hii ni picha ya luninga ikonesha laivu bunge la jamhuri ya muungano sasa hivi wakati linapitisha kwa kura ya wazi na ya mbunge mmoja mmoja ya ndio ama ya hapana bajeti ya makadirio na mapato na matumizi ya serikali ya mwaka 2008/2009 baada ya waziri wa fedha na mipango mh. mustafa mkullo kuwasilisha na kuitetea katika majumuisho yake.
jumla ya wabunge 318 walikuwepo kupiga kura na karibu wabunge wote wa upinzani waliipinga wakati wa chama tawala waliiridhia.
aidha, katika kura hiyo neno 'abstain' ambalo wabunge wengi wa kambi ya upinzani waliitamka kuonesha kutoikubali bajeti hiyo, lilizua mjadala baada ya spika mh. samuel sita alipolitaja neno hilo kama halina uzito katika kukubali ama kukataa. kisheria kwa hoja kukubaliwa ama kukataliwa inabidi wabunge wapatao theluthi mbili za wabunge wote 391 wawe upande mmoja.
matokeo:
Jumla ya wabunge waliopiga kura - 276
kura zilizoharibika - 0
wasiokuwepo - 41
kura za hapana - 0
kura za 'abstain' (kutokuwa ndio ama hapana, kwa mujibu wa spika) - 35
na kura za ndio 241.


Ningependa kujua Mh. Mama Anne William Melecela (Mtetezi wa wanyonge) alisema neno gani?
ReplyDeleteHapa kuna mambo mawili ambayo ningependa muyajue Ndugu Wabunge kabla ya kupiga kura.Kwanza,mtambue kwamba zikipigwa kura nyingi zaidi za kusema HAPANA,HATUITAKI BAJETI HII,mtambue hatua itakayo fuata ni Rais Kulivunja Bunge na Kuitisha Uchaguzi Upya wa Wabunge.Sijui kati yenu wangapi watarudi tena Bungeni(?).La Pili, ni kwamba wote mtatakiwa mpige kura ya wazi na kila mbunge ataulizwa kwa sauti na yeye atajibu kwa sauti sana iwapo ni NDIYO AU HAPANA, iwapo anaikubali Bajeti ipite au Hakubali Bajeti ipite.Very Simple.Uamuzi ni wenu tu.Kusuka au Kunyoa.Haya,sasa tuta anza kuwauliza mmoja mmoja.Baada ya maswali Bajeti ilipitishwa kwa KISHINDO!.Hongereni sana Wabunge wetu kwa ujasiri wa kutambua Biashara Asubuhi!
ReplyDelete