Habari yako kaka Michuzi.
Mimi ni mtanzania ninayeishi Italy yapata miaka sita toka nitoke Tanzania.Niko kwenye ndoa miaka 15, nina watoto wanne. Limetokea tatizo ambalo linanitatiza moyo wangu. Tumegundua mme wangu nimuathirika wa Ukimwi. Mimi sijaathirika na watoto pia.
Nimejaribu kumwambia nihame chumba anielewi, anadai tutumie kinga nathani umenielewa.mimi siko tayari kukutana naye. Sasa watanzania wenzangu ninaomba ushauri wenu.... nifanyeje ?
Wadau wa blogu hii ya jamii nategemea ushauri wenu utakuwa wa busara.
Ahsanteni
Kaka michuzi address yangu naomba weka kapuni.
Ahsanteni
Kaka michuzi address yangu naomba weka kapuni.


USIKONDE DADA , HAPO MWANZO MUNGU ALIUMBA BINADAMU AISHI MILELE, MAANA YAKE KULIKUWA HAKUNA CHA KWENDA MBINGUNI WALA MOTONI. BAADAE SHETANI AKAMMSHAWISHI BINADAMU AMUASI MUNGU. MUNGU AKAMFUKUZA ADAMU NA HAWA TOKA BUSTANI YA EDEN, SASA HAPA KAWA KWAMBA AKAKA DUNIANI NA HAPO NDIPO MAMBO YA MINGUNI ,MOTONI NA DUNIANI YALIPOTOKEA. SASA KUWA NA SWALA KWAMBA BINADAMU ATAISHI MIAKA MINGAPI. WANA WA ADAMU KAINI NA ABELI WAKAONEAA WIVU KAINI AKAMPIGA ABELI BILA KUJUA KITAKACHOOEA. NA HUU NDIO ULIKUWA MSIBA WA KWANZA. MALAIKA KAMTOKEA KAINI KAMUONYESHA ISHARA YA KUMZIKA MWEZIE NDIO MAZISHI YA KWANZA. BINADAMU WA KWANZA KUFA NA UKIMWI AALIKUWA ADAM.UKIMWI MAANA YAKE NIUKOSEFU WA KINGA MWILINI YAANI KAMA HAUJAGONGWA NA GARI , AU HUJAANGUKIWA NA MTI, UMEKUFA KOKANANA MWILI WAKO KUSHINDWA KUPAMBANA NA HALI YEYOTE YA MWILI WAKO KATIKA HIZO PROCESSS ZOTE KAMA ANABOLYSIM WICH IS BUILDING UP OF ---, CATABOLISM -- BREAKING DOWN METABOLISM NDIO YENYEWE YAANI UMEKUWA MA MAPUNGUFU YA KINGA IMMUN DEFFIENCE. KWA HYO WATU WOTE DUNIANI LAZIMA WAFE NA UKIMWI. SASA WAMEJITOEZA WAJASRIAMALI WAKATUMIA UHALISI HUO WA UUMBAJI WA MUNGU KAMA MIRADI YAO WAPATE PESA ZA KUTANULIA WAKIJISINGIZIA WANAFANYA TAFITI. KINACHO WAUA WATU NI UGONJWA WA KISAIKOLOJIA KWAMBA LAZIMA WAFE. SASA SIJUI NANI ALIWAAMBI WASIO NA HUO UKIMWI WATAISHI MILEE NA WENYE UKIMWI SIKU ZAO NI ZA KUHESABIKA. NI USANII HUO USIHOFU HUKO HURU MUNGU ANAKUPENDA NA KANIAMBIA NI KUPE HUJUMBEE HUU UKIWA WA MOTO NAOMBA UUPOKEE NA USEME AMENI
ReplyDeletepole sana dada yangu..tatizo lako ni kubwa bila kuongopa!
ReplyDeletekatika nyakati hizi rudia sala na sambamba na hilo shikilia msimamo wako wa kutenga chumba ..tafuta msaada wa watu wa karibu na wewe..nafikiri familia yako ni muhimu wajue hili ..pole sana
We mmama hujatulia nini? mumeo kaathirika na ww upo poa harafu umemuomba uhamie chumba kingine na hutaki kutoa unyumba...kwa upeo wako mtakuwa mkiishi kama mume na mke au wapangaji flani ivi? maadam umesema haupo tayari kutoa unyumba nakushauri dai taraka na kama ni ndoa ya kikristo kuna taratibu za kutengana. Jambo lingine inawezekana mumeo kapata ngoma si kwa ajiri ya ukicheche mnaweza kutafuta washauri na mkaendelea na maisha yenu ya ndoa kama mwanzo istoshe kuna mifano dhairi waathirika walivyoishi na kupata watoto ndani ya ndoa ktk hali hiyo ya uathirika. Kuhama chumba na kubania unyumba utakuwa umemnyima haki mwenzio na ninahisi mshika ndo atakuwa nakuweka huko italy kwahiyo ukisema udai taraka ujue unakuja kuonja joto ya jiwe Bongo...akili kumkichwa.
ReplyDeletepole sana ndugu yangu kwayaliyo kupata. inaonekana mume wako hajaawa muaminifu katika ndoa yake ila siku zote Mungu amtupi mtu wake kwani unaonekana mama ulikuwa mwaminifu ndiyo maana Mungu kakuepushia. ushauri wangu nikwamba nenda hosp wanakieleza jinsi ya kuishi na huyo mume wako kwani bado ni mume wako tu. pole sana Mungu akupe nguvu katika kipindi hicho kigumu ulichonacho.
ReplyDeletesweet,
Arusha.
We michuzi unatuchora unataka tuoshe vinywa baada ya muda mrefu..mwambie huyo dada aweke picha yake kama ni mzuri aje kwangu...kwani lazima kungangania huyo mwanaumme???
