inaelekea sasa imekuwa fasheni wa machinga kugombana na askari wa jiji na kusaula hadharani. hii imetokea leo maeneo ya soko kuu la kariakoo ambapo jamaa alijitokeza kumtetea mama ntilie aliyevamiwa na askari wa jiji na kumkabili askari huyo kwa kumtaka awatafutie cha kufanya..

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 37 mpaka sasa

  1. bongo tambarareeeeeeee

    Ila huyo mwanaume kujiweka uchi hivyo hadharani yaani kumekuka kama porini bongo ...adamu na hawa....

    Kutembea uchi jambo la kawaida tu

    ReplyDelete
  2. ila huyo machinga sijui anaenda Gym kila siku...Yaani mwanaume wa nguvu....ouch...

    Anamwambia mgambo wamtafutie cha kufanya....tengeneza kalenda na mwili wako huo shoga itauzika...mtaji unaukalia hapo

    Pia kuna playgirl na chippendale dance

    ReplyDelete
  3. Tanzania sasa tunaelekea kubaya! huku si kwenyewe kabisa! Tunapotea njia njamani! Naisikitikia sana nchi yangu! Ehe! MUNGU IBARIKI TANZANIA!
    Mdau,
    Göteborg,Sweden.

    ReplyDelete
  4. sipati picha ya matusi ambayo huyu chinga alikuwa anashusha yaani unaweza toboka masikio, au kama mtu angekuwa anatoboka akitukanwa huyu mgambo angakuwa kama chekecheke

    ReplyDelete
  5. Imekua heri siku hizi ukamatwe na vijana wa Said Mwema kuliko hao mugambo. Jamaa sasa wamekua waporaji walioruhusiwa kisheria. Ukiona life imekua tight jiunge na mgambo utapora kiulaini tu na mambo yako yatakua shwari tu,si unaona mwenyewe jamaa alivyonona?

    ReplyDelete
  6. Mzuka wangu ukinipanda nguo ntavuaaaa.......

    ReplyDelete
  7. Hii nayo tutaiona gazetini kwa kutumia picha hizi hizi kwenye magazeti pendwa a.k.a ya udaku

    Halafu huyu askari mbona kama JKT haya sio magandwa ya mgambo

    ReplyDelete
  8. Kwa wale ambao mnaishi au kusoma nchi za ngambu kwanu kusoma habari kama hizi ni faraja kwenu kwani ndio bahati ya kuona matokeo yanayotokea hapa nyumbani kwa kifupi watu wamesha choswa kufanya makasuku na wasikuwa na mawazo na dio wamefikia hatua kama hiyo watu wameshakufa wadudu Mshawahi kuisikia hadisi ya vifaranga vya kuku humuomba mama yao maziwa wanyonye lakini kwakuwa hana hayo maziwa huwambia kesho kesho mapaka nawao wanajikuta wankuwa wazizi basi hayo ndio maisha yetu hapa Viongozi wetu kwa maneno matamu kuliko asali

    ReplyDelete
  9. SASA KAKA SIUNGEGEUKA HUKU KIDOGO NA SISI TUFAIDI

    ReplyDelete
  10. Inasikitisha kuona kwamba, ukijiripua ulaya, wazungu wataku-treat vizuri kuliko ukikaa katika nchi yako Tz.

    ReplyDelete
  11. Huyo jamaa mvuta bangi tuu,MWANAUMME NA AKILI ZAKE AWEZI KUVUA NGUO NA KUONYESHA UUME WAKE HADHARANI...NA BANGI LENYEWE ANAVUTIA CHOONI...SASA MBONA HUYO MGAMBO KASIMAA TUU BILA KUMPA VIBOKO VYA MAKALIONI??

