habari zilizagaa jijini kutwa nzima leo kwamba jamaa kavuta. nimeongea naye muda mfupi uliopita paschal akaniambia kwamba hata yeye kapata habari hizo kwamba amefariki, akisema huenda hiyo ruma ilisababishwa na yeye kuhamishiwa chumba kingine na kuna mdau aliyefikia chumba chake cha awali kukuta kitanda kitupi akajua tayari na kusambaza uvumi.
amesema anaendelea na matibabu japo mkono wake wa shoto bado umekufa ganzi na kichwa kinamuumauma.
amenituma nitoe asante sana kwa wote waliotuma na watotuma salamu za kumtakia apone haraka. anasema hana cha kuwalipa anamuachia jalali..
Hi Michu,
ReplyDeleteKwanza pole sana ndugu yangu Mayalla.Pili I dont think if it was a smart decision to ride a motor cycle all the way from Dar to Dom kaka Michu na wadau wenzangu,Hasa ukizingatia historia mbaya sana ya barabara hiyo tangu kifo cha hayati Edward Moringe
Sokoine.
Mdau,
USA.
Tunashukuru Michuzi kwa kutuletea kinachoendela, maana ni kawaida ya waandishi kufukua habari halafu wanaiacha hewani.
ReplyDeletePaschal, ugua upone.
asante michu kwa habari na picha hii inanipa moyo kwa kweli si kama zile za mwanzo
ReplyDeletemi binafsi nimefurahi kumuona kwenye hali ya matumaini ya kupona tunamuombea apate matibabu mazuri arudi kwenye shughuli zake
Pole ndugu Mayalla kwa ajali,ninakutakia matibabu mema upone haraka.Haikuwa vizuri kusafiri safari ndefu Dar-Dom kwa piki piki hasa ukizingatia kama ilikuwa ya kikazi.
ReplyDeleteasante mungu kwa kuwa kaka ye2 Pascal anaendelea vema na pia asante kaka michu kwa ku2pa taarifa hii. SASA 2NAKUOMBEA KAKA UPONE HARAKA ILI URUDI KTK HALI YAKO YA KAWAIDA UENDELEE NA SHUGHULI ZAKO NINAKUKUMBUKA SANA ULIKUWA MC KTK HARUSI YANGU. MUNGU BABA AKUPE UNAFUU, AMEN. NYAMMY
ReplyDeletemungu atakujaalia utapona haraka kwa hali uliyonayo sasa ni ya kutumaini kwa kuelekea ktk uzima.
ReplyDeleteTunakushukuru Michuzi kwa kuktutioa wasiwasi. Pili naomba nimpe pole Paschal Mayalla kwa ajali iliyomkuta napenda nimwambie kuwa Mwenyezi Mungu atamjaalia na atapona. Just apumzike na kutumia dawa au ushauri anaopewa na madktari ili apone haraka na aendelee na shughuli zake za ujasirimali.Pole kaka. I wish U all the best. RSJ
ReplyDeletepole sana kaka mayala!!lakini mie sio kwanini uliendesha pikipiki toka dar kwenda dodoma!!ni ubahili wa mafuta au kulipa nauli??naomba usirudie tena kaka yangu..dada norway
ReplyDeleteNdugu yangu Mayalla natoa pole na ajali. La kushukuru ni kukuona katika afya njema. Safari ya Dar to Dom ni ndefu ukizingatia udogo wa barabara na madereva wasivyokuwa waangalifu inakuwa ni hatari. Imagine kuna mabasi na trucks yanakuja mbele na nyma yako risk ya kupata ajali inakuwa ni kubwa. Kote duniani mwendesha pikipiki uko katika risks kubwa hivyo kuwa safe labda ni kwa safari fupi za mjini. Najua kutokana na ugumu wa maisha you have to do what you have to do na ndio maana sitakulaumu asilimia mia moja. Hata hivyo kumbuka kama una familia na ndugu na jamaa wanakutegema. Na pia bado uko kijana nadhani ungeweza kufikiria vizuri zaidi.
