JK akimjulia hali mtoto Desderius Mrongo mwenye umri wa miaka miwili na nusu aliyelazwa katika Hospitali ya Consolata Ikonda,wilayani Makete.Aliyembeba mtoto Desderius ni nyanya yake ambaye alimweleza Rais kuwa mama mzazi wa mtoto huyo amefariki Dunia. JK yupo Mkoani iringa kwa Ziara ya kikazi kukagua na kufungua miradi ya maendeleo
JK akiongea na watoto mapacha walioungana Maria na Consolata wakati alipotembelea Hospitali ya Kanisa Katoliki inayoendeshwa na wamissionari wa Shirika la Consolata iliyopo Ikonda Makete,Mkoa wa Iringa leo.Mapacha hao ambao sasa wana umri wa miaka kumi na moja( 11) hawawezi kutenganishwa kwa upasuaji kutokana sababu za kitaalamu, ni yatima ambao wazazi wao wamefariki kwa ugonjwa wa ukimwi lakini kwa bahati nzuri wao hawakuathirika na wanaendelea vizuri kiafya.Mapacha hao ambao wanahudumiwa na watawa wa Shirika la Consolata hivi sasa wanasoma darasa la tano katika shule ya Msingi Ikonda Makete na hivi sasa wanaishi nyumbani kwa Bi Betina Mbilinyi karibu na shule wanayosoma.
Matroni Katika Hospitali ya Consolata Ikonda, Sr.Egle Casiraghi(kulia) akimweleza JK jinsi wanavyotoa huduma za afya katika hospitali hiyo iliyopo wilaya ya Makete wakati Rais alipoitemebela hospitali hiyo leo.Wakwanza kushoto ni Padre Sandro Nava Mkuu wa hospitali hiyo na Watatu kushoto aliyeshikwa mkono na Rais ni Sr.Magda Boscolo.
JK akiwahutubia wananchi wa Igagala Njombe baada ya Kufungu Soko Jipya
JK akiongea na watoto mapacha walioungana Maria na Consolata wakati alipotembelea Hospitali ya Kanisa Katoliki inayoendeshwa na wamissionari wa Shirika la Consolata iliyopo Ikonda Makete,Mkoa wa Iringa
JK akiangalia mboga aina ya Figiri muda mfupi baada ya kufungua soko La Igagala Njombe
JK akiongea na mfanyabishara wa Nyanya katika Soko la Igagala,Njombe, Bi Grace Shirima baada ya kufungua Soko
JK akiangalia kipande cha Makaa ya mawe wakati alipokagua eneo la mradi wa makaa ya mawe ya Mchuchuma,wilayani Ludewa leo.Pembeni ya Rais ni Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la maendelo la Taifa NDC Bwana Gideon Nasari.
JK akifunua jiwe la msingi wakati wa hafla ya kufungua soko la Igagala,Wilayani Njombe
JK akiwahutubia wananchi wa eneo la Kilocha,wilayani Njombe jana baadaya kuzindua ujenzi wa shule ya wasichana ya Anna Makinda
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Bwana Adam Malima akimwonesha JK eneo la Mradi wa Umeme wa Ludewa
JK akikagua majengo ya shule ya sekondari ya wasichana ya Anna Makinda katika kijiji cha Kilocha,Ihunda, wilayani Njombe
JK akisalimiana na watoto wa shule ya msingi Kilocha muda mfupi baada ya kuzindua ujenzi wa shule ya wasichana ya Anna Makinda jana. Picha zote zimepigwa na mdau Fred Maro wa Ikulu
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Hii picha ya mwisho chini inaongea mambo mengi sana. Pamoja na mambo mengine (usafi wa hao watoto au sijui baridi imewafana wawe na huo mpauko katika nyuso) nimeshangazwa na huyo mtoto ambae haonyeshi kujali uwepo wa Rais hapo karibu (no attention at all to the prez).
Mdau unasema watoto hawajali uwepo wa prez..Je ulitaka wafanyi nini?
Wacheze ngoma au washangilie kwa kelele zisizo na kifani!
Hiyo ndyio hali halisi ya maisha yao na nimependa jinsi rais alivyokuwa akionyesha roho ya upendo.
Tuache kupenda ku-ACT,kujionyehsa NDIVYO SIVYO!!!
Ukitaka kwenda kwa undani utajua sura za hao watoto zinatoa taarifa ndefu!! Wanaonekana wamekosa amani, Je nini chanzo cha sura zisizo na furaha! Yawezekana kuanzia kwenye kaya hakuna furaha kwanini Why!? Hiyo ndio TAKE AWAY kwa wana kijiji wa blogu hii.
na hii sio politik ; kama mchangiaji mwingine alivyosema!
anaon wa kwanza.. I hope jina lako ni ignorant, kama ulivyo-type hapo kwenye comment.. kwa sababu wewe ndo' ignorant haswaaaa sasa hao ni watoto, unataka wafanyeje!!!!!, picha unaona msongamano,haionekani kama ilikuwa ni gwaride maalum la watoto kumpokea raisi. Pia kuhusu sura zao, kama zimepauka, kwanza inaweza kuwa ni baridi.Au wewe geography ya iringa hauijui?! pili kama wazazi hawana vitu vya kuwafanya watoto wanawiri unataka waende wakaviazime kwa sababu raisi anapita?! ili raisi asijue hali halisi ilivyo?! umenishangaza ndugu yangu!
