Habari za leo Brother Michuzi,
Napenda kukupongeza kwa blog yako kufanya kazi nzuri ya kupeana update za moto moto.
Baada ya pongezi zangu napenda kutoa malalamiko yangu ya dhati kwa Waandaji wa bongo starsearch kwa kuonyesha hadharani kuwa wako biased na mmoja wa washiriki.
Nasema hayo kwa kuwa nina ushahidi na kielelezo,
Mfano:
Baada ya Rogers lucas kuonyesha umahiri mkubwa kwa kuimba kwa hisia kali nyimbo zake mwenyewe huku akipiga ala yake ya gitaa kila mtu aliamini kuwa yule ndiye msanii na mwanamuziki.
Kichekesho kinakuja pale ambapo chief judge alianza kumjudge, alimsifia sana na kasha kusema neon ambalo limeukwaza ulimwengu mzima wa muziki, alimweleza kuwa anatamani bongo star search ingekuwa inatoa washindi wawili ili na rogers awe mshindi.
Swali linakuja, kauli hiyo haionyeshi kuwa chief judge alikuwa amekwisha muandaa mshindi??
Naomba kutoa hoja ndugu michuzi.
Tafadhali naomba usitoe email yangu.
Wako,
Mdau
Brenden
FREEDOM IS THE RIGHT TO BE WRONG BUT NOT THE RIGHT TO DO WRONG
Napenda kukupongeza kwa blog yako kufanya kazi nzuri ya kupeana update za moto moto.
Baada ya pongezi zangu napenda kutoa malalamiko yangu ya dhati kwa Waandaji wa bongo starsearch kwa kuonyesha hadharani kuwa wako biased na mmoja wa washiriki.
Nasema hayo kwa kuwa nina ushahidi na kielelezo,
Mfano:
Baada ya Rogers lucas kuonyesha umahiri mkubwa kwa kuimba kwa hisia kali nyimbo zake mwenyewe huku akipiga ala yake ya gitaa kila mtu aliamini kuwa yule ndiye msanii na mwanamuziki.
Kichekesho kinakuja pale ambapo chief judge alianza kumjudge, alimsifia sana na kasha kusema neon ambalo limeukwaza ulimwengu mzima wa muziki, alimweleza kuwa anatamani bongo star search ingekuwa inatoa washindi wawili ili na rogers awe mshindi.
Swali linakuja, kauli hiyo haionyeshi kuwa chief judge alikuwa amekwisha muandaa mshindi??
Naomba kutoa hoja ndugu michuzi.
Tafadhali naomba usitoe email yangu.
Wako,
Mdau
Brenden
FREEDOM IS THE RIGHT TO BE WRONG BUT NOT THE RIGHT TO DO WRONG
Naunga mkono hoja yako. Na kama hiyo haitoshi baada ya misoji kuimba wimbo wake wa pili majaji wote walisimama na ilionekana wazi kabisa walipanga matokea hasa pale jaji mkuu madame ritha aliposema misoji you the winner. Ndio maana hata misoji hakuonyesha mshtuko wowote alijaribu kukamua machozi hayakutoka. Na crowd haikushangilia. Na pia nauliza kwanini hawakutuonyeha kura kama mwaka jana? Na mchemsho mwingine badala ya mgeni rasmi kuitwa jukwani kumpongeza na kumpa zawadi mshindi alipada jukwaani madam ritha kwakweli joel Bendera alidhalilish
ReplyDeleteMDAU USIWE NA WASI WASI KAMA HUYO JAMAA NI MZURI KIASI HICHO BASI ATAFANIKIWA KUENDELEZA KIPAJI HICHO .NASEMA HIVYO KWA VILE WATU WOTE WAMEMUONA NA MA MENEJA WA MZIKI PIA WAMEMUONA WANAWEZA KUMPA MKATABA.NI MAMBO YA KAWAIDA YANATOKEA KOTE DUNIANI MBONA HATA KWENYE "AMERICAN IDOL" YAPO HAYO.