ReplyDeleteNi mambo ya kawaida hayo kwa dunia ya siku hizi.Nenda kwa washauri nasaha na viongozi wa dini utapata ushauri wa kukusaidia, ni vizuri umpeleke na huyo mumeo ili nyote muwe katika level sawa ya uelewa wa hilo jambo usijefanya kitu akajihisi anabaguliwa. angalia wachafuzi wa hali ya hewa wa hii blog wasije wakakuchanganya akili. All the best, kuwa muangalifu usimuathiri kisaikolojia.
ReplyDeleteNakumbuka Tajiri mkubwa mmiliki vyombo vya habari vingi bwana "Many" kipindi kile Condom ndio inatajwa tajwa aliambiwa "Kuna binti mrembo ila muathirika, unaonje wewe uwe mfano umwingie kwa kondom" Jamaa mbali na kampeni alisema "Mi nna mke wangu, tuheshimiane"
ReplyDeleteNataka kusema nini? Hata wanaozinadi hizo kinga hawana uhakika nazo, sijui za nyumbabni hapo ila nyingi huku wameandika si kwa 100%. Sasa kwanini ujitoe mhanga namna hiyo? je ikipasuka?
Mbili. KIDINI ZAIDI.
Kama wewe ni mkristo tena mkatoliki hapo ndoa haivunjiki, uliahidi utampenda katika tabu na raha, tabu ndio hiyo, vumilianeni mpaka kifo kitapowatenga, yeyote atapotangulia. huo ndio mwisho halali wa ndoa. Kudumisha ndoa kumeingia dosari haina budi kuacha (fikiria hata angepoteza nguvu za kiume ghafla na asitibike, usingemuacha na usingevunja ndoa kikatoliki hakuna ruhusa hiyo)
TATU: KIMAADILI. Si vyema kumuacha maana ameteleza na ni kosa lake kama alitembea nje ya ndoa ila kama dini yenu inaruhusu uolewe tena, olewa ila itabidi awe mwenza kumfichia siri yake maana ndio upendo wa kweli.
NNE: KISHERIA. Yeye akilazimisha ikiwa ni pamoja na kukubaka atakua amekusudia kuua na ana kesi nzito na ataweza kuishia jela au kitanzi, heri umfahamishe mapema atambue hilo. Saa kumi na mbili akalale chumba chake na wewe chako. kulala kimoja ni kumtamanisha na kuhatarisha kubakwa, na utashindwa kesi utasemaje umebakwa na mtu uliyelala nae chumbani kwake?
TANO: Hapa ushauri utaupata si wa kitaalamu (baadhi) ni heri ukaonana na waliobobea maswala haya. Kama huamini angalia hwa hapa chini baadhi watasema nini
MWISHO: POLE SANA, POLE NA JIPE MOYO UTAFIKA MAANA SISI HATUJAPIMA KWAHIYO HATUNA UHAKIKA PIA.
Mimi: mchochole, maskini, kapuku, Hamnazo The Have Nots
Pole sana dada kwani najua kwa sasa upo kwenye wakati mgumu sana.
ReplyDeleteNi kweli HIV inatisha kwa sababu ukiwa navyo unajua nini kitakutokea baada ya miaka kadhaa ijayo na ndiyo maana inaumiza watu sana kisaikolojia ukilinganisha na matatizo mengine kama malaria.
Mimi naungana na wewe kwamba mtengane vyumba kwani hata mkitumia condoms bado risk ni kubwa ukizingatia huyo ni mmeo na kuna uwezekano mkubwa hata wa kulana mate kabla ya tendo. Muweke chini mumewe na umueleze risk ziliopo na athari zitakazowapata watoto wenu kama wote mtakuwa na HIV, ni vizuri ubaki kama ulivyo ili uitunze familia na kama hakuelewi basi dai talaka kwani hayo ni maisha yako binafsi hivyo unapaswa kuyalinda mwenyewe. Lakini unatakiwa ukapime tena baada ya miezi 3 ili uthibitishe kama nawe upo salama
aka mwenzangu wala usikubali muache afe peke yake hayo ndio malipo yake malipo ni dunian hapa hapa au aende kwa wanawake zake huo wakapakazane vizuri tena ningekuwa mimi na nyumba ningehama kabisa maana huyo mumeo mmuuaji kabisa,
ReplyDeleteHi! dada, kwanza wewe mwenyewe umepima mara ngapi mpaka ukajiamini kuwa huna maambukizi, maanake kabla hujamgundua kuwa ameathirika mlikuwa mkikutana kimwili kama kawaida maana hukuwa ukijua kuwa tayari ana ngoma.
ReplyDeletePili, huyo ni mumeo kumbuka mliahidiana kwa shinda na raha, kitendo cha kuhama chumba si chema utakuwa umemnyanyasa kisaikolijia, pia watoto wako watagundua tofauti zenu, so naona mtumie kinga kwani zinasaidia wakati huo mkatafute ushauri kwa viongozi wenu wa dini na wataalam zaidi, wote wawili mkiwa na lengo moja na kujenga na si kubomoa, nadhani na yeye hana nia mbaya ya kukuua kumbuka hata akitangulia leo wewe utalinda na kuhudumia watoto wenu, lakini si lazima yeye atangulie maana mambo ya mungu hayatabiriki leo yeye mgonjwa lakini anaweza tangulia yeyote hata asiyeathirika.
Hamna jinsi tatizo limeshatokea muhimu tafuta njia nzuri ya kusolve na si kuharibu zaidi usalama kwako wewe na yeye pia kwani anaweza akaishi miaka mingi zaidi na kuendelea kulea watoto wenu.
Mwombe Issa email yangu tuwasiliane nikushauri vizuri.
ReplyDeleteKabla ya hapo ninacho kuomba acha ku panic hiv sasa sio issue ya kutisha kama zamani halafu uko Italy kuna facilities.
We marry for the good and the bad so mpende mumeo kama zamani hata zaidi.