ReplyDeleteN:B Michuzi vicheko kama hivi huwa tunavitoa kwenye harusi. Najua utasingizia ni furaha baada ya kukuta jamaa hajatutoka. lakini pia najua unashabikia safari ya Dar-Dom
Ahsante 'me-choose' kwa kuweza kufika mwenyewe kumuona mpendwa wetu.Ugua pole paschal.
ReplyDeleteuncle Paschal:Ndugu,jamaa na marafiki(95%) wamekushauri kupunguza usafiri wa pikipiki kwa masafa marefu.Nadhani umesikia.Attendons-Voir.
pole sana kaka,
ReplyDeleteikiwa ni mipango ya Muumba, upone haraka na uwe na afya njema
Mimi pikipiki ilivyoniumiza nilivyotoka tu hospitali siku hiyo hiyo nliiuza. Tena nilikuta mke wangu keshaitengeneza na imerudi hali yake ya upya lakini niliipiga bei bila kuangalia nyuma, tena kwa bei rahisi.
ReplyDeleteSasa hivi nagombania mabasi na kupata tabu ya usafiri dar. Kila ninapofikiria kununua pikipiki nakumbuka maumivu makali iliyonipa.
Mungu akubariki upone haraka ila cha muhimu uwe muangalifu au kama huwezi kama mimi, achana nayo.
Pole sana Pascal.Mungu akujalie upate ahueni mapema ili urudi vitani tena.Najua kwa pikipiki ulikuwa na shughuli pevu ya kufuatilia lakini ndiyo hivyo tena,bahati mbaya.Isikukatishe tamaa.Pata nguvu kwanza,mshukuru Mungu wako na baada ya mapumziko mafupi karibu tena ulingoni!Good work Michuz! tny.
ReplyDeleteugua pole p. Jamani mnaposikia pikipiki mnadhania ni skuta ?? kuna pikix2 zina cc kubwa kuliko gari. na waweza toka mwanza mpaka mtwara kama una ria vile. ajali ni ajali tu . naomba p usikatishwe tamaa. na hii ajali. endelea kujali mazingira. just imagine wafanya kazi wote town centre wangeendesha pikix2 leo hii tungekuwa tunaongelea swala la foleni dar?naomba master p apewe ngao ya uanamazingira bora siku atakayotoka moi.
ReplyDeletePole sana na mungu akujalie salama. Michu mshauri shwahiba wetu huyo kuwa awe anavaa kofia wakati anaendesha pikipiki kwani mara nyingi nimemshuhudia mitaani akiendesha pikipiki yenye cc kubwa bila ya helmet wala nguo stahiki kwa ajili ya kukinga afya na mwili wake. nilidhani ile ajali aliyoipata wakati akitoka morogoro kuja dar ingempa tahadhari hiyo.
ReplyDeletejamani pamoja na yote usafiri wa mabasi ya kwenda mikoani huwa na mda maarumu na huyu kaka ni mwandishi wa habari je ikitokea anaitajika wakati mda wa mabasi umeshapita mnategemea afanye nini???
ReplyDeletetrain ndiyo hiyo mmeshaiona mambo mengi husababisha na hali ya maisha ilivyo.
kaka mayalla pole sana hiyo ni ajali tu ndugu yangu tunashukuru mungu umepona ila umepona kwa vile mwenyezimungu bado anamakusudi ya kukuacha na utambue kama yupo, anataka ufanye kazi zako anazozikusudia.
ugua pole
Pole sana Paskali kaka yangu. Mungu akutie nguvu na tumia muda huu kwa ibada na kukaa karibu na Mungu zaidi maana hauko bize kama ukiwa mzima. Wakati mwingine ni speed gavana ya Mungu ktk kutukumbusha uwepo wake.
ReplyDeleteHaiye msoro Mangiieee!