mdau anauliza hapa ukiwa na ki-bajaji chako utaendelea na safari kwa kupanda hiko tuta ama...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 37 mpaka sasa

  1. Hii lazima sumbawanga!

    ReplyDelete
  2. Hili ni tuta au ni nyoka mnene??
    sitanii, nimeogopa kweli.

    ReplyDelete
  3. Huyo nyoka kwa lugha ya kwetu anaitwa EKIZIRAMIRE...haya wadau hiyo ni lugha ya wapi?naomba kuwakilisha

    ReplyDelete
  4. we michuzi hilo tuta au joka?/ Mi hata nikiwa ndani ya gari sipiti nageuza kazima. I can not stand snakes

    ReplyDelete
  5. Hapo inabidi kujiuzulu na hiyo safari kama alivyofanya Lowasa, Karamagi na Msabaha

    ReplyDelete
  6. Bajaji hapa haifui dafu baba'ake.

    Duh, hapa ni wapi aiseee, huyu jamaa anaranda randa to freely hivi.

    BABAT - Dar es Salaam

    ReplyDelete
  7. napenda kuuli za je hii ngoma iko hai au ime uliwa?

    mimi ningeingia mitini si wafichi

    ReplyDelete
  8. HII NGOMA SOO BABAAKE INAKUMEZA MZIMA MZIMA DUUU, NJIA YA KISARAWE NINI HII?

    ReplyDelete
  9. Kaka michu tumeshindwa kumwelewa huyo mdau na picha yake hapo juu. Huyo ni nyoka au gogo? Na hiyo barabara ni ya wapi hiyo? Kisarawe ama bagamoyo shamba? Kwani hajajieleza yakutosha.

    ReplyDelete
  10. Hilo dude ni MALI kweli, hasa ngozi yake.

    Hawa jamaa wa wanyamapori hawajapata taarifa waje kumchuna?

    ngoja msomali apite hapo na Landcruiser lake. atamvuta pembeni na amchune ngozi vizuuuri halafu aondoke nayo.

    Watanzania kweli wa ajabu. Si ajabu magari yanaweza kupondaponda.

    HIYO NI MALI JAMA.

    ReplyDelete
  11. Duh! mi nilifikiri chatu kalala barabarani! Kama una bajaj itabidi utelemke, manake huo ndio msaada kwenye tuta kama unajipenda!

    ReplyDelete
  12. Hilo TUTA lazima litakuwa linapumua. bajaji ikikutana na hilo tuta lazima itahairisha safari na kurudi ilipotoka hata kama wese litakuwa limekata.

    ReplyDelete
  13. Tutazz kama nanihiii ya tembo... KUDADEKI

    ReplyDelete
  14. Hapa kwa bajaji, nitasubiri hadi hili tuta litoweke, lakini nikiwa na semitrela, napandia hako ka tuta

    ReplyDelete
  15. Mwenetu hii inaitwa NGATA wale wa vijijini tunoteka maji kwa utosi.

    owani mwana owani kitunguu na ubani
    nyoka kalala njiani tumkanyage kichwani. Tuwapishe wenda kuni na wendao kisimani oo mtotoo oo mtotoo

    ah! nakumbuka enzi zileee niko mdogo mamangu alipokua anamchuchiza mdogo wangu ili alale, sasa nikawa naimagine nyoka alale njiani kisha umkanyage kichwani nikawa naipata simple ni kiasi cha kumtimba mara moja,sasa nikiangalia hilo tuta lililotandawaa hapo sijui utaanzia wapi kumkanyaga

    ReplyDelete
  16. Hilo tuta linafanana na lile joka linaloitwa Nondo mla Watu ..Ssssssss

    ReplyDelete
  17. huyu nyoka anamiguu nini mbona ni mkubwa namna hiyo?
    Naomba mnisaidie jina la huyo nyoka kwa kiswahili au kiingereza tafadhali wadau

    ReplyDelete
  18. Michuzi umenitisha jamani,uwiii kama mjamzito ni balaa kuangalia

    ReplyDelete
  19. MIchu aisee angalia picha za kuweka..kidogo niitupe coputer..nimeogopa.dah!!

    Joka la vipi hili? kama vipi itoe hii picha bro

    MWTYM

    ReplyDelete
  20. ebana michuzi una uhakika huyu si yule chatu-mtu wa buguruni mwishoni mwa miaka ya '80?Dah,hii imenikumbusha mbali sana.kile kisanga cha chatu-mtu nilikuwa kama darasa la kwanza ama pili,sema kumbukumbu yangu ni ngangari.