ReplyDeleteDear Michu, mimi namuunga mkono aliyetoa hoja ya BSS 100%. BSS wanaonesha wazi upendeleo na inaonesha walikwisha panga matikeo. Rogers Lucas ni mshindi wa wazi, hakuna ubishi kwetu wananchi. Hii inazidi kudhihirisha jinsi gani Baadhi ya watanzania hawajakomaa in terms of openness and integrity,Hawana uzalenda wala uwazi na hawatumii haki ya wazi katika masuala ya jamii. Tunaomba ufikishe ujumbe huu kwa muandaaji mkuu wa BSS kwamba ametuangusha sana na amejishusha chini sana kwa upendeleo alioonesha.
ReplyDeletehawakutenda haki kabisa ktk shindano la bss siku ya final,kwanza ilitakiwa wawe wanatupa matokeo ya kura tunazopiga kila wakati kama wanavyofanya kwenye bigbrother africa na sio wanachagua mtu wao alafu wanatufanya sio wote wajinga.kama mshindi ni rogers pekee na yohana alistahili nafasi hata ya pili na sio ya nne
ReplyDeletehawakutenda haki mshindi ni rogers
ReplyDeletemisoji amekuwa kwenye danger zone mara kibao lkn rogers na yohana wamekuwa kipenzi cha watu sana iweje mwishoni ambae amekuwa kwenye danger zone kwa kupata kura chache apendwe ghafla na watu na awe mshindi eti amepata kura nyingi kuzidi wenzake? kuna usanii ulifanyika.
ReplyDeleterogers u rock baby
ReplyDeleterogers na yohana ndo walitakiwa waongozane kwa nafasi za ushindi
ReplyDeletewezi wa beats za watu sikubaliani nao kabisa kama kina abubakar mzuri anaiba beats za 2 face ila anaimba wimbo wa kiswahili sasa ndo kipaji hicho?hamna tofauti na misoji sasa hapo
ReplyDeleterogers u are my winner bro
ReplyDeletenaomba kumuuliza huyu ndugu aliekwazwa na BSS kama alimpigia Rogers kura ngapi?
ReplyDeleteManake hata mimi japo ningependa mtu wangu ashinde maadam sikupoteza hela yangu kupiga kura, nadhani sina haki ya kulalamika, you will never know ndugu wa misoji walimpigia kura ngapi.
Kigezo wanachotumia majudge ni kuhesabu kura tu.
Labda uwaombe wakibadilishe. Hata mimi pia sikipendi sana.
Lakini kwa kweli Misoji ana sauti kuliko wote, sijui vipaji vyake vingine, ila Rogers ana sauti nzuri tu, anatunga nyimbo nzuri, ana personality, anajua muziku na ala.
Ingekuwa mimi BSs ningeweka mshindi kwa upande wa washabiki, na mshindi mwingine apendekezwe na majudge wenyewe kwa kigezo wazi, na mshindi mwingine na wanamuziki wengine kwa kigezo wazi pia.
Ndugu,
ReplyDeletePole kwa kutoa report yako feki.
Hivi kwanini wabongo tunapenda ku judge mambo kila siku, Mama Ritha kaanzisha jambo lake zuri tu, hata kama lina makosa tunapaswa kumshauri kitaalamu, sio kulalamika bila vigezo. unaposema mshindi alipangwa, hukujua kuwa washindi walikuwa wanatumiwa SMS kila siku na ndio maana walikuwa wanaomba kura zetu?
Kitendo cha yule dada kushinda kilijulikana sio na majaji tu hata wengine ambao tupo nje ya jengo, nje ya ujaji, nina maana mtaani, tuliona kabisa mshindi ni yule dada kwa kuwa ana tumiwa sms nyingi sana, ingawa kulikuwa na mchuano mkali.
Je! wewe unayelalamika ulishawahi kutuma sms? na kama ulituma ulitumaje, maana isije kuwa unalalamika hata sms namba hujui wala huyo mshindani hujui alikuwa anatumia namba gani.
Fanya mambo yako ya msingi, na toa ushauri wa maana.
Tusipende kuongea kimtaani zaidi, tuongee kitaalamu zaidi
Hongera Washiriki wote wa BSS, Hongera mshindi wa BSS, hongera majaji, na hongera wale wote waliokuwa wanfuatilia kwa umakini BSS.
