miss tz UK 2008 tusekile mwakibinga na washindi wa pili na wa tatu. nyuma kulia ni mshereheshaji sauda simba kilumanga
Balozi mwanaidi maajar akimpongeza kimwana Tusekile Mwakibinga ambaye alitawazwa rasmi wikiendi ilopita kuwa Miss Tanzania Uk 2008 kwenye sherehe zilizofanyika ukumbi wa Silver Spoon New Light Complex karibu na wembley Stadium. Pichani Miss Tanzania Uk 2008 Tusekile Mwakibinga akiwa katika picha ya pamoja na Mshindi wa pili Jacqui Majebele(kushoto) na mshindi wa tatu Alice Kapya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 34 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 17, 2008

    Hongera Tusekile. Tunaomba kujua washindi wa tatu wamejishindia zawadi gani?. Ahsante!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 17, 2008

    Hongera dada Tuse.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 17, 2008

    mwaka huu ilipendeza, Hafsa na Banan Zorro walitumbuiza, ila kama kawaida ya waandaaji walidanganya kuwa washiriki ni 11 lakini walioparticipate walikuwa 9. Sijui kwa nini wa Tz hatuna ukweli.Mwaka jana mlim-blackmail mshiriki mmoja eti hakuwa na vigezo baada ya kumpotezea muda wake na kumtumia, Its time you need to change from uswahili and get real.Otherwise nasubiri waosha vinywa waamke ili comments zianze kuhusu mamiss wetu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 17, 2008

    Sasa nimejua mahali pa kukutana na mama balozi maana ukitaka kumpata kiofisi huwa ni haiwezekeni utadhani unaomba ajira lakini kwenye function hakosekani, Basi tutakuwa tunaandaa hizi social events ili angalau tumpe matatizo yetu kwenye hizo events maana ubalozi hauko reachable kama humfahamu mtu pale, utazungushwa weee mpaka uahirishe ukabebe box zako.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 17, 2008

    Mi nashangaa sana huyo aliyetokea wa pili kashinda vipi, kwa mwili ule kweli Lundenga waliona nini?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 17, 2008

    ni kweli kabisa hivyo asemavyo mdau wa 9:27 kwani wanaoshi ughaibuni wana hiyo shida! kumuona balozi au hata msaidizi wake ni kazi ikiuliza uaambiwa wana kazi kazi zenyewe nizipi?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 17, 2008

    Wadau! KWANINI MADEMU WAZURI HUWA WANANYIMWA VISA?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 17, 2008

    Hogera sana Kalumbu, Huku Kyela, Tukuyu tunasema Kyala akutule Tsekile

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 17, 2008

    MIE BINAFSI SIONI MAANA YA KUWA NA MISS TZ UK. KWANI KILA NCHI INATAKIWA KUTOA MREMBO MMOJA AMBAYE ATAKWENDA KUWAKILISHA NCHI YAKE KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA MISS WORLD.
    NATAMBUA KUWA WAMEJIELEZA SABABU NI RAIS KIKWETE AMESEMA UK NI KAMA MKOA, HALAFU ALOSHINDA ANAKUJA HAPA DAR KUSHINDANA KWENYE UMISS TZ.
    UK NI KAMA MKOA WA TZ. WAPI NA WAPI? WADAU NISAIDIENI HAPA. TUNA MIKOA YA NCHI YETU AMBAYO INATOA WAREMBO KAMA MISS ARUSHA, MISS MBEYA, MISS DODOMA NAKADHALIKA. NI MIKOA YA TANZANIA. UK INATOA MISS UK. NAO KUTOKA VITONGOJI VYA NDANI YA UK, KAMA MISS MANCHESTER, MISS CROYDON, NAKADHALIKA. KUMPATA MISS UK KWA UJUMLA KWENDA KUWAKILISHA UNITED KINGDOM. KWENYE KINYAN'GANYIRO CHA MISS WORLD.
    SASA KULIKONI???????????????

