Mkurugenzi wa Utanduni, Profesa Hermans Mwasoko, akikabidhi fedha, cheti na ngao maalum kwa Mh. mkuu wa nanihii ya tegeta, aliyemwakilisha mshindi wa tuzo ya upigapicha bora wa picha za sanaa, Mroki Mroki a.k.a Mzee Kidevu kutoka Tanzania Standard Newspapers Ltd (TSN) wachapishaji wa Daily News na HabariLeo ambaye hakuwapo wakati wa utoaji wa tuzo hizo juzi. Mroki, ni miongoni mwa waandishi wa habari kadhaa waliokuwa kwenye vita vya kumng’oa muasi katika kisiwa cha Anjouan Mohammed Bacar.


NB: wadau kunradhi, hivi zawadi kama hii tunaita tunzo ama tuzo?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Tunaita TUZO

    ReplyDelete
  2. MWENYEWE ALIKUWA ANJOUN ANAPIGA PICHA MADEM NA MIJUSI SEMA, HEHEHHE BRO MICHU..

    ReplyDelete
  3. Bora umeliuliza hilo swali Mkuu wa nanihii, maana hata mie limekuwa likinitatiza siku nyingi tu......kwani wengine husema "mcheza kwao hutuzwa" na wengine "mcheza kwao hutunzwa" Ipi ni sahihi wadau nisaidieni

    ReplyDelete
  4. mkuu wa wilaya vp naona habari za manu hujatoa kama hakijatokea kitu wala kudraw kwa chelsea

    haya bwana tutakumbana moscow huko kam mwanaume kweli

    ReplyDelete
  5. Hapo Michuuuuz umeji blogu mwenyewe!Acha Wilaya,karibu utapewa Wizara mze,fununu nilizo zipata toka jikoni kabisa!tehe tehe

    ReplyDelete
  6. Utanduni ni nini na mimi nataka nione hizo picha zake maana lazima intakuwa inavutia sana.

    ReplyDelete
  7. Huyu jamaa anapiga picha vizuri michuzi tunaomba uirudie ile picha alipiga wakati wa sherehe fulani ya kiserikali ikionyesha baadhi ya vigogo wakiwa wamelala wote .. kwenye halaiki hiyo..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...