mhariri wa picha wa gazeti la habari leo athumani hamisi akiwa amelazwa hospitali ya muhimbili kitengo cha mifupa ama MOI. hali yake inaendelea taratibu, inagaw bado ana maumivu makali kichwani na shingoni, na pia mawasiliano ya mwili wake kunzia kifuani kwenda miguuni ni hafifu kwa kile madaktari walichoeleza kuumia kwa mshipa wa fahamu nyuma ya shingo.
mipango inafanywa na mwajiri wake tanzania standard newsapers mgonjwa apelekwe nje ya nchi kwa matibabu zaidi, na endapo madaktari wanaomtibu wataafiki safari hiyo inaweza kuwa wakati wowote kuanzia kesho. kampuni ya vodacom imeeleza nia yake ya kusaidia gharama za safari hiyo, kwa mujibu wa mkuu wa kitengo cha uhusiano, mwamvita makamba.
globu hii ya jamii kwa niaba ya wadau wake wote inamtakia mpiganaji athumani hamisi nafuu ya haraka

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Tunamwombea kwa Mungu Athumani matibabu mema apone na arudi salama ofisini aendelee kuchapa kazi kama ilivyokua siku zote.

    Wanablog tumuombee mwenzetu apone haraka.

    Our Prayers are with You,
    Jiang & Sixtus.

    ReplyDelete
  2. Tunashukuru kwa taarifa. Ninamwombea apate nafuu mapema. Nimefurahishwa na moyo wa TSN wa kujali wafanyakazi wake.
    Mdau
    http://drfaustine.blogspot.com/

    ReplyDelete
  3. Hivi Tanzania hatuna Patient Right kama Privacy? Maanake mwenyewe hajitambui na sidhani kama yeye au familia yake iliidhinisha hizi picha. Katika nchi za wenzetu watu wanakuwaga matajiri kwani wata-SUE hospitali na waliomuanika hewani bila idhini yake. Sidhani kama angependa dunia imuone katika hali hii. Anyway I wish him a quick recovery Mungu amsaidie aweze kupona haraka.

    ReplyDelete
  4. Mungu amsaidie apate nafuu ya haraka na kurejea kazini. Naomba kuliza swali hivi huyu mbali na kuwa mpiga picha (mwanahabari) ni mpiganaji wa nini?

    ReplyDelete
  5. Wadau tunamuomba mwenyezi Mungu amsaidie Mpiganaji apate wadhili haraka ili apatiwe matibabu apone Sie tupo pamoja nae kwa Maombi Ishaallah atamsaidia atpona na kurudi nyumbani salama

    ReplyDelete
  6. Mungu akusaidie upone haraka ili urejee kulijenga taifa letu

    ReplyDelete
  7. Kama kawaida mwandishi kachukulia kuwa kila anayesoma taarifa hii anajua kilichomtokea mwenzetu huyu. Binafsi sijui. Kapigwa na majambazi? Kapata ajali ya gari? Kaanguka? Kwa nini usiwekwe hata mstari mmoja kuelezea kiini?

    ReplyDelete
  8. wishing you a quick recovery kaka Athumani!

    ReplyDelete
  9. Tunamuