HABARI ZILIZOIFIKIA GLOBU HII YA JAMII SASA HIVI ZINASEMA WATU WANANE AMEFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA HELIKOPTA YA JESHI LA ULINZI ILIYOKUWA NJIANI IKITOKEAZ ARUSHA KUELEKEA DAR.
INASEMEKANA ABIRIA WAKE AMBAO BADO HAIJATHIBITISHWA KUWA NI RAIA AMA ASKARI WALIKUWA WANATOKEA ARUSHA KWENYE MKUTANO WA SULLIVAN.
INASEMEKANA WALIOKUFA NI ABIRIA SITA NA MARUBANI WAWILI WA HELIKOPTA HIYO.
HABARI KUTOKA KIKOSI CHA ANGA AMA AIRWING UKONGA IMETHIBITISHA HABARI HIYO NA TAYARI NDEGE IMEENDA ENEO LA TUKIO NA KWAMBA TAARIFA KAMILI ITATOLEWA BAADAYE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 09, 2008

    MY GOODNESS!!

    ReplyDelete
  2. Misupu kuna mtu mmoja aliwahi kukupa ushauri wa bure kwamba ukitoa habari ya kusikitisha kama hii usiandike kichwa cha habari BREAKING NYUUUUUUUZ kwa sababu inakuwa kama unatoa habari nzuri na za furaha badala yake uandike BREAKING NYUZ (NEWS)otherwise RIP wote waliofariki, Misupu hili onyo la mwisho usirudie tena nasema ohooo nitakuloga shauriyako!!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 09, 2008

    Mwenyezi Mungu alaze Roho zao mahali pema peponi, Poleni wafiwa na wa-Tz wote....

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 09, 2008

    Ebwanaeeeeeeeeeeeeeeeeee! duuuuuuu!INASIKITISHA SANA

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 09, 2008

    mla vumbi kweli wewe nimeamini kwa kusikitika ni MLA VUMBI.. hujui uliongelealo. unaelewa maana ya breaking news. eti habari za kufurahisha,nani aliekufundisha hilo?? DONT TALK BOLOCKS

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 09, 2008

    Sensationalism (kiswahili?) ni chakula cha wana-habari, na Michuzzzziiii ni mwana habari. Kinacho-matta ni ile habari na tunaelewa kwamba mwandishi hashabikii bala amesssshtushwa!!!!

    ReplyDelete
  7. wewe mla vumbic tuondolee pumba(mavumbi yako)
    unajua journalism au unaisikia?
    mithupu amekula nondoz za hii fani kwa hiyo hawezi kutushushia vumbi katika blog yetu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 09, 2008

    Ni kweli unachosema Mlavumbi!

    Kichwa cha habari kina uzito mkubwa sana na kinabeba muudhui nzima ya habari.

    Unapotuletea habari nzito kwa lengo la kututaarifu tayari umeshaacha ile kawaida ya libeneke au utani wa kiosha-kinywa; ila unageuka kuwa chombo cha habari, hasa kwa sisi tulio mbali na nyumbani.

    Basi, tunaomba kichwa cha habari kiendane na uzito wa taarifa, yaani jambo zito kama vifo basi uandike bila utani, kwenye michezo kama Liverpool ikifungwa, basi chombeza utani hata kama itakuuma.

    Asante!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 09, 2008

    Wewe anon June 09, 2008 6:48 umekurupuka na hujamuelewa Mlavumbi.

    Mlavumbi hajaongelea maana ya breaking news, nashangaa kwanini unamtukana. Mlavumbi anaongelea jinsi Michuzi alivyoandika hilo neno: ukiandika breaking nyuuuuzzz na breaking news ni mitindo tofauti ya uandishi, la kwanza lina masihara ndani yake na haliendani na habari ya vifo na la pili liko formal.