Nimegundua rais wetu ana tabia ya kutia mikono yake katika mifuko ya suruali kama ni pose yake, picha zake nyingi ni hivyo, hata hivyo nadhani kuna haja ya washauri wake wa karibu kumuasa na tabia hiyo hasa pale anaposalimiana au kuzungumza na wazee wetu, kwa mila zetu hilo sio jema na linaashiria dharau, naamini hafanyi kwa makusidi lakini ipo haja ya kuambiwa
1) Raisi wetu anajitahidi sana. I hope mafisadi wa nchi wangeona hili angalau wamuachie muda wake ukiisha tuwe na surplus na maendeleo tele nchini kwetu ..
2) Heheheheh wanasema mchagga hatajirikii nyumbani na wachagga kwa kuchacharika na kutapakaa kama wahindi. Shirima sokoni Iringa. Angekua mkoani kilimanjaro nakwambia ingekua shida kumpata mtu kutoka mkoa mwingine.
3) Ukisoma habari hizi ndio unapata the real story ya nchi yetu,. Nimeona hurua sana huyo bibi ana take care mjukuu wake baada ya wazazi kufariki.
Dogo alikuwa anaona wanamwekea usiku tu, kuna mitkasi alikuwa anafikiria kwenda kuipiga. Mkuu anapiga ziara za nchini ina maana mafisadi wameikombea serikali hadi nauli ya kuendea ughaibuni nini...
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...
Hii picha ya mwisho chini inaongea mambo mengi sana. Pamoja na mambo mengine (usafi wa hao watoto au sijui baridi imewafana wawe na huo mpauko katika nyuso) nimeshangazwa na huyo mtoto ambae haonyeshi kujali uwepo wa Rais hapo karibu (no attention at all to the prez).
ReplyDeleteIgnorant,
Jeremani
Michu sasa kwa politiki?!
ReplyDeleteMdau unasema watoto hawajali uwepo wa prez..Je ulitaka wafanyi nini?
ReplyDeleteWacheze ngoma au washangilie kwa kelele zisizo na kifani!
Hiyo ndyio hali halisi ya maisha yao na nimependa jinsi rais alivyokuwa akionyesha roho ya upendo.
Tuache kupenda ku-ACT,kujionyehsa NDIVYO SIVYO!!!
Ukitaka kwenda kwa undani utajua sura za hao watoto zinatoa taarifa ndefu!!
Wanaonekana wamekosa amani,
Je nini chanzo cha sura zisizo na furaha!
Yawezekana kuanzia kwenye kaya hakuna furaha kwanini Why!?
Hiyo ndio TAKE AWAY kwa wana kijiji wa blogu hii.
na hii sio politik ; kama mchangiaji mwingine alivyosema!
anaon wa kwanza.. I hope jina lako ni ignorant, kama ulivyo-type hapo kwenye comment.. kwa sababu wewe ndo' ignorant haswaaaa
ReplyDeletesasa hao ni watoto, unataka wafanyeje!!!!!, picha unaona msongamano,haionekani kama ilikuwa ni gwaride maalum la watoto kumpokea raisi.
Pia kuhusu sura zao, kama zimepauka, kwanza inaweza kuwa ni baridi.Au wewe geography ya iringa hauijui?! pili kama wazazi hawana vitu vya kuwafanya watoto wanawiri unataka waende wakaviazime kwa sababu raisi anapita?! ili raisi asijue hali halisi ilivyo?! umenishangaza ndugu yangu!
K
Nimegundua rais wetu ana tabia ya kutia mikono yake katika mifuko ya suruali kama ni pose yake, picha zake nyingi ni hivyo, hata hivyo nadhani kuna haja ya washauri wake wa karibu kumuasa na tabia hiyo hasa pale anaposalimiana au kuzungumza na wazee wetu, kwa mila zetu hilo sio jema na linaashiria dharau, naamini hafanyi kwa makusidi lakini ipo haja ya kuambiwa
ReplyDeleteIringa baridi, ametia mikono mifukoni kuitia joto. kama inavyokuwaga winter huko nje.
ReplyDelete1) Raisi wetu anajitahidi sana. I hope mafisadi wa nchi wangeona hili angalau wamuachie muda wake ukiisha tuwe na surplus na maendeleo tele nchini kwetu ..
ReplyDelete2) Heheheheh wanasema mchagga hatajirikii nyumbani na wachagga kwa kuchacharika na kutapakaa kama wahindi. Shirima sokoni Iringa. Angekua mkoani kilimanjaro nakwambia ingekua shida kumpata mtu kutoka mkoa mwingine.
3) Ukisoma habari hizi ndio unapata the real story ya nchi yetu,. Nimeona hurua sana huyo bibi ana take care mjukuu wake baada ya wazazi kufariki.
Dogo alikuwa anaona wanamwekea usiku tu, kuna mitkasi alikuwa anafikiria kwenda kuipiga.
ReplyDeleteMkuu anapiga ziara za nchini ina maana mafisadi wameikombea serikali hadi nauli ya kuendea ughaibuni nini...