dunstan tido mhando (shoto), mmoja wa nguli wa habari bongo, akiwa kazini enzi hizo akiwa redio tanzania na viongozi wa klabu cha simba. kulia ni mzee omar bawazir wakati huo mhariri michezo wa uhuru na mzalendo. hivi sasa tido ndiye bosi wa shirika la utangazji la tanzania (tbc) linalojumuisha redio tanzania na tvt. na endapo kama umaarufu unaoongezeka kila siku wa vyombo hivyo ni kiashirio, basi hivi sasa tvt ndio kituo kinachoangaliwa zaidi bongo kwa sasa kutokana na vipindi vizuri na uwezo wa kukava habari moja kwa moja wakati wowote na popote nchini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Pia nawaona Abdallah 'king'Kibaden na Abdulrahman 'Muchacho'...Simba ndio ilinguruma wakati mababe ya jangwani yaliroroma!!!

    ReplyDelete
  2. Mzee Abdalla Kibaden anafanya nini siku hizi???...je mnaweza kunisaidia kunipatia kitabu kinachoitwa Yanga na Simba lenye picha ya Sunday Manara na Abdallah Kibaden lililoandikwa na Bwana Haji Konde?Ni kitabu pekee chenye historia ya kandanda nchini enzi hizo...wasalaam..

    ReplyDelete
  3. Na Radio yetu ya Taifa inayokoroma nayo inasikilizwa sana kuliko hizi za FM siku hizi.Big up Tido.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...