
Hi Bro Michuzi!
Kwanza kabisa ninakusalimu sana, na kukupa pole kwa kazi unazo zifanya kila siku. Pia ninawasalimu wapenzi na wakereketwa wa blog hii.
HABARI:
Kwenye gazeti moja la hapa Italy, nimekutana na habari moja wakimzungumzia Baba wa Taifa letu la Tanzania Mwl.Nyerere. Nimesoma habari hii inayosema kuwa. Nitatafsiri kwa kifupi maana imeandikwa kwa kirefu sana, na baadhi ya kipande cha gazeti hilo ni hilo hapo.
Tanzania/ Daiosesi kuomba Julius Nyerere kuwa mwenye heri.
Kuanzishwa kwa swala hili au uombaji wa swala hili huko Vatican, kutakua na utata, na upingwaji mkubwa kutokana na Mwl. kuacha inchi maskini sana.
Mtu mkubwa ( Hodari sana ) Lakini kaacha inchi maskini. Kama lilivyo andika gazeti hili.
Swala hili lilisha anza kujadiliwa na litajadiliwa sana, ina maanisha litakuwa sio rahisi kama matarajio ya waTanzania wengi.
Kwanza kabisa ninakusalimu sana, na kukupa pole kwa kazi unazo zifanya kila siku. Pia ninawasalimu wapenzi na wakereketwa wa blog hii.
HABARI:
Kwenye gazeti moja la hapa Italy, nimekutana na habari moja wakimzungumzia Baba wa Taifa letu la Tanzania Mwl.Nyerere. Nimesoma habari hii inayosema kuwa. Nitatafsiri kwa kifupi maana imeandikwa kwa kirefu sana, na baadhi ya kipande cha gazeti hilo ni hilo hapo.
Tanzania/ Daiosesi kuomba Julius Nyerere kuwa mwenye heri.
Kuanzishwa kwa swala hili au uombaji wa swala hili huko Vatican, kutakua na utata, na upingwaji mkubwa kutokana na Mwl. kuacha inchi maskini sana.
Mtu mkubwa ( Hodari sana ) Lakini kaacha inchi maskini. Kama lilivyo andika gazeti hili.
Swala hili lilisha anza kujadiliwa na litajadiliwa sana, ina maanisha litakuwa sio rahisi kama matarajio ya waTanzania wengi.
Gazeti lenyewe linasifia sana na kuongea vizuri sana kuhusu Baba wa Taifa, kwa mengi aliyo yafanya hasa mambo ya Ujamaa na kujitegemea, mawazo yake ya kuziunganisha inchi za Afrika yaani umoja wa Afrika, kuunganisha makabila yote ya Tanzania kuwa ndugu au kitu kimoja bila kutokea vita.
Pia wamefurahishwa na kusifia sana kitendo cha waTanzania kumwita kwa kutumia jina la Mwalimu, kwakiitali MAESTRO, hili neno linamaana kubwa sana hapa Italy.
Na waTanzania kuwa na heshima ya hali ya juu kwa Mwalimu. Ambapo inchi nyingine sio rahisi kuwaheshimu marais wao hata kama walikuwa ni wazuri kwenye uongozi, yaani tumesifiwa waTanzania.
Pia liliendelea kusema gazeti: alikuwa mtu wa watu na aliishi maisha ya kawaida kabisa, mpenda kusali, kufanya kazi za kawaida kama watu wa kawaida kabisa, sio mpenda makuu, sio mpenda madaraka n.k, ambapo kwa inchi changa sio kitu rahisi na wala sio kitu cha kawaida.
Pia liliendelea kusema gazeti: alikuwa mtu wa watu na aliishi maisha ya kawaida kabisa, mpenda kusali, kufanya kazi za kawaida kama watu wa kawaida kabisa, sio mpenda makuu, sio mpenda madaraka n.k, ambapo kwa inchi changa sio kitu rahisi na wala sio kitu cha kawaida.
Wameeleza kuwa Jimbo kuu la Dar es salaam walikaa na kuongelea kuhusu swala hili, na kuamua kumwita Baba wa Taifa ni mtumishi wa Mungu kwa mambo mazuri aliyo yafanya hapa duniani, anastahili kuitwa hivyo.