Tumieni kinga...Mengi kwa email
Pole sana mdada wangu! Hii ni kawaida sana katika jamii yetu hii iliyoathirika na janga hili.
ReplyDeleteKwa upeo wangu mfinnyu naona unachokifanya ni KUMNYANYAPAA huyo mume wako. Kwanini hutaki kumpa unyumba? Kisa eti kaathirika? Kwa kweli unachokifanya sio vizuri hata kidogo.
Inaonekana wewe ni msomi na uja fika Ukimwi unaambukizwa vipi, kwahiyo ombi la Mumme wako la kutumia kinga ni sahihi kabisa. Unataka kumuua mume wako kabla yasiku zake lol
is he Tanzanian? please keep far from him come back home.If he is Italian things will be worse, he might try and infect u.please dont nyanyapa him the so 'kuhama chumba' he will come drunk and rape u, its a childish move.please pima tena then contact me sunasset@hotmail.com I will advise you accordingly
ReplyDeletePole dada, yote ni mitihani ya dunia. kama wenzangu walivyosema hapo juu, usihame chumba, utakuwa unazidi kumuumiza kisaikologia. lakini usitembee naye kamwee! ukihama chumba, italeta picha mbaya kwa watoto, na itamuumiza baba. either bakia chumbani na msimamo wako wa kutompa sukari majojo, lakini aelewe kwamba unataka kuwahai, kuendelea kutunza watoto, which is the most important thing. kwa zaidi, ni bora muende counseling, either kanisani kwa padree mnaemuamini kama ni wakristo, or to couseling centers. lakini elewa ni kipindi kigumu kwake, so usimnyanyapae. u never know aliutoa wapi.
ReplyDeleteits me Nana
waosha vinywa mpooo??????Lol
ReplyDeleteIla pole sana Dada yetu.
Atumie dawa, na kuishi kwa matumaini, na nyie mnaosema kuwa ampe au asimpe unyumba, kwani kustareheshana ni ngono tu? Mbona anaweza kumstarehesha huyo mumewe bila ngono, ila hapo ninavyoona mimi tatizo ni kubwa zaidi ya hilo la kunyimana unyumba. Tatizo hasa ni ila hali ya kuona umesalitiwa, kufadhaika na kutokuamini kuwa huyu bwana kumbe hakuwa muaminifu kwako. Hiyo imekuumiza zaidi kuliko hata yeye kuwa na huo ukimwi. Maana mtu aweza kuwa na hisia kuwa mumewe ni kicheche lakini pasina ushahidi anajipa moyo kuwa si kweli lakini likitokea kama hilo lilitokea unaona kama dunia yote imekuangikia wewe. Cha msingi ni kupata ushauri nasaha, kuhusu jinsi ya mtakavyoendelea na maisha yenu ya ndoa kama watu wawili mnaoishi nyumba moja kisha kama mume na mke. Hapa namaanisha kusolve hiyo ishu ya usaliti na kusameheana kwanza ili kuondoa hiyo hasira uliyonayo. Hasira hiyo ikishaisha mengine yatakuwa rahisi kuyakubali otherwise hata watu wakikwambia utumie kondom ya chuma ikiwa bado moyoni una hasira pia hutakubali kwa sababu kusalitiwa kunauma sana
ReplyDeletehILO WALA SI LA KUULIZA.
ReplyDeleteNi rahisi NGONO NO. NOOOO KABISA KWA NJIA AU UTAALAMU WOWOTE. TENA HAKIKISHA HUAMBIKIZWI KWA NJIA YOYOTE HATA KWENYE KUFUA NGUO ZAKE.
au AKUBALI MUISHI BILA UNYUMBA UENDELEE KUMHUDUMIA YEYE NA WATOTO AMA MUACHANE.
Huna sababu ya kufa mapema na yeye pia afe mapema kwa itu mnachoqweza kujizuilia. Strehe yenu itawatesa watoto.
Ukipata ukimwi wakt umeshajua ni sawa na kuamua kula sumu hiyo ni dhambi kwani umeudhuru mwili wako kwa makusudu. Wee unaambiwa hii chupa ndani yake kuna sumu mwenzio anakuambia lamba lamba kwa nj hutakufa. Ukubali basi utakuwa mwenda wazimu.
Mungu alishafanya kazi yake ya kukulinda siku zote hujaambukizwa sasa amekupa ufahamu ujilinde mwenyewe. Ukifanya nae mara moja zaidi nakuhakikishia utaibuka na ukimwi. Tumia ufahamu wako aliokupa mungu. NGONO NO. NOOOOOOO.
Pili hutakuwa umewatendea haki hao watoto.
NArudia au muishi bila kutiana na kama hawezi muachane ulee watoto wako.
Mi nafikiri wewe ukiwa kama mama ukumbuke suala la watoto yatima, mumeo sasa lazima kaathirika kisaikolojia haiwezekani akakubali ukweli na kuelewa kuwa kuna suala la watoto mbele yenu. Ngono ni nini mpenzi wangu, give up lea wanao. Hata maisha yawe magumu vipi kaza roho lea wanao, ila usimbague mumeo, Kazania kuhamia chumba kingine ila umuahidi kumuuguza mpaka mwisho, ukimlea vizuri anaweza akaishi kama kawaida na asife mapema bila wewe kuathirika, ila jisimamie wasimamie watoto. usiwe dhaifu huu ni wakati wa kupima ukubwa wako. Ila kwa kweli pole sana siwezi kuimagine position yako. Mtazame Mungu muulize akujibu kuwa na imani, muapproach taratibu mumeo muinvolve kwenye maombi ili Mungu awaongoze namna ya kulihandle bila kusacrifice watoto wenu. Huko Bongo usikute ndugu zenu kibao wameathirika na nyie mkifa nani atawalea watoto wenu, angalia from both perspectives. Nitakuweka kwenye maombi. Ila usifungwe na sheria yoyote ya dini wala ya serikali huo ujinga siukubali kabisa kwa kuwa its the matter of life and death here na tunaongelea kuhusu watoto wako. Je ufe kulinda dini/serikali utelekeze wanao? Hao wanaoenslave wenzao kwa ticket ya dini waache unafiki. Hebu jiulize ungekuwa umeathirika wewe mumeo mzima wangesema hivyo? Kama sio ungefukuziwa kijijini kwenu na wanao mume akaoa mke mwengine. Tuache kuwa bias, Mwaya mtazame Mungu na sio sheria, sikiliza moyo wako usiwasahau wanao hata sekunde moja.