Shukrani nyingi kwa Mama Ritha (big up)
mimi mreketwa na mdau Buberwa
HAPO SASA!!! NADHANI WALILEWA POMBE MPAKA WAKAJIKUTA WANATOA SIRI ZA NDANI, KUSEMA UKWELI BAADA YA KUTANGAZWA MISOJI, SIKUONA TENA MAANA YA BSS, NA NILIJUTIA SANA MSG ZANGU NILIZOTUMA KUTUMA KURA!!! YANI MAANA HALISI WAMEIONDOA KABISA, MADAME RITTA NA UZURI WAKE ULIPOTEA GHAFLA, NAFUU HATA SALAMA ANAYESEMA UKWELI KUANZIA MWANZO, NA SALAMA NDO ALIYEKUWA ANAMPENDA ROGERS KWA UKWELI, SAA NYINGINE TUNAMLAUMU SALAMA ILA KWENYE ZOEZI ZIMA ALIMSIFIA SANA ROGERS FROM THE START!!
ReplyDeleteWELL, YOTE MAISHA ILA SIKUPENDA MWISHO WA BSS KABISA!!!
NAWAKILISHA
aisee ndugu yangu, pale hakuna biased ya aina yeyote since wapiga kura ni wananchi wennyewe. na kwakusema kwamba Rogers anauwezo kuliko Misoji unakosea nikiwa na maana hata misoji siwezi judge kwamba anauwezo kuliko Rogers sababu sina kipimo ila kwa haraka haraka na kwa ufikiri ni kwamba wote wana vipaji vya hali ya juu, palikuwa na uvumi kwamba Rogers anauwezo wa kutumia chombo, utunzi n.k kuliko msanii yeyote yule, ni kweli sikatai ila mbona alipopewa kazi ya kutunga nyimbo za ukimwi still akawa wa nne na huyo misoji ambaye hakustahili amekuwa wa kwanza!! waweza kutilia mashaka hata nyimbo alizokuwa akiimba Rogers siyo ajabu alitungiwa.
ReplyDeleteKingine jamani fair enough, hivi kuna nyimbo ngumu kuziimitate kama nyimbo alizoimba misoji?????? labda nakosea ila kwa kiwango fulani huyu mdada alijitahidi saaana na uhakika zile nyimbo angepewa Rogers angejikamua mpk ushuzi wa mwisho ungemtoka lakini still angeshindwa. watanzania tusiwe na roho ya kwanini Misoji, she deserve bwana" zile level ndo majaji wa american idol wanazitafuta, mtoto hajikamui, anacheza na sauti yake kama Ronaldinho anavyocheza na mpira afterall hakuna mahala palipoandikwa kwamba ukiimba nyimbo zako watakuconsider zaidi.
ROGERS IS GUD BUT MISOJI IS THE BEST
aisee ndugu yangu, pale hakuna biased ya aina yeyote since wapiga kura ni wananchi wennyewe. na kwakusema kwamba Rogers anauwezo kuliko Misoji unakosea nikiwa na maana hata misoji siwezi judge kwamba anauwezo kuliko Rogers sababu sina kipimo ila kwa haraka haraka na kwa ufikiri ni kwamba wote wana vipaji vya hali ya juu, palikuwa na uvumi kwamba Rogers anauwezo wa kutumia chombo, utunzi n.k kuliko msanii yeyote yule, ni kweli sikatai ila mbona alipopewa kazi ya kutunga nyimbo za ukimwi still akawa wa nne na huyo misoji ambaye hakustahili amekuwa wa kwanza!! waweza kutilia mashaka hata nyimbo alizokuwa akiimba Rogers siyo ajabu alitungiwa.
ReplyDeleteKingine jamani fair enough, hivi kuna nyimbo ngumu kuziimitate kama nyimbo alizoimba misoji?????? labda nakosea ila kwa kiwango fulani huyu mdada alijitahidi saaana na uhakika zile nyimbo angepewa Rogers angejikamua mpk ushuzi wa mwisho ungemtoka lakini still angeshindwa. watanzania tusiwe na roho ya kwanini Misoji, she deserve bwana" zile level ndo majaji wa american idol wanazitafuta, mtoto hajikamui, anacheza na sauti yake kama Ronaldinho anavyocheza na mpira afterall hakuna mahala palipoandikwa kwamba ukiimba nyimbo zako watakuconsider zaidi.