Kwangu mimi ninasema hata kama ameacha inchi maskini, lakini ameacha mafundisho makubwa sana kwetu sisi waTanzania, hasa kuwa na amani na upendo mwingi si jambo dogo leo hii hapa duniani, ni jambo la kujivunia sana kwetu sisi Watanzania. Pia utajiri ni nini? Kama huna upendo na Amani kwa wenzio.
Kwangu mimi ninasema hata kama ameacha inchi maskini, lakini ameacha mafundisho makubwa sana kwetu sisi waTanzania, hasa kuwa na amani na upendo mwingi si jambo dogo leo hii hapa duniani, ni jambo la kujivunia sana kwetu sisi Watanzania. Pia utajiri ni nini? Kama huna upendo na Amani kwa wenzio.
Kwangu mimi binafsi ninachangia sana swala hili, kuwa Baba wa Taifa Mwl.Julius Kambarage Nyerere, anastahili kuwa mwenye heri au mtakatifu kabisa kwa mambo mengi mazuri aliyo tuachia Tanzania.
Tuzidi zaidi na zaidi siku zote kudumisha upendo na amani walio tujengea wazee wetu Baba wa Taifa na mwenzake Amani Abed Karume.
Salamu sana kwa Watanzania wenzangu popote pale mlipo.
BARAKA CHIBIRITI.
Salamu sana kwa Watanzania wenzangu popote pale mlipo.
BARAKA CHIBIRITI.
Hili swala la Nyerere kuitwa mtakatifu kwangu mimi naliona sensitive sana. Iam a normal person who is trying to be a good catholic, but sina uwezo wa kusema mwalimu awekwe kwenye hilo kundi au lah. Ngoja wahusika huko Vatican wataamua.
ReplyDeleteNyerere was a good man with his own dark spots in his personal and professional career.
All in all as a human aliitendea mema mengi nchi yetu kadri alivyoweza.
Kwa hiyo kigezo kimojawapo cha kuwa mwenye heri ni watu wako wawe tajiri na sio utu,amani na upendo. nisaidieni. Na huo utajiri wanauangalia kwenye vigezo vipi? vya pesa au?
ReplyDeleteKama ni utajiri basi Bush na wengine walio na utajiri ktk nchi zao wakifa waitwe wenye heri.
HAWA WAZUNGU WAJANJA WANAPENDA KUTUPUMBAZA KIMAWAZO KILA SIKU TUJIONE MASKINI MIMI NIKO HAPA EUROPE KAMA NI UMASKINI HATA WENYEWE WANAO WATU HAPA WENGINE NI OMBAOMBA; HAWANA PA KULALA; HAWANA CHAKULA; UKIPITA MZUNGU ANAKUOMBA EURO 1 NIKAMUULIZA YA NINI AKASEMA AKAPIGE SIMU KUMBE MAMBO YA MSOSI HAYAELEWEKI: WATANZANIA TUSIPUMBAZWE KWA KUITWA MASKINI TUFANYE KAZI KWA BIDII MAFANIKIO TUTAYAONA:
ReplyDeleteHUKU SASA WANA MIKAKATI WANASEMA HAKUNA HAJA TENA YA KUWASAIDIA WAAFRICA NA WAASIA INATOSHA SASA WANATAKA KUWASAIDIA WENZAO KWANI HATA KWAO KUNA MASKINI NA NI KWELI WAPO:
TENA USIOMBE UMASKINI WA EUROPE HUKU KILA MTU KIVYAKEVYAKE HAKUNA UJIRANI WALA NDUGU WA KUKUPA CHAKULA AU KULALA:
Michuzi ulikua huku ulionesha picha zenye sifa nzuri tu (mfano yale magari yalikua yanatoka kiwandani kwenda kwenye soko/bandarini wewe ukaandika yanaenda kutupwa)ni vizuri ungeonyesha na upande mwingine watu waelewe hali halisi. Mbona vyombo vya habari huku vinaonyesha mambo mabaya tu ya Africa vipi nyie mkitembelea huku? onyesheni pande zote.
Nitajitahidi nikutumie picha.
Akha! Chibiriti Chibatali hivi unafanya kazi ya kuuza magazeti huko!! mwe! habari zote za magazeti unazo!! tunashukuru kwa kutu update, and i dont think Mwalimu qualifies to be a saint anyway, he did good things, and he will just remain to have been one of the great presidents we ever had in AFRICA. may he rest in peace.
ReplyDeleteTunashukuru mh.kiberiti cha moto,toka kwa mammmmama mia pale italiano.