    ReplyDelete
  12. HAWA MGAMBO WA JIJI NDIO WANA FASHENI YA KUWAVUA NGUO CHINGAZ, TUMEONA TUKIO LINGINE LILILOPITA KWAMBA MGAMBO WALIMVUA NGUO CHINGA, WAKAMPORA NA KUANZA MBELE SASA HUYU JAMAA NAFIKIRI ALIONA BORA AWAONESHE MGAMBO KWAMBA SIO LAZIMA WATUE MISULI ILI KUONA CHINGA WAMEFICHA NINI DOWN STAIRS SO KAMVULIA NA KWELI IME WORK OUT SI UNAONA BONGE LA MTU KATULI (KWELI HILI GAMBO MICHUZI)..........HALAFU MSHIKAJI ANA MPINGO SIO WA KAWAIDA DIZAINI!!!!!!!!!LOL!.
    MDAU UK

    ReplyDelete
  13. Oo baby jamaa amejaza mwili vizuri...ningependa tu kumsaidia mengine...my my hamna wanaume namna hiyo tena these days...huyu ni original ..bwana Michu,..tupe full unedited pics basi.

    ReplyDelete
  14. Leo sasa ipo kazi!! Siku itafika wote watavua nguo! uuuwi sijui itakuwaje! Haya ngoja tusubiri!!

    ReplyDelete
  15. Oh, GHOSH!
    THIS IS MORE THAN SERIOUS. TANZANIA, TANZANIA; WHERE ARE WE GOING? FOR US HISTORIANS, THE SITUATION IS NOT DIFFERENT FROM WHAT ACTUALLY HAPPENED IN SOUTH AFRICA, TO BOTH THE MIDDLE AND POOR CLASS, WHO WERE DEPRIVED OF ACCESS TO POLITICAL, ECONOMIC AS WELL AS SOCIAL RIGHTS, IN THEIR OWN COUNTRY OF ORIGIN. THE BLACK REACTED IN A VERY SIMILAR WAY. IT IS AN INDICATIVE OF SOMEONE WHO GAVE UP (REMEMBER THE SHARPERVILLE AFTERMATH). it was like this: The White police would shoot 500 African, and then a couple of thousand others would emerge, unarmed but ready to die. No meaning to life they could see at that moment.


    HUO NI MSISITIZO TU: NAKUJA KWENYE POINT:

    1) KAMA SERIKALI HAWAJUI YANAYOTOKEA, MICHUZI PELEKA HIZI PICHA MAGAZETINI.

    2) SITASHANGAA KUONA MAMBO YA KENYA YANATOKEA TANZANIA.

    3) TUJIULIZE SWALI, HAWA MAMA NTILIE WAKAIBE? MACHINGA WAFANYE NINI? JE, WAWE VIBAKA?

    4) MBONA HATUONI HELA ZOZOTE ZA AKINA BUSH ZIKILENGA KUINUA WATU KAMA HAWA WASIO NA NYUMA WALA MWELEKEO???

    HII INASIKITISHA SANA. MIMI KAMA NI KIONGOZI SERIKALINI NA SIWEZI KUTAFUTA SULUHISHO LA KUWAINUA WATU HAWA, NAJIUZULU. ILA WAPENDA MADARAKA NA UFISADI HAWAWEZI KUNIELEWA KABISA.

    ReplyDelete
  16. Tarehe Thursday, March 6, 2008 11:17:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

    Wewe umegonga kabisa...wazungu walisema desrate situations require desparate actions...huku ndiko tunakoenda watu wanaelekea kuweka desparation zao hadharani..tuendako si kwema hata kidogo.

    ReplyDelete
  17. Miaka ya nyuma pale mahakamani Kisutu na Mkwajuni(Mnazi mmoja) washtakiwa waliokuwa wakifikishwa mahakamani baada ya kukaa rumande muda mrefu walianza tabia ya kujipaka kinyesi (mavi) wakiwa mahabusu. Walikuwa wakijipaka kinyesi (mavi) ili wasishikwe na maaskari wakati wakiondoka mahakamani kupinga kuwekwa kwao rumande kwa muda mrefu. Pia ilikuwa ni ishara ya kupinga kuwepo kwao rumande kwa muda mrefu.

    Sote tujiulize "..Inakuwaje mwanadamu mwenye akili timamu aamue kuvua nguo hadharani?.." Baada ya kujiuliza, tuangalie majibu tutayoyapata. Natumaini wengi wetu tutapata jibu kwamba "..Ni ishara ya kupinga hatua zinazochukuliwa na askari/serikali dhidi yao.." Ndiyo kusema kwamba Wamachinga kuanza tabia ya kuvua nguo hadharani ni ishara ya kuchoka na yanayowajiri.

