mkuu wa itifaki wa kamati ya miss tz albert makoye akikagua gwaride la warembo wa vodacom miss tz 2008. mrembo mpya atayemrithi miss tz 2007 richa adhia atapatikana agosti 2, 2008 kwenye viwanja vya leaders club, kinondoni, dar ambapo wadau watalipa sh. 80,000 kiingilio

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 24, 2008

    Jamani hiyo elfu 80 ya kiingilio ni ya VIP au ndo ya wananchi wote kwa ujumla??

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 24, 2008

    Hivi huyo Albert Makoye anakagua gwaride au anachagua ni msichana gani amtongoze?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 24, 2008

    Jamani swali makoye bado ana ile travel agents nataka niwasiliane nae ili nichukue ticket.michuzi nishtue basi

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 24, 2008

    Elfu 80 Tshs, halafu ni Leaders Club, wajameni ni nini hasa, halafu hiyo pesa inaenda wapi? Charity au? maana kuna Sponsers kina Voda nao wanatoa pesa vile vile.... tutafika kweli?? Halafu mnasema bongo TAMBARALE.....

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 24, 2008

    watoto wazuuuuri.nawatakia kila la heri na mshindi wa dunia atoke bongo.aunt tina bgham

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 24, 2008

    anko makoye kashachagua wake tayari,anakaguchulia bazazi wenzake

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 24, 2008

    Weye anon wa pili unaongea kinyume. Hebu waangalie hao wasichana kutoa hao wa nne wa mbele, hao nyuma wanaofuata wanamwambia nini huyo baba wa watu hapoooo? usimsingizie Makoye waangalie hao wadogo zako wanavyojitahidi kumtia majaribuni, baba wa watu hata kuwaangalia hawaangalii anaogopa anajitahidi amalize zoezi akakae apumzike lol!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 24, 2008

    Nyie mabinti hongereni sana kwa hiyo hatua mlipofikia.Ushauri wangu kwenu ni kwamba haya mashindano ni zaidi ya Urembo,jitahidini sana mzidi kujielimisha kupitia vitabu,internet,vijarida,Tvs,radios, blogs,n.k mnaweza kupata habari za kuwawezesha kujiamini kujibu maswali yenu ambayo mwaweza ulizwa huko mbeleni.Dada zetu mnatuangusha kwenye kujibu maswali jamani!Mfano unaweza kuulizwa swali dogo tu kama."unawezaje kuzungumzia mabadiliko ya hali ya hewa yanayoendelea kutokea hapa duniani"(Global climate changes)ukaanza kujikanyaga kwa sababu magazeti husomi,TV hauangalii,Radio hausikilizi,kwenye website hauingii.Pliiz Ladies

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 24, 2008

    i don kno its been longtime but off all places leaders...?mashindano yana hadhi ya kimataifa fanyeni sehemu zenye hadhi basi na hiyo 80,000 isije ikawa kama mambo ya columbus kwenye warehouse...manalazimisha kutengeneza profit

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 24, 2008

    Jamani mbona tanzania na yenyewe mnataka kuifanya kama zimbabwe kipi hasa kigeni yaani mtu kiingilio ulipe shs 80,000/= sasa hizo ni shilling za kitanzania au za kizimbabwe na pia kiingilio hicho ni cha siku moja tu mtu ulipe hiyo hela sasa labda mnamahesabu yenu maana sio kawaida kabisa yaani labda kama unakwenda unapewa na vitu vifuatavyo unaondoka na mlembo mmoja....unapewa guest ya kulala week nzima...unapewa chakula cha kula week nzima na unapewa gali la kutembelea ndio hiyo gharama ya hizo hela alafu wanadhani watu wanachuma hela watu wanakufa na maisha alafu mnaona rahisi kuzitaja hizo hela alafu pia ukumbi wenyewe huo mliotaja kweli maisha kitendawili maana kama mimi hata kukanyaga sikanyagi bora hizo hela nikawape watoto yatima zoteeeee

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 24, 2008

    Makoye ni msanii huyo,anaangalia demu wa kutongoza na hakawii kupitia angalau wawili - hadi watano nina uhakika,ila sasa ndio fani ya urembo TZ bado ina safari ndefu kufikia mafanikio kwa sababu warembo wako radhi "kuuza mwili" kuliko sifa walizo nazo!!

    kuna mambo mengi mabaya yanayoendelea kuhusu hawa warembo na viongozi pia wale wanaojiita "Mapedeshee"

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 24, 2008

    Bora niowe retired prostitute kuliko hao 20zomezing. maaana wakitoka hapo wanakuwa wameshazibuka, wanajiona nao superstars, wanaishia mitaa ya posta, kwao wanatoka mapemaaa kupita wakitega watu... nasema 20 ZOMEZING sio mchezo.. kwani mara zote wanawaza ZOMEZING.

    lakini watoto wanapendeza we acha tu.

    G7
    UK

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 24, 2008

    mbona huyo anayejiita David Villa sijamuelewa vizuri??
    inakuwa anajiita jina la kiume halafu maelezo yake yanakuwa ni ya kike??

    Kazi Mbaya

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 24, 2008

    hivi huyo anayejiita David Villa mbona simuelewi?
    inakuwaje anatoa maelezo ya kike??

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 24, 2008

    Jamani huyu si ndiye Makoye aliyekuwa ATC-Mwanza kwenye miaka ya 80-89..akituuzia ticketi za kuja Dar .(student fare) wakati tuko Lake secondary ...Eee bwana kama ni yeye jamaa hazeeki mie ninamjua nikiwa mtoto mdogo mpaka leo yuko hivyo..kweli huo ni mpingo asilia..
    Na ninavyo mjua lazima jamaa avute mmoja...maana alikuwa kiwembe pale 7floor mwanza hoteli disco la jumamosi ..kweli tumetoka mbali..
    Good luck..
    Doctor...

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 25, 2008

    Eeeehhh hii kali watanzania wenzangu emu nichamulieni hiii
    commitee ya miss. tanzania hamna mwanamke hata mmoja??

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 25, 2008

    Sorry, Tenende ni yupi wewe?? maana kuna dingi mmoja alikuwa anaitwa Tenende pale Mafinga -Iringa unamjua?Marehemu baba yangu alikuwa rafiki sana na huyo mzee!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...