ReplyDeleteNi kweli kabisa heshima,hekima,busara,imani na ustaarabu wa mwalimu ni kuzidi hata mzee madiba ila watu hawajui tu.Kwa kweli kama sio mwalimu basi ya kenya yangetokea kwetu ila sisi wote ni watanzania bila kujali wapi unatoka na dini wala kabila lako,so mwalimu ninamkubali,mwalimu enzi zake alisema madini yasichimbwe maana hatuna utaalam na uwezo wa kuchimba so tuyaache tu mpaka tutakapokuwa na uwezo na utaalam na sasa mafisadi wanauza kama mali zao kumbe za umma,miaka 27 ikulu na katoka maskini,tunaona watoto wake walivyo,wakati marais wapya hawa mfano che ben nkapa na mali zake,ingekuwaje angekaa miaka 27??tunaona watoto wa jk sasa miaka miwili sijui tu na ma x5,so imani ya mwalimu ndio ilikuwa dira ya uongozi bora na swala la kuwa maskini kwani wao wa italiano ni matajiri kushinda wengine???so sisi kwetu pesa ni muhimu ila amani na upendio ni mwanzo na mwisho.
Matatizo ya Nyerere yalikuwa:
ReplyDelete1.Wakati haki za Binadamu zinaruhusu mtu kuishi popote apendapo Nyerere alilazimisha watu na kuwahamishia kwa nguvu kuishi kwenye vijiji vya ujamaa kinyume na matakwa yao kitu kilichosababisha umaskini mkubwa kwa watu wengi.
2.Alitaifisha mali za watu walizopata kihalali kutokana na jasho lao na kuziweka mikononi mwa umma wakati wa Azimio la Arusha.
3.Alikandamiza uhuru wa kuabudu kwa kulazimisha watu wa imani zingine kama wasabato,Wapentekoste na Waislamu kushiriki miradi haramu kwenye vijiji vya ujamaa kama vile ufugaji nguruwe na kilimo cha tumbaku.Wenye imani hizo Waliokataa waliitwa wapinga maendeleo ya vijiji na waliteswa na kusumbuliwa sana.
asante kaka chibi kwa kutuhabarisha mambo mazuri km haya..ila hiyo INCHI INAMAANISHA NN VILEEEEEEEEEEE mana mh!!!!!!! hata wifi yangu MDHUNGU mnaelewana kweli??.. na akitaka kujua lugha yako unamfundishaje THATHA hapo mambo yenyewe km ndo hayo
ReplyDeletemdau XXXL
mdau wa hapo march 31,11:37 am eat,imagine wewe au mzee wako mngepewa madaraka miaka ya sabini au sittini ungekuwa wapi leo??na enzi za zamani kulikuwa na mafisadi ila walikuwa wanaitwa wahujumu uchumi so mali zao zilichukuliwa na sio kwa kila mtu hao wachache walikuwa matapeli,toka enzi na enzi tz tuna kila dini usitudanganye hapa kingunge mfano ni mpagani mpaka kesho so hizo no story zako za kumake tu,na watu kuhamishwa ni urahisi wa vitu wakati huo na kila mtu ana mazuri na mabaya yake ila wewe kama mtanzania kweli basi mwalimu ndio wa kumpa sifa hapa tulipo leo nasio mwinyi wala mkapa kama hujui
ReplyDeletekwa wakatoliki nafikri ndio wahusika wa swala hilo so tunaomba mkutane ktk vigango vyenu na mjadili hapa ni wrong place na maoni ya wengi ni ya kutoa hasira zao
ReplyDeletemazuri ya nyerere ni kwamba enzi zake watu wakubwa waliokuwa wanamkiuka ama kwenda kinyume na matakwa yake walikuwa wanapotea na kufa vifo vya kiaina aina hivi na jinsi alivyokuwa hamaindishi UFISADI hiki kilikuwa kipindi kizuri sana cha watu kupata ajali za magari na kuharisha mpaka kufa kwa masaa machache !Mafisadi mngekiona cha moto bahati yenu! na justice ingekuwa served ! Baba wa Taifa Alikuwa ni mtetezi wa wanyonge, he was a great man well done nyerere !