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 17, 2008

    Hongera.
    lakini ukweli ni kwamba nikiwa na mtoto wakike hata siku moja sintomshauri aingie kwenye mchezo huu.
    Nitamwambia 'yeye hata kama ni mzuri hana haja ya kwenda kujitembeza au kujitangaza mbele za watu kuprove she is beautiful/
    Na wazazi ambao wana mifano hii nimeona London. MARIAM KILUMANGA ana mtoto MZURIIIIII Huyooooo.
    LAKINI WALA HAKUMRUHUSU AJIINGIZE KWENYE MCHEZO HUU. Laiti agemruhusu. nawahakikishia ANGESHINDA. Ni mawazo ya kiungwana anayo huyu dada kama yangu. Hongera Mariam Kilumanga kwa kulea watoto vizuri. pamoja uko ulaya lakini unaheshim utamaduni na mila za kiafrika.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 17, 2008

    anonymous 9:27 umesema ukweli kabisa, viongozi wetu ofisini hawapatikani ila ukipiga simu kuwaomba kuja kufungua Miss au majengo ya mahali hapo watakuja bila kukosa, ila huhudimia watu waowafuta tena ofisini kwao hapo shida, tena unakutana na secretary anakuweka kwenye hold mpka unakoma kusikiliza vimuziki tu visivyo na kiitikio, halafu jibu hayupo ama yupo busy sana
    Tutaendelea kwelii watanzania, tubadilike

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 17, 2008

    Unaweze kumwona Balozi, Alhamisi ya kwanza ya mwezi,unless umejaribu kupata appointment, ukakosa..anyway just to let you know.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 17, 2008

    Kwa mamia ya vijana wa kike wa kitanzania waliopo uk kuwepo washiriki tisa tu kumenichanganya. yaani vijana wote waliopo huku na wanavyojiona na kuringa kumbe deep down wanajuwa kuwa si warembo kabisa! ha ha ha,

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 17, 2008

    We mbeba box June 17 9:27 unapeleka matatizo gani huko!? Huyo mama anashughulikia issues za Tanzania na Watanzania halisi home. Mbeba box unataka appointment naye ili useme nini? Kwamba bix zimepungua kwa sababu ya bei ya mafuta? Hizo siyo issue za balozi. Mbeba box, mind you that London is one of Tanzanian embassies zilizo-busy kabisa. Box marufuku shida za hovyo hovyo hapo!

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 17, 2008

    Hongera mrembo wa kwanza wa kinyakyusa

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 17, 2008

    wewe bumba wa 4:16 wacha ushamba wako na anza kusoma na uelewe kazi na wajibu wa balozi nchi za nje. Mtu yeyote yule anapokuwa nje ya nchi yake ubalozi wa nchi yake ndio unaokuwa nyumbani kwao. Matatizo yote ya wananchi wa balozi hiyo ni wajibu wa balozi mhusika. iwe kukamatwa mwananchi kwa kosa lolote, kutafuta jamaa wa mtu aliefariki nje ya nchi, na mengineyo yote wajibu wa ubalozi. sasa leo unakwenda ubalozini kulalamika kuwa passport yako haijarudi mwezi wa nane sasa jawabu unalopewa na ofisa ni kuwa wasiliana nyumbani, sasa kama niwasiliane mweneyewe nyumbani kuna haja gani ya kuwa na afisa wa uhamiaji hapa ubalozini? kuna haja gani ya kuripoti ubalozini unapofika nje ya nchi ikiwa hawataki kukusaidia unapofikwa na matatizo? lakini sema kuna sherehe ya kula na kunywa basi balozi, msaidizi wake na kila afisa mdogo atafika. lakini waambie kuna kifo kila mmoja anatoka dharura. Mwaka 1993 aliekuwa balozi uk wakati ule alianzisha mpango wa maafisa kutembelea wanafunzi kwenye vyuo vikuu wanavyosoma, pia kutemebelea wagonjwa walioletwa kwa serikali au binafsi as long as wameujulisha ubalozi kuwepo kwao nchini. ni mpango mzuri lakini haukudumu muda mrefu.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 17, 2008

