Mwanza, Julai 19, 2008:
Mchakato wa kumtafuta Balozi wa Mitindo wa REDD’S wa mwaka 2008 ambao umefanyika Mwanza unafikia kilele chake kesho Jumamosi usiku katika tukio la aina yake kwenye ukumbi wa NSSF jijini Mwanza.
Hii inafuatia wiki nzima ambayo ilijaa shughuli mbalimbali ndani na nje ya jiji hilo zote zikilenga katika kuhakikisha mshindi wa mwaka huu ni wa kipekee. Safari hiyo ya washiriki wa mchakato huo kwenye Kanda ya Ziwa pia ilijumuisha nafasi ya kihistoria ya kutembelea kaburi la Baba wa Taifa hayati Mwl. Julius Nyerere.
Akizungumzia kilele cha mashindano hayo, Meneja wa bia ya REDD’S, Bw. George Kavishe alisema,”Nina uhakika mchakato huu umefanikiwa kupata Balozi wa kweli wa Mitindo wa REDD’S, mtu ambaye anashabihiana na sifa za kinywaji chetu. Kinywaji cha REDD’S kina sifa za umahiri, utulivu, na mwonekano mzuri ambazo ni baadhi tu ya sifa zake na ninaamini tukio la leo litatuonyesha sifa hizi kama zilivyo.”
Akisubiri fainali za leo kwa hamu kubwa, Mkurugenzi Mkuu wa Beautiful Tanzanie Agency, Bi. Irene Kiwia aliongeza, “Washindani wana hamu mno na wako tayari kwa shindano la leo, siku ya leo imekuwa na shughuli nyingi lakini wasaa ukifika naamini kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa.”
Angela Lubala, Mrembo wa Temeke wa mwaka 2008 alisema, “Kwa kweli hili litakuwa tukio la kukumbukwa kwa muda mrefu hasa miongoni mwetu washindani. Wakati mwingine ilionekana kama kazi ngumu sana lakini ilikuwa nzuri tu, tumejifunza mambo mbalimbali na nina hakika yote tuliyoyapata yataonekana leo usiku.”
Mchakato kumtafuta Balozi wa Mitindo wa REDD’S mwaka huu ulikuwa hivi:
Ijumaa Julai 11, 2008 – Washiriki walihudhuria semina Bagamoyo ambapo walipatiwa utaratibu mzima wa shindano la kumtafuta balozi wa REDD’S.
Jumamosi Julai 12, 2008 – Warembo waliondoka kuelekea Mwanza kwa ndege ya Air Tanzania na walipowasili walilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, baadaye walitalii mitaa ya jiji la Mwanza kwa gari na baadaye walikwenda Yacht Club kwa ajili ya chakula cha mchana. Jioni walifanya mazoezi yaliyofuatiwa na chakula cha usiku kwenye mgahawa wa Kiss Pub.
Jumapili Julai 13, 2008 – Baada ya kifungua kinywa warembo walicheza mpira wa wavu, chakula cha mchana kilifuata baadaye Tunza Lodge. Siku yao ilimalizika kwa chakula cha jioni Yacht Club baada ya bonanza iliyofanyika BoT.
Jumatatu Julai 14, 2008 – Washiriki waliianza siku kwa mazoezi na maandalizi kisha mkutano na waandishi wa habari La Kairo Hotel. Walibaki hapohapo hotelini ambapo baada ya chakula cha mchana walipima na kujaribu nguo kisha kurejea tena kwenye mazoezi. Chakula cha jioni kilikuwa hapohapo La Kairo Hotel.
Jumanne Julai 15, 2008 – Siku ilianzia studio za Kiss FM, baadaye warembo walielekea makao makuu ya Vodacom kabla ya kutembelea Hospitali ya Sekou Toure kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kijamii. Walikula chakula cha mchana makao makuu ya Vodacom kabla ya kuingia tena kambini kwa ajili ya mazoezi. Siku yao ilimalizika kwa hafla ya jioni iliyofanyika Tilapia Hotel.
