Baada ya msemaji wa Jeshi la Polisi kuihusisha Jambo Forums na Ugaidi niliamua kutafuta msimamo wa wale wanaochunguza kweli watuambie kweli wana amini kuwa JF inahusiana na Ugaidi.

Nilipata nafasi ya kuzungumza na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) Kamanda Robert Manumba na kumuuliza mambo kadhaa yanayohusiana na Jambo Forums na kukamatwa kwa wawili kati ya wanachama wake kama 4000.

Tafadhali karibu usikilize mahojiano hayo na kwa habarii za kutwa nzima usikose kuingia
http://www.klhnews.com

Title: KLH News Episode: Mahojiano na DCI : "Jambo Forums haihusiani na Ughaidi"
http://mwanakijiji.podOmatic.com/entry/eg/2008-02-21T22_39_09-08_00
Enjoy!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. MUNGU IBARIKI TZ NA WANABLOG JF!HAWANA MAKOSA JAMANI.NUSU YA WANAINCHI WA TZ WAMECHANGANYIKIWA WAMEZOEA AU WANAPENDA KUDANGANYWA!MANAKE MTU YEYOTE AKIJIFANYA ANATAKA KUSEMA UKWELI BASI HUYO MTU HAWAKAWII KUMCHUKIA NA KAMA ASIPOANGALIA ATAJIKUTA KATIKA HARI MBAYA SANA NA HATA KUPOTEZA MAISHA YAKE.HIVI NI MAISHA GANI HAYA JAMANI?MSISHANGAE SIKU MOJA ITAFIKA WATU WATAAMBIWA WASIANGALIE TV WALA WASIWE NA SIMU AU WASIWE NA COMPYUTA-INTERNET.MIYE NASEMA TUU!TUOMBE MUNGU JF IRUDI HARAKA IWEZEKANAVYO!HATA USINGIZI SIPATI!!EHEE MUNGU NAKUOMBA WACHUKUE WOTE WANAOICHUKIA JF.AMENI

    ReplyDelete
  2. Jamani Mwanakijiji ni nini lakini? Mbona hata Michuzi anajua kwamba Jambo imefungiwa, si uache atatujulisha kwa wakati wake jamaniii?
    Binafsi unanibore unapenda misifa hata isiyokustahili, kujifanya mtu flani Bab kubwa, Oooh nimeongea na flani (We huongeagi na wadogo, bali TZ Big Fishes), ili tukuone nani?
    Bad enough, kucriticise kila kitu kifanywacho Bongo. Oooh, kiongozi flani mbaya, ooh, kitu flani kibaya na kushauri watu/watanzania wafanye hivi mara vile. Mbona wewe unayeona mapungufu ya Tanzania usije kurekebisha ukiwa huku unang'ang'ania Marekanai kama kwenu, makaratasi yenyewe huna ndio maana miaka nenda rudi hata likizo huji kwenu mtu gani wewe???! Uchochezi tu, Mwanakijiji baadhi tumekuchoka na misifa /uchochezi wako.
    Isitoshe na wewe unayo Blog yako tunaifahamu, si ukae kimya tutakuja huko huko jamani mwe!
    I am sick and tired of you! Kujifanya mtu flani kwamba Viongozi wa Serikali yetu wanakuogopa kama unavyopenda kusema (Which is not true), who the hell do you think you are Mwanakijiji?
    Mbona hao wenye Jambo Forum (At least Invisible could have said something/Post something to Michuzi if need be. Take a note, you are Just a member kwenye JF kama sisi wengine, get life and punguza sifa.
    Guess what........, watu wanashughulikia suala la hao wanachama wawili waliokamata and they don't see the reason kupublish mambo kabala hayajaiva. It's unfortunately you don't know much about the issue boy.

    ReplyDelete
  3. Michuzi kuwa makini kaka.

    Sawa, kuna uhuru wa habari lakini watu tusivuke mipaka.

    Rejea "Media case" with ICTR Arusha (Rwandan Genocide). Kangula Newspaper na RTM Radio, wapo wapi Hassan Ngeze, Nahimana na Ntagerura?

    Tuwe huru lakini tusivuke mipaka. Uchochezi haufai kabisa, sio fresh kuharibu uhuru na Amani iliyopo Tanzania. Tunaweza kuziaddress shida zetu kwa njia nyingi kwa kutumia huu huu uhuru wa kuongea pasipo kuwa na uchochezi.

    Tusitumie exposure tunayoipata kwa kukaa nje ya nchi kuvuruga Amani iliyopo nyumbani kwa kiburi kwamba if anything happen it won't affect us vile tupo nje ya Tanzania, lets think of our relatives/family left behind bwana.
    Tusikae kimya sawa, ila tuongee kwa njia zozote pasipo kuvuruga Amani, isitoshe hata sisi tukipewa hizo nafasi tunazocriticise si ajabu hatutaweza pia (Huwezi kumridhisha kila mtu).