    WE ANNON 17 5:08 ACHA USHAMBA MWENYEWE. KAMA UMEENDA HUKO NA SHIDA ZAKO ZAKO ZIKAPIGWA CHINI INA MAANA GANI? KWAMBA ISSUE ZAKO SI MUHIMU KAMA JAMAA ALIVYOSEMA PALE JUU. TATIZO KUBWA LA UK WABEBAJI KIBAO! HUWEZI JUA YUPI NI HALISI NA YUPI NI BOX. WOTE NDANI YA BOX. HUYO MAMA HANA TIME HIYO

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 17, 2008

    Problems zako Michuzi ndiyo hizo!. Kuminya comments za watu. Mimi nilitoa maoni yangu kuhusu haiba za hao warembo kwa kufananisha na hawa wetu. Wewe kwa sababu zako ukaiminya hiyo comment! Haikuwa na shida yoyote, wasi wasi wako.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 17, 2008

    wewe 11.32 unaongea pumba humu,kama maisha yamekushinda rudi africa,na haka katabia ka kutaja majina ya watu katika blog ukome kabisa

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 17, 2008

    wewe anon wa 11;27 inaoneka unawivu ndio maana unaongea bumba sasa huyo maliamu mwanawake kama akushiliki haina maana ndio anatabia nzuli ama malezi mazuli kwani huyo binti umesikia ana tabia mbaya ama ndio zenu zakibongobongo mmeshaanza

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 17, 2008

    Wewe anonymous wa 11:27am elewa kuwa nia ya kuwa na wawakilishi wa kitanzania toka kwenye miji nje ya Tanzania ni kuwapa watoto wetu wa kitanzania nafasi ya kujisikia ni watanzania na kushiriki kwenye mashindano ya miss Tanzania kama watanzania. Wakishinda huko basi wataiwakilisha Tanzania na sio nchi wanazoishi.

    Na wewe mshamba mwingine anonymous wa 11:32am kama unafikiri kulea watoto vyema ni kutowaruhusu kushiriki mashindano ya urembo kwa sababu na fikra zako finyu kuwa huo ni mchezo mbaya, basi unahitaji kurudi kwenye karne chache nyuma or fall into a coma and leave others to enjoy the revolution that women of this century have.
    Remember if a participant holds a UK or any other country citizenship then they won't qualify to participate into a Miss Tanzania pageant, hivyo ukiona watu wengine wana watoto warembo na hawa participate then there could be a reason behind that or may be binti mwenyewe hana interest hiyo.


    JK - Toronto.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 17, 2008

    NDAGA gwa kukaja !!huyo siyo mnyakyusa wa kwanza kushinda, wapo kibao walioshinda.anyway hatuhitaji kuambiwa mezani kwamba dada zetu wazuri, tehe tehe tehe !!

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 17, 2008

    Kama kawaida ya wabongo hatutaendelea kwasababu ya rushwa. Kwa kweli inasikitisha kila sehemu rushwa.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 17, 2008

    nani kasema umiss ni umalaya,wewe anon 11:27 DONT TALK STUPIDITY.huyo mwanako wa kike unaesema utamlinda asishiriki i guarantee you 95% she'll probably get pregnant under 20, and even do worse than kushiriki umiss ambao hauna ubaya wowote.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 17, 2008

    wewe pumba wa 5:47 wacha wivu na chuki kwa kuwa tu uko tanzania na kila watanzania tuliopo nje tunapolalamikia ubalozi wetu mnakuja na kasumba ovyo. kwanza mimi niko huku si kwa kubeba maboksi, nimekuja huku mwaka 1990 kabla ya mambo ya ukimbizi au uzamiaji kuanza, nimesoma huku na nafanya kazi ya uhakika. Na kabla hujaruka na vicomments vyako sikusomeshwa na serikali. Miaka yote nilioyokuwepo huku nimeona uhusiano wa balozi na watanzania kwa aina mbali mbali lakini uhusiano wa balozi wetu wa sasa ni mbaya kupita wote. Tena ujinga wa baadhi ya watu kama wewe ni kutojua madhumuni hasa ya kuwepo na balozi nchi za nje. Naona hata hakuna haja ya kujibishana nanyi kwani hamtaki kujua ukweli na kwa maoni yenu kila alo nje ni mbeba maboksi asostahili kuishi nje au kuthaminiwa na ubalozi wake.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 18, 2008

    we jk uko toronto wanasemaje wanacuf wa mzee sharif wasalimie sana, uko wana cuf na wanatoronto.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 18, 2008

    mtoto wa kinyakyusa ulifunika ule ukumbi kisawa sawa, haters hate, she was on top of the game.

