mwanakijiji maggid mjengwa baada ya kumaliza mbio za nusu marathon ya kilomita 21 asubuhi hii hapa dar. ametumia saa moja na dakika 52 ambayo ni rekodi yake binafsi. kwa niaba ya wadau wote tunakupa hongera mwanakijiji pamoja na kaka luihamu ambaye naye alimaliza bila kuchemsha rejeta. mie nilikuwa nanihii kunanihii, hivyo sikuwepo azawaisi ningepiga mbio...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Hongera mwanakijiji mwenzetu Magid kwa kazi nzito uliyoimaliza.... Duh kumbe upo fiti mtu wangu, wengine tungeshiriki basi hata pale kona ya Mwananyamala ingekuwa shughuli kweli kweli.... wakuu mmekula basi ruti kama nne flani....

    ReplyDelete
  2. hongera sana kaka yangu maggid
    mdau
    HILD

    ReplyDelete
  3. Michuzi na maggid nyie wa2 cool sana! nawafagilia sana.. nikija bongo lazima niwaone..

    T Texas.!

    ReplyDelete
  4. Bora ulikuwa nanihii kunanihii hivyo kushindwa kushiriki kwenye mbio hizo. Mara ya mwisho ulikimbia mwaka gani? nadhani kama sikosei ilikuwa miaka 18 iliyopita ulipokuwa Form IV kwenye yale mashindano ya shule ya kukimbiza kuku wa kienyeji.

    Bado Watanzania tunakuhitaji hivyo kila ukisikia kuna mbio hata za masafa mafupi, kama vile mita 50 ujiendee zako nanihii kunanihii usije ukaanguka bure ikawa tafrani.

    ReplyDelete
  5. Hongera sana Maggid!!

    Mimi nimecheza sana riadha na ninaelewa huu si mchezo lelemama!!!

    ReplyDelete
  6. hongera sana kaka ila mara nyingine ukishiriki tafuta fulana iliyo nyepesi.

    ReplyDelete
  7. hiii!hiii!Maggid hongera sana!!!
    mwanakijiji kwa kutuwakilisha!
    Heti Kumbe Mzee Small wa Ngamba na Majuto nao waarishiriki?
    hila aliyemaliza alikuwa KINGWENDU!

    ReplyDelete
  8. hiii!hiii!Maggid hongera sana!!!
    mwanakijiji kwa kutuwakilisha!
    Heti Kumbe Mzee Small wa Ngamba na Majuto nao waarishiriki?
    hila aliyemaliza alikuwa KINGWENDU!

    ReplyDelete
  9. misupu pamoja sipati picha ngoma ingekuwa vipi, maana fegi na kufukuza upepo ni vi2 viwili tofauti!

    ReplyDelete
  10. Jamani sasa hizi talenti kwanini hatuzilei ili baadae tupate akina Ikangaa, Nyambui na Bayi? Mimi natamani kuona wabongo tena wakidomineti hii field.

    Mdau - Boston, US

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...