ReplyDeletePole sana dada kwa tatizo lako, binafsi nimeguswa kwa namna ya pekee na hali ya mumeo. ila kwa upande mwingine nimesikitishwa sana na uamuzi unaotaka kuchukua wa kumtenga mumeo, uamuzi wako na michango ya baadhi ya wadau wanaokubaliana na uamuzi wako. ujue kwa namna moja ua nyingine unaharakisha kifo cha mumeo. nadhani unajua kuwa muathirika wa ukimwi anakufa haraka kwa matatizo ya kisaikolojia kuliko kimwili, hapa nina maana kwamba hata kama mtu mwenye HIV atakuwa na afya njema lakini akakosa social and psychological support hawezi kuishi kwa muda mrefu. lazima ufahamu kuwa kumtenga ni kuharakisha kifo chake na hii inaonyesha kuwa mapambano dhidi ya unyanyapaa kwa waathirika bado ni safari ndefu sana na hii inachangia watu wasijitokeze kupima afya zao wakijua fika kuwa ikijulikana wana HIV basi watatengwa na wanandoa wenzao na jamii kwa ujumla wake. naungana baadhi ya wadau hapo juu wanaoshauri kuwa wote wawili mwende mkapate ushauri nasaa jinsi ya kuishi na hali hiyo.
ReplyDeleteWhat i think
ReplyDeleteKwa mtazamo wa juju tu inaonesha bado unampenda mume wako. Unataka kutengana naye chumba kwasababu yeye ni muhathirika wa ukimwi.
Facts
Ukimwi Hauwezi kuambukizwa kwa kujaamiana mkitumia protection. Sema inaweze ikapasuka au kama ilikuwa imeexpire ikaleta matatizo, ndo maana ni 85% safe.
Mfano wa kweli.
Binamu yangu ni mgonjwa wa ukimwi na mke wake sio mgonjwa. lakini hadi sasa hivi wanaishi vizuri tu bila matatizo, including kujamiana na mabusu tele. Upendo unaooneshwa na mke na watoto wake ni mkubwa sana na unaompa ngufu ndugu yangu huyu kuishi hadi leo.
- Ukimtenga mme wako anahathirika sana kipsychologia. Na utakuwa unamuongezea matatizo mengine.
- Kama wewe utakuwa unaogopa sana na hujisikii vizuri kufanya naye mapenzi unaweza ukakaa naye chini vizuri ukamuelewesha unavyojisikia na mkawa mnaishi chumba kimoja mkikumbatiana na mabusu tele bila kujaamiana. ndoa sio lazima kufanya tendo la ndoa... upendo ndo muhimu.
-Ukimbagoa vyovyote italeta picha mbaya kwa watoto.. na wao itakuwa rahisi kumbagua baba yao na kuwa na picha mbaya kwa wahathirika wote wa ukimwi.
Mama pole na Mume wako pole zake pia , maana wote poleni mpo katika mtihani mgumu. Mimi kama mwanandoa ambae sijapima I can feel for you maana sisi wengine hatujui tuna hali gani dunia ya leo. lakini wewe usimuadhibu mwenzako kama ni makosa yake basi muachie mungu wake, mimi ushauri wangu ni kwamba rudini kwa mungu wenu msali sana kama ni waislamu basi hakikisheni wewe na mume wako swala tano na usiku muamke kuswali sala za maombi za usiku ni nzuri sana na kama wakristu basi ndio maombi yasiwaishe na kanisani msikose mkaombewe. pili mmejaaliwa mko huko Italy huduma za afya sio kama za kwetu bongo hivyo tafuteni kwenye ushauri nasaha na mkajue jinsi ya kuendelea na maisha yenu wakati mmoja wenu ameathirika. tatu mimi naona hapa mtumie Condomu mwambie mumeo avae tatu tatu na hakuna tena mambo ya denda sijui, just in case mna vidonda mdomoni. kumbuka ukimwi unaambukizwa kwa damu na si kitu kingine. na saa nyingine kama wewe mwanamke uko okay kwenye sehemu zako za siri huna michubuko basi mngeweza hata kula kavu lakini bi dada sikushauri uriski maana kuna watoto hapo na asikwambie mtu biashara ya kunywa dawa kutwa mara tatu maisha yako yote sio mchezo so bora mtumie kinga avae mbili mbili tatu tatu moja ikipasuka bahati mbaya nyingine inakukinga . Nne ndugu yangu mimi binafsi sikushauri umuache huyo bwana ingawa kwa kweli ni ngumu na hata kama mimi ningekuwa kwenye situation yako sijui ningefanyaje sema fikiria ya kwamba huyo ndio mume wako Mmungu aliekujalia na tunajua wanaume ni viumbe dhaifu l hali hawana maana yeyote ikifika kwenye ngono sasa wewe ukimuacha saa hizi ndio hatatulia na ataupeleka huo ugonjwa nje na kuambukiza watu wengine na wengine wataambukiza wengine so mlolongo ndio utazidi na hii circle itaendelea na watu wengi wataishi kwa mashaka na wengine hata kufa. Sasa hii ikitokea mama yangu mimi somehow naona wewe concious yako haitakuwa clear ukijua ya kwamba ungemsaidia asiende huko na kama mzazi utakuwa unajali maisha ya watoto wa wwengine sijui unaonaje mwenyewe maana somehow ingawa si makosa yako ,utachangia katika huyu bwana kuutoa huu ugonjwa nje ya nyumba yake na kuupeleka nje kwa kuwa umemnyima ujumba kwani sidhani kama ataweza kuvumilia kuishi bila ngono mwanaume rijali na akitoka nje huwezi