simba wakishangilia baada ya muda wa kuwasubiri yanga walioingia mitini kwisha, na kuwa washindi watatu wa kombe la kagame cup kwa kulamba mabao 3 na pointi 3 za che sasa hivi hapa neshno. sasa tunasubiri fainali yenyewe kati ya tusker na uganda revenue authority.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 27, 2008

    Naona Michuzi leo umejitahidi sana kuvumilia mpaka kuleta hizi habari. Du, ama kweli safari ni ndefu sana kama mambo yetu ndo hivi, yaani hawa yeboyebo na tambo zote zile kumbe hakuna kitu, ohh, usajili mkali sijui Kaseja na kadhalika, hii ni aibu sana kwa timu kama Yanga kufanya hivyo, ukizingatia kiongozi wao ni kiongozi wa TFF pia, aibu sana hii kwa mpira wetu jamani!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 27, 2008

    Michuzi mimi ni mpenzi wa Yanga,lakini naomba niwapongeze Simba(wachezaji,makocha na viongozi wao), kwanza kwa "professionalism" waliyoonyesha (ingawa nao walikuwa na madai yao)na kwa kuwa mshindi wa tatu.Naomba TFF na CECAFA na TFF zikuchukue hatua kali kwa Timu ya Yanga kwa kitendo hiki ambacho naweza kukiita cha kiuni.Viongozi wote wa Yanga wanapashwa kuwajibika kwa hili.Wameleta aibu kwa nchi.Maximo akiwambia nidhamu mnamwona mwendawazimu.Hii inawafundisha nini wachezaji wetu?.Kocha kama Kondic anakubali uamuzi wa kijinga kama huu,kweli yeye ni kocha wa mpira wa miguu???.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 27, 2008

    brother michuzi nadhani unatakiwa utupatie habari za kichunguzi na zakina kuhusiana na mkasa wa watani kutoingia uwanjani.
    some where umetaja milion 35 naomba utpashe zaidi. tuambie mashabiki wa yanga wanasemaje na wale wa msimbaje wanasemaje? tuambie TFF pia wanasemaje??

    Najuwa Mnyama kashinda kwa technical 'knockout' lakini huwa nafurahia sana tunaposhinda uwanjani kwani hakuna kelele zaidi kama hapa kwani majungu lazima yatatapakaa tu.

    well nawatakia maaandalizi mema watani wetu!

    G7
    UK

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 27, 2008

    Hahahaha Kweli Simba Pori hawiki ananguruma Jogoo wa shamba hawikii mjini ndio yanga, KWakwa michuziiiiiiiiiiiii Simba kidedea hapo Yanga wanyela wanakimbia uwanja au walikuwa Zanzibar? mfazili wao wa Boti na Mganga hawajatokea? hahaha Simba tunatisha niliwaambia Simba ni Dume akiwa Jike ndio kabisa Anangata awaachie watoto chakula. Wadau mpoo au jangwani kuna mafuriko? from Mdau Mikocheni B. Malik.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 27, 2008

    naona misupu umeandika kiunyoonge...SIMBA Oyee!! utajiju na yeboyebo yako..!hiyo ndiyo dawa ya kuifunga simba kama mlivyokuwa mikijitamba...!!na kwenye ligi mfanye hivyohivyo..! mipesa ya kumnunuwa kaseja mnayo mnataka mlipwe milioni 35 kwa lipi ovyoo...!!auunguramapo simba mcheza nani?..nguruma..nguruma..ngurumaaa..! mdau sitokihom!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 27, 2008

    Mieeeeeeeee Kiboko ingieni Ile sehemu imeeandikwa Simba nje, Utaona nimesema Kesho Simba watashinda Tatu Bila. Mumeona sasa ni 3-0 japo za chee lakini mnakimbia uwanja mnaogopa simba dume Malapa yanakanyaga CHOONI tu jamani sawa. na NDALA zenu za BORA. Popo-pooooooo Eh Kidedea. poleni Yanga sikunyengine kuweni na nizamu alafu mnasema mnaonewa mahakamani mnamuumiza tu mzamini wenu msubiri kuchapana viboko from Haji Tumbo Chake Chake Pemba.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 27, 2008

    Mimi ni yanga ma nitaendelea kuwa yanga ila nina hojhawa viongozi ni machizi walitegemea hiyo milioni 50 itoke wapi wakati hata uhamasishaji haukuwepo na pale neshno uwanja ulikua empty kabisa hayo mapato wanayoingiza ni yapi jamani? kama wangetaka hiyo milioni hamsini katika mpira wangejiandaa mapema kucheza mpira washinde wawe washindi wakwanza mbona hiyo pesa wangepata sasa kwa masikitiko wameikosa na cha motowatakiona. Tangu lini mpira ukachezwa mdomoni kazeni hata kaseja atawashangaa na atajuta kuja yanga