Jumatano Julai 16, 2008 – Washiriki walifanya safari ya kihistoria kwa kutembelea kaburi la Mwl. Julius Nyerere. Hii ilifuatiwa na chakula cha mchana na Mkuu wa Mkoa wa Mara na siku yao ilifungwa kwa chakula cha jioni na dansi iliyofanyika Multi Villa, Musoma.
Alhamisi Julai 17, 2008 – Warembo waliondoka Musoma kurudi Mwanza mapema asubuhi na baadaye kutembelea kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ambapo pia walikula chakula cha mchana. Baadaye walitembelea kituo cha kulelea watoto cha Starehe ambapo waliungana na wafanyakazi wa TBL katika shughuli za kijamii. Usiku walikula na kucheza dansi Kirumba Pub.
Leo Ijumaa Julai 18, 2008 – Siku itaanza kwa warembo kupima nguo wakiwa na wanamitindo na kisha kufanya mazoezi kabla ya kwenda Yacht Club kwa chakula cha mchana. Baadaye watakwenda La Kairo Hotel ambapo watafanya majaribio kwa ajili ya fainali na chakula cha jioni watakula TGIF Villa Park.
KESHO USIKU: Jumamosi Julai 19, 2008 – Siku iliyosubiriwa na kila mtu. Warembo wanatarajia kufanya mazoezi yao ya mwisho masaa ya asubuhi, kisha majaribio yatafuata na baadaye watakula chakula cha mchana kwenye ukumbi wa NSSF. Hiki kitafuatiwa na maandalizi ya urembo kwa ajili ya tukio la usiku huo.
Itakapofika takribani saa 2 usiku wageni watakaofurika kwenye ukumbi wa NSSF watapata fursa ya kujionea tukio kubwa na la kipekee katika jiji la Mwanza.
Kama ilivyokusudiwa, mchakato wa kumtafuta Balozi wa Mitindo wa REDD’S wa mwaka 2008 ulikuwa na mfululizo wa shughuli nyingi kuliko miaka ya nyuma.
Mshindi atatangazwa kwenye shindano la kumtafuta Mrembo wa Tanzania litakalofanyika jijini Dar es Salaam mwezi ujao.
Tanzania tumezidi mambo ya ushabiki ktk mambo ambayo hayana fyucha au manufaa kwa taifa miaka ya mbele. I really wish tungekuwa na motisha kama za umiss/star search ktk mambo ya maana kama kuinua vipaji vya vijana wetu ktk masuala ya Elimu: I mean nationwide competitions and things like that. Kwanini nasisi tusiwapeleke vijana wetu kwenye International Science Olympiads?
ReplyDeleteKama;
http://ipho2008.hnue.edu.vn/
http://www.imo-official.org/
Tufikirie mbele
Mwesiga
Jamani kwani mamis lazima wavae uchi hata kama hawako kwenye mashindano? wananichefua
ReplyDeleteNatombe
Moshi
yap yap!keep it up ma girls lukin gud.....all the best kille
ReplyDeletewewe mdau wa kwanza kabisa unapoint muhimu sana....ila mafisadi wa ngono ndio wanaodhamini hayo mashindano so dont expect any changes in this lifetime maybe Mwalimu Nyerere arudi yafutwe kabisa.
ReplyDeleteHaya mashindano ya kuwaweka jukwaani wanawake kila siku tanzania yamezidi mipaka. Naam naona tumawapa ujumbe mzuri sana watoto wetu wanaokuwa kusahau elimu na bidii katika kujijengea maisha bora na badala yake wajipe tamaa ya kuwania ma miss hili na lile. Idumu tanzania! Tanzania; mwenye pesa ndio mwizi!
ReplyDeleteMamiss wanakunywa fanta. Sukari yote hiyo.