ROGERS IS GUD BUT MISOJI IS THE BEST
Hivi nyinyi mnao lalamika mmewahi kuona Pop Idols au similar programme? Judges wanaruhusiwa kuonyesha hisia zao 100%. Inaitwa appreciation of talent! Rogers is good no doubt but Misoji is the best! Tunajuaje, pengine Misoji amemeshinda rogers by just 1 sms!! Hata kweneye mbio, aliyeshinda by 1 second ndiye mshindi!!
ReplyDeleteHivi nyinyi mnao lalamika mmewahi kuona Pop Idols au similar programme? Judges wanaruhusiwa kuonyesha hisia zao 100%. Inaitwa appreciation of talent! Rogers is good no doubt but Misoji is the best! Tunajuaje, pengine Misoji amemeshinda rogers by just 1 sms!! Hata kwenye mbio, aliyeshinda by 1 second ndiye mshindi!!
ReplyDeleteMatokeo yalipangwa ilifika wakati fulani tukiendelea ku vote kwa ajili ya Rogers zikawa hazipokelewi zinarudishwa. Audience wenyewe walinyamaza kimya hakuna hata kumshangilia. Waandaaji acheni ubabaishaji hadharani. Muwe munaonyesha hadharani upiganji unavyoendelea. Kama lilikuwa ni swala la mwanamke safari hii kushinda basi mgetueleza kuwa kubalance gender@
ReplyDeleteRogers usikate tamaa wewe ni mwanamuziki endeleza libeneke lako la muziki na utakwenda mbali sana. Huyo Misoji ataendelea kuinga nyimbo za watu mpaka mwisho wa dunia!
rogers ameonewa mimi nilikuwa nikifatilia kila siku BSS kwenye mtandao niliona yeye ndio mshindi kwa kipaji chake sasa wakampa yule binti ambae wig lilidondoka sio najua rogers utafanikiwa tu kimaisha
ReplyDeleteKwa kweli lile tukio lilikuwa full KERO...Tukiacha upande huo wa kumpika mshindi bado ukumbi ulikuwa na Joto mno.Mlalahoi nilijikunja na mai waifu wangu kukata tikiti za VIP ambazo nilizipata kwa tabu lakini niliishia kusimama nyuma karibu na meza ya vinywaji eti ukumbi umejaa.Nini maana ya kuuza tikiti kabla ya tukio then??
ReplyDeleteNaunga mkono hoja kwa 100% Rodgers alideserve kushinda bt sijui kilichotokea ni nini,wanasema wanatafuta kipaji sasa sijui cha aina kwa kua rodgers anajua kuimba,anajua kutunga na kupangilia nyimbo,anajua kupiga gitaa hivi kipaji zaidi ya hapo ni kipi?katika bss naomba muniambie wadau mwenye sifa kama hizo za rodgers ni nani?si changa la macho hili?wameboa sana.
ReplyDeleteRogers ameonewa sana bwana, nyie mnaobisha bisheni tu kwa vile ni ndugu wa misoji or friends, wee unaesema ushuzi umtoke unaonekana wee ushuzi unakutokaga hata ukipiga muayo kwa hiyo unadhani na wenzio screw zao zimelegea kama zako!!!
ReplyDeleteYule kijana anaimba sana, kubalini tu waandaaji wa BSS mwakani mfanye kitu cha maana, tumeona kuanzia mwanzo, na madame Ritta alichemka na kusema mwenyewe, sasa sijui mnabisha nini!!! ile bahasha ilishafungwa saa nyingi tu, na madame ritta alishakuwa na uhakika na anachokisema ndo mana!! Bongo ni bongo tu.
Rogers u Rock...to me u are the winner!!!
