Wanachama na Wazalendo wa TPN,
Mkutano Mkuu wa TPN umependekezwa ufanyike Tarehe 31-08-2008.
Tunatoa wito kwenu nyote tuanzee kujiandaa kwa mkutano huo. Na pia napenda kuwakumbushia kuwa ni jambo jema kama inawezekana kutoa michango ya uanachama na kwa wale ambao walitoa ahadi katika Fund Raising Dinner ya 2007 ni vizuri wakaiikamilisha.
Kuna mengi ya kuongea na kujadili pia kuna changamoto nyingi tumepewa na wanachama na wapenzi wa TPN.
Huenda tukafanya mabadiliko makubwa sana ya kikatiba na kiuongozi na hata Structure ya TPN.
Tunapenda wote mjiandae kwa hayo na kushiriki kikamilifu. Katika kipindi hiki, kumejitokeza wanachama ambao ni wakereketwa sana na wana hamu ya kuona TPN ikileta mabadiliko ya kweli.
Tunapenda kuwakaribisha kutoa maoni yenu ya kuboresha au mengineyo katika link ifuatayo:
Maoni yote ya kuboresha yatafanyiwa kazi kwa faida yet sote.
Wasalaam wenu
Tanzania Professionals Network
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...