kujua ghadhabu zake akitoka nje labda atakuwa hajali nani analala nae tena bila kinga.sasa bi dada please msitiri mumeo ili uweze kuiokoa jamii. Na mwisho kabisa please usivunjike moyo kwani siku hizi huo ugonjwa sio unamaanisha kifo, advancement ya technology na madawa watu wanaishi miaka zaidi ya 30 tena maisha yanalingana na kawaida tuu cha msingi ni kufuata tu masharti mume wako ataishi kwanza na hiyo ngono anayoitaka ukiwa na ugonjwa hutakiwi kufanya mapenzi mara kwa mara maana unatumia energy mno katika hilo tendo na ni zoezi kubwa na wewe mwili wako uko weak defense system yake so nmkienda kwa washauri wenye taaluma yao watawapa ushauri nasaha ya jinsi ya kuishi maisha yenu as normal as you can. samahani nimesema sana ni kwa sababu kwa kweli umenigusa na tutazidi na tutaombeana Mungu mtakuwa salama na familia yako . Pole kwa hayo lakini endeleeni tu maisha yenu kwani Ukimwi sio mwisho wa maisha.Ndimi
ReplyDeleteMdau wa Ukerewe
wasiliana na wizara ya afya ya hapo ulipo haraka hiwezekanavyo na waelezee ulichoelezea hapa simple.hapa unajichoresha tu mawazo utakayo pata hapa ni hayo hayo ambayo wewe mwenyewe umeyafikiria na umeshindwa kufanya its not that easy like u think .wasiliana na wizara ya afya na utapata msaada mkubwa wa nini cha kufanya na pia mume wako atapewa darasa na ataelewa hali alisi.
ReplyDeletePole Aunty Au Dada Au Mama vyovyote Heshima zikuendee.
ReplyDelete1. Sio Kila Binadamu anapata UKIMWI kwa Uzinzi Ukimwi Hata Sindano,Kubadilishana Herini wanawake mambo mengi tu.
2. Mumeo Lazima aelewe kama anakupenda wewe na wanao lazima atakueelewa na kuwaweka salama na wewe uvumilie mpaka kufa kwake. Kama hataki kuelewa ongea na wakubwa dai talaka haijakatazwa na wala sio zambi ila mungu ndio anajuwa kapata kwa njia gani.
3. Watoto na Wewe nawaombea salama muishi salama na mumeo msomee mungu amsamehe ndio kilicho baki.
yani ukisikia mitihani ya maisha ndo hii haki ya nani, hii imenikumbusha dada yangu alitelekezwa na mumewe zaidi ya miaka 10 na mume wake kuhamia kwa mwanamke mwingine mwishowe yamemshinda huko kapata na ukimwi anamfata dada amsamehe warudiane kwa kuwa ni mkewe halali wa ndoa.baadhi ya watu wakawa wanasema msamehe tu mrudiane kwa kuwa ni mumeo wa ndoa,what a non sense yani baada ya dunia kumgeukia analia anaomba hifadhi? hii story inataka kufanana na hii
ReplyDeleteila mi binafsi simshauri aendelee kushiriki na huyo bwana maana ni hatari na anaweza pata HIV pia ambapo itakuwa tabu kwa watoto baadae.dunia ya leo hamna mtu anaelea mtoto wa mwenzie pia atafute na washauri wa ndoa kwa maelekezo zaidi
Pole sana dada yetu.
ReplyDeleteHakuna jibu rahisi wala la dhahiri kwa tatizo lako. Lakini zingatia mambo kadha. Kwanza kabisa inakupasa kuondoa hofu na badala yake kujielimisha zaidi juu ya jambo hili. Zungumzeni na madaktari, washauri nasaha, viongozi wa dini, zungumzieni hofu zenu. Maarifa mengi yako kwenye vitabu na kwenye internet.
Pili, jambo hili kumbe linajulikana sana. Jozi ambazo mmoja ni muathirika na mwingine si muathirika huitwa discordant couples. Google phrase hiyo na upate maarifa zaidi. Inaonekana kuna mambo kadha yanayoweza kupelekea hali hiyo. Miongoni mwa mambo hayo pengine muathirika ana virusi vichache, na pia yeye na mwanandoa mwenzie hawafanyi tendo mara nyingi sana, au hawana mikwaruzo inayoharakisha maambukizi, nk Kuna mengi sana.
Tatu, ukweli kwamba mmeishi ilhali mmoja wenu ni muathirika inadhihirisha kwamba kuna hali fulani iliyozuia maambukizi.
Nne, tafuteni uwezekano wa kuendeleza hali hiyo. Endapo muathirika atatumia dawa za kuzuia mfumuko wa ugonjwa na kwa hivyo kuwa na virusi vichache katika damu yake, pia asipate virusi vipya, yaani asifanye ngono na mwathirika mwingine anaweza kuishi maisha marefu. Sasa, inawezekana kabisa kutumia kondomu, na kuhakikisha fluids zake zisimwingie mwenzie, mnaweza kuishi maisha marefu bila kuambukiza.
Kwa yote, wewe sasa ndiyo mwenye uamuzi wa kutoka au kubaki. Lakini kumbuka mlipofunga ndoa mliahidiana kuwa pamoja katika afya na katika maradhi. Kuhama chumba ni kuvunja ndoa. Kubaka ni mauaji. Sasa muafaka katika masuala ya unyumba ni muhimu kabisa. Na ni lazima ujilinde pia.
Kila la heri
mwendesha blog anaweza kukupa anuani yangu.
kimbia shoga, tena haraka sana, kupendana wa shida na raha siyo maana hiyo, sasa mkifa wote nani atawalea watoto? hata hizo dawa za kurefusha maisha zina ukomo wake.
