nasikia usipobukulia hapa kupata nondo mlimani ni majaaliwa... je hii ni kweli wadau?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. ASANTE KWA UDHAMINI WA PICHA HII MICHUZI. USEMI HUO UPO, KUWA BILA MDIGRII HUJAPATA SHAHADA. INA MAANA KUWA KILA MWANAFUNZI LAZIMA KWA NAMNA FULANI ALISHAPITIA HAPO, JAPO WAPO WACHACHE HAWAJAWAHI KUKAA HAPO HATA SIKU MOJA. NIMEPAKUMBUKA SANA. TUMETOKA MBALI!

    MDAU,
    UNITED STATES OF AMERICA
    YES, WE CAN (OBAMA SLOGAN)

    ReplyDelete
  2. si kweli bila kukamulia hapo maana yake hakuna degree hapo ni kwa mangwini tu!nakumbuka mimi nilikuwa naenda kwa discussion za DS basi!DS ilivyoisha sikukanyaga hapo na degree nilipata!
    Scientist!

    ReplyDelete
  3. labda kwa enzi hizooooo chuo kilipokuwa na wanafunzi wachache. Hivi wanafunzi wote wa chuo wakitaka kukaa mdigrii patatosha?by the way Nkrumah tu yenyewe imekuwa ndogo.

    ReplyDelete
  4. Kwakweli labda hii ni imani ya MANGWINI,ila kwa watu kama wa uhandisi-FOE(kwa wanaokumbuka enzi hizo,kabla ya COET) huwezi kukanyaga hapo labda kwa sababu nyinginezo na si kwa ajili ya digrii. Mfano mie sijawahi kukanyaga hapo na nimekula FIRST CLASS DEGREE ya uhandisi.

    So nalipinga hili kwa nguvu zote

    Mdau,J

    ReplyDelete
  5. Mimi naona ni kuwa panaitwa mdigree kwasababu kwa njia moja au nyingine ulishapita kwenye huo mti si kwakusoma tu bali ata kwa kazi nyingine ndio panaitwa mdigree.
    Wanaposema watu kupita haimaanishi wote kwa pamoja waende pale la hasha,ukiona watu wamejaa unaangalia kiwanja kingine hasa kwenye maeneo ya vimbwete.watu hupenda kutumia mdigree kwa discussion kwani vimbwete navyo viko.
    Michuzi bado haujatueleza kwanini hivyo vitu walivyokalia hao wanafunzi vinaitwa vimbwete na kumbuka kuwa kunadaraja hapa linaitwa Daraja la taaluma(academic bridge).

    Unanikumbusha mbali michuzi

    ReplyDelete
  6. Ha ha ha masupuuuuuz, sio kukaa tu mpaka uangukiwe na japo jani moja la huo mdigirii ndo utaipata degree!
    Nathubutu kusema kwamba hakuna mwanafunzi alie maliza degree UDSM bila kukaa chini ya huo mti japo mara moja, hata kama nikwakusubiri ID au chochote kama sio discussion!

    ReplyDelete
  7. Kwanza, kuitwa mdigirii haina maana kama usemavyo ila ni kwamba uo mti unatabia ya 'kwenda Makka' kwa lugha ya kizanzibari,yaani huangusha majani wakati wanafunzi wanapokua wanafanya mitihani ya kumaliza mwaka, na baadae mwezi wa kumi na moja wakati wanafunzi wanavaa majoho kwa kupokea digrii zao huu mti nao hurejesha majani yake,hii ndio sababu ya kuitwa mdigirii,hakuna sababu nyengine kaka. Yaani kusema kwamba huu mti nao kila mwaka hua unachukua digrii yake.Kama ungelikua unasema nafkiri mpaka sasa ungekua ushapewa uprofessor:) Kwahiyo usifananishe kupasi au kufaulu na mdigirii.Pili ni kweli kabisa kuna wanafunzi akina sisi kukaa hapo ni kusubiri mambo mengine na sio kusoma.Wanafunzi waitwao MANGWINI yaani wale wanosoma masomo ya arts na social sciences au 'ungwini' ndio ambao husoma kwa njia ya discussion katika mdigirii huo.Lakini wanafunzi wa sayansi kama engineering na wengine si rahisi kuwakuta wanasoma hapo kwani concentration ni ndogo sana kwa sababu ni njia kuu ya wanafunzi na mambo mengine na hata wadudu hudondoka dondoka.

    ReplyDelete
  8. hahahahaa!!!michuzi umenikumbusha mbali kwa huo mdegree,yaani kwa hapo mwanafunzi yeyote aliyesoma UDSM lazima awe kwa maana moja au nyingine amekaa hapo japo hata kama anafanya registration ya 1st year.ndo maana panaitwa mdigree.
    kwanza hapo ni kwa wajanja wa arts sio wale wanaosoma historia ya sayansi na kujiona wanasayansi wakati wanasoma mpaka kumaliza hapo kwa kudesa.
    wadau wa blog hii nauliza hao wanasayansi wanaojinadi wamewahi kugundua nini?kama sio kusoma historia ya wanasayansi wakubwa duniani kama wakina izack newton na wengine,halafu wenyewe wakafundishwa jinsi ya kuaply law za wanasayansi wakajiita wanasayannsi.
    mi najua hapo udsm kunafundishwa historia ya wanasayansi.ila watu wa management ndo wa kuongea.
    cheaz wadau

    mdau kutoka kenya.

    ReplyDelete
  9. Asante sana Alwatan kwa maelezo yaliyoenda shule. Halafu mijitu mingine bwana, hivi nyinyi mliosoma Uhandisi ndio mnajiona watu wa maana sana au ni vipi? k kujisifu tuuuuuu? Kudadadeki.
    Huo mdigrii bwana, kila mtu kakaa hapo chini.

    UD Alumni
    Yu ES Ei

    ReplyDelete
  10. MAMBO VIPI? WADAU WOTE!
    KUUSU HAPO MDIGRII SIO KWAMBA USIPOSOMEA HAPO HUPATI DEGREE HIYO SIO KWELI ILA ASILIMIA KUBWA YA WANAZUONI WALIO WAHI KUSOMA UDSM WAMEWAHI KUSOMEA PALE/KUDISCUSS/KUPIGIA STORI AU HATA KUPEANA APPOINTMENT ILI MKAKAMUE SEHEMU NYINGINE.KWA UFUPI UKUBALI UKATAE UMESHAWAHI JAPO KUPITA TU KA MA SIO KUSOMA.WENGINE WANAITA KUFLASH MIND.
    MDAU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...