Kura zimehesabiwa saa ngapi??Mimi nilikuwepo na hakukuwa hata na Mtu wa Ufundi(IT) pale aliyekuwa akihesabu kura...ile ni sms gaming kwa taarifa yenu..wanataka mpige kura at a premium rate wao wale hela.Majaji ndo wanaamua kila kitu.U knw why??kwa sababu mwisho wa siku ni biashara yao ku-deal na yule msanii after winning.Misoji ule wimbo wa pili kauimba Flat kinoma mwishoni na hakuuanzia mwanzo angepasuka mapafu...shouting is not singing wadau
ReplyDeleteBSS wamechemsha mno,huyi misoji aliandaliwa nakumbuka hata ktine alisema anafurahi anapoona mtoto wa rafiki yake ambaye nae ni mwanamziki akifwata nyao za baba yake...hata akadiriki kupanda jukwaani kumpongeza...madam Ritha ndo kabisa akasema mshindi ni mmoja anatamani wangekuwa wawili ili rogers nae ashinde!!!!!siku nyingine msituambie tupige kura mchaguage wenyewe sio kutuchezea kama watoto...kwanza majaji wenyewe hawana nidhamu esp Salama na Master J sijui walikuwa n nye...... wale.Misoji ukaimbe bagamoyo sasa na mawigi yako mana nywele huna!!wamechesha kama mwaka jana...houo jumanne idi kwanza nidhamu hana anapiga makelele tu..ye ye ye ye ndo nini imba kama lea mud tukuone na hela zako za mawazo.halafu michuzi uibanie comment yangu kama kawaida yako
ReplyDeleteHuyo bwege aliyetoa hoja hana isue,lazima ni kitafunio cha rogers...mshindi alitakiwa awe na kura nyingi kwahiyo hata kama rogers aliimba na kupiga gita sana lkn hakuwa na kura za kutosha kumfanya mshindi sasa nani alaumiwe? kumbuka hata kama misoji kabebwa anastahili cz alibebeka na nahisi huyo bwege katumia tathmini za wale madada wa brick n lace walimvyomsifia TABASAM lake istoshe huyo jamaa hakumpigia kura....tuwasubiri kwenye game la kitaani ndo tutaona nani mwenye kipaji na nani mzushi
ReplyDeleteSIIUNGI MKONO HOJA:
ReplyDeleteMAJAJI HAWAJAPANGA MSHINDI ILA SISI WATANZANIA KURA TULIZOKUWA TUNAPIGA NDIZO ZILIZOMUONGEZEA MISOJI NAFASI YA KUSHINDA:
NAOMBA TUKUMBUKE KADIRI MTU UNAPOPIGIWA KURA KWA NJIA YA SMS NDIO NAFASI YAKO YA KUSHINDA IPO JUU: LABDA TUOMBE UTARATIBU UBADILISHWE KWANI MAJAJI WANAKUWA NA UAMUZI MDOGO SANA KUHUSU MSHINDI: ILA KWA KWELI ROGER ALISTAHILI TATIZO NI KURA LABDA MISOJI ANA WAPENZI WENGI KULIKO ROGER
Haya mashindano safari hii ni longolongo tupu kwani hata hizo idadi za sms hatukuonyeshwa kama jana. To me and the majority mshindi wetu ni Rodgers Lucas na pengine labda Misoji na mbili. wewe mdau unayeitwa Speed hatukatai kuwa misoji aliigiza kuimba nyimbo za high pitch, je umeshajiuliza kuwa tukimwambia aimbe nyimbo anazoimba Rodger na yeye ataziweza?! si atakuwa anakuwa anaunguruma tu!!! Lucas anacover pitch zote bwana wamembania tu!!!!
ReplyDeleteNAOMBA NIWAFUMBUE MACHO KUWA KURA ZA AUDIENCE/VIEWERS NI 40% NA ZA MAJAJI NI 60%. KWA HIYO KURA ZENU NI COURSEWORK NA FINAL MARKS AMBAZO NI 60% NI ZA MADAME RITA ETC. HIVI PALE MLIONA MTU KUNA MTU ALIKUWA ANAHESABU KURA? YALE YALE YA MWAKA JANA JUMANNE IDD ANABWEKA TU MPAKA LEO WAKATI KINA KALA JEREMIAH NA LEA MOODY NDIO WANAMUZIKI. NADHANI HATA HIZO PESA NI CHANGA LA MOTO ANAWARUDISHIA WAANDAAJI! SASA UKIWA MJANJA HUPATI.
ReplyDeleteWELL KAMA KAPENDELEWA MTU OR HAPANA SIJALI SANA. ANGALAU LITA KAFANYA KITU TUNAKIONA KULIKO NYIE MUNAOLIA BILA KUFANYA CHOCHOTE. ANZISHA KITU CHAKO UWAPENDELEE NDUGUZO-BIG UP.