ReplyDeletepole sana dada.
ReplyDelete1. sasa ukihama chumba utawaeleza watoto nini? ndio mwanzo wa kuwapa watoto matatizo ya kisaikolojia na ndahani watoto wako hakuna aliye zaidi ya miaka 15 labda kama walikuja kabla ya ndoa.
2. kama alivyosema mdau mmoja hapo juu kuna njia nyingi za kupata ukimwi hivyo usifikiriae aslani kwamba mumeo kapata kutokana na ukicheche
3. pia mdau mwingine kasema hapo juu mapenzi sii kujamihiana tuu, kuna njia mbali mbali za kufanya na wote wawili mkastarehe na kuridhika kwa kuzingatia hali inayowakabili. tulieni mkubaliane katika hili.
endelea kuishi na mumeo mlee watoto.
Je,Mumeo yeye mwenyewe anajua kwamba ni Muathirika?Kama hajui ni wewe tu unayejua ushauri wangu utakuwa rahisi kwako.Utakacho takiwa kufanya ili uepukane naye katika tendo la ndoa fanya chini juu uwasiliane na Daktari yeyote au Kituo chochote cha Afya uwaeleze kwa undani matatizo yako,kisha waombe wakupe cheti cha hospitali hiyo kitakacho thibitisha kwamba umepima na ukagundulika kwamba umeathirika kwa ukimwi.Kwa hiyo utakapo mjulisha Mumeo kuhusu kuathirika kwako huko lazima hata yeye mwenyewe atapata mshituko na kuanza kukukwepa katika tendo la ndoa.Na itakuwa rahisi kwako hata kuishi katika vyumba tofauti wewe na mumeo kwa faida ya watoto wenu.Ushauri huo utakuwa wa maana iwapo bado una mapenzi na mumeo.Sasa ikiwa Mumeo mwenyewe kesha tambua kwamba ni Muathirika itabidi uwe mwangalifu zaidi.Fanya mipango na Daktari au Hospitali yoyote kwamba utakwenda pale kupima pengine ukiwa na Mumeo au bila ya Mumeo kisha wao mwishowe wakupe cheti kitakacho onyesha matokeo kwamba umeathirika kwa ukimwi.Baada ya hapo maisha yenu yatachukua mwelekeo mpya,kila mmoja wenu atatambua tahadhari ya mwenziwe akiogopa kumwambukiza mwenzake kwa faida ya malezi bora ya watoto wenu.Hata mumeo akilazimisha mfanye tendo la ndoa usionekane kama unamkatalia kikatili bila ya kujali ni mumeo bali mfikishe mahali atambue kwamba kutokana na kuathirika kwako umepoteza kabisa raha ya tendo lenyewe la ndoa.Litakupa maumivu makali na pengine kufupisha zaidi uhai wako kwa kupoteza nguvu za mwili zaidi.Uwe wazi na mkweli kumruhusu Mumeo ajisikie huru kutafuta Machangudoa wa Nje ikiwa hawezi kabisa kujizuia.Lakini usimkimbie wala kumtenga wala kumnyanyasa wala kumbagua katika mahusiano yenu ya kila siku.Mchukulie kama ni mgonjwa au mtoto wako mwenyewe ambaye bado atahitaji matunzo yako na msaada wako wote ili kumhakikishia usalama wake.Nyakati zote uwe makini kwa kuchukua tahadhari za kutosha asije akakutumbukiza katika hali ambayo itamrahisishia yeye aweze KUKUBAKA wewe bila ya ridhaa yako au bila ya wewe mwenyewe kuwa na fahamu zako kamili.Jitahidi sana hali hiyo kati yako na mumeo isije ika waathiri watoto wenu kisaikolojia na wakaharibikiwa katika masomo au maisha yao.Hkuna jambo ambalo huwa na athari kubwa sana kwa watoto kama tendo la Mama kutengana na Baba katika maisha ya ndoa.Lakini iwapo hupendi tena kuishi na Mumeo kutokana na sababu nyinginezo zaidi ya hiyo ya kuathirika basi ushauri wangu ni kwamba fanya haraka Upate TALAKA RASMI ILI KILA MMOJA WENU AISHI KIVYAKE bila ya kuwa athiri watoto wenu katika masomo yao au maisha yao.Ukiona maisha huko ugenini hutayaweza fanya mipango urudi huku nyumbani na watoto waje wasome na wewe utaishi maisha mazuri tu.Wakikua kama watoto watapenda kurudi tena Italy basi watarudi tena muda huo ukiwadia.Ukiwa na matatizo zaidi tuwasiliane zaidi kupitia blog hii ya Michuuz.
ReplyDeleteJamani waosha vinywa jiwekeni kwenye nafasi ya huyu dada hata kama ungekua ni wewe ungekubali kuambukizwa kwa kujua. wengine hapa ndio wasambazaji wazuri wa virusi ndio sababu wanamshauri aendeelee kushirikiana na huyo muathirika je kama huyo muathirika angekua hajaadhirika yeye angekubali. Dada usikubali kufa uache watoto wenu bado wanahitaji wazazi kwani mkifa wote watabaki yatima ila wewe ukiwa mzima utaweza kumuhudumia mume wako wakati wa ugonjwa na pia kuangalia watoto hapo baadae. Cha msingi uongee vizuri na mumeo na pia umsamehe kwa kosa alilolifanya kisha muongozane kituo cha afya muelekezwe jinsi ya kuishi na mmoja wenu akiwa muathirika. Nadhani kwanza mfikirie watoto wenu, watakavyopata shida kwa kuwakosa wote wawili.
