bosi wa migahawa ya break point daudi machumu akisimamia ukarabati wa sakafu ya kusakatia rhumba katika ukumbi wa break point ya mjini (zamani posta club, usoni pa billicanas) ili mambo yawe mswano kila ijumaa wakati inafrika band wanapopiga kuanzia saa 12 jioni hadi usiku wa manane.
msosi wa nguvu wa vyakula vya kiasili (brenda fassie, kichuri, vibambala, upuuzi wa mfalme, makange, magege, kambale satto bila kusahau mbojhu na senene) na vilaji si vya kuuliza maana ni jadi ya break point iwe ya kijitonyama, udassa ama ifm restaurant ama buffet park nairobi kwa watani wa jadi na matongee ya mjini ya a-taun, kwa gado wa reading ya ukerewe na la kairo mwanza na pia guangdzhou break point, china - hii yote itakuwa ni kama ulikuwa hujui yote hiyo ni katika mnyororo wa migahawa ya break point...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 06, 2008

    ha..ha..ha Michuzi we kiboko! Huu "upuuzi wa mfalme" ndio msosi gani? Ebu tufahamishe tusije kwenda Break Point na kufanya order kisha kukashindwa kula!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 06, 2008

    kaka Michuzi una hisa hapa nini au hao jamaa ndiyo wanaotufanya tujadiane bure humu? Jamaaa umewafagilia sana na siyo mara ya kwanza kuona jinsi unavyowaosha hawa jamaa na migahawa yao katika hii blog. teheee!!! teheee!!! teheee!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 07, 2008

    Acha jamaa apete maana he is hard working and committed. Wenye wivu mjinyonge. Katoka na "Upuuzi wa Mfalme" sasa subirini "Ujinga wa Sultani".

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...