ReplyDeleteKITU PEKEE AMBACHO NAPENDA WATU WAJUWE NIKWAMBA INAWEZEKANA YOHANA NA MWENZAKE WALICHUANA SANA SO WAKAGAWANA MASHABIKI PIA HUMSAIDIA HUYO MSHINDI. PIA WATANZANIA TUJIFUNZE KUSHABIKIA UKWELI MBALI YA KUJUWANA OR BILA UPEO. MWAKAJANA JUMANNE IDDI SIDHANI KAMA ALIKUWA ANAMSHINDA KALA KAMA WATANZANIA WANGETUMIA CREATIVITY KUWA KIGEZO, SIO HAPA TU HATA SHULENI, KUNA WATU WANAKUWA BEST STUDENTS AMBAO VILAZA KABISA AND VYUO VINAWABAKISHA KUFUNDISHA KUMBE HAO WALIKARIRI TU.
SO LET US BE HONEST NA VIGEZO VYAKUMCHAGUA MTU POPOTE PALE.
HONGERA WASHINDI, YOTE MAISHA.
nadhani mwakani waanzishe mashindano ya search wa mapambio na nyimbo za dini, kwani nadhani kuwaleta hapa inabore.
Nimtazamo tu.
mdau Uk.
SIUNGI HOJA MKONO HATA KIDUCHU..
ReplyDeleteWANAOMTETEA ROGERS HAWAJUAI UIMBAJI.. NA PALE WALIKUWA WANATAFUTA KIPAJI CHA KUIMBA NA SI KUPIGA VYOMBO..
MLISIKIA MISOJI ALIVYOIMBA WIMBO I'LL ALWAYZ LOV U?????? ILIKUWA BALAA WATU WANGU..
ROGERS ANAIMBA ITS OKAY LAKINI HAMPATI MISOJI HATA KWA NUKTAA... BINTI ANATISHA YULEEE.. KIPAJI ANACHOOOO...
ME NDO ALIKUWA BINGWA WANGU.. NA THNX GOD KASHINDA.. ASINGESHINDA NINGEJUA WAMEMBANIA TUU..
IMAGINE LAST YEAR.. NANI ALISTAHILI KUWA BINGWAA????? KAMA SI LEAH???
MSITISHWE NA KUTUNGA SJUI KUPIGA MUZIKI... KITUUU GANIII GANIII BANAAA .. WAT MATTERZ IS SAUTI NYIE WATU.. KINA JZ, RKELLY SJUI NANI HUKOOO WANATUNGIWAA WALEEE.. VYOMBO WANAPIGIWAAA.... U PIPO HEBU FUNGUENI MACHO SASA MUONE ULIMWENGU UNAVOENDAAA.... AGHHHH
MISOJI U ROCK GIRLLL... GO MISOJIII GOOOOO
naona wengi mnaocomment ktk hii mnaona bora kucomment tu. BSS ni kumtafuta star na star si mtu bingwa wa kuigiza. basi hata kama anaigiza basi afanye vizuri. mwaka jana leah alikuwa anaigiza ila tulisikia nyimbo alizoimba she was soooo good
ReplyDeletehuyu misoji jamani hakustahili ushindi, nyimbo alizochagua tulizipenda alipoimba kiganda na lugha tusizozielewa, alipoemba kiingereza jamani msibishe maneno yalikuwa hayatoki as they are.
kuimba anaimba, kama ninavyoweza kuimba ila yeye ana sauti kubwa... nzito sasa at times alipokuwa anajaribu kuitoa alikuwa anatishia hata amani kwa sisi watazamaji kama anataka kutumeza.
nyimbo zinatakiwa kutuburudisha sio kutuogopesha jamani.... kumpa ushindi wa nyimbo za ukimwi wamaempa tu ili kujustify ushindi wake.... ukweli u wazi alietunga na kuimba wimbo mzuri wa ukimwi ni Yohana. Rogers was ok na wimbo wake ila misoji wimbo wake haukuwa na maana iliyostahili jamani....
BSS walishaharibu last yr kumpa J4, nae hakustahili sasa mwaka huu wakaamua kumpa mwanamke tatizo mwanamke mwenyewe hakustahili.... yule namba 3 ingemfaa.
kuhusu kura waandaaji walikuwa wanatuencourage tupige kura ili tu wagenerate hela upane wao ila hawakuzihesabu hata kidogo. misoji hakuwa na kura nyingi si tumemwona ktk danger zone mara kibao... rogers hakuingia sasa utasemaje kura hazikutosha.... BSS are crap.... na kwa style hii hawatofika mbali