    Wamachinga wanapata adha kwa kuishi kwa mashaka kwa kutokuwa na uhakika wa maisha ya shwari na huru, kunyang'anywa bidhaa na fedha zao, kupoteza fedha kwa kunyang'anywa bidhaa au kwa kutoa rushwa ili kupata uhuru, kupigwa, na kuwekwa rumande na magerezani.

    Hali hii isipotafutiwa ufumbuzi kwa kuangalia hoja za pande zote inaweza kusababisha machafuko ya amani ya kitaifa. Kuna haja ya serikali kupitia kwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Waziri wa Mambo ya Ndani, Kamanda Mkuu wa Mgambo wa City na wadau wengine wowote kama Mkukuta na Mkurabita kukutana na kujadili kwa kina suala hili na kulitafutia ufumbuzi wa kudumu utakaoridhiwa na serikali na Wamachinga. Vinginevyo tunaweza kustushwa vibaya sana litakapotokea ambalo hatujawahi kulifikiria wala kilitarajia.

    Amani iwe nasi. Amen.

    ReplyDelete
  18. Michuzi tupe contact zake basi. Ukieka picha za wanawake wanawake wako nusu uchi huku kila mwanaumme anaomba contact zao. Na sisi wengine basi usitunyime contact zake huyu chinga.

    Mimi nitamtumia ticket isiwe shida kuangaishana na mgambo kwa mwili huo mwaliko atapata.

    ReplyDelete
  19. MIE NATAKA NA HUYO MGAMBO AVUE NGUO...MAANA CHA KWAKE KITAKUWA KAMA KIDOLE CHA MTOTO. NAFIKIRI MACHINGA ANAMWAMBIA AVUE, NDO MAANA HAWEZI KUMPA MKONG'OTO, MAANA WANANCHI WENYE HASIRA WATAMAKE SURE ANAVUA KU-AVOID MKONG'OTO

    ReplyDelete
  20. Si unajua bongo kila kukicha wao ni tizi kutembea mji mzima ni sawa na kukimbia marathon zaidi ya nne na usheee...sasa Gym la nini?? yuko 'natural' Mnaokaa ughaibuni tumieni hizo Gym na chakula chenu 'Mc Donald' hizo 'six packs' za chinga kama unazitamani utaziona kwenye magazeti tu!!

    ReplyDelete
  21. Badhi ya Watanzania wameanzisha mtindo wa kuvunja sheria halafu wakibanwa wanataka waonewe huruma..kwa mfano wanavua nguo ili jamii ihuzunishwe na kitendo cha askari wa jiji kusimamia sheria. Sheria ndogondogo zinatungwa na kusimamiwa na madiwani tunaowachaguwa sisi wenyewe! wao wanajua madhara ya biashara ndogondogo kufanyika sehemu ambazo haziruhusiwi...lakini kuna baadhi yetu sisi wananchi tunalazimisha mambo..hivi jamani kila mtu akiamua kujifanyia mambo anayotaka patakalika kweli hapa mjini???kila mtu kwa mfano akiamua ajipangie bidhaa mitaani aanze kuuza kutakuwa na mitaa ya kupita kweli jamani??

    ReplyDelete
  22. HABARI INASEMA TATIZO LILIKUWA KATI YA MGAMBO NA MAMANITILIE, SASA HUYU MMACHINGA ALIINGILIA VIPI HILO JAMBO, INAELEKEA HAKUNA MTU ALIYEMGUSA SASA IWEJE KUJIBISHANA NA MGAMBO NGUO ZIKAMVUKA? JE, KILA MARA TUTETEE WAHUNI WANAOVUA NGUO HADHARANI KWA KILE KINACHOITWA KUDHARALISHWA NA MGAMBO? LAZIMA TUWE MAKINI KWA HILI. VILEVILE HAWA VIJANA LAZIMA WAFIKISHWE MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUKAA UCHI HADHARANI KWANI INAELEKEA HAWAJUI KUWA KITENDO HICHO NI KOSA. KWA WALE WANAOPENDA KUTETEA UHALIFU WAENDELEE TU KUTETEA.