    Mtake radhi Mlavumbi!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 09, 2008

    Ohh my God! Kweli mkutano utaondoka na watu wengi, kwani hata sisi wakati tunarudi jana toka huko Sullivan bwana Michuzi, tulikutana na ajali zaidi ya moja njiani kurudi Dar,moja pale Korogwe kwa Kombo katoto kaligongwa na kakafa hapo hapo..
    Poleni wafiwa! lol Sullivan meeting.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 09, 2008

    mwenyezi mungu awaweke pema peponi marehemu na awape faraja familia zao huu ni msiba mzito.familia ya mama mayenga(irene) na marehemu sinda
    nzehe

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 10, 2008

    Ni watu sita sio nane kama ulivyoandika

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 10, 2008

    Jamani Mungu awalaze pema marehemu wote ila watu humu wanakurupuka sana alivyosema mlavumbi ni sahihi kabisa ile breaking nyuuuuuz ni kama kitu cha kufurahisha hata kwa kuitamka tu unahisi sio sahihi kutumia kwenye habari kama ya msiba. Ila ukiandika breaking nyuz inaleta maana zile zzzzzz za masihara. Najua Misupu ni binadamu wa kawaida na kukosea na kukosolewa ni kwa binadamu yeyote haijalishi yuko kwenye fani gani. hivyo kwa ushauri wa mla vumbi naungana nae musupu chonde badilisha hilo neno.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 10, 2008

    This is very sad manake hii helikopta for the whole week wkt wa mkutano wa sullivan ilikuwa part and parcel of our town manake ilikwua ikipiga round throughout the day kuhakikisha usalama wa mji wa Arusha , halafu kusikia imeanguka na wamekufa wote waliokuwamo imenigusa sana tulishaizoea ni kama hata tulijua hao pilots , though at times watu walilalamika hii helikopta inasumbua manake ilikuwa inapita chini sana sana ila yote ni kazi ya Mungu. RIP Makamanda wetu!!!

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 10, 2008

    This is very sad manake hii helikopta for the whole week wkt wa mkutano wa sullivan ilikuwa part and parcel of our town manake ilikwua ikipiga round throughout the day kuhakikisha usalama wa mji wa Arusha , halafu kusikia imeanguka na wamekufa wote waliokuwamo imenigusa sana tulishaizoea ni kama hata tulijua hao pilots , though at times watu walilalamika hii helikopta inasumbua manake ilikuwa inapita chini sana sana ila yote ni kazi ya Mungu. RIP Makamanda wetu!!!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 10, 2008

    Michuzi

    Kwa mtazamo wangu nadhani hili neno " BREAKING NEWS" liende na mazingira ya tukio. Hivyo basi kama ni habari ya kawaida au ya kufurahisha basi ivute hivyo kama ulivyofanya hapo juu lakini kama ni habari ya masikitiko naona iandikwe tu "BREAKING NEWS"

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 10, 2008

    Ni safari ya wote mbaya kutangulia.Mungu azilaze Roho zao mahali pema AMINA.
    Sweet,
    Arusha.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 10, 2008

    RIP ndg zetu, mbele yenu nyume yetu, Mungu awape faraja wafiwa.


    WEWE UNAEZUNGUMZIA HABARI MBAYA, HALAFU UNASEMA LOL SULLLIVAN MEETING, UNA KICHAA, UNAELEWA MAANA NA LOL?

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 11, 2008

    lol = laughing out loud

    sasa wewe cutecathy u mean unacheka huu msiba! kwa kweli unashangaza

    nakataa kumuomba radhi mlavumbi,because these are my opinions

    ReplyDelete
  20. Mla vumbi you have a point, raha ya humu ndani kuna vichaa, wasomi na waliokimbia umande. Pia wapo wajinga ambao hataki kutolewa ujinga na wengine wajinga ambao hawajui kama n wajinga naanza kuwalist, nyie ma'anon' wa June 11 5:52 PM, June 9 6:48, 7:42 wewe unayejiita Mpaka, hivi msichoelewa anchokieleza Mlavumbi ni nini? Boksi noma!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...