Mpeli Nsekela 'Kiongozi', ambaye ni meneja wa kilaji cha Ndovu Special Malt kinachotengenezwa na Tanzania Breweries Limited, akizungumzia udhamini wa kilaji hicho kwa kongamano ya utawala ifanyikayo kila mwezi katika ukumbi wa British Council jijini Dar








ALICHOKISEMA MPELI NSEKELA 'KIONGOZI' KUHUSU UDHAMINI WA NDOVU SPECIAL MALT WA MANAGEMENT FORUM IFANYIKAYO BRITISH COUNCIL, DAR, LEO:

"Ndovu Special Malt ina mwaka na zaidi tangu izinduliwe na toka izinduliwe imekuwa ikitangazwa kama Chaguo Makini kwa watu anaojua wanachokitaka katika maisha.

"Lakini katika tamaduni mbali mbali za binaadam vitendo vinapewa uzito zaidi kama uthibitisho wa hulka ya mtu ilivyo au uhalisi wa kitu. Kwa mfano wimbo maarufu wenye swali utajuaje mimi ni mtu wa aina fulani na kibwagizo kama jibu kisemacho matendo’. Usemi mwingine wa kiswahili unasema ‘Ada ya mja hunena, Uungwana ni vitendo’

"Ndovu Special Malt ina furaha na heshima ya kutangaza kujumuika na British Council kufanikisha vikao vya kila mwezi vifanyikavyo hapa British Council vijulikanavyo kama Management Forum.

"Ushirikiano huu ni wa udhamini na unaanza mwezi huu wa 6 na utadumu mpaka mwaka ujao. Thamani ya udhamini wa NSM ni takribani 32,000,000/=.

"Mangement Forum ni fursa ya mameneja na wadu wengine wa mabo ya uchumi kukutana na kujadili mada inayotolewa na mzungumzaji ambae ni bingwa katika eneo fulani la uchumi au menejimenti.

"Hii ni mara ya nne katika siku za hivi karibuni kwa Ndovu Special Malt kufadhili shughuli za kuwaongezea umakini na maarifa wa kijasiriamali, kiuchumi na kifedha vikundi mbali mbali.
"Mtakumbuka tarehe 14 Mei 2008 tulifadhili warsha ya kina mama ya ujasiriamali na amali (‘careers’) iliyoandaliwa na Confederation of Tanzania Industries iliyofunguliwa na Mama Salma Kikwete, at the Waterfront in Dar-Es-Salaam.
"Tarehe 22 Mei tulidhamini kongamano la Tanzania Professionals Network kuhusu karadha kwa ajili ya ujasiriamali mdogo na wa kati. Jana tulifadhili mafunzo yaliyotolewa kwa njia ya satellite kutoka Mahatt Institute Florida USA, yaliyohusu Attitude Shift Management.


"Kwa vitendo hivi vinne vya udhamini Ndovu Special Malt inaendelea kuthibitisha kwamba kweli ni Chaguo Makini kwa ajili ya watu wanaojua ni nini wanachokitaka maishani na ambao wako makini kujiongezea mbinu maarifa ya jinsi gani ya kutawala mazingira yao ili kujiletea maendeleo.

"Udhamini wetu wa Management Forum una mwanzo mzuri kwa maana unaanza na kwa kishindo na magwiji wawili wa kimataifa wa maswala ya uongozi na mageuzi katika menejimenti- Philip Goodwin and Tony Page- ambao watazungumzia: jinsi viongozi wanavyoandaa viongozi, jinsi anvyotawala mabadiliko na jinsi wanavyoweza kufanikiwa katika haya katika mazingira yanayobadilika kila wakati.

"Uhusiano wa NSM na wasomi, wanataaluma, viongozi wa makampuni wa ngazi mbali mbali na wajasiriamali ni wa kudumu na tutaendelea kuwatangazia taarifa za mwendelezo wa ushirikiano katika shughuli zingine na vikundi na mitandao mbali mbali kati yao na NSM; kwa maana NSM ni chaguo makini, hivyo NSM ni yao".

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 14, 2008

    MHE, MICHUZI,
    NIWASILISHIE HUU UJUMBE KWA KAKA MPELI. JE KAKA YAKE CHARLES NSEKELA HAJAMBO? MIE NI RAFIKI WA ZAMANI NIKO MAREKANI KWASASA NA TULIPOTEZA MAWASILIANO. SHUKRAN.
    FATMA MAHAMOUD.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...