SIMBA WAKIWATANIA YANGA JANA NESHNO. TEMBELEA TOVUTI YA DAILY NEWS www.dailynews-tsn.com AMBAYO LEO IMEANZA RASMI KUTOKA HABARI KWA VIDEO IKIWA NI YA KWANZA KABISA KATIKA HISTORIA YA TOVUTI ZA HABARI ZA BONGO


KLABU ya Yanga imefungiwa kushiriki michuano inayoandaliwa Shirikisho la vyama vya soka vya nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) kwa miaka mitatu sambamba na kupigwa faini dola za Kimarekani 35,000 kutokana na kugomea mchezo wa kuwania nafasi ya mshindi wa tatu ya michuano ya kombe la Kagame.


Akitangaza uamuzi huo uliofikiwa na kikao cha kamati ya uendeshaji wa michuano hiyo ya Kagame jana usiku mara baada ya michuano hiyo kukamilika, Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicolas Musonye alisema mbali na adhabu hiyo ya kufungiwa pia Yanga imepigwa faini hiyo ambayo inatakiwa kulipwa katika kipindi kifupi iwezekanavyo.


Musonye ambaye alikuwa akizungumza huku akionyeshwa kukerwa mno na kitendo hicho cha Yanga kugomea mchezo huo, alisema jambo walilofanya Yanga ni kitendo cha aibu na ndio maana wameamua kuchukua hatua hiyo ili iwe onyo na fundisho kwa timu nyingine.



"Adhabu hii haina suala la kukata rufaa na adhabu hiyo itakuwa ikitekelezwa pale tu Yanga itakapokuwa imefuzu kucheza michuano ya Cecafa na endapo hatalipa faini yake iliyotozwa haitoshiriki michuano yoyote ile ya Cecafa hadi ilipe faini hiyo" alisema Musonye.


Musonya aliongeza kuwa wao kama Cecafa wameliomba pia Shirikisho la soka Tanzania ambao ndio walikuwa wenyeji wa michuano hiyo ya Kagame kwa mwaka huu kuichukulia hatua Yanga kutokana na utovu huo wa nidhamu iliyoonyesha.


Aidha Musonye alisema pamoja na kuwapa adhabu hizo mbili pia italiandikia Shirikisho la soka la Afrika (CAF) kuielezea juu ya kitendo hicho cha utovu wa nidhamu kilichofanywa na klabu ya Yanga ili kuonyesha ni jinsi gani timu hiyo haina nidhamu.


"Unajua kitendo walichofanya Yanga kinaonyesha upambavu wa viongozi wa klabu hiyo na kwa kweli wana bahati sana mimi si kiongozi wa soka hapa la sivyo ningewafungia maisha" Musonye alisema.


Musonye aliongeza kuwa uongozi wa Yanga mbovu wa Yanga umeiletea hasara Cecafa na TFF kwa sababu ya uamuzi wa viongozi wachache wa klabu hiyo na wasipoangalia klabu hiyo ina hatari ya kuporomoka kabisa katika soka.


Aidha Musonye alikanusha kuwepo makubaliano ya aina yoyote kati ya Cecafa, TFF na klabu za Simba na Yanga za kupeana fedha kama ilivyodaiwa na viongozi wa Yanga na kusema huo ni uongo wa mwaka kwani kanuni za Cecafa zinajulikana wazi kabisa kuwa hakuna suala la timu kupewa mgao wa mechi na timu zote zinatambua hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 28, 2008

    safi kabisa cecafa,naona miaka mitatu mbona kiduchu yakhee hao wangekula mvua tano ingekuwa mwake sana,na nyie tff msilete ZENU tunataka kuona na nyinyi mnachukua action,hawa wametuaibisha sana wanaleta mambo ya mtu kushauriana na mke wake NYUMBANI KWAKE kisha anakuja hatupeleki timu uwanjani,kwani timu ya baba ako.PUMBAFU KABISA WAMENIKERA KWELIKWELI

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 28, 2008

    TFF iwafungie viongozi wote waliohusika kutokuendesha shughuli zote za kimichezo kwa miaka mitano with immediate effect!!

