kipa wa zamani wa taifa staaz na pan african juma pondamali mensah akitoa mawaidha kwa vijana wake wa timu mchanganyiko ya tanzania association of youth soccer academies. mensah ni mmoja wa wachezaji wakongwe kadhaa ambao wameamua kusaidia chipukizi katika kulisakata kabumbu kwa kuwa makocha. wengine ni kama mohamed adolph rishard, mohamed bakari 'tall', charles boniface mkwasa, thomas 'uncle tom' kipese, james kisaka, sekilojo chambua, fred felix kataraia minziro, khalid bitebo 'zembwela' na kadhalika

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. vijana wa siku hizi wamejaaliwa kuchezea viatu vya mpira, Enzi zetu tulikua tunachezea chachacha.

    ReplyDelete
  2. MIMI NASUBIRI KUONA HAYO MATUNDA YA SOKA AKADEMIZ HIZI. MAANA TZ BWANA......!

    ReplyDelete
  3. mnyonge mnyongeni lakini kwenye hili la kuendeleza soccer we are in the right track, msisitizo kwenye timu za vijana ni mzuri sana na matunda yatafuata hapo baadae, HONGERA SAAAAAAAAAAANA RAISI JAKAYA KIKWETE. hizi ni juhudi zako na tunaziona ila kaza kamba kidogo kwa rafiki zetu mafisadi.

    ReplyDelete
  4. walikotokea Adolf na pondamali ni kwenye timu za vijana kama hizo mpaka kufikia ngazi ya kimataifa,mchango wao ni muhimu naamini tuta fika pia,mashindano ya shule za msingi na sekondari(umiseta)yarudishwe na viwanja vya jangwani kama bado avijauzwa vifanyiwe matengenezo kwa muonekano ule wa zamani tutafika tu.

    ReplyDelete
  5. pesa na muda mwingi unatumika kuendeleza vipaji vya mpira na urembo.

    Watanzania tuelekeze nguvu zetu zote kwenye elimu, haswa sayansi na teknolojia.

    India,China,Japan,na Brazil, zinaogopeka kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia. siyo cricket,ping-pong,sumo, au football.

    ReplyDelete
  6. wewe unaedai kwmba pesa na muda mwingi unatumika ktk soka, tuambie wewe binafsi umetumia $$ ngapi so far, na umetumia muda kiasi gani ktk soccer ?
    Halafu utuambie wizara inayohusika na michezo imetoa kiasi gani ktk kuandaa mechi hii .

    ReplyDelete
  7. mbwegelembwegele,

    usinishambulie binafsi, shambulia hoja yangu.

    hoja yangu ni hii: hakuna taifa lililopata maendeleo ya watu kwa kuelekeza nguvu na rasilimali zake ktk michezo na mashindano ya urembo.

    tuelekeze muda na rasilimali zetu katika kuendeleza elimu ya watoto wetu. elimu ya ufundi,hisabati,teknolojia, na lugha.

    tuige mfano wa India,Uchina,Taiwan,Malaysia,Singapore,Japan,South Korea. haya ni mataifa yenye nguvu kwasababu yamezingatia mambo hayo niliyoyaelekeza hapo juu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...