ReplyDeleteAsante mkuu Chibiriti kwa habari hii. kwa maoni yangu ni kwamba Mwalimu Nyerere anastahili kuwa mwenye heri na hatimae mtakatifu. hilo suala la kupata upinzani katika mchakato ni suala la kawaida sana katika zoezi hilo ndani ya kanisa katoliki, kwani huwa wanahoji mambo mengi sana mpaka kufikia hatua hiyo. mwalimu mpaka anafariki au anang'atuka madarakani alikuwa katika vita dhidi ya umaskini, na kila alichokifanya mwalimu ilikuwa ni kwa nia njema ya watanzania na alitupenda sana kuliko hata wanae wa kuzaa mwenyewe, ndo maana hakuwaachia kitu cha pekee wanae, hiyo nayo ni sifa mojawapo njema, na naweza kukupa mfano wa watakatifu ambao wamepata heshima/tuzo hiyo kwa kazi kama hiyo, mfano ni Mama Teresa wa kule India, yeye alikuwa mstari wa mbele kusaidia maskini, lakini mpaka anafariki sio kwamba aliutokomeza umaskini, sema ule moyo wake wa kujitolea kufanya hiyo kazi imestahili tuzo aliyopata. pia nitakupa mfano wa watakatifu waliopata tuzo hiyo huku wakiacha nchi katika mateso makubwa, mfano ni mfalme Luis 16 wa Ufaransa, nchi ilikuwa katika hali mbaya kiuchumi, watu walikuwa wanakufa kwa njaa, mpaka wananchi wakalazimika kufanya mapinduzi yaliyomuondoa madarakani, lakini hatimae alipata tuzo kama hiyo ya kuwa mtakatifu, ndo kusema kuacha nchi katika umaskini sio kigezo cha pekee sana cha kumnyima mtu utakatifu, kinachoangaliwa ni pamoja na nia njema ya mhusika. nina mengi ya kueleza, lakini naona ni bora nikaishia hapo.
ReplyDeletemkereketwa wa Unyerere.
Kiimani Nyerere hastahili kuwa mtakatifu kwa sababu aliufunga Tanzania ubalozi wa Israeli (Taifa teule la Mungu) halafu akaanzisha uhusiano na Wakomunisti wa Urusi,Cuba,China na Korea ambao ni wakana Mungu wasiokuwa na Dini akaanzisha balozi zao na kuwa karibu nao sana.
ReplyDeleteKuwa mbali na kulipiga vita Taifa la Mungu hakuwezi mfanya mtu kuwa mtakatifu hata siku moja.
Hivi ni kwa nini watakatifu wengi katika kitabu cha majina ya watakatifu asilimia 92 ni waitaliano na waafrika hawafiki watu 20 ina maana miaka yote ya ukatoliki waafrika ni wapagani tu?
ReplyDeleteCHIBIRITI CHIBIRITI..
ReplyDeleteMSALIMIE SANA WIFI YETU, MWAMBIE ANAKARIBISHWA SANA BONGO SALIDALAMA
waulizwe Wakatoliki wenzake Christopher Kassanga Tumbo, na Joseph Kasella Bantu.
ReplyDeleteMwalimu alisaini hukumu za kifo, hilo tu linatosha kumuondoa katika mchakato wa kuwa Mtakatifu.
