Home
Unlabelled
simba oye!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Naona Michuzi leo umejitahidi sana kuvumilia mpaka kuleta hizi habari. Du, ama kweli safari ni ndefu sana kama mambo yetu ndo hivi, yaani hawa yeboyebo na tambo zote zile kumbe hakuna kitu, ohh, usajili mkali sijui Kaseja na kadhalika, hii ni aibu sana kwa timu kama Yanga kufanya hivyo, ukizingatia kiongozi wao ni kiongozi wa TFF pia, aibu sana hii kwa mpira wetu jamani!!
ReplyDeleteMichuzi mimi ni mpenzi wa Yanga,lakini naomba niwapongeze Simba(wachezaji,makocha na viongozi wao), kwanza kwa "professionalism" waliyoonyesha (ingawa nao walikuwa na madai yao)na kwa kuwa mshindi wa tatu.Naomba TFF na CECAFA na TFF zikuchukue hatua kali kwa Timu ya Yanga kwa kitendo hiki ambacho naweza kukiita cha kiuni.Viongozi wote wa Yanga wanapashwa kuwajibika kwa hili.Wameleta aibu kwa nchi.Maximo akiwambia nidhamu mnamwona mwendawazimu.Hii inawafundisha nini wachezaji wetu?.Kocha kama Kondic anakubali uamuzi wa kijinga kama huu,kweli yeye ni kocha wa mpira wa miguu???.
ReplyDeletebrother michuzi nadhani unatakiwa utupatie habari za kichunguzi na zakina kuhusiana na mkasa wa watani kutoingia uwanjani.
ReplyDeletesome where umetaja milion 35 naomba utpashe zaidi. tuambie mashabiki wa yanga wanasemaje na wale wa msimbaje wanasemaje? tuambie TFF pia wanasemaje??
Najuwa Mnyama kashinda kwa technical 'knockout' lakini huwa nafurahia sana tunaposhinda uwanjani kwani hakuna kelele zaidi kama hapa kwani majungu lazima yatatapakaa tu.
well nawatakia maaandalizi mema watani wetu!
G7
UK
Hahahaha Kweli Simba Pori hawiki ananguruma Jogoo wa shamba hawikii mjini ndio yanga, KWakwa michuziiiiiiiiiiiii Simba kidedea hapo Yanga wanyela wanakimbia uwanja au walikuwa Zanzibar? mfazili wao wa Boti na Mganga hawajatokea? hahaha Simba tunatisha niliwaambia Simba ni Dume akiwa Jike ndio kabisa Anangata awaachie watoto chakula. Wadau mpoo au jangwani kuna mafuriko? from Mdau Mikocheni B. Malik.
ReplyDeletenaona misupu umeandika kiunyoonge...SIMBA Oyee!! utajiju na yeboyebo yako..!hiyo ndiyo dawa ya kuifunga simba kama mlivyokuwa mikijitamba...!!na kwenye ligi mfanye hivyohivyo..! mipesa ya kumnunuwa kaseja mnayo mnataka mlipwe milioni 35 kwa lipi ovyoo...!!auunguramapo simba mcheza nani?..nguruma..nguruma..ngurumaaa..! mdau sitokihom!
ReplyDeleteMieeeeeeeee Kiboko ingieni Ile sehemu imeeandikwa Simba nje, Utaona nimesema Kesho Simba watashinda Tatu Bila. Mumeona sasa ni 3-0 japo za chee lakini mnakimbia uwanja mnaogopa simba dume Malapa yanakanyaga CHOONI tu jamani sawa. na NDALA zenu za BORA. Popo-pooooooo Eh Kidedea. poleni Yanga sikunyengine kuweni na nizamu alafu mnasema mnaonewa mahakamani mnamuumiza tu mzamini wenu msubiri kuchapana viboko from Haji Tumbo Chake Chake Pemba.
ReplyDeleteMimi ni yanga ma nitaendelea kuwa yanga ila nina hojhawa viongozi ni machizi walitegemea hiyo milioni 50 itoke wapi wakati hata uhamasishaji haukuwepo na pale neshno uwanja ulikua empty kabisa hayo mapato wanayoingiza ni yapi jamani? kama wangetaka hiyo milioni hamsini katika mpira wangejiandaa mapema kucheza mpira washinde wawe washindi wakwanza mbona hiyo pesa wangepata sasa kwa masikitiko wameikosa na cha motowatakiona. Tangu lini mpira ukachezwa mdomoni kazeni hata kaseja atawashangaa na atajuta kuja yanga
ReplyDeleteKwa mtindo huu,itahukua miaka kwa soka la bongo kufikia malengo.Kwa kweli Uyanga na Usimba ndio unaoua soka hapa Bongo.Kabla sijaendelea naomba wadau mnifahamishe ni vigezo gani vilivyoifanya SIMBA ishiriki katika Kagame wakati katika Vodacom League Prison ndio walikuwa nafasi ya pili.Kama hakuna sababu za msingi,basi ni tamaa ya TFF na hao CECAFA,kupata pesa za viingilio,na matokea ndio hayo ya kutokuja kuelewana na vilabu,matokeo yake Yanga wanagoma kuingia uwanjani.AIBU.!!!