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 27, 2008

    Kwa mtindo huu,itahukua miaka kwa soka la bongo kufikia malengo.Kwa kweli Uyanga na Usimba ndio unaoua soka hapa Bongo.Kabla sijaendelea naomba wadau mnifahamishe ni vigezo gani vilivyoifanya SIMBA ishiriki katika Kagame wakati katika Vodacom League Prison ndio walikuwa nafasi ya pili.Kama hakuna sababu za msingi,basi ni tamaa ya TFF na hao CECAFA,kupata pesa za viingilio,na matokea ndio hayo ya kutokuja kuelewana na vilabu,matokeo yake Yanga wanagoma kuingia uwanjani.AIBU.!!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 27, 2008

    Hawa Yanga walisha shituka kwamba leo nikipigo nd' maana wakaanza kisingizio cha mkwanja lakini hiyo siyo sababu kwani wangecheza kwanza halafu huo mkwanja baadae na pia ili kuwaridhisha mashabiki wao, mimi namshauri huyo Manji ajiondokee zake tu mana hapo mnamchuna tu na watu wenyewe ni wajinga watupu..........Hasara ni ya nani?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 27, 2008

    Hapa ndipo kuna tofauti kubwa kati ya mpira wa bongo na wenzetu huku. Mi ndio maana mpira wa bongo niliishajitoa siku nyigi toka simba afungwe 2-0 na Stalla sijaingia uwanjani tena.

    Hapa inatakiwa Yanga wapigwe faini kali na kufunguwa mashindano ya kimataifa miaka 10. Watu wanalipa hela kuja kuona burudani na siyo kitu kingine, mpira ni burudani ila kwa timu za bongo umekuwa Politics.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 27, 2008

    ha ha haaaa, kaaazi kwelikweli!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 27, 2008

    Michu! hahahaha! umejikaza kweli kisabuni ila ndio huna ujanja wewe unafikia goli 5 mchezo hii inaitwa bora ya lawama kuliko fedheha... wangebonyezwa kizenji mpk basi

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 27, 2008

    Sasa mnabidi muanzishe utani wa jadi na timu kubwa kama Tanzanite Fc. Kwanza mmeshawafunga kama mara kumi mfululizo sasa huo utani wa jadi unatoka wapi! Nyie simba tualikeni tuje kuwaonyesha kandanda! Achanneni na hao Yanga Mdobwedo!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 27, 2008

    Kusema kweli haya mambo yanarudisha nyuma soka letu na yanga wanastahili kupewa adhabu kali sana.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 27, 2008

    Hi Bro Misupu mbona hutupi matokeo nani Bingwa wa Kagame?

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 27, 2008

    Jibu kwa anon wa July 27, 2008 3:31 PM, ni kwamba Simba wameshiriki kama bingwa wa ligi iliyoisha kabla ya hii ya mwaka huu, ni kwamba katika ligi ya 2006/2007 Simba ndo walikuwa mabingwa wa ligi, na yanga walishika nafasi ya pili, na hawa ndo walioshiriki. Mashindano yalikuwa yafanyike mapema zaidi, lakini yalisogezwa mbele kutokana na mabadiliko ya ratiba za uendeshaji wake, ndo kusema Simba hapa wameshiriki kama mabingwa na yanga wao walishiri kama mshindi wa pili. Yanga na Prisons watashiriki mashindano yatakayofuatia. Ila hilo la tamaa uliloliongelea ni kwamba tuwaulize TFF kwamba yanga wameshiriki kama mwanachama wa shirikisho gani? kwa vile mpaka sasa hivi yanga sio mwanachama wa TFF hivyo hawastahili kushiriki mashindano yoyote yanayoandaliwa na TFF au yale ambayo washiriki wake ni wale waliotokana na mashindano yaliyoendeshwa na TFF mpaka hapo watakapokuwa wanachama, nadhani hali kama hiyo ingekuwa ni kwa Simba, tungezungumza mengine, akina Kaijage ungewaona wanachonga. Na pia hata ukiangalia leo, ni kwamba kwa kawaida timu inasubiriwa kwa muda wa dakika 15, lakini leo yanga kwa vile ni timu ya TFF na ikulu, basi ilisubiriwa kwa dakika 45 huu sio uhuni jamani wa hawa viongozi wa TFF? natumaini nimekujibu mkuu!!

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 28, 2008

    Mara nyingi wenye upeo wa mawazo huwa wachache...ANGALIA PICHA VIZURI,utawaona walioshusha mikono!!! Ingawa ni wanasimba.Kweli AKILI NI MALI.Miaka hii si ya akina Kajole.Kipato.....

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 28, 2008

    Upeo gani wewe mgongo wazi unatetea ujinga.Nyoo mmezoea kubebwa na marefa wenu wa TFF mngeingiza pua kwa refa wa nje muone.Jana ndio ilkuwa siku ya kurudia 6 bila.Nyau nyie mna bahati sana.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 28, 2008

    si simba wala yanga wote uozo tu kudadadeki zao

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...