ReplyDeletemichuzi hii habari sio ya ukweli kwa maana hiyo basi nachangia kama ifuatavyo,wewe mwanamke unakumbuka siku ya ndowa yenu ulisemaje?kama ukumbuki nitakukumbusha ulisema mwenyewe na hakuna aliekulazimisha kuwa mtakuwa pamoja kwenye raha na shida na mpaka kifo kiwatenganishe,sasa basi mwenzio yuko kwenye kipengele cha shida. ili kutimiza ahadi ya ndowa inabidi uendelee kula nae uroda bila kutumia mpira kwani mke na mume huwa hawatumii mpira, mwezio hatakapo kufa utamzika na wewe utakapo kufa watoto kwa kuwa wao hawajaadhirika watakuzika. hapo utakuwa umetimiza ahadi ya ndowa na mlango wa peponi utakuwa wazi kwako mama. Kwani ukisema uhame chumba mumeo atakuvizia umelala usiku akubake ili ngoma iwe droo
ReplyDeleteMbega mweupe hapa
HUJAFA HUJAUMBIKA! INGEKUWA WEWE NDIYE ULIYE ATHIRIKA UNGEPENDA MUMEO NA WATOTO WAWE NA MSIMAMO GANI KWAKO?
ReplyDeleteUnaposoma maoni hapa ndiyo una elewa kwanini TZ bado tuko mbali sana na swala la ukimwi.
ReplyDeleteInasikitisha maana wengi wanaochangia hapa ni wasomi lkn bado mawazo ya kubomoa na sio kujenga.
Tz watu bado wanaendelea kujificha na kufa kimya kimya wakati uwezekano wa endeleza maisha upo. Jamii bado ina chukulia huo ugonjwa ni wa aibu, dhambi....nk
Popote duniani kuna vituo vya haya mambo iweje ndugu yetu inaonekana huna habari kwamba wapo watalaam wanaoweza kukusaidia au labda huko Italy?
Hapa pata kuchanganya tu kila mtu atasema lake. Utajikuta hujui ufanye nini.
Ushauri wangu nendeni kituoni na wala usimkimbie mumeo.
pole sana dada kwa matatizo yaliyokutokea ila yote maisha,, huwezi kumkimbia mumeo kwakuwa eti ameathirika..shukuru Mungu wewe na watoto hamjakumbwa na hilo ila msimtenge..endelea kumpenda na kumjali hayo yatampa faraja na yatamuongezea nguvu ..kuhusu bed issues, kuhama chumba ni kama unamtenga mwenzio unaweza kulala nae kitanda kimoja na msifanye kitu chochote itabidi aelewe situation kuwa hata kinga sio 100% na kama wote mkiathirika itakuwaje kwa watoto?therez no point. so lala nae kitanda kimoja mbusu mkumbatie ila shuguli ya kikubwa nafkiri hapo labda wadau wenzangu wanisaidie ila naona kama itakuwa haiwezekani....Pole sana dada na nakupa hongera kwa ujasiri wako.
ReplyDeleteKwani ugonjwa aliupataje?? Inaonekana mumeo ni mtu asiyejali maanake haoni risk ya wewe kuambukizwa. Ushauri wa chumba chako ni poa kabisa na kama hataki chukua separation. Nimejionea kwa macho yangu wanawake wanaathirika kutokana na tabia kama hizi. Tena wengine mke anakufa halafu yeye anaenda kuoa dogodogo kutoka kijijini. Baada ya miaka mitatu anakufa anamuacha dogodogo na maambukizi. So kama hataki kuelewa somo kimbia kuokoa maisha yako. Kimbia ili uweze lea wanao. Mungu akutangulie
ReplyDeleteMLIPOKUWA KWA PADRI MLIKUBALIANA KWA SHIDA NA RAHA,UGONJWA NA UZIMA...BIBIE LEO UNAMKIMBIA MWENZAKO VIPI?
ReplyDeleteIKUMBUKWE KUWA JAMAA INAWEZEKANA HAKUUPATA KWA UZINZI KWA HUKULIELEZEA HILO, HIVYO NAKUSHAURI BIBIE MMMH PAGUMU ILA KAMA VIPI USIMPE ATAKUUWA....ILA KUNA MAMBO KAMA (KAZI ZA MIKONO) HANDJOB UNAWEZA KUTUMIA KUMPA NAFUU...OTHERWISE UPATE NA WEWE MUENDE SAWA!
hata wewe unao kacheck tena vile vidudu so kuna wakati havionekani kama cd4 zako ziko juu na ngangari kama ni kweli Mshukuru Mungu na ukatowe sadaka.....
ReplyDeleteNi kweli pole sana dada yetu manake nakuonea huruma...ila kwa upande mwingine,pamoja na hayo yote yalosemwa hapo juu,kumbuka kwamba huyo ni mumeo.Najua wengine watkwambia hama chumba (kama unavyotaka) au mtengane...au tumia kondomu...
ReplyDeleteMaoni yangu ni kuwa wewe kwa sasa ndo unaweza kuwa tatizo zaidi kuliko yeye alivyo tatizo kwako na watoto..kumbuka maamuzi mengine unayoweza fanya yanaweza kusababisha matatizo zaidi kwenye hiyo ndoa yako tete ulonayo.
Nakushauri ufanye maamuzi (japo yatakuwa ni magumu kwako)kwani unataka mtengane chumba wakati bado ni mumeo...kwa hilo kama unaona huwezi tena kumpa unyumba ukiamini kuwa amekusaliti katika ndoa yenu..basi omba talaka urudi kwenu..nasema hivyo kwani kama wengine walivyokwambia anaweza kukubaka na kuleta usumbufu zaidi
Pili, ukumbuke huyo ni mumeo..hali unayotaka kuifanya ndo tunaiita "unyanyapaa" hivyo basi nakushauri upate ufahamu zaidi kuhusu ugonjwa huu...hilo litakusaidia kufanya maamuzi yaliyo sahihi kulingana na uelewa wako na jinsi unavyoithamini ndoa yako na familia yako..kama ulifunga ndoa na ni Mkristo basi huyo ni mumeo mpaka kufa..na vile vile hiyo ni sababu tosha ya kumpatia talaka (utakuwa umemuokoa zaidi kuliko akapata kesi ya kubaka au hata akakuletea fujo) kwani wewe bado ni mkewe.