    ReplyDelete
  4. anon wa Saturday, February 23, 2008 1:32:00 AM EAT, na wa Saturday, February 23, 2008 1:59:00 AM EAT, wote ni MAFISADI.

    Comments zenu zinawafanya muwe "HIGHLY QUALIFIED" kama MAFISADI

    ReplyDelete
  5. Nyinyi ma-anon wa juu wawili lazima mtakuwa baba zenu MAFISADI au wenyewe MAFISADI. Hivi wewe unategemea MAFISADI itafika siku wataamua tu kuiba basi, pesa ni kama asali, unapoilamba kidogo utataka zaidi.

    Na wewe anon wa kwanza unaonekana una chuki binafsi na Mwanakiji. Hulazimishwi kusoma anachokiandika, mwenye blog Michuzi hana noma nae na amebandika hilo tangazo ije kuwa wewe kajamba nani, Nyambaaaaf kabisa Sura kama Bundi anapuliza Moto tehtehte hahahah.

    ReplyDelete
  6. Huyo Mwanakijiji kihere here kimemzidi!Halafu anaficha jina lake halisi.Anajificha sura yake sijui mlemavu?Mbona akina Michuzi tunawaona hawajifichi?Pia anaona tuliopo hapa Tanzania matahira sana yeye mwenye akili ni yeye!Acha kuja huku kwa michuzi na kutuletea blah blah zako!Who are you??Sie hatuwezi ku deal wala kumsikiza mtu anayejificha ficha hatuna muda naye

    ReplyDelete
  7. Ndugu yetu Michuzi ametupa uhuru wa kila mtu kutundika mawazo yetu hapa!sasa kwanini nyie mna panic anavyo semwa mwanakijiji?Kama nyie mnamuona Mungu wenu huyo Mwanakijiji nini ninyi!wenginge tuma mchukilia wa kawaida hana lolote la maana zaidi ua kujiona yeye ndiye bingwa wa kuwasemea watanzania akiwa nje ya nchi!wengine wote hawana akili!
    Kama kweli ana uchungu na uzalendo wa nchi yake arudi nyumbani hata likizo tumwone kwenye harakati akupambana na ufisadi!halafu kwanini ajifiche????Tunataka profile yake kamilifu!
    Michuzi anzisha mada kwa kuuita"Mwanakijiji ni nani???
    Ili wadau tuchangie humu!

    ReplyDelete
  8. Nyinyi watoto wa mafisadi na wawakilishi wao.... tuko na nyinyi mpaka kieleweke! Tumenyanyasika vya kutosha kama taifa..., tumechoka kupewa vyandaraua na Bush kama zawadi!!! Tumechoka! Mwanakiji...wewe kanyaga twende mwanangu..ma-sell out ya mejaa katika nchi zetu. wamezoea kutuona sisi wote malofa...lakini huu moto uliowashwa...hauzimiki tena. Eti jamaa hana makaratasi..wewe inakuhusu nini? jamaa alienda kwa nguvu zake hakupelekwa na mafisadi wanaoiba kodi zetu......

    Ohh yeah, tunaheshimu uhuru wenu wa mawazo..lakini mbona wa wengine hamuuheshimu?

    Tanzania is changing and we are making the history, kama tumefanikiwa kuanzisha vita vya kimawazo..intellectual debate! we are winning and the winning team is...Tamnzanians!

    JF imesharudi...ngoja twende huko huko.....ni kumkoma nyani mchana kweupeeeeeeeee!!!!!!

    ReplyDelete
  9. SALAAMU KUTOKA UJERUMANI.Jamani ehe TZ hapendwi mtu!inapendwa pesa.hakuna mtu mzuri hapa duniani 'No BODY IS PERFECT'sioni sababu ya kumsema M/kijiji na sio vizuri kabisa!mimi binafsi wala sina haja ya kumjua anaishi wapi?au anaonekanaje!Tz ni nchi HURU.Sisi wenyewe mbona tunajificha majina yetu !hata mimi sitaki mtu anijue mimi ni nani!Huyo M/kijiji hatulishi hatumlishi na bila yeye hatuwezi kuwa masikini na wala matajiri 'People should mind their own bussiness!Pls Pls pls!!!!!watu wote tunajificha majina yetu sembuse itakuwa yeye M/kijiji ajitangaze jina lake kwani yeye ni mjinga!EXCUSE ME!!!!

    ReplyDelete
  10. THANX GOD!JAMBO FORUM IMERUDI.TUKUTANE HUKO!MICHUZI UR THE BEST.

    ReplyDelete
  11. HUYO ALIYEULIZA MWANAKIJIJI NI NANI, ANA HAKI YA KUHOJI. IWEJE YEYE MWANAKIJIJI ANA DIRECT ACCESS NA VIONGOZI WA SERIKALI, ALISHAMUHOJI HATA JK PIA. HATA KITOKEE NINI HUYU MWANAKIJIJI ANA DIRECT ACCESS NA UONGOZI WA JUU NA WANAMPA HIYO ACCESS AJISIKIAVYO! MBONA WAANDISHI, NA WENYE BLOGU WENGINE HAWANA DIRECT ACCESS.