WE UNAYE ZUNGUMZIA URUSI, CUBA, CHINA MARA ISLAELI TAMBAA MBELE. APA WATU WANAJADILI KUUSU BABA WETU WA TAIFA KUWA MWENYE HERI,MTAKATIFU NA UMASIKINI ALIOUACHA TZ. KWA TAALIFA YENU BABA YETU AJAACHA UMASIKINI KIIVYO. HAKUIUZA NCHI KAMA ..., TZ BILA MZEE WETU MTAKATIFU WA KIFIMBO. LEO II TUSINGEJUA KUPENDA NA KAMA TULIVYO NA HILO NI LA KWELI ATA MILEMBE WANALIJUA. KUWAONGOZA WATU MIL 30 NA UCHACHE WAALIOKUA NA MAKABILA TOFAUTI KWENYE BARA LILILO TIWA NUKSI NA WAZUNGU KULETA SILAA NA WATU KUPIGANA VITA ZA KILA AINA, IKIWEMO UKABILA BASI UNAITAJI WADHIFA FULANI KUTOKA KWA MWENYEZI MUNGU MWENYEWE. MUNGU ALIMZAWADIA BABA KITU ADIMU SANA NA AKILI ZA ALI YA JUU SANA. NA WATU KAMA HAO MUNGU HUWA HAWAPI TAMAA YA KUWA NA UTAJIRI KWA KUWA UKO NDIPO ALIPO SHETANI. MIFANO HALISI TUNAYO, FIKIRIENI!! WAITALIANO NI BINAADAM KAMA SISI TENA USIKUTE GENERATIONS ZAO ZOTE HAWAKUPATA MTU KAMA MWALIMU. NA II NI KWA WAZUNGU WOTE WANAO TUITA WAAFRIKA MASIKINI. YOU CANT CALL SOMEONE POOR, WHEN YOU'D AREADY BEEN AT HIS HOUSE AND ROBBED THEM REGARDLESS OF THE TIME YOU DID IT. CONSIDER YOURSELF TO BE A MATERIALISTIC AND EMPTY SAUL WITHOUT THE REALISATION OF ANY REALM. IN OTHER WORDS I MAY SAY YOU ARE PRETTY FAR FROM THE MERCYNESS OF THE CREATOR. PEACE STANDS FOR WHICH ALLOWS US TO LOVE. HATE STANDS FOR HATE WHICH LEADS TO NAGETIVE CRITISISM, PAIN MANY BAD CHARACTERISTICS OF THE HUMAN BEING. HAINA AJA YA WAITALIANO KUMTEUA BABA YETU WA TAIFA KUWA MTU YEYOTE KATIKA HUU ULIMWENGU. MWENYEZI ALIYE MUUBA ALISHAGA MTEUA KUWA YEYE NI NANI KABLA HATA HAJA MUUMBA. NA SISI WA TZ MIOYONI MWETU TUNAJUA KUA YEYE NI NANI KWETU. NA ULIMWENGU WAO WATAJIJUA MBELE KWANZA NA HAO MAASKOFU WAO WANAO BAKA WATOTO WANA WATEUA KUWA NANI?? CHAA!! YANI ILI SWALA LIMENIGUSA VIBAYA. LINI TUTA HESHIMIKA HAWA JAMAA HAWATAKI. KWANZA KWA MKWALA BONGO WANGEWAOMBA WASIMJADILI BABA YETU WA TAIFA. WAMUACHE ALALE MAHALI PEMA PEPONI. AMINA.
ReplyDeleteHASH.
Jamani annonymous 31/3.hr 10:04EAT....nakushukuru sana kwa kuniwakilisha.Bro Michu ukija Ulaya pls onyesha yote kama wanavyofanya wao na picha za kwetu ok.Si tambarare tuuuu...!Hata mimi ntajitahidi nitume picha za umaskini wao hapa,si jambo la kufurahia lakini ni vyema kusema vitu kama vilivyo.
ReplyDeleteHima waTanzania!
kwa wewe anon unayeuliza kwanini watakatifu wengi wametoka Italia, na kwanini Afrika tunao wachache, kimsingi hilo sio tatizo la kanisa Katoliki makao makuu, ni tatizo la sisi au watu wa sehemu husika, kwani mtu akishafariki, ili awe mtakatifu, inabidi kanisa la mahali husika/alipoishi waombe kibali toka Vatican ili mchakato uanze, sasa mara nyingi ndugu zetu wamekuwa hawafanyi hivyo. mtu anafariki na sifa anazo, lakini hakuna wanaoshtuka kufanya hivyo, kwa wenzetu imekuwa rahisi sana kwa vile wapo karibu na Vatican hivyo kwenda kuomba kuanza mchakato ni sawa na kutoka posta ya zamani kwenda posta mpya. tunao watakatifu wengi sana Afrika na sehemu zingine ambao hawajatangazwa kwa vile hatujaomba. na Vatican kimsingi huwa hawakatai kuanzisha mchakato. mimi mwenyewe babangu anastahili hiyo tuzo, lakini mpaka sasa sijaenda kuomba mchakato uanze, kwa vile napisha kwanza Nyerere apate au mchakato wake uishe, ukishamalizika tu nalianzisha na nitaenda mwenyewe mpaka Vaticano. unaweza kuuliza kivipi Mama Teresa alipata fasta fasta, ni kwamba kila mtu alimfahamu na kazi zake zilifahamika, hata hivyo alipofariki Baba Mtakatifu Johannes Paulus II aliliagiza jimbo la huko alikokuwa anaishi kuanzisha mchakato mara moja, ndo kusema sometimes kama Vaticano wanamfahamu mhusika wanaweza kuagiza wahusika waombe mchakato(hapo nasisitiza kwamba ni lazima wahusika wa kule alikoishi waombe kwanza). nafikiri nimeeleweka.