Suala la wewe kutumia kondomu au la tafadhali wasiliana na wataalamu watakufahamisha..ni kweli watu wanaambukizwa pamoja na kondomu wanazotumia...tatizo ni kwamba ukitumia kondomu inabidi muwe na staha katika mapenzi..yakiwa yale yasiyo na utaratibu unafaa kwenye ngono (abusive sex) uwezekano wa kupata ugonjwa upo pale pale..kwani kondomu sio chuma kwamba itahimili vitendo visivyo stahili.
Nenda uwaone wataalamu wa aina tofauti,kuanzia wanasaikolojia, washauri nasaha na hata viongozi wa dini pia watakusaidia...la unazidi ongeza tatizo juu ya tatizo.
Wengi watakwambia hama chumba au usifanya nae unyumba...yote hayo si jibu sahihi kwa hali mliyonayo...jiulize kama wewe ndo ungekuwa nafasi yake ungekubali akuache au ungeondoka mwenyewe (kujipa talaka)?sio kweli...!
Mwisho kuna watu wengi tu kwa sasa ambao wanafahamika mmoja kaathirika, lakini bado wanaishi pamoja na wanatunza familia zao,umoja kati yao ndo unawawezesha kukabiliana na matatizo walonayo..na wengine hata wanapata watoto wakiwa kwenye hali hiyo uloelezea...hivyo kaza buti na utafute jibu mapema kwani unavyozidi kuchelewa kufanya maamuzi ni shida zaidi unazikaribisha..
Kila la kheri..na pole kwa yote
Nyaningedere
Pole sana Dada! Huu ni wakati mgumu lakini nakuombea ufanye maamuzi mazuri! Mi nakushauri mwende wote hospitalini mkapime na mwombe ushauri pia wewe uwasilishe mawazo yako. Mi nakushauri uache kabisa tendo la ndoa na huyo mmeo. Ndio mmeoana kwa shida na raha lakini naona ukiathirika hata wewe watoto watateseka sana. Bora ubaki wewe ulee watoto. Pia watoto wenu waambie ukweli kuhusu hali halisi hakuna haja ya kuwaficha. Wewe na wanao muendeleze upendo na kumjali baba watoto ili kumsaidia kisaikolojia. Mimi sikushauri hata kidogo ukutane naye kimwili kama majibu mtayopata yataonyesha wewe sii muathirika. Kinga zinazotajwa sii asilimia 100. Kuwa strong naamini mungu atakuongoza maana yeye anafahamu hufanyi kwa nia mbaya. Kama itashindikana mahakamani wanatoa talaka na sababu yako ni mojawapo ya sababu kuu tano Za mahakama kutoa talaka kwa wanandoa( Tanzanian Court Laws). Naomba usichanganyikiwe majukumu uliyonayo ni makubwa. Nakutakia maamuzi mema Mungu yuu pamoja na familia yako siku zote!
ReplyDeletejamani nyie mnao ongea pumba kuhusu hili swala fikirieni kwanza kabla hamjatoa comment. This is a serious issue,there's kids involved and i understand the womans concerns. Using a condom does not protect you 100% because it can split anytime, it might come off during the session so it's not safe to advice the poor woman to carry on. The best advice is to visit sexual health clinics and get better advice because this blog will stress the hell out of you.explain the risks to your husband and if he truly love you and the kids he will understand. All i can ask you to do is to support him as this is a difficult time for him.
ReplyDeletesawaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
ReplyDeletewote mmeongea na hakuna, nasema hakuna hata mmoja aloweza pata jibu kwa huyo dada.............
mnamchanganya tu
kupata comments kutoka kwa wadau aimaanishi kuwa hajawaona wataalamu wa swala hili, anataka tu kupata mawaidha kusikia je? ingelikuwa wewe ungefanyaje? thats how I understand her concernds
ReplyDeleteHmmm... Mie sikushauri chochote zaidi ya kufikiria watoto. Kwa maana nyingine hama chumba kabisa kwani ukipata hiyo HIV huwezi jua, siajabu wewe ukakumaliza mapema zaidi ya mumeo. Hao watoto atawalea nani? Siku hizi hakuna kulelea mtu watoto, si unaona mwenyewe?
ReplyDeleteHili tatizo ni kubwa lakini halihitaji ushauri kwani ufunmbuzi uko wazi. Mapenzi ni wakati wa raha sio kuuwana. Hata watu wakipendana, ili mradi hawajafa pamoja hawazikwi pamoja. Hamna zawadi kama uhai. Kachezea wake, lea wako. Labda kama we ni tegemezi saana kwake, sikiliza maoni, lakini wasichana wa kimagharibi wanajuwa cha kufanya.
ReplyDeletehuyu aliyesema kuhusu dada wa magharibi wanajua ni nini hicho wanajua ambacho sisi hatujuhi tuelezane basi hili sote tuna interest na hili swala kwani wengine tulinyamaza lakini shida hii si ya mmoja, na nikwamba, wakina mama wengi ndani ya ndoa hawajuhi mambo ya michizi........... tungelisikia mengi kwahiyo longa tu tupate elimu, usisahau msemo wa mjinini shule! sasa hivi ni michizi shule!
ReplyDeleteUsilete mchezo, wadada wa magharibi hutaliki kwa kukataa au kuchelewa kupika, seuze kuwa na killa diziz.
ReplyDeleteHapo yale maswala ya ndoa imefungwa mbinguni isifunguliwe ardhini ndo yanaonyesha ni imani tuu si lazima iwe reality.
Maana nchi zoote duniani, magharibi wanafuata saana dini lakini kwa talaka wanongoza duniani.
Mwacheni dada wa watu ashike hamsini zake alinde uhai wake.