    ReplyDelete
  23. Uwiiiiiiiii... Yalaaaaaaaaa.....
    looo.... jamani Tanzania tutafika kweli
    sasa ndiyo nini tena hii,,,
    mambo hadharani.....
    ITOLEWE ELIMU YA AWALI

    YAMSEBO .A.

    ReplyDelete
  24. Tusilichukulie suala hili kimzaha ndugu zangu!Hii ni ishara ya kukata tamaa(a gesture of protest against humilitiation,an indication of hopelessness and desperation!)na kilio dhidi ya unyanyasaji wanaofanyiwa vijana wetu waliokosa elimu kwa sababu ya uzembe wetu sisi viongozi na wazazi,vijana waliokosa ajira na nafasi hizo za ajira kutokuwepo kutokana na ufisadi uliokithiri na kukumbatiwa na Dola!This is a Product of our own making!Hawa vijana wangepata fursa ya kusoma na wakapata ujuzi wa fani yoyote ile usingemuona hata kijana mmoja barabarani akiuza UKWAJU na maji ya barafu!Hawa Mgambo mishahara wanayolipwa kweli inatosheleza mahitaji yao muhimu ya kila siku?Au ndiyo tumezidisha genge la wezi na wazulumaji katika mitaa yetu?Ukiona katika nchi Mahabusu zimefurika kupindukia,Jela hazitoshi na uhalifu unazidi kupanda chati,Uhalifu wa kijinga tu mtu atagongwa hukumu ya jela miaka 30 au maisha!,Wizi Ubadhirifu na Ufisadi umetapakaa katika safu zote za Uongozi hakuna anayesema kweli au kumuogopa Mungu,Watu kununua nafasi za uongozi wa uwakilishi au siasa,kukithiri kwa fitna na kuhujumiana BASI UJUE HALI SIYO SHWARI NA JAMII INAPARAGANYIKA!Naiota siku ambayo nchi yetu nzuri ya Tanzania itakapo kuwa haina Jela hata moja,hakuna wahalifu wa kufikishwa mahakamani,tofauti zote zitasuluhishwa kifamilia au kikaya,Hakuna ulazima wa kuwepo Mapolisi,hakuna tofauti za kidini na ubaguzi wa aina yoyote ile,hakuna matabaka ya kiuchumi tajiri wa kupindukia na masikini wa kutupa,ziwepo huduma zote za kijamii zitakazo tolewa kwa wote bila kutanguliza uwezo wa kipesa...........endeleza wewe sasa........!

    ReplyDelete
  25. Michuzi hiyo picha siyo ya Bongo. Aliyekutumia kakuingiza mjini. Kwanza Bongo askari wa Jiji hawavai uniform za namna hiyo, pili hawana pingu kama huyu kibonge, tatu ukisoma maandishi kwenye jengo moja kwenye hiyo picha sio Kiswahili wala Kiingereza. Wabongo tuwe tunaangalia mambo kwa umakini kabla hatuja-comment na kulaani.

    ReplyDelete
  26. WE ANON WA 11:58 SIDHANI KAMA UNALIJUA SOKO LA K'KOO VIZURI. HAPO WALIPOPANGA NYANYA NA HOHO UKIKATA KULIA KUNA MSIKITI KWA MBELE. HIYO NI BONGO WANGU. HUYO ANAWEZA KUWA NDIO BOSS WA MGAMBO.

    ReplyDelete
  27. Wewe Kweli kariakoo huijui hapa kariakoo bwana huyo ni mgambo, wagambo wanatembea na pingu kaa huko beba box lako tu.

    ReplyDelete
  28. Hata kama ingekuwa Swisstzerland,haya mambo yapo hapa Bongo!We si useme tu Kiongozi Ofisi gani na sasa unaona Haya!

    ReplyDelete
  29. Ni ukiukwaji wa sheria kutembea uchi hadharani!

    ReplyDelete
  30. MICHUZI MIMI NAKUBALIANA NA MTOA WA MARCH7 TIME 11:58.HUYU MGAMBO BARLET YAANI KOFIA ALIYOVAA INANEMBO KAMA YA KIJESHI ASKARI MGAMBO ARUHUSIWI KUVAA HIVYO LABDA AWE JKT.
    PILI MITAA YA KARIAKOO KIPINDI HICHO INGEKUWA IMESHEHENA MAGARI KIBAO.NA

    ReplyDelete
  31. Unayesema hapa sio Bongo.......this is Bongo....