    Mimi Yanga sana ila hawa jamaa wamenikera kwelikweli!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 28, 2008

    Kwa kweli hata mimi nimekereka sana na hatua ya Klabu ya Yanga kutoingia uwanjani hasa katika mashindano ya kimataifa... kweli hii ni aibu ya mwaka kwa klabu, na kwa uongozi mzima wa Yanga.... du.. yaani nchi yangu Tanzania naisikitikia sana.. ubabaishaji kila mahali.. kuanzia EPA hadi michezoni!!!!!!!!Basi nimeghairi, sirudi tena bongo.. bora niendelee kula boxiz huku Uswazini!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 28, 2008

    Wangefungiwa na ndani ya nchi nyau hawa.Wapuuzi sana wametuabisha sana wanayanga.Ndio makosa ya kuwa tegemezi.Kupokea amri kutoka kwa tajiri bila kutafakari.Tumechagua viongozi wanini???

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 28, 2008

    Yanga is a national institution
    You cant destroy an institution because of some unfortunate and misguided judgements of some individuals.Kama madhambi makubwa yamefanyika kwa upumbavu wa viongozi inabidi wao wasulubishwe. I dont know the legallity of the action and fine imposed but to me its excessive and could not justify an attempt to destroy the club. Yanga has history, Yanga has had a momentum in Tanzania and facts have to be recognised.Those football officials sound vindictive give them a chance

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 28, 2008

    Michuzi leo kulikoni, kuna habari nimezipata usiku huu kuhusiana na mbunge Chacha Wangwe, naomba tuletee uthibitisho mkuu, maana naona mpaka dakika hii kimya na wakati sio kawaida yako mkuu, au upo kwenye pombe nini? kumbuka wewe ni ustadh!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 28, 2008

    Safi sana cecafa na tunasubiri tff kwani kuna kundi wa shabiki wasoka tumeshatuma barua nzito kwa FiFa kulifuatilia hili swala na kuakikisha wamepewa hadhabu kubwa kuliko kwani wanarudisha nyuma soka letu na kukatisha tamaa wadhamini wamchezo huu ambao tunafanya juhudi kuukuza.ndio maana kaka michuzi kaona bora aanzishe tawi la bwawa la maini.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 28, 2008

    Michuzi Breking Nyuuzzzzzzzzzzz!
    M-bunge Chacha Wangwe wa Chadema amefariki dunia usiku huu kwa ajali ya gari Toyota Corola huko Dodoma!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 29, 2008

    Mimi ni Shabiki wa Yanga naishi USA
    Ni aibu kwa viongozi wa Yanga kufanya kitendo hichi hawa ndio watu wanaoua Soccer back home --- how long this clubs (Yanga na Simba) being run by people without sense? tunaitaji vijana waliosoma
    wanajali pesa na sio maendeleo kimpira... shame on them... shame

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 29, 2008

    Ni aibu kwa viongozi wanaopenda pesa -- wanashusha mpira back home
    mimi ni shabiki wa Yanga naishi NY

    We really need change of leadership; this is shame leadership without a common sense
    Tutafika kweli????

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 29, 2008

    Sawa kabisa CECAFA, ili kuwepo na maendeleo ya soka katika ukanda wetu wa afrika mashariki na kati, na kusini mwa jangwa la sahara. Maamuzi kama haya ni muhimu sana, Yanga wameliletea Taifa la Tanzania aibu kubwa sana, pia wamemkosea adabu Rais Paul Kageme wa Rwanda kwa maana shindano hili limechukuwa jina lake. na hili pia litaathiri sana mipango ya muda mrefu ya uwekezaji katika soka la Tanzania.

    TFF na Serikali inabidi isimame kidete kuona upuuzi wa Viongozi wa Yanga hauenei katika mipango yao ya muda mrefu. ni muda mrefu sana umepita tangu tusikie tabia ya Timu kususia michezo husika na hii baada ya kucheza michezo ya awali.

