Mkurugenzi wa Utanduni, Profesa Hermans Mwasoko, akikabidhi fedha, cheti na ngao maalum kwa Mh. mkuu wa nanihii ya tegeta, aliyemwakilisha mshindi wa tuzo ya upigapicha bora wa picha za sanaa, Mroki Mroki a.k.a Mzee Kidevu kutoka Tanzania Standard Newspapers Ltd (TSN) wachapishaji wa Daily News na HabariLeo ambaye hakuwapo wakati wa utoaji wa tuzo hizo juzi. Mroki, ni miongoni mwa waandishi wa habari kadhaa waliokuwa kwenye vita vya kumng’oa muasi katika kisiwa cha Anjouan Mohammed Bacar.NB: wadau kunradhi, hivi zawadi kama hii tunaita tunzo ama tuzo?


Tunaita TUZO
ReplyDeleteMWENYEWE ALIKUWA ANJOUN ANAPIGA PICHA MADEM NA MIJUSI SEMA, HEHEHHE BRO MICHU..
ReplyDeleteBora umeliuliza hilo swali Mkuu wa nanihii, maana hata mie limekuwa likinitatiza siku nyingi tu......kwani wengine husema "mcheza kwao hutuzwa" na wengine "mcheza kwao hutunzwa" Ipi ni sahihi wadau nisaidieni
ReplyDeletemkuu wa wilaya vp naona habari za manu hujatoa kama hakijatokea kitu wala kudraw kwa chelsea
ReplyDeletehaya bwana tutakumbana moscow huko kam mwanaume kweli
Hapo Michuuuuz umeji blogu mwenyewe!Acha Wilaya,karibu utapewa Wizara mze,fununu nilizo zipata toka jikoni kabisa!tehe tehe
ReplyDeleteUtanduni ni nini na mimi nataka nione hizo picha zake maana lazima intakuwa inavutia sana.
ReplyDeleteHuyu jamaa anapiga picha vizuri michuzi tunaomba uirudie ile picha alipiga wakati wa sherehe fulani ya kiserikali ikionyesha baadhi ya vigogo wakiwa wamelala wote .. kwenye halaiki hiyo..
ReplyDelete