    USE YOUR BRAIN GUYS MLISHATAHADHARISHWA SIKU NYINGI LAKINI HAMKOMI. MWANAKIJIJI YUKO KAZINI NA ANAENDELEA NA KAZI YAKE KAMA KAWAIDA.

    HAYA NENDENI BASI NA NYIE MKAMUHOJI MKUU WA UPELELEZI KWA NINI HAO VIJANA WAMEKAMATWA! SIKU MWANAKIJIJI YUKO SAWA NA NYIE? NENDENI MKAMHOJI HATA WAZIRI MKUU AU HATA JK MWENYEWE SI NYIE NA MWANAKIJIJI MKO SAWA?

    ACHENI KULEWA PUMBA ZA MAHINDI! TAKE CARE OF YOURSELVES, HIYO DEMOKRASIA MNAYOISEMA HAIJAKUWA KWA KIASI HICHO HAPA TZ! TUTAWASAHAU!!! OOHOOO

    ReplyDelete
  12. Mdau wa Ujerumani HOYEEEEEEEE!!!

    Hata na mimi najiandika kama "anonyomous" kama hao mafisadi wa juu. Ila mimi sio fisadi hata kidogo.

    Nyie mafisadi kama mnataka Mwanakijiji aweke picha yake na jina lake basi nyie tangulieni kuweka picha zenu na majina yenu kwenye blog ya michuzi halafu na mwanakijiji naye atafatia (kama akiona ni appropriate). Kuna msemo wa kiswahili unaosema "NYANI ALIONI KUNDULE, HULIONA LA MWENZIE". Msemo huu unawagusa moja kwa moja nyie mafisadi mnaoleta za kuletwa.

    ReplyDelete
  13. Hata wewe pia lako hulioni ungekuwa unaliona usingejiandika annon. Swali ni hili, kuna blogu kibao TZ, na wote wenye kuendesha au kuisimamia hizo blogs ama wameweka majina yao au hata na picha zao, kwa majina kuna Michuzi, Mjengwa, Chemi Che Mponda, Bukuku, Kisima cha Fikra (ambaye kaamua kuacha recently), Jikomboe ya Ndesanjo, Na nyingi tu zinazojadili issue za Tanzania. KULIKONI YEYE NA KLH NEWS YAKE AJIFICHE? NI NANI YEYE!

    HAKUNA MTU YEYOTE HUMU ANAYEWEZA KUJIBU HILO SWALI NI YEYE TU, KAMA NI MKWELI NA SI MNAFIKI AJITOKEZE SASA MAANA HANA CHA KUOGOPA KILA AKISEMACHO NI CHA UKWELI! SIO KUACHA WANA WE WENZIWE WANASOTA KWA AJILI YAKE! JITOKEZE KAMA KWELI NI MWANAUME WA SHOKA!

    ATAKEIJIBU HII MSG BASI YEYE NDIYE MWANAKIJIJI! KAMA SIO USIJIBU!!mhsu!!

    ReplyDelete
  14. Kaka Michu unatuharibia blogu yetu kwa kubandika hawa wapenda sifa kama wapenda sifa. Huyu Mwanakijiji mpenda misifa anatia kichefuchefu, aende kwenye blogu yake.

    ReplyDelete
  15. Mchawi lazima atamjua mchawi mwenzie si huwa wanakutana kwenye anga huko wanakoruka kwa ungo au makaburini kula nyama za watu au usiku wakipita wakiwanga.

    The same applies to Fisadi, Fisadi lazima atamjua fisadi mwenzie huwa wanakutana huko kwenye misheni zao, sasa wakiziadiana kete ndio utawasikia ooh fulani fisadi, fulani fisadi ulijuaje kama na wewe si fisadi. Hata wauza unga hivyo hivyo, wakishazimana tu basi wanatangazana.

    Michuzi tuondoleeni timu ya mafisadi kutoka JF waarabu wapemba hao wanajuana kwa vilemba. Walikula wee enzi ya shemeji yao sasa awamu hii mrija umezimwa kelele nyiingi. Rudini kwenu mkapande miti maana hata mlima unaanza kuyeyuka barafu kwa ajili ya ufisadi wenu! Tokeni humu!

    ReplyDelete
  16. LETS get this straight,tukubali, tusikubali if you want to know in depth whats happening in tanzania,JAMBO FORUM and now KLH NEWS are unavoidable. where praise is due tusiwe na roho mbaya,na chuki za binafsi will get us nowhere.MWANAKIJIJI,i have said it,and i am saying again,KUDOS to him,he has taken the art,to a level hitherto unknown in our shores,sooner it will be wrongdoings in the pipeline,being nipped in the bud

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...