ReplyDeleteAnonymous wa kwanza,Kaazi kweli kweli
ReplyDeleteNakubaliana na Brother Mwesiga, mashindano hayo warembo yamezidi mno siku hizi !!!
ReplyDeletewazazi wa wasichana hao vile walaumiwe kuwachia binti zao waingine kwenye mambo hayo. Huu ni uwanja ambao unawaweka hawa wasichana kutumiwa na kuwalaghai ili washinde. Wengi inajulikana wako tayari wafanye cho chote ili washinde, ni ukweli kabisa.
I mean exploitation by that !!
Hawa akina dada kuweka priority ya uso na mwili kuliko ubongo kichwani hautoi msingi wa maisha ya baadae hata kidogo.
Wazungu wanaita hii "Bimbo Mentality" Yaani mwanamke ambae ameona rasilimamli yake yote ipo kwenye uzuri wake wa sura na mwili, matokeo yake? wanaume watamtumia na kumlipa kile ambacho huyo dada anahikitaji, soon or later anatatokea Bimbo mwingine mzuri kuliko yeye na yeye anaachwa nyuma, wakati hana elimu au ujuzi mwimgine wowote wa kumsaidia kikazi. I am proud to see my very beautiful sisters but jamani they are just too many beauty contests !!!
Nyoro
Bwana Mwesiga, comment nambali moja naona point umeipigilia msumari.
ReplyDeleteHata mimi sipati picha kabisa, sielewi ni kwanini tumekuwa obsssed na hivi ambavyo kusema ukweli fyucha yake ni ziro. Kuna watu watasema mimi kama sitaki hii kitu basi nisiangalie, ila ukweli ni kwamba madhara ya hivi vitu nia makubwa kuliko watu wanavyofikiria. Hakuna creativity kama tutakaa kwenye hizi shughuli za warembo, kama hakuna creativity manake hakutakuwa na innovation. Na mwisho wake tuna import chumvi, sukari mpaka maji ya kunywa.
Tangu huu mwaka huu uanze nimeona matangazo ya urembo na umiss kwenye globu hii yasiyoesabika, inawezekana hii inaonyesha true character yetu..
Brother Michizi, ahsante sana
Don't stop thinking about tomorrow
Kayanga
Bwana Mwesiga, comment nambali moja naona point umeipigilia msumari.
ReplyDeleteHata mimi sipati picha kabisa, sielewi ni kwanini tumekuwa obsssed na hivi ambavyo kusema ukweli fyucha yake ni ziro. Kuna watu watasema mimi kama sitaki hii kitu basi nisiangalie, ila ukweli ni kwamba madhara ya hivi vitu nia makubwa kuliko watu wanavyofikiria. Hakuna creativity kama tutakaa kwenye hizi shughuli za warembo, kama hakuna creativity manake hakutakuwa na innovation. Na mwisho wake tuna import chumvi, sukari mpaka maji ya kunywa.
Tangu huu mwaka huu uanze nimeona matangazo ya urembo na umiss kwenye globu hii yasiyoesabika, inawezekana hii inaonyesha true character yetu..
Brother Michizi, ahsante sana
Don't stop thinking about tomorrow
Kayanga
yaani inasikitisha mno. Ni majuzi tu mlisikia Tigo ikitoa shilingi Milioni 2 ili ku'sponser a scientific symposium. Even though ni hatua kubwa walioitoa ktk hilo jambo, utashangaa kusikia tigo ama kampuni nyingine za hapo Bongo zikitoa milioni 10 au zaidi ktk masuala ya Bongo star search ama miss Songombingo. Y? Wenzetu makampuni yao yanainvest ktk kutafuta vipaji ktk sayansi na hisabati mfano
ReplyDeletehttp://www.intel.com/pressroom/kits/education/ists.htm
Sisemi tuige, ila we need to start somewhere. Angalau Celtel ninawapa hongera kwa kuanzisha mashindano ya vyuo. That is commendable. Tunahitaji hayo zaidi