kocha wa vijana wa yanga wa enzi hizo, mzee kwala (shoto) akiwa na kikosi chake cha yanga kids. inashangaza kukuta siku hizi inabidi vilabu vishikiwe bakora ili kuwa na timu kama hizi ambazo zilikuwa chachu ya nchi hii kufanya vizuri katika mashindano ya ndani na nje. ukiangalia kwa makini utakuta katika picha hii kuna vijana waliokuja kuwa nyota wakubwa, ikiwa ni pamoja na mohamed rishard adolf (wanne toka shoto, waliochuchumaa) mohamed mkweche (wanne shoto waliosimama), akifuatiwa na mohamed yahaya tostao na kassim manara. leo hii utakuta kocha wa taifa kama maximo inamlazimu afundishe wachezaji wake hata kupiga danadana....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 13, 2008

    halafu akisema hawafundishiki mnamuona m'baya. Kumbe hajui aanzie wapi. Mpira hawana uzoefu nao, lugha ndo usiseme bora ajichumie zake kwa ulaini.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 13, 2008

    Tatizo watu wabishi wanaambiwa mivilabu yao hio ndio inaua soka hawataki wamemshikilia maximo, maximo.wanasifia hao wachezaji wa zamani bila kujua walitokea wapi sasa unaona timu za watoto zinavyosaidia? Mivilabu yetu ndio inaua sokaaaaaaaaaaaaaaa watanzania hamkeeeeeeeeeeeeni toka lini watu wakalisi huendawazimu? Tuacheni kuwa wendawazimu wa kujitakia vizazi vipya lazima tutumie mfumo mpya.hata huyo mbuzi ukimpigia gita kwa mda mrefu nina huakika mziki ataucheza.michezaji mijitu mizima haina hata akili ya mpira.mtu unashindwa kumsoma mwenzako mpira atapiga wapi au ukimbilie wapi hili mpira uje kama sio kutofundishika nini?
    Na mishabiki yao kwa vile kuna kocha wakigeni ndio wanaona huyo wakumtupia lawama.watu mtasema hamkucheza timu za mtaani,hamkumbuki mtaani ukiboronga mtu unazomewa mpaka unajirekebisha.wakati umefika tukimuona mchezaji anaboronga tunamzomea na kumuimba kwa jina lake mpaka ajirekibishe sio tunawapa kichwa kwa kumlaumu maximo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 13, 2008

    Kila kocha mtaalam anayekuja kufundisha soka hapa bongo anasema kwamba tunahitaji zaidi ya miaka minne ili tufikie kwenye kiwango cha kimataifa

    Sisi wabongo kwa sababu ya kujifanya tunajua kila kitu..tunaanza kuleta ubishi wa kipuuzi..tunamtupia Maximo mzigo wa lawama kwa sababu ya uzembe wetu wenyewe , tena uzembe wa miaka mingi tu.

    Cameroon wamekuja na timu nzima yenye wachezaji kutoka ulaya..maana yake ni kwamba wachezaji hao wameweza kupata namba katika timu kubwa duniani kama vile Barcelona , St Etienne , Marselle , Liverpool , Atletico Madrid na nyingine nyingi tu..wameweza kuthibitisha ubora wao..wakati wao walipokuwa wanawaandaa kina Eto`o na Makoun , ambao sisi tunawababaikia na kuomba kupiga nao picha..sisi tulikuwa tunaendesha siasa za akina Ndolanga na wakati huo huo kina Mungai walikuwa wanapiga marufuku michezo shuleni!!.

    Maximo amekuja bongo akawakuta hawa kina Machupa, Mgosi na Gabriel ndio mastaa wetu..wachezaji ambao hawawezi kucheza mpira kwenye ligi zenye ushindani (mgosi anayepigiwa kelele kwa sasa,alishindwa kucheza mpira uarabuni!!). Maximo amekuta hakuna lolote linaloendelea kwenye timu zetu zaidi ya majungu ya kipuuzi kabisa , kila siku wanaishia kugombea uongozi wa timu zao halafu wakipewa uongozi hawafanyi lolote la maana zaidi ya kuendekeza siasa za kwenye vipindi vya michezo vya radio zetu.

    Leo hii watu wanadai kwamba eti pesa zilizotolewa na wadhamini ni nyingi sana kwa hiyo eti mafanikio lazima yaonekane!!..wachezaji wetu hawana misingi ya soka.. sasa pesa zitasaidia vipi kumbadili mchezaji wa aina hiyo?..pesa zinaweza zikasaidia vipi kumbadili Mwaikimba akawa mchezaji bora?..pesa zitasaidia vipi ikiwa Gabriel anabaki yeye na kipa zaidi ya mara moja na anakosa magoli?.

