MAHAKAMA ya Rufaa jana imemsafisha Rais wa klabu ya Moro United Ismail Aden Rage baada kushinda rufaa ya hukumu iliyotolewa wakati akiwa Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Tanzania (FAT) na sasa TFF miaka sita iliyopita.
Majaji Damian Lubuva, John Mroso na Mbarouk S. Mbarouk wamefuta hukumu ya miaka mitatu jela iliyotolewa mwaka 2005 na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya jijini Dar es Salaam na baadaye kuthibitishwa na Mahakama Kuu.
Imebainika kuwa hakukuwa na vielelezo vya kutosha kuonyesha kuwa Rage alitenda kosa alilohukumiwa nalo. Wakati wa kusikiliza rufaa hiyo, mwendesha mashitaka alikiri kuwa hatia aliyokutwa nayo Rage kutokana na makosa mawili haikuwa sahihi.
Makosa aliyokuwa akikabiliwa nayo ni yanayomhusisha kuiba Sh milioni 1 kutoka Salvation Army ya jijini Dar es Salaam ambako timu ya Taifa iliweka kambi kwa ajili ya maandalizi na michezo ya kimataifa na Sh 400,000 alizodaiwa kuwalipa posho wachezaji. Habari kamili bofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Hongera Bw. Rage. Wadau ninauliza, ile nafasi aliyokuwa nayo TFF ya makamu wa pili wa rais anarudishiwa automatically au zengwe jingine linaanza maana wakati rufaa yake inasuburi kusikilizwa katiba ya TFF ilibadilishwa ki-aina(bila shaka ikilenga baadhi ya watu) na inawezekana hata yeye ikamtupa nje. Wadau mnasemje?

    ReplyDelete
  2. Hongera sana Adeni Rage kwa kuthibitisha uma kwamba wewe ni msafi na hayo yalikuwa matope tu yakichafua suti sasa hiyo suti haku nayo,

    Me kwakweli nimefurahi na nilikuwa na hamu kubwa sana ungekuwepo tena pale TFF kwani naoana kweli panalegalega sana eti uwanja ukijaa maji mchezo hakuna hivi kweli tuna kiwanja kimoja hata Tanzania? Basi ujuwe kiutendaji hapo TFF wamechemsha mambo kama hayo wakati wako yalikuwa hakuna.

    Natamani Rage arudi tena TFF kwa sababu ni nyingi kwani kweli yeye administrative mzuri wa mpira wa miguu. Kweli angekuwepo kwa kipindi hiki chote tungekwenda cup of nation kwa yeye anajuwa fitina, mbinu kubwa sana za mpira wa miguu na kama unavyojuwa kwa kipindi chote Taifa Stars imepata wadhamini wa uhakika sana tatizo bado liko kwenye management ya mpira wa Tanazania .

    Ulivyotoka mahakamani ulisema umezaliwa upya sasa twende kazi baba .

    HONGERA SANA RAGE

    ReplyDelete
  3. Rage alionewa kwanini kwa nini aliyekuwa mwenyekiti wa FAT wakati huo (Muhidini Ndolanga) hakufungwa yeye?

    (mbarikiwa@gmail.com)

    ReplyDelete
  4. Kwa ufupi wanataka kutuambia alifungwa kimakosa?? etehehhe BONGO bwana....sasa Rage anaruhusiwa kudai fidia, cz amechafulia na kupotezewa muda siyo? TFF wamesema wanamjadili cz bado wanahisi harufu ya ufisaidi na hawataki kujiaribia

    ReplyDelete
  5. HATA HUYO RAGE NAYE ANGEPEWA NAFASI YA KURUDISHA PESA KIMYA KIMYA (EPA).TENA HAWA SIO WA KUFUNGA BALI NI WAKUNYONGA PALE MNAZI MMOJA.RAGE "NEVER TRUST ANY ONE IN YOUR LIFE" That's my free advice.

    ReplyDelete
  6. Huyu kosa lake kubwa ni kutaka ukingia kwenye siasa. SIASA NI VISA NA MIKASA!

    ReplyDelete
  7. Kwakua Dito ni mwislam mwenzio ndio maana unabania point yangu? Ama unapewa bakshishi na Dito kwaiyo unaona ukiweka hii point utaiweka bakshishi yako katika nafasi mbaya? Wewe Michuzi ni FISADI pia!!!!

    Nilisema Tusishangae tukisikia na Dito anafutiwa mashitaka then wewe ukaibania point.

    Acha UFISADI bwana Michuzi.

    ReplyDelete
  8. WE michuzi una mkataba gani na Rage?? maoni yote yanayomkandia huyaweki au na wewe alikugawia nini?? Au na wewe fisadi?? Tuambiane basi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...