    ReplyDelete
  32. Anony wa 11:58 naona hujarudi nyumbani muda mrefu. Hapo ni mtaa wa Congo na eneo hilo walilosimama nalifahamu fika. Aliyekuambia askari wa Jiji hawana pingu nani??

    ReplyDelete
  33. wanawake tukitembea na vimini vyetu mnatutupia mawe lakini wanaume waionyesha vitu vyao kabisa wala jhamna anayewahukumu...This is not fair

    ReplyDelete
  34. Mimi naomba kuuliza mana kwa Mgambo ninayoijua mimi ya enzi hizo physical Training yake sio mchezo sawa na mwanajeshi hata ya Polisi nyuma sasa swali langu ni kwamba huyu mgambo wa Kandoro na huo mtumbo wa kukokota hiyo tizi alienda wapi na anafanya kazi kweli huyu ama ndio katika kula na kujuana ??? Bora huyo Machinga wa watu akajiombee yeye hiyo kazi ya mgambo na hilo li-mgambo well sijui lifanye kazi gani mana hata hiyo ya umachinga haiwezi kabisa purukushani zake !!
    ha ha ha !! halafu hawa chinga wanakuwaga wagomvi mana hapa atakuwa anampa dare mgambo wapimane uume ndio mana kabaki kuvimba kama nduli amini dada ! Yaani i wish ningesikia hiyo argument ilivyoenda! Ingawa naimiss sana nchi yangu na vituko vyake but kwa kweli bongo sio mchezo ,Yaani ni uharamia tuu hakuna haki kabisaaaa!! halafu ndio nyie viongozi mmeng'ang'ania kutuambia oooh vijana wetu mlio nje rudieni mjenge nchi !! kwa huu mfano mnaotupa U MUST BE JOKING AND VERY MAD!!! Mungu tusaidie ndugu, jamaa , marafiki na wanyonge woote huko BONGOLAND !!

    ReplyDelete
  35. jamani biashara haikatazwi lkn tufate sheria sasa huyu ni muhuni tu kashavuta bangi.Hivi hatuoni jinsi miji ya wenzetu ilivyo misafi hakuna mambo ya kupanga bidhaa barabarani tujifunze wabongo iyo ndo effect ya maendeleo lazima baadhi ya wa2 waumie angalia ilivyokuwa morogoro road wa2 waliobomorewa nyumba zao lkn iyo barabara ndo leo njia kuu ya uchumi tubadilike

    ReplyDelete
  36. HAO WAMACHINGA WATAFUTIWE SEHEMU NZURI YA KISASA YA KUFANYIA BIASHARA..HALAFU WAPEWE SEMINA YA NAMNA YA KUFANYA/ANZISHA BIASHARA NDOGONDOGO....HALAFU WAHAMISHWE WOTE HOKO MITAANI/MJINI

    ReplyDelete
  37. Mimi ni yule anony niliyesema hii picha sio bongo. Wale wanaodai eti hapo ni bongo kwasababu vitu vimepangwa chini hawajatembea Afrika hii, vurugu kama hizi ziko kote Afrika ukienda Freetown Abidjan Conakry kote masokoni ni kama karioakoo tu hivi. Hii picha ni ya Afrika mangharibi tena nchi ya francophony. Toka lini mgambo wa bongo akafunga buti kama huyu jamaa alivyofunga buti? toka lini mgambo wa bongo akawa na kofia yenye nembo kama hiyo? mgambo bongo hawabebi fimbo, wanabeba virungu. mgambo wa bongo hawapewi pingu. Hii picha hata ukijaribu kuweka caption ya kiswahili haiji kwasababu midomo ya hili limgambo haionyeshi anaongea kiswahili. Michu kwa heshima ya bulogi yako wadau tunaomba uondoe utata wa hii picha. Imepigwa lini na imepigwa na nani na hapa ni mtaa gani pale Kariakoo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...