Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 11, 2008

    KP hii kali yake. Hongera sana kwa usanii. kuna wakt nakusaga lakini kwa hii ujumbe umeufikisha na burudani umetoa wala haina shobo.

    Hekoooooo. Sasa Mkuu-loo unakwenda kusoma bajeti ipi wakt tayari mambo hadharani na imeshaanzaujadiliwa??????????????

    ReplyDelete
  2. MAMBO YA BAJETI YANA UTATA SANA, NILIJARIBU KUANGALIA UTARATIBU WA KUONDOA HUO UNAOITWA UMASIKINI AMBAO NAPINGANA NAO NIMEGUNDUA NCHI ZILIZOENDELEE NDIO ZINA UMASIWA HALI YA JUU. SASA KAMA WEWE UDAI WALA UDAIWI SI UTAJIRI WA HALI YA JUU. SASA HAWA WENZETU WA NCHI ZILIZOENDELEA WANATUMIA CREDIT YAANI PESA AMBA ZO SIO ZAO . UKIANGALIA KATIKA MASOMO YAO YA KIUCHUMI WANAVYO NGALIA MATUMIZI AU PATO LA MTU WANATA GDP WANATAKIWA WAWEKE MADENI PALE ILI UTAONA PATO LAO NI NEGATIVE. KWA HIYO WANA UMASIKINI ULIOKITHIRI, WANANANYNG'WANA NYUMBA WANA HIFADHIWA KWENYE SHELTA UMASIKINI WAO UNATISHA.LAKINI MSAADA WAO UKO HEWANI.SASA NIKO KWENYE ZIARA KIMASOMA HAPA INDI KATIKA CHUO KIMOJA KINAITWA MADURAI KAMARAJ UNIVERSITY IDARA YA BIASHARA NA NYONYA NONDO KIDOGO ILI BAJETI YETO 2090 ISIWE TEGEMEZI. TUTAKUBALI MISAADA YA MITAMBO NA SIO PESA YA KUNUNU SARUJI WAKATIPO HAPO WAZO (TWIGA) HILL , WAZEE WA TEMBO MBEYA NA SIMBA TANGA.HATUTAKI MISAADA YA KUPANGISHIWA MATOFALI YAANI JENGO. TUNATAKA MISAADA YA LAP TOP AU DESK TOP. NYUMBA TUTAJEGA WENYEWE. KWA KUWA TEMBO CEMENT WANALIPA KODI BASI TUTAMALIZANA JUU KWA JUU. NACHOTAKA MIMI WACHUMI WA TANZANIA WAJE NA SERA MPYA KABISA ZA KIUCHUMI KUIKWAMUA HII NCHI NA SIO SERA ZILIZO ELEWEKA KUNA KIJANA WE PALE JAPAN JM SIJUI HATATUSAIDIAJE. KUNA TOPIC HAPA YA ANATOMY AND PHYSIOLOGY OF UNDERDEVELOPMENT. ANATOMY MAANA YAKE STUDY OF THE PARTS OF and STUDY OF THE FUNCTION OF THE PARTS OF (UNDERDEVELOPMENT). BADO NI NGUMU HAYA MAMBO SI MARAISI KILA MKAKATI NI RISK

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 12, 2008

    duuh mdau hapo juu hio nondo yako unayochukua hapo India sijui ni vipi, kwani kiswahili chenyewe hujui broken kibao kama hukwenda shule siuseme tuu, kuliko kubabaisha watu hapa!POLE.Sijapata point yoyote kwenye ujumbe wako ingawaje umeandika paragraph nzima.RUDI VIDUDU NDUGU YANGU,SHULE BADO KABISAAAA.