    Kwenye Copa Coca Cola ndiko tunakotakiwa kupeleka nguvu zetu zote..tupambane na viongozi wa timu za mikoa ambao bila aibu wanachomekea vijeba kwenye under 17..hizo Tshs bilioni 6.5 ambazo zimewekezwa kwenye timu ya taifa ni pesa ambazo timu kama yanga na simba walitakiwa wawe nazo!!..leo hii zinaonekana ni nyingi sana kwa sababu viongozi wa vilabu vyetu sio creative..hawana ubunifu wa kubuni miradi mikubwa..wanaishia kusajili wachezaji kutoka kwa wapinzani wa jadi ili wawakomoe..viongozi wa soka letu wamejawa na tabia ya kupenda sifa za kijinga kiasi ambacho wanashindwa kuziendeleza timu zetu.

    tuko katika kipindi cha kujenga timu kwa hiyo ni vizuri wabongo tukaacha kujidanganya eti tatizo ni kocha..kwa jinsi kiwango cha wachezaji wetu kilivyo chini , kocha yoyote mwenye hadhi ya kawaida anaweza kufundisha timu yetu ya taifa..hatuna aina ya wachezaji ambayo eti itatufanya kwa sasa tutamani kuwa na kocha bora kama Guus Hiddink, Felipe Scolari au Alex Ferguson..tusiendelee kuwadanganya wachezaji wetu kwa kuwaambia kwamba eti tatizo ni kocha na sio wao..wachezaji wanatakiwa wapambane kweli kweli ili dunia iweze kuona thamani yao..tunawavimbisha vichwa wachezaji wetu wakati wengi wao hawawezi hata kucheza daraja la nne barani ulaya!!.

    Tunajifanya tuna haraka ya mafanikio kiasi cha kufikia hatua ya kumdhalilisha kocha wa timu ya taifa..wakati vilabu vyetu havina mafanikio yoyote yale zaidi ya kuendekeza majungu na fitina.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 13, 2008

    SI MICHEZO WALA UCHUMI,TUMEKUWA TUKIFUKUZA KIVULI KWA MUDA MREFU SANA,TENA KWA MWENDO WA KONOKONO.
    NASHINDWA HATA KUENDELEA,MAANA INATIA HASIRA NA UCHUNGU VILE VILE.
    I WISH WAHUSIKA WANGEKUWA WANASOMA SAFU ZA MAONI KAMA HIZI.
    LABDA WANASOMA ILA NI KIBURI KIMEWAJAA.
    WE NEED A HUGE CHANGE IN OUR COUNTRY! YES, IN ALMOST EVERYTHING AND IT IS TIME TO TAKE RESPONSIBILITIES!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 13, 2008

    Inashangaza sana kuona mtu anayejifanya ana uchungu na kupenda kukuzwa kwa vipaji vya watoto wa bongo na soka la bongo, ndiye huyohuyo anaanzisha tawi la Liverpool ndani ya bongo.
    Fisadi ni fisadi tuu, litajificha lakini kuna siku litajifunua.....

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 13, 2008

    ASANTE KWA MJADALA HUU,TATIZO SI VILABU TU NA SERIKALI PIA IMECHANGIA KIASI KIKUBWA,KABLA YAGA KUANZISHA TIMU YA VIJANA KUTOKANA NA USHAURI WA KOCHA WAO WAKATI HUO PROFESA VICTOR,BAADAE SIMBA KIDS NAYO IAKAUNDWA TAYARI VIJANA NAO WALIKUA NA MUAMKO KUTOKANA KULIKUA NA VIWANJA VINGI VYA MICHEZO(MPIRA WAMIGUU)KARIBU KILA MAENEO,JANGWANI NDIO USISEME KABLA YA KINA ADOLPH KUJIUNGA YA NGA TAYARI WALIKUA NA TIMU YAO YA MTAANI SCOTLAND YARD,TEMEKE KULIKUA NATIMU KM EVER GREEN,KIGAMBONI SHABABY,KINONDONI WONDER BOYS ILALA P.ENGLAND NA ZINGINE NYINGI AMBAZO UWEZO WAO WAKATI HUO UWEZI ATA KUFANANISHA NA TAIFA STARS YA LEO,KULIKUA NA MWAMKO NA PIA HALI YA UCHUMI ILIKUA NEMA,LEO VIWANJA VYOTE VIUZWA KAMA VIPO NI MRADI WA CCM KULAZA MAGARI,MAISHA MAGUMU MTU ANAKIPAJI CHA TOKOMILE ATAJIPACHIKA KWENYE MPIRA KWAKUA UNALIPA ANA MJOMBA WAKE SIMBA,YANGA ATAMBEBA MPAKA STARS,TURUDISHE MICHEZO MASHULENI NA VIWANJA VYA MCHANGANI VIBORESHWE NA VIKOMBE VYA MCHANGANI VIRUDI KA ZAMANI NA HAO WAZILI WAZIFAZILI TIMU ZA MIAANI PIA KAMA KWELI NIA YAO KUINUA MPIRA NA SIO KUFUKUZIA TENDA ZA BISHARA ZAO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...