ReplyDeleteMkereketwa wa Mt. Francisco wa Asis
acheni ujinga Nyerereni ni baba yake kivipi..? niyeye aliwaambie mmuite hivyo au woga wenu tu kama yeye baba na watemi wa jadi waliopigana na wakoloni tuwaite..? aliwabatiza ktk utanzania ili iwe yeye ndio baba yenu.eleweni amani ya tanzania ipo tangia enzi na enzi ndio maana kuna utani yani mzaramo mtani wake mtanzania na watu hawa walishilikiana kupigana na wakoloni..hao wataliano wanamsifia nyerere kwa kuwa aliwaachia waibe madini kwa kamba za kidini
ReplyDeleteNyerere kafanya mengi mazuri kwa taifa, Africa na dunia nzima. Anastahili heshima na kukumbukwa daima. Inapokuja kuwa swala la kuwa mwenye heri...give ma break...ili utick checkboxes zote ni ngumu sana, kwa mfano;
ReplyDelete1. Tanzania ni kati ya nchi chache zilizokuwa na concentration camps na watu kuteswa, kuhasiwa na kuuwawe...wakati wa Nyerere.
2. Watu walinyang'anywa maeneo ya kuishi na kugeuzwa mashamba (ya taifa) bila wao kuambiwa wapi pa kwenda...waliokataa waligongwa na magari, nakuamatwa na kuteswa mnoo.
3. Vyama ma ushirika vilipokwa 'too strong' Nyerere alivisambaratisha
4. Hakutaka kukosoliwa ndo maana hakuanzisha kozi za uandishi wa habari katika vyuo vikuu
5. Anatuhuma za kuwa na 'afairs'...
and the list continues...
Nadhani anastahili kuwa kwenye great wanamendeleo Hall of fame..sio mwenyeheri.
Umesema ukweli kabisa hapo uliye nitangulia. Baba wa Taifa ni mtakatifu toka utoto wake. Mambo mengi sana aliyafanya bila upendeleo wa kabila, dini n.k. Kwangu mimi sio lazima mpaka wamtangaze, Baba yetu ni mtakatifu wakutosha kabisa hata kama wasipo mtangaza. Watanzania tujivunie sana tena sana kwa hili, ni jambo kubwa sana.
ReplyDeleteKwa kuwa ili mtu awe mtakatifu inabidi maombi yapelekwe Vatican na watu wa mahali husika naiomba Vatican kupitia Blog hii imtangaze Issa Michuzi kuwa mtakatifu sababu katufanyia mema mengi bloggers duniani tuliosambaa sehemu mbalimbali.
ReplyDeleteChibiriti si umwombee mkeo muitaliano awe katika kundi la watakatifu au unamwonaje huyo mkeo ? Hawezi kukubaliwa kuwa mtakatifu hadi ung`ang`anie Nyerere?
ReplyDeleteAu mkeo hapendi utakatifu?
We una wivu na mke wangu, inaonekana ni msichana umenipenda, na wala sio mke wangu ni mpenzi wangu, nilikuwa sina mpango wa kumwoa lakini sasa nitamwoa kabisa. Hapo hunipati kabisa ulie tuuuuuu..... Tunaongelea swala la Baba wa Taifa wa nchi yetu, wewe unaniambia kuhusu mke wangu, hilo la mke wangu linakuuma sana inaonekana. Baba wa Taifa lazima atangazwe mtakatifu upende usipende.
ReplyDeleteNyenyere, mtakatifu na baba wa kifo, hawa ndo wadudu gani ee? mbona mi siwajui? au wale wanaokuja siku za mvua?
ReplyDeleteAsante sana Chibiriti kutuletea habari hii ingawa nimeisikia muda kiasi. Kwa muelekeo wangu naona sio vibaya Mwalimu Nyerere kutangazwa mtakatifu.