    ReplyDelete
  4. ANON 1:29 SASA NISOME LUGHA HIPA HAPA TAFADHALI NAOMBA MSAADA WAKO.MAANA NAONA HAPA NI KIHINDI TU, NDIO KWANZA NIKO VIDUDU KUTOKANA NA NA MTAZAMO WA MASOMO YANGU YA BAADAE. SIJAHITIMU BADO NASHUKURU KWA USHAURI NITAJIREKEBISHA

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 12, 2008

    Congratulations Kipanya for Foresight Creativity!Jamaa anadengua na funguo mkononi wajanja wamesha komba kila kitu na kitasa cha mlango wamechukuliza!Tusubiri hilo Tokomile la Bajeti ili tuanze kupashana.Kila nchi duniani uchumi wake umeathirika na mfumuko wa bei umezidi kuongezeka zaidi lakini hapa kwetu maajabu ya mtende kuota jangwani,mfumuko wa bei umezidi kupungua,uchumi umeimarika zaidi,na unakua kwa kasi ya papasi,umaskini wetu uliobaki ni ule wa kujitakia tu,ka nchi ketu kazuri kamezidi kuvutia wawekezaji katika kila sekta.Ujumbe uliopo katika katuni yako ni mzito na mkubwa kuliko makala ya kurasa 30.Big Up Kp!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 12, 2008

