba tayari huyu bwana ana Degree na sasa anazidi kupanda na muda si mrefu atakuwa na Phd katika fani yake.KEEP IT UP kp.Maneno yao yasikuzingue,hawana uwezo wa kukuzibia.Bro Senyandumi

    ReplyDelete
  4. Sheria ya uhujumu uchumi itumike kufilisi mafisadi
    Na Theodatus Muchunguzi

    RIPOTI ya Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza utata wa utoaji wa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura kwa Kampuni ya Richmond Development Corporation imebainisha kuwa maofisa kadhaa wa serikali wamehusika kuliingizia taifa katika hasara kubwa ya fedha za walipa kodi kwa kuipendelea kampuni hiyo ya kitapeli.


    Matokeo ya Kamati Teule ya Bunge iliyofanya uchunguzi huo chini ya uenyekiti wa Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe, iliyowasilishwa bungeni mjini Dodoma Februari 6, yalisababisha mtikisiko wa kisiasa, kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Ngoyai Lowassa na mawaziri wawili, Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi siku iliyofuata, kutokana na kuhusishwa moja kwa moja na kashfa hiyo.


    Wakati Lowassa alipochangia hoja ya Kamati Teule Februari 7 asubuhi akilalamikia kusingiziwa, kudhalilishwa, kutokupatiwa fursa ya kuitwa na kuhojiwa na kuwa kilichokuwa kikitafutwa ni uwaziri mkuu wake na kisha kutangaza kuwa amewasilisha barua ya kusudio lake la kujiuzulu kwa Rais Jakaya Kikwete huku wabunge wakionekana kuchanganyikiwa na kumlazimisha Spika Samwel Sitta kuahirisha kikao hadi jioni. Ni kweli kabisa kwamba wabunge na spika walikuwa na haki ya kuchanganyikiwa kwa maana ya kutokujua nini kingefuatia kutokana na kujiuzulu ghafla kwa kiongozi mkuu wa shughuli za serikali bungeni. Kuchanganyikiwa huko pia kulitokana na tukio hilo kuwa la kihistoria tangu nchi hii ilipopata uhuru wake mwaka 1961.


    Lakini katiba yetu tuliyoirithi kutoka katiba ya Uingereza (Westminster) inaelekeza uwajibikaji wa pamoja (collective responsibility) kwa maana ya kuwa waziri mkuu kama kiongozi mkuu wa serikali anapojiuzulu baraza zima la mawaziri linajiuzulu.


    Katiba ya Republican ya mwaka 1962 iliyoirithi Westminster ilimpa madaraka rais kuwa ndiye mkuu wa serikali na dola hivyo waziri mkuu akabakia kuwa mkuu wa shughuli za serikali bungeni. Kwa kuelewa hivyo, hapakuwepo na sababu ya spika kuchanganyikiwa na kulazimika kuomba mwongozo wa wabunge, ambao nao walionekana pia kuchanganyikiwa. Kilichokuwa kinatakiwa kwa wabunge ni kusubiri maelekezo kutoka kwa rais, ambaye jioni hiyo hiyo aliamua kulivunja baraza la mawaziri.


    Kamati Teule ya Dk Mwakyembe ni miongoni mwa kamati ambazo ziliwahi kuundwa na Bunge na kutoa ripoti ambazo zimeibua aibu ya viongozi na watendaji kadhaa wa serikali kukosa uadilifu, uzalendo na kuhusika katika kuhujumu uchumi wa taifa letu maskini. Yalitokea maneno mengi kuhusu wajumbe wa Kamati Teule. Wapo waliodai Mwakyembe na wajumbe wake wamehongwa ili kuficha ukweli kuhusiana na sakata hilo. Wengine wakadai Mwakwembe ameahidiwa uwaziri ili kuisafisha Richmond. Inawezekana uvumi huo ulisambazwa kuhakikisha umma unapoteza imani kwa Kamati Teule na kwa kweli wengi wetu tunaomfahamu vizuri Mwakyembe aliyebobea katika taaluma za Sheria na Uandishi wa Habari ilikuwa vigumu kukubaliana nao. Mwishowe Kamati Teule iliwapatia Watanzania zawadi nzuri ya siri ambayo waliisubiri kwa muda mrefu kuhusu sababu ya kupanda mara kwa mara kwa gharama za umeme.


    Matokeo ya ripoti tumeyaona na hatua za awali zilizochukuliwa, kwa maana ya kuvunjwa kwa baraza la mawaziri na kuteuliwa mawaziri wapya chini ya uongozi wa waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Kwa habati nzuri, moja ya mapendekezo ya Kamati Teule ya kutaka masuala ya biashara na uongozi kutenganishwa tumeona kuwa Rais Kikwete amelitekeleza wakati wa kuunda baraza jipya la mawaziri. Mengine hasa ya kuwachukulia hatua za kisheria na kinidhamu maofisa wote wa serikali na vyombo vya dola waliozembea ama kukaidi kutekeleza wajibu wao ni dhahiri kuwa yatatekelezwa kama Rais Kikwete alivyoahidi wakati akizungumza na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhamis na kauli ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera), Philip Marmo wakati akichangia mjadala wa hoja ya Kamati Teule, Ijumaa.


