maulid baraka wa kitenge akimpongeza bwana harusi ridhiwani
JK na Mama Salma Kikwete wakisakata ngoma ya MUNGODO ya kabila la Wakwere, wakati wa sherehe ya harusi ya mtoto wao Ridhiwani Kikwete na Arafa Mohammed
Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein akimpongeza Ridhiwani Kikwete na Arafa Mohammed kwa kukamilisha kufunga ndoa wakati wa sherehe ya harusi yao .

baada ya ndoa yao ubungo plaza jana, maharusi ridhiwani na mai waifu wake arafa waisherehekea harusi yao na ndugu, jamaa na marafiki katika viwanja vya wanawake na maendeleo (wama) usiku huu

njenje walikuwepo kuduwarisha harusini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Mtotongwa Arafa kapendeza jamani!!. Nawatakia kila la kheri katika maisha mapya ya ndoa Bw Ridhwani na Bi Arafa.

    Choonde chonde waosha vinywa msianze kutubughudhi. Mara Halohalo, mara baba na mwana sijui nini n.k

    Nadhani mnaona wenyewe, ukumbi bomba sana, amakweli bongo tambarare sikuhizi.

    ReplyDelete
  2. Michuzi tuwekee picha nyingi bwana!!!

    ReplyDelete
  3. Baba mkwe yupo wapi au anaogopa kuona vazi la mkwe mabegazzzzzzzzzz out!!!

    ReplyDelete
  4. Wamependeza mashallah.......inshallah ndoa idumu....

    ReplyDelete
  5. Duuuuuuh mbona nawaona tayari wameshafanana vile??kama mtu na dada yake pllzzz sielewi mie.

    ReplyDelete
  6. Soshi kinywa ila nauliza? mbona raisi ni muislamu na naona majina yao ni ya kiislamu?

    Lakini harusi naona ni kama ya kikristo vile. Hayo mavazi sikujua harusi za kisslamu wanavaa hivi..

    Mnitoe ushamba sijahudhuria harusi ya kislamu zaidi ya jirani yetu na niliona wamevaa kanzu na bibi alivalishwa ushungi vile

    ReplyDelete
  7. ANASA hizo............

    `WATU BADO WANAENDELEZA LIBENEKE``


    ``WANANCHI VUMILIENI``

    ReplyDelete
  8. We Anon. Wa kwanza MMhhh. Ngoja nitulie. Ila huo ukumbi ulifurika haswaaaa. nadhani Wakwere wote walikuwepo.

    Kumbe Rais wetu anajua kuyarudi, ama kweli Rais Tunaye. Salaam Zako baba Moo' zikufikie kwa karo washup! Maana ungekuwa Bongo usingekosa huo mnuso

    ReplyDelete
  9. bi harusi kaumbika, kapendeza kweli. jamani na ndoa idumu, Allah awaongoze. natamani ningekuepo, michuzi pliiiiiiiiiz ongeza picha, hi harusi muhimu bwana!!!!!!!! hata wazazi wa bi harusi hatujawaona

    ReplyDelete
  10. Lol Anonymous said... wa August 24, 2008 11:35 PM.

    Yes wote ni waislamu sio kwa majina tuu. Lkn ni hivi kwenye ahrusi inategemea na mavazi yako bi kharusi na bwana harusi. Kwani unaruhusiwa kuvaa vyevyote utakavyo. Example sie kwetu kwenye Aqdi unavaa green dress ambayo unaweza changanya na gold, na bwana harusi huvaa Jokhho. Na wenye hall twavaa White dress na bwana harusi huvaa suite.

    Sasa wewe unaoa kina kikwete kma wakristo sababu ya mavazi yao, i mean ujamuona Kikwete kwenye hall na kanzu na koti. hehehhe hyo yataka wenyewe babu weh Kikwete hayawezi yeye kashazoea uite. Lkn kwenye mavazi ya Kharusi hkuna ukristo wala uislamu. Yote huenda tuu. Tc

    ReplyDelete
  11. Kwa kweli harusi imependeza sana, hongereni sana mungu awabariki na awajalie furaha tele katika maisha yene, kaka Michuzi tunaomba utuwekee picha zaidi, wazazi wa bi harusi hatujawaona pls michuzi

    ReplyDelete
  12. Namsupport huyo hapo juu wakristo hatu vai ushungi wala kanzu kwenye harusi

    Tunajua maana ya shella na nguo nyeupe kwetu sio kila gauni laenda tu

    ReplyDelete
  13. Uncle Michu, huyo msimamizi wa bibi harusi ni Nurubibi au???tupe basi masnepu zaidi...

    ReplyDelete
  14. Kikwete naona hapo baba na pinda mugongoooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo

    ReplyDelete
  15. nataka kumjibu huyo aliyesema kwamba sisi wakristo hatuvai kila gauni kwa sababu unajua maana ya shela. mimi ninavyofahamu shela nyeupe inavaliwa na mwanamke ambaye yuko chaste, untouched..nk, wangapi unaowajua wewe ambao ni wakristo wameolewa mabikira? acha za kuleta hapa. waislam wenye uwezo harusi inaanzwa na ndoa(aqdi) pale bi harusi anavaa gauni la rangi moja na hijab, ukitaka kuita ushungi haya, ukitaka kuuita shela haya, maana shela ziko za aina nyingi za kujitanda na kuachia kichwa wazi na bwana harusi anavaa kanzu au joho. kwa wenye uwezo wao wanaendeleza libeneke kwa kuwa na reception, na hipo ndipo bwana na bibi harusi wanavaa western style suti na shela.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...