    ReplyDelete
  21. piga ua hiyo njia iko maeneo ya kisarawe, nakumbuka minaki tulishaua joka kubwa hama hilo, ililokuwa na mimeno mikubwa kuliko hata mbwa! Lili tisha bababke infact lilikubwa kubwa zaidi la hilo hiyo misitu ya pugu ni balaa kwa chatu

    ReplyDelete
  22. Michuzi na Wadau,
    hilo sio Tuta... huyo ni Nyoka

    kwa haraka haraka nadhani huyo ni ANACONDA, yule nyoka anayepatikana Ameriak ya kusini.

    nahisi hiyo mandhari pia imekaa ki-amerika kusini...

    ReplyDelete
  23. ka-mchuzi,Mdau mchina mmoja ameona hii pic, anatafuta cm no. ya ka-mchizi. analitaka JOKA kwa gharama yoyote.Sijui anataka kulila.

    ReplyDelete
  24. Hapo Lupa Tinga Tinga Chunya...swila la kazi hilo likikunasa basi wewe na bajaj wote ndio mlo wa mchana!!!

    ReplyDelete
  25. hii kitu inaitwa sawaka, nilienda kijijini kwa bibi dec hii ngoma huwa inakatiza barabara kila jioni kwenda mtoni kunywa maji, inakula mbuzi ka haina akili nzuri.

    ReplyDelete
  26. Aisee hii ni nadra sana kutokea! huwa hawa 'Wadudu' (kama wanavyo julikana maeneo ya Pwani)hawavuki barabara mchana mchana namna hiyo,labda alikuwa anaepuka moto ulowashwa na wanapori fulani,au alikuwa na KIU cha maji.safari zao huwa ni usiku mara nyingi.

    Anyway inanikumbusha sana Maeneo ya Nyumbu,Msangani(Kambi za Jeshi)Mkoa wa Pwani.

    ReplyDelete
  27. Na ndio maana huwa najiuliza kila siku huyo Eva/Hawa alikuwa kabila gani? Maana angekuwa mswahili angemwambia snake, ngoja kwanza nikaombe ruhusa kwa mume wangu (Adam) Na angekuwa mchina, aah huyo snake angekula kipondo, nyama ikaliwa ngozi ikatengenezwa viatu na kipochi. Na hapo hiyo picha hao wachina wa Dar wakiiona watatafuta hapo mahali mpaka wampate huyo snake.

    ReplyDelete
  28. hapo ni mlima kinyanyiko-kisarawe karibu na shule ya seco ya minaki.hilo joka lipo maeneo hayo tangu mi nabukua hapo miaka ya tisini mwanzoni.

    ReplyDelete
  29. Hii Kitoweo KIBAHA nini??mdau hebu tupe ufafanuzi kidogo.

    ReplyDelete
  30. Hao CHATU walikuwepo pale UDSM Campus. Kuna moja alikuwa anaishi kwenye bonde karibu na nyumba ya Mzee Biswalo. Halafu kuna couple walikuwa wanakaa bonde la Kileleni Rd. Na kulikuwa na mwingine kwenye ile bonde la Ubungo/Polisi Flats za Campus karibu na Engineering. Huyo alikuwa hana haya, anatoka mchana mchana anakula kuku halafu anarudi zake kwenye bonde!

    ReplyDelete
  31. Hii ni lazima ni Tanzania kwa sababu hakuna lami barabarani.

    ReplyDelete
  32. Duhh, Chemi Unakumbukumbu! ni kweli kabisa nakumbuka wakati fulani nikitokea maeneo ya Hall II,nikielekea Udasa club,nilipata kuliona moja karibu na Iliyokuwa nyumba ya akina Abuu Maghimbi...long time!!

    ReplyDelete
  33. Ngozi dili hiyo unapata pair kazaa za viatu hapo. Mimi ningemtwanga risasi ya kichwa ili nimchune ngozi hiyo kiatu chake si chini ya $600/pair.

    ReplyDelete
  34. That thing is scary bro!!i almost feel like its going to come through the computer screen.

    ReplyDelete
  35. Audhubillahi mindhalika,Michuzi unaweza ukaua mtu na picha kama hizi.Kitu kimetulia katikati ya barabara,ila nimekata mbavu na maoni ya wadau.

    ReplyDelete
  36. Acheni masihala,hilo treni la kitanzania sijawahi kuliona na utuuzima wangu huu.Inaniwia vigumu kulijua jina lake kama ni la tazara,tra au viberenge vya mkonge!kwenye uchatu,usawaka,ukoboko, hayupo,hii kazi kwelikweli huko aishipo atakuwa malikia au mfalme.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...