ReplyDeleteHawa Yanga walisha shituka kwamba leo nikipigo nd' maana wakaanza kisingizio cha mkwanja lakini hiyo siyo sababu kwani wangecheza kwanza halafu huo mkwanja baadae na pia ili kuwaridhisha mashabiki wao, mimi namshauri huyo Manji ajiondokee zake tu mana hapo mnamchuna tu na watu wenyewe ni wajinga watupu..........Hasara ni ya nani?
ReplyDeleteHapa ndipo kuna tofauti kubwa kati ya mpira wa bongo na wenzetu huku. Mi ndio maana mpira wa bongo niliishajitoa siku nyigi toka simba afungwe 2-0 na Stalla sijaingia uwanjani tena.
ReplyDeleteHapa inatakiwa Yanga wapigwe faini kali na kufunguwa mashindano ya kimataifa miaka 10. Watu wanalipa hela kuja kuona burudani na siyo kitu kingine, mpira ni burudani ila kwa timu za bongo umekuwa Politics.
ha ha haaaa, kaaazi kwelikweli!
ReplyDeleteMichu! hahahaha! umejikaza kweli kisabuni ila ndio huna ujanja wewe unafikia goli 5 mchezo hii inaitwa bora ya lawama kuliko fedheha... wangebonyezwa kizenji mpk basi
ReplyDeleteSasa mnabidi muanzishe utani wa jadi na timu kubwa kama Tanzanite Fc. Kwanza mmeshawafunga kama mara kumi mfululizo sasa huo utani wa jadi unatoka wapi! Nyie simba tualikeni tuje kuwaonyesha kandanda! Achanneni na hao Yanga Mdobwedo!
ReplyDeleteKusema kweli haya mambo yanarudisha nyuma soka letu na yanga wanastahili kupewa adhabu kali sana.
ReplyDeleteHi Bro Misupu mbona hutupi matokeo nani Bingwa wa Kagame?
ReplyDeleteJibu kwa anon wa July 27, 2008 3:31 PM, ni kwamba Simba wameshiriki kama bingwa wa ligi iliyoisha kabla ya hii ya mwaka huu, ni kwamba katika ligi ya 2006/2007 Simba ndo walikuwa mabingwa wa ligi, na yanga walishika nafasi ya pili, na hawa ndo walioshiriki. Mashindano yalikuwa yafanyike mapema zaidi, lakini yalisogezwa mbele kutokana na mabadiliko ya ratiba za uendeshaji wake, ndo kusema Simba hapa wameshiriki kama mabingwa na yanga wao walishiri kama mshindi wa pili. Yanga na Prisons watashiriki mashindano yatakayofuatia. Ila hilo la tamaa uliloliongelea ni kwamba tuwaulize TFF kwamba yanga wameshiriki kama mwanachama wa shirikisho gani? kwa vile mpaka sasa hivi yanga sio mwanachama wa TFF hivyo hawastahili kushiriki mashindano yoyote yanayoandaliwa na TFF au yale ambayo washiriki wake ni wale waliotokana na mashindano yaliyoendeshwa na TFF mpaka hapo watakapokuwa wanachama, nadhani hali kama hiyo ingekuwa ni kwa Simba, tungezungumza mengine, akina Kaijage ungewaona wanachonga. Na pia hata ukiangalia leo, ni kwamba kwa kawaida timu inasubiriwa kwa muda wa dakika 15, lakini leo yanga kwa vile ni timu ya TFF na ikulu, basi ilisubiriwa kwa dakika 45 huu sio uhuni jamani wa hawa viongozi wa TFF? natumaini nimekujibu mkuu!!
ReplyDeleteMara nyingi wenye upeo wa mawazo huwa wachache...ANGALIA PICHA VIZURI,utawaona walioshusha mikono!!! Ingawa ni wanasimba.Kweli AKILI NI MALI.Miaka hii si ya akina Kajole.Kipato.....
ReplyDeleteUpeo gani wewe mgongo wazi unatetea ujinga.Nyoo mmezoea kubebwa na marefa wenu wa TFF mngeingiza pua kwa refa wa nje muone.Jana ndio ilkuwa siku ya kurudia 6 bila.Nyau nyie mna bahati sana.
ReplyDeletesi simba wala yanga wote uozo tu kudadadeki zao
ReplyDelete