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 18, 2008

    Anon wa 17/06 at 04:16pm kwanza nakushauri nenda darasani usome maana upeo mdogo kama hujui wajibu wa balozi. BALOZI ANAWAKILISHA WANANCHI WALIO NJE YA NCHI, sasa kama unasema kuwa anawalikilisha walio nyumbani kwanini awe nje ya nchimbali na walengwa? na kama anatakiwa kutuwakilisha sisi wa TZ tulio UK iweje iwe tabu kumpata? eti anapatikana alhamisi ya mwanzo ya mwezi. Hivyo nikiwa na emergency nisubiri mpaka next month, thats rubbish! Nyie mnaotetea urasimu unaoendelea ubalozini nadhani hamjapata matatizo, I had an emergency and needed to go home(TZ), my passport was yet to be changed, nilipoomba kusaidiwa ni vipi ntapata pass mpya mapema, mmoja wa vijana pale ubalozini akaniomba nitoe rushwa ili nifanyiwe chapchap! jamani rushwa hata ughaibuni. It is sad.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 18, 2008

    mimi namomba kuuliza huu umiss TZ umezidi now days does peolple have anything to do? yaani miss uk; miss tanzania mnatuchanganya mimi ndahani ingekuwa jambo la busara tungesikia nani kafanya vizuri shule keep umiss wenu for yourselves kwani ukishakuwa miss then what watanzania tumezidi is about time tuamke na tuangalie maendeleo i will appreciate nikasikia watanzania wa UK wametoa vyandarua vya mbu 100 hospital ya muhimbili watu wanakaufa na malaria na wengine wankazana na u miss tumechoka na hao ma miss ni bora tutoe misaada nyumbani kuliko kupoteza hela kuungalia na mzuri kama mzuri mleni basi ---
    mdau-USA

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 18, 2008

    We annon 17. 11:16 acha kuweweseka! Umeenda UK 1990 na hujarudi maana yake unabeba box! Au hujui mbeba box ni nani? Ni mtu yoyote anayevamia nchi ya wengine na kujipendekeza kufanya kazi yoyote. Wewe kama ulienda 90 na hujarudi, unafanya nini huko? Ni raia wewe huko?

    Pili, kama Balozi alikupiga chini kukuona ujeu kuwa huna umuhimu wowote. Kama definition zako ni kuwa ubalozi lazima uwe na wajibu wa kusikiliza hoja na problem zako na ubalozi umekataa, sasa unaweweseka nini?! Rudi bongo wewe.

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 18, 2008

    Wewe jinga la june 18 8:04 kwanza hiyo sio maana ya ya wabeba box kama inavyotumiwa na watu tele hata katika ukumbi huu. Na wapi nilisema kama sijarudi nyumbani? nimesema nimekuja huku mwaka 1990 na kuwepo nje ya nchi sio lazima uwe raia wa nchi hiyo uliyopo, kuna watu wako huku toka 1972 na bado wana passport za kitanzania na ni raia wa kitanzania, tunaishi na kufanya kazi nje ya nchi wa sababu tumepata ruhusa kihalali kukaa na kufanya kazi. (hata pale ubalozini wape wafanyakazi wa kawaida wanaishi huku toka miaka ya 80 na ni watanzania)
    Ni watu kama wewe wenye roho mbaya na wasiowapendela wenziwao mema, walojaa wivu na chuki zisizo na sababu yeyote ile ndio wanaotuletea ukorofi.
    Sasa wewe kama tatizo langu ni passport na ambayo ubalozi ndio nilipopeleka maombi yangu unataka nisilalamike?
    Tena wewe unaonyesha ikili zako ni finyu hukumbuki sio muda mrefu kulikuwa na mjadala kwa nini watanzania hawaripoti kwenye balozi wanapokuwa nje ya nchi? sasa kuna haja gani ya kuripoti kama balozi anakataa kuwaona mnapokuwa na malalamiko yanayohusu masuali ambayo hushuhulikiwa na ubalozi wake? Ni mwisho wangu kwenye mjadala huu, maana kuna watu walivyo na roho mbaya na chuki hata ubongo wao hupata nafasi ya kufikiri kabla ya kuropoka ovyo.