    Pia serikali kupitia wizara husika itoe tamko rasmi la kulaani upuuzi huu, kwa niaba ya Watanzania wote. Yanga ni Meli kubwa isiyokuwa na Nahodha.. Tambwe Leya!.. ni jina la kitabu alichokiandika wakati wa uhai wake.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 29, 2008

    Chonde chonde wachangiaji mnaodai Yanga imelitilia aibu taifa. Yanga imejitilia aibu yenyewe peke yake. Wazee wa Msimbazi tunazidi kuzoa sifa maana haijapata kutokea duniani kwa timu inayojiita hasimu wa timu nyingine kutoka baruti. Muziki wa Msimbazi unatisha, japo sio wa usajili wa hela nyingi. Haya mambo ya kujitia eti mnaweza kucheza na Simba siku yoyote kasoro siku mliyopangiwa kucheza mechi nayo hatutaki kuyasikia. Simba ni hodari kwa soka la kitabuni, Yanga ni hodari kwa soka la magazetini.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 29, 2008

    ze fulanas hata mimi naungana na wadau kupinga vikali hatua ya Yeboyebo kula kona namna hii hatutafika mbali soka yetu itabaki kua blaablaa tu, Ron tuwasiliane bwana longtime NY!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 29, 2008

    Naona ni uwajibikaji mzuri wa cacafa, na tff nao wafuate nyayo. Sijui adhabu hiyo imeyolewa kwa kipengele gani, ila nimefurahi tuu kwamba suala kama hili halikunyamaziwa kimya. Cecafa au tff wangekaa kimya, basi ksho au keshokutwa timu nyingine ingefanya hivyo hivyo. Yanga ni timu kubwa na yenye heshima kwa Tz, ila kitendo walichofanya ni cha aibu, ni mambo yaliyopitwa na wakati. Wahusika sijui walifikiria nini kuamua uamuzi kama ule, maamuzi haya yanarudisha maendeleo ya soka nyuma kwa Tz. Hongera Cecafa, natumai tff mtafuata mfano huo, adhabu ni adhabu, haijali ukubwa wala udogo, muhimu ni kwamba wahusika wapate fundisha siku nyingine wao au wengine wasirudie kufanya tena kitendo kama hicho.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 29, 2008

    Hii balaa, hivi unakuwa na mwenyekiti wa klabu kama ya Yanga aliyekwenda shule na wakili, halafu unaona maamuzi yake yanakuwa ya hovyo kabisa kuliko maamuzi ya viongozi wengine waliopita. Ni aibu sana, nadahni klabu kama hiyo inahitaji kiongozi mwenye busara na wala si lazima awe ameenda shule kama Imani Madega.
    Wazee wa Yanga kaeni chini mzungumze juu ya hili kwani Yanga tayari imekwisha poteza mwelekeo.
    Imani Madega tafadhali jiondoe katika uongozi kwani umetia aibu klabu ya Yanga na wanayanga wote.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 29, 2008

    kwendeni zenu hukoo nyie wote mnaoisakama yanga kwa makosa mbayo yamelElewa na FAT mpaka sasa TFF huko nyuma kama nyie ni wafuatiliaji wazuri mtakumbuka sio mara ya kwanza kwa timu zetu kugoma kutia timu uwanjani au kugomea kuendelea kucheza kwa hiyo ndio hasara yake sasa!! kama mnakumbuka simba iligoma kuingiza timu uwanjani mara 2 zidi ya yanga mara ya pili simba walitoa timu kipindi cha pili!!! sikumbuki kama kulikuwa na adhabu ya uhakika iliyotolewa. TFF ijifunze sasa kwa makosa haya zimezidi mno kuzitegemea timu za simba na yanga kuendesha ligi ndio maana wanashindwa kuzipa adhabu zinazostahili

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 29, 2008

    kuna mdau mmoja amenikera hapo juu.Yanga ni timu kama timu zingine mfano Tusker even URA.Sasa CECAFA wamsikilize yanga kwani yeye anatofauti gani ktk mashindano hayo timu zingine?Kama hela alikuwa anahitaji angejitoa kabla ya mashindano hayajaanza kama ethiopia.Vile vile baada ya kutoka ratibu nafikiri kila timu hupewa pamoja na masharti ya mashindano ikijumuisha fedha za kujikimu watakazopewa wa wadhamini.Hayo ni mawazo duni ya viongozi wa yanga waliokaa pale kwa maslahi yao.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 29, 2008

    Ronshuma (NY) mshkaji una kiingereza kibaya..

    ..it's just AWFUL, man

    ..drop it!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...