Michuzi,
Mimi kaka naomba unitangazie kuwa ninahitaji kukunua gari toka Uingereza na kulipeleka Tanzania.
Ttatizo sijui nianzie wapi na niishie wapi , nikiwa namaana kampuni gani au mdau yupi aweza kunisaidia kufanikisha ikiwa ni pammoja na ununuzi bila kusahau usafirishaji.
Nitashukuru saana kwa msaada huo.
Aliyetayari kutoa msaada aweza kuwasiliana na mimi kwa mail hii
au akaweza wazi kwenye globu hii ya jamii ili hata kama kuna wengine waweze kufahamu.
Ahsante sana.
Mdau Makanzo
Kama una mtu unayemfahamu mwaminifu yuko UINGEREZA unaweza kupata gari tena zuri sana kwa bei nafuu na imara, mimi nipo hapa LONDON lakini niko busy kidogo nisikudanganye ningweza kukusaidia kuna website lakini hii ni kwa ajili ya local market inafaa kama unamfahamu mtu huku akakununulia akakuletea, kwanimara nyingi wanaotangaza kwenye web hii hawataki usumbufu wa mtu wa nje kwani mambo ya kutafuta kampuni ya kusafirisha na mambo kama hawataki ni kwa ajili ya local market tu, hivyo jitahidi kumpata mtu unayemfahamu mwaminifu akununulie na akutumie, mimi mwaka 2005 nilinunua gari zuri tu kwa £1400 usafiri ulikuwa £1800 kwa vili niliweka kwenye container na vyombo vingine, kama empty s container waliniambia £900 mwaka huo. SASA NAKUPA WEBSITE NI HII http://www.autotrader.co.uk utaona kila aina ya magari kwenye web hii, kuifungua tumia google.com
ReplyDeleteASANTE NA MUNGU AKUBARIKI UFANIKIWE.
Watu wanawaumizeni tu huko huku magari ni bei poa sana, niliona NISSAN MISTRAL 2.5L MZUNGU ANAUZA £1000. AMENUNUA GARI INGINE HIYO HAITAKI TENA UKIINGALIA NI KAMA MPYA, KISA HANA MAHALI PA KUI-PARK. NA GARI KAMA HIYO HIYO SHEMEJI YANU DAR ALINUNUA
ReplyDeleteTHS 17,000,000.00 PALE KINONDONI KWA MWARABU HUU NI WIZI HIZO NI KAMA £7500. MIMI NI YULE YULE NILIYOKULETEA MAELEZO HAPO WALI ASANTE.
wewe, usiyeelewa huyu mtu kaomba kusaidiwa jinsi ya kununua gari uk hajalalamika kuuziwa gari kwa bei mbaya mbona unarukia topic isiyohitajika?
ReplyDeleteNdugu yangu makanzo wasiliana na freightswift au tzuk ndio wanaotuma magari na ushauri watakupa jinsi gani ununue. All the best
Mimi nakushauri uje mwenyewe huku (kaa kwa washikaji-natumaini unao) na uchague gari unalolipenda. Mambo ya kumpa mtu hela au kununua kupitia kwenye mtandao (online) ni kujitafutia matatizo mengi.
ReplyDeleteNimejaribu kukutumia email lakini imekataa kwa hiyo cha kufanya nitumie email yangu ni nasriya@hotmail.co.uk,nitakufahamisha na nakuhakikishia utapata kwa bei nzuri tu.Au njia ya mkato ukinitumia email niandikie no yako ya simu nitakufahamisha.
ReplyDeleteJaribu kuangalia kwanza mwenyewe kwenye http://www.autotrader.co.uk usiingie kichwa kichwa wanaweza "wakakukunywa"... Tumia postcode yoyote ya UK
ReplyDeleteMakanzo chabooooooooooo kuibiwa ndio huko take care kaka usitoe pesa kwa nia yakununuliwa gari namtu usiyemfahamu.
ReplyDeleteAl-Musoma..
ReplyDeleteMdau anafahamu POST CODE ni nini?
WASILIANA NA KAMPUNI MOJA YA MTANZANINIA INAITWA VIVIENNE UK LTD, HUYO JAMAA ANADILI NA KITU CHOCHOTE KUTOKA UK.
ReplyDeleteEmail yao ni 'vivienneukltd@aim.com'
Babuu..... magari hapa bongo jamani yamezidi mno, Hatujui hata tupite wapi. We kaka tafadhali nunua hayahaya yaliyopo humu nchini tayari. Foleni, Pollution imezidi.
ReplyDeleteUSINUNUWE GARI KUPITIA KAMPUNI YOYOTE HAO WOTE, WANAUMIZA WATU TU, KAMA NILIVYOKUAMBIA HAPO AWALI JUU KAMA UNA MTU MWAMINIFU MUULIZIA ATAKUSAIDIA, ACHANA NA HAO WANASEMA KUNA KAMPUNI YA MTANZANIA BLA BLA BLA KAMA HIVYO NI BORA BASI UKANUNUA HAPO HAPO BONGO, OF COURSE WHEN SOMEBODY WANTS TO BUY SOMETHING ONE OF THE FACTORS TO LOOK AT IS PRICE, HIVYO BEI NI TOPIC INAYOHITAJIKA, ACHANA NA HIVYO VIJIKAMPUNI UCHWALA. UNGEWEZA KUJA MWENYEWE LAKINI SIDHANI KAMA UNAWEZA KUPATA VISA KWA KUJA KUNUNUA GARI USED!!! OTHERWISE HIYO VISA IWE YA KUJA KUMTEMELEA MTU ALIYEKULETEA MWALIKO THEN UKAUNGANISHA NA MAMBO YAKO.
ReplyDelete