    Kwa mara nyingine tena Bajeti ya Serikali ya mwaka huu wa Fedha 2008/2009 imefinyangwa finyangwa ili kuficha ukweli kuhusu hali mbaya ya kiuchumi inayolikabili Taifa.Ni Bajeti ambaye haikuweka bayana hali halisi ya kiuchumi ilivyo sasa bali iliyolenga katika kuwapa matumaini Watanzania ili kunyamazisha hasira zao kuhusu ubadhirifu mkubwa katika menejimenti ya uchumi wa nchi kama ilivyo dhihirika katika matukio kadhaa katika mwaka huu uliopita unaoishia Juni 30,2008.Mahitaji ya Bajeti ya Serikali kwa Mwaka huu wa 2008/09 yatazidi mahitaji ya Bajeti kama hiyo kwa Mwaka uliopita wa 2007/08 kwa zaidi ya shilingi trilioni 1.149 ambazo haijulikani zitatoka katika vyanzo gani vya fedha au sekta zipi za uzalishaji mali.Ni Bajeti ambayo utafikiri kama vile licha ya kuongezeka kwa gharama za matumizi au mahitaji ya fedha zaidi kwa mwaka huu wa fedha 2008/09 hakutakuwepo ongezeko lolote lile la kodi katika bidhaa mbalimbali.Lakini katika maelezo ya ziada katika Bajeti hiyo imedhihirika kwamba kutakuwepo na ongezeko au marekebisho katika viwango vya kodi za bidhaa fulani fulani.Katika hali ya kawaida,kwa ongezeko la namna hiyo la mahitaji ya fedha kuliko mwaka uliopita,lazima watu watarajie kupanda kwa bei za bidhaa mbalimbali na kuongezeka kwa gharama za maisha pamoja na gharama za uzalishaji mali na zile za kufanya biashara.Hakuna namna nyingine.Hapa tusidanganyane kama watoto wadogo.Bajeti haizungumzii lolote kuhusu sekta ya viwanda(?).Tutaondokaje hapa tulipo bila ya kuipa upendeleo maalum sekta ya viwanda ambayo ndiyo itakayo zalisha bidhaa karibu zote zitakazo uzwa nchi za nje na kulipatia Taifa Fedha za Kigeni na kutengeneza nafasi nyingi zaidi za ajira kwa vijana wetu?Au tumepumbazwa na mapato yatokanayo na sekta ya Madini ingawa sehemu kubwa ya mapato hayo hatunufaiki nayo,inakwenda nje ya nchi?Muhtasari wa Bajeti hauonyeshi ni Pesa kiasi gani ambacho Serikali itatarajia kukusanya hadi Juni 30,2008 kwa mujibu wa kiwango kilichopatikana hadi Aprili 30,2008?Kwa uwezo huo ni kiasi gani ambacho Serikali itatarajia kukipata katika miezi 12 ya mwaka ujao wa Fedha 2008/09?Kwa makusanyo hayo na kwa mujibu wa Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2008/09 ni pengo kiasi gani la Fedha ambalo litahitajika kuzibwa ama kutokana na ongezeko la kodi zaidi za bidhaa mbalimbali au kutoka kwa wahisani wa nje?Hayo yote hayakuwekwa bayana katika Bajeti hiyo.Katika Jumla ya Mapato ya Serikali,utaona kwamba Mapato yatakayo tokana na Wahisani wa Nje ni shilingi Bilioni 2,429.535.Na ukiangalia Bajeti ya Maendeleo,mchango wa Wahisani kutoka Nje ni shilingi Bilioni 1,551.1.Hizi nyingine za ziada tokana na Wahisani wa Nje jumla ya shilingi Bilioni 878.435 zitatumika wapi au katika nini?Zipo zilizo fichwa katika shilingi Bilioni 938.380 za Maendeleo lakini zimetamkwa kuwa ni mkusanyiko wa fedha kwa ajili ya Mauzo ya Hisa za Serikali;Ziada ya Mapato ya Ndani;na Fedha za Wahisani-misaada ya Kibajeti(?).Kwanini katika kifungu hichi fedha za wahisani wa nje hazikutenganishwa ili ijulikane wazi ni sehemu gani ya Bajeti ya Maendeleo itakayo lipiwa na Wahisani kutoka nje?Nini kinachofichwa?Kuogopa aibu?Why?Kuishia kusema tu kwamba Bajeti hii imepunguza UTEGEMEZI kutoka asilimia 42% hadi asilimia 34% na ikitolewa mikopo itakayo lipwa na serikali utegemezi utapungua hadi asilimia 20% takwimu hizo zitatusaidia nini iwapo hali halisi haiko vile?Suala la kupanda kwa bei za vitu limeachwa nje kabisa ya Bajeti hii ili kuepuka lawama za watanzania kuhusu kupanda kwa gharama za maisha.Lakini ukweli ni kwamba Bei za Vitu mbalimbali zimekuwa zikipanda kiholela siku hadi siku.Hakuna anayezungumzia kuzidi kupanda kwa gharama za Uzalishaji Viwandani.Lakini ukweli ni kwamba gharama viwandani zimekuwa zikipanda kiholela siku hadi siku.Kinachofichwa na Bajeti hii ya Serikali kwa mwaka 2008/2009 ni kwa faida ya nani?Je,Bajeti hii haipaswi kuwa BAJETI YA WATANZANIA WENYEWE KWA AJILI YA MAHITAJI YAO WENYEWE NA KWA MAENDELEO YAO WENYEWE?Hawahitaji kutengenezewa Bajeti yao kwa ajili yao na Mtu mwingine wa pembeni ambaye hatathamini matatizo ya kimaisha yanayo wakabili na hali halisi ya vipato vyao?Tutasubiri tuone Wabunge wetu wana Maoni gani kuhusu muundo na mustakabali wa Bajeti hii ya 2008/09 katika maendeleo yetu!Mengi tutapashana katika matoleo ya kila siku kupitia Blog hii.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 12, 2008

    Big up KP,unawakilisha vilivyo.
    Ila mdau Tumaini tunahitaji namna nzuri ya kuwasilisha hoja kutoka kwako,sio kama ulivyojieleza ,umetuangusha sana maana mtu akisoma ulichoandika atakachofanya ni kuhoji je,umefikajefikaje hatua ya kielimu uliyopo? isije ukatuletea ubao ndugu ,sie tunataka uje na nondo bana,pana taka veve leta ubao?

    ReplyDelete
  8. annon5:44 natamani nipate bahati ya kuwa mwanafunzi wako. tafadhali ni xt at tgeofrey@yahoo.com mungu akubariki

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...