Michuzi,
Mimi kaka naomba unitangazie kuwa ninahitaji kukunua gari toka Uingereza na kulipeleka Tanzania.
Ttatizo sijui nianzie wapi na niishie wapi , nikiwa namaana kampuni gani au mdau yupi aweza kunisaidia kufanikisha ikiwa ni pammoja na ununuzi bila kusahau usafirishaji.
Nitashukuru saana kwa msaada huo.
Aliyetayari kutoa msaada aweza kuwasiliana na mimi kwa mail hii
au akaweza wazi kwenye globu hii ya jamii ili hata kama kuna wengine waweze kufahamu.
Ahsante sana.
Mdau Makanzo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 29, 2008

    Kama una mtu unayemfahamu mwaminifu yuko UINGEREZA unaweza kupata gari tena zuri sana kwa bei nafuu na imara, mimi nipo hapa LONDON lakini niko busy kidogo nisikudanganye ningweza kukusaidia kuna website lakini hii ni kwa ajili ya local market inafaa kama unamfahamu mtu huku akakununulia akakuletea, kwanimara nyingi wanaotangaza kwenye web hii hawataki usumbufu wa mtu wa nje kwani mambo ya kutafuta kampuni ya kusafirisha na mambo kama hawataki ni kwa ajili ya local market tu, hivyo jitahidi kumpata mtu unayemfahamu mwaminifu akununulie na akutumie, mimi mwaka 2005 nilinunua gari zuri tu kwa £1400 usafiri ulikuwa £1800 kwa vili niliweka kwenye container na vyombo vingine, kama empty s container waliniambia £900 mwaka huo. SASA NAKUPA WEBSITE NI HII http://www.autotrader.co.uk utaona kila aina ya magari kwenye web hii, kuifungua tumia google.com
    ASANTE NA MUNGU AKUBARIKI UFANIKIWE.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 29, 2008

    Watu wanawaumizeni tu huko huku magari ni bei poa sana, niliona NISSAN MISTRAL 2.5L MZUNGU ANAUZA £1000. AMENUNUA GARI INGINE HIYO HAITAKI TENA UKIINGALIA NI KAMA MPYA, KISA HANA MAHALI PA KUI-PARK. NA GARI KAMA HIYO HIYO SHEMEJI YANU DAR ALINUNUA
    THS 17,000,000.00 PALE KINONDONI KWA MWARABU HUU NI WIZI HIZO NI KAMA £7500. MIMI NI YULE YULE NILIYOKULETEA MAELEZO HAPO WALI ASANTE.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 29, 2008

    wewe, usiyeelewa huyu mtu kaomba kusaidiwa jinsi ya kununua gari uk hajalalamika kuuziwa gari kwa bei mbaya mbona unarukia topic isiyohitajika?
    Ndugu yangu makanzo wasiliana na freightswift au tzuk ndio wanaotuma magari na ushauri watakupa jinsi gani ununue. All the best

    ReplyDelete
  4. Mimi nakushauri uje mwenyewe huku (kaa kwa washikaji-natumaini unao) na uchague gari unalolipenda. Mambo ya kumpa mtu hela au kununua kupitia kwenye mtandao (online) ni kujitafutia matatizo mengi.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 29, 2008

    Nimejaribu kukutumia email lakini imekataa kwa hiyo cha kufanya nitumie email yangu ni nasriya@hotmail.co.uk,nitakufahamisha na nakuhakikishia utapata kwa bei nzuri tu.Au njia ya mkato ukinitumia email niandikie no yako ya simu nitakufahamisha.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 29, 2008

    Jaribu kuangalia kwanza mwenyewe kwenye http://www.autotrader.co.uk usiingie kichwa kichwa wanaweza "wakakukunywa"... Tumia postcode yoyote ya UK

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 29, 2008

    Makanzo chabooooooooooo kuibiwa ndio huko take care kaka usitoe pesa kwa nia yakununuliwa gari namtu usiyemfahamu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 29, 2008

    Al-Musoma..

    Mdau anafahamu POST CODE ni nini?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 29, 2008

    WASILIANA NA KAMPUNI MOJA YA MTANZANINIA INAITWA VIVIENNE UK LTD, HUYO JAMAA ANADILI NA KITU CHOCHOTE KUTOKA UK.

    Email yao ni 'vivienneukltd@aim.com'

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 29, 2008

    Babuu..... magari hapa bongo jamani yamezidi mno, Hatujui hata tupite wapi. We kaka tafadhali nunua hayahaya yaliyopo humu nchini tayari. Foleni, Pollution imezidi.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 30, 2008

    USINUNUWE GARI KUPITIA KAMPUNI YOYOTE HAO WOTE, WANAUMIZA WATU TU, KAMA NILIVYOKUAMBIA HAPO AWALI JUU KAMA UNA MTU MWAMINIFU MUULIZIA ATAKUSAIDIA, ACHANA NA HAO WANASEMA KUNA KAMPUNI YA MTANZANIA BLA BLA BLA KAMA HIVYO NI BORA BASI UKANUNUA HAPO HAPO BONGO, OF COURSE WHEN SOMEBODY WANTS TO BUY SOMETHING ONE OF THE FACTORS TO LOOK AT IS PRICE, HIVYO BEI NI TOPIC INAYOHITAJIKA, ACHANA NA HIVYO VIJIKAMPUNI UCHWALA. UNGEWEZA KUJA MWENYEWE LAKINI SIDHANI KAMA UNAWEZA KUPATA VISA KWA KUJA KUNUNUA GARI USED!!! OTHERWISE HIYO VISA IWE YA KUJA KUMTEMELEA MTU ALIYEKULETEA MWALIKO THEN UKAUNGANISHA NA MAMBO YAKO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...