ReplyDeleteAlikuwa na kipaji cha hali ya juu kuongoza taifa letu hasa lenye makabila mengi tofauti. Kila nikiangalia nchi za jirani na Tanzania na Africa kwa ujumla kumekuwa na mapigano, chanzo kikubwa ni ukabila. Kama nchi haikuwa na mfumo mzuri wa kuunganisha makabila yake tokea mwanzo basi wananchi wake hawawezi kuelewana. Mwalimu Nyerere alitumia akili sana kutuunganisha. Watanzania hata tunapokuwa nje ya nchi tuna undugu wa aina yake ambao ni tofauti na watu tuka nchi nyingine za Africa. Utashangaa ukienda Malawi hadi leo kuna tatizo la ukabila ambalo liko miaka mingi.
Michuzi,
ReplyDeleteNaomba kuchangia ktk habari hii ya Chibiriti. Ni kweli Mwl. Nyerere alikuwa mtu mwenye mipaka ktk kuwabana waliotofautiana naye. Hakuwa kama viongozi wengine wa Afrika ambao walikuwa msitari wa mbele hata kuwa kutoa amri watu wauliwe kwa vile walitofautiana nae.
Na hii ilipelekea hata vyombo vya usalama vya Tanzania kuwa na kiasi ktk kuwa 'shugulikia wapinzani' maana Mwl. alikuwa mtu wa hatua za kiasi.Nenda ktk link ya 'the dark Side of Nyerere Legacy by L.S Mwijage mmojawapo wa wanaharakati www.zanzinet.org/files/darkside.txt
Mdau
Wa Historia ya Tz
Wazungu wanatapatapa hawaoni chema kwa rangi nyingine isipokuwa wakwao tu. Kimsingi kupinga Julius Nyerere asitangazwe Mtakatifu hasa kukifanywa na wazungu msingi wake ni ubabuzi wa rangi!
ReplyDeleteMtakatifu Francis wa Assisi alikiacha Kijiji chake masikini kuliko alivyokikuta, alivua nguo zake zote na kumtupia babake mbele ya askofu na kuondoka uchi kabisa.
Leo anasifika duniani kote na ndiye aliyekuwa mfano wa Mwalimu Nyerere.
Nauliza hivi fedha ndio msingi wa utakatifu? Hawa wazungu lazima wawe wapagani kabisa!
Tanzania ni nchi pekee katika Bara la Afrika kwa kuwa na Amani. Na hakuna kitu chenye thamani katika dunia hii kama amani. Amani hii ilitengenezwa na Julius Nyerere.
Wakati mwingine ni vizuri kuwauliza hawa wazungu hivi wanasema Tanzania ni maskini wakilinganisha na nchi gani?
Katika kusoma historia ya Kanisa Sijawahi kusikia kwamba kuna Mtakatifu aliyeipatia nchi yake mahela mengi. Je, Yesu aliitajirisha Israel? Au Yesu aliongeza mikate kwa ajili ya Mama Bikira Maria?
Mbona hawa wazungu wanaakili finyu.
Zamani watu waliposema wazungu wana akili nilidhani ni kweli. Toka miaka kumi iliyopita nimefuta kabisa dhana hii.
Kama kutajirisha nchi kimekuwa kigezo cha kutangazwa mtakatifu basi watakatifu wote tulio nao ni fake! Maana sifa kuu ya utakatifu ni unyenyekevu na matajiri wengi wana kiburi. Ni rahisi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano, kuliko tajiri kuingia mbinguni; Yesu alimwambia yule kijana aliyetaka kumfuata!!
Wazungu hawa wa Magharibu ndio waliotangaza kuwa Nyerere ni Mkomunisti na walimnyima misaada yote, ndio hawa ambao leo wanaiba dhahabu ya Tanzania bila kulipa kodi na kudanganya eti wanajaribu waone kama biashara hiyo ina faida!!!!!!! The criticism is a loud sounding nothing
Mungu ibariki Afrika Wabariki na na watu wake!
Blessed are the poor for they shall inherit the earth!
Ahsante Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kutufundisha njia ya Amani, Upendo na kujali kila binadamu.
Ee Mwalimu Julius Nyerere umwombee mtumishi wako Baraka Obama, afuate nyayo zako, siku moja naye auone uso wa Mungu. Umwombee Baraka Obama awe na busara, upendo na amani kama wewe.Awe mvumilivu katika kutukanwa na apewe hekima ya kuwashinda adui zake. Tunaomba utuongezee akina Obama hapa Marekani na akina Julius Nyerere barani Afrika. Hadi dunia hii iwe mahali pema pasipo na choyo wala ubaguzi wa rangi. Amina
Denyutali