    Suala la Mwasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika kujiuzulu ni muhimu, ingawa yeye anadai hahusiki. Dhana ya wajibikaji wa pamoja na uzembe wa ofisi yake hawezi kuvikwepa. Jaji Damian Lubuva alijiuzulu wadhifa huo na maofisa wengine wa serikali kuwajibishwa wakati Zanzibar ilipojaribu kujiunga na Jumuiya ya Kiislamu Duniani (OIC) mwanzoni mwa miaka ya 1990.


    Serikali itarejesha imani ya wananchi ni kurejesha fedha zilizopotelea katika mradi huo kupitia utaifishwaji wa mali za waliohusika. Fedha hizo kama serikali itadhamiria kuzirejesha itakuwa rahisi kwa kuwa wahusika wengi mali zao zinajulikana ziliko. Kwa bahati nzuri, mfumo wetu wa sheria unaruhusu kufilisiwa mali za wahujumu uchumi kwa njia mbalimbali, kama mradi wa Richmond, ambao unaligharimu Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) jumla ya Sh 152milioni kila siku kuilipa kampuni ya Dowans iliyoirithi Richmond.


    Tanzania inayo Sheria ya Uhujumu Uchumi ya Mwaka 1984, ambayo ilitumika kuwafilisi watu waliohujumu uchumi kwa njia za ulanguzi wa bidhaa wakati wa matatizo ya uchumi mwanzoni mwa miaka ya 1980. Vile vile, Rais ana mamlaka ya kumuweka kizuizini mtu yeyote kwa tuhuma inayohusiana na kuhatarisha usalama wa taifa ili mradi mtuhumiwa apatiwe maelezo ya sababu za kukamatwa kwake ndani ya saa 24. Sheria zote mbili zikitumika serikali inaweza kuokoa fedha zaidi ya Sh 170 bilioni ambazo Tanesco inalazimika kuzilipa katika mradi huu wa kitapeli huku wananchi maskini wa Tanzania wakiendelea kubebeshwa mzigo wa kulipa gharama hizo.


    Napenda kutofautiana na Mbunge wangu wa Muleba Kaskazini, Ruth Msafiri ambaye wakati akichangia hoja hiyo, alipendekeza fedha zinazolipwa kwa Dowans zihamishiwe Wizara ya Nishati na Madini. Sikuelewa msingi wa hoja yake. Inawezekana alidhani hatua ya fedha hizo kulipwa na wizara mwananchi wa kawaida atakuwa amepunguziwa mzigo wa bili za umeme zinazopanda kila siku pamoja na gharama nyingine za Tanesco. Ukweli ni kwamba, kwanza hilo haliwezekani kwa kuwa jukumu la kufanya biashara ya umeme ni la Tanesco na hata kama hilo linatokea, serikali itapaswa kuzirejesha fedha hizo kutoka kwa wananchi hao hao kwa njia ya kodi.


    Serikali inaweza kukwepa kuwafilisi wahusika kwa hoja za kuheshimu utawala bora, ambayo ni ajenda kuu ya dunia ya leo. Lakini kwa nchi maskini kama zetu hatua za aina hiyo zikiachwa kuchukuliwa, watu wengine wataendelea kutumia madaraka yao kufanya ufisadi unaoendelelea kuitafuna nchi na kusababisha maisha ya ufukara kwa wananchi wa kawaida. Baadhi ya nchi za Asia kama China na Korea Kaskazini zinajivunia sana nidhamu kuwa ndiyo iliyoweza kuwasukuma kupata maendeleo. Ndiyo maana kila raia wake analazimika kufanya kazi kwa bidii na kwao adhabu ya ufisadi ni kifo.


    theodatusm@yahoo.com 0752450235

    ReplyDelete
  5. Wee Anony wa Pili inaelekea una GUBU wewe! Mambo ya Beast tumeishayaacha huko nyuma lakini wewe kila likitokea jambo la KP unayakumbushia! ACHA HIZO! SIKU HAZIGANDI, ndugu yangu!!

    Kipindi tutasikiliza!
    Dukani kwake tutakwenda!
    Bia Serengeti tutakunywa!

    Wewe Panda JUU ukazibe...........!!

    ReplyDelete
  6. The Beast bado ni gumzo ... Lo Kipanya wewe mbunifu kweli yaani ukakaa ukaona ngoja umwite mtu the Beast ka ... kweli wewe hodari

    ===================================

    Umeshawasiliana na mtu uliyemwita the Beast?

    ===================================

    Duh Kijana mtundu wewe ...!!!!

    Naughty in negative side

    Nakupa asilimia -90%

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...