    ReplyDelete
  32. AnonymousJune 18, 2008

    Annon June 18, 2;20 bora iwe mwisho wako wa mjadala! Utakoma. Beba box tu. Iweje wewe pekee ukataliwe ku-renew passpart wakati wenzako tuna-renew kirahisi tu hapo?! Balozi na wafanyakazi wengine hapo Embassy wanajua yupi ni yupi. Wenzako walijaribu hata ku-foul mheshiwa Rais alipokuja hapa UK kwamba wanakataliwa passport mpya. Mnachana na kukataa uraia wenu mnategemea nini?! Nahisi na wewe ni mmojawapo. Ukishagundua box halina mpango unataka appointment ya BALOZI?!!That is crazy!

    Hamna mtu mwenye wivu na chuki ya box. Ni ajabu kama unaona box ni deal na kujiona unaonewa wivu! Mtu wa ajabu sana weye! Wenzako tunapiga deal mkupuo. Siyo box zako tokea miaka ya tisini mwanzoni. Pole sana.

    Zaidi zaidi, Box ndo maana yake na habari ndo hiyo!. Kama ulikuwa hujui maana yake!. Sisi ndo waanzilishi ha hiyo terminology. Beba box tu.

    Ndo maana ukaambiwa Balozi hana time ya appointment na wewe.

    Enjoy box lako. Sasa utalijua jiji na passport yako iliyo-expire!

    ReplyDelete
  33. AnonymousJune 20, 2008

    wewe msemaji wa june 18 saa 7:12 kwanza hongera sana kwa kuwa muanzilishaji wa msemo beba boksi, watu wanajisifia ya maana wewe unajivuna neno hata faida halina. pili wacha kutudanganya hapa unadhani wote hapa ni watoto wadogo? ubalozi hawajui yupi ni yupi kabisa! hawana uwezo wala resources za kuweza kujua hayo, na ndio maana wakashindwa hata kujua ni watanzania wangapi wapo hapa uk. huyo jamaa anaesema passport yake mpaka leo hajaipata kama anatokea zanzibar hilo sio ajabu kwani wazanzibari wengi walio nje wanatatizwa na uhamiaji zanzibar, kule zanzibar wana sababu zo lakini zi za msingi ila ni ubaguzi wao wenyewe.

    ReplyDelete
  34. AnonymousJune 20, 2008

    Nimerudi tena, naona michuzi hakuweka comments zangu za awali, sitorudia niliyoyasema ila namshauri huyu jamaa mwenye matatizo passport yake, ikiwa unatokea zanzibar basi tatizo liko zanzibar, wazanzibari wengi nchi mbali mbali wamo katika tatizo hilo na wanalalamika ile mbaya, balozi hawezi kukusaidia kwa suali hili kwani wao wenye (mabalozi waliopo nchi mbali mbali) hawapati majibu kutoka uhamiaji zanzibar, wote wanawashauri watu wawatumie ndugu na jamaa zao waliopo byumbani kuwafuatilia masuali ya passport zao. Pia kama passport yako ya mwisho ulibadilisha ukiwa nje ya nchi (yaani kutoka lilie buku kubwa kuja dogo) basi ndio kabisa watakuletea nyimbo tele, haileweki ni kwa nini ila wanawapa wenziwao homa za bure, urahisi ni jamaa zako waende uhamiaji WAZUNGUMZE mambo yanakwisha haraka. ikiwa umetokea bara na bado hujapata passport yako kwa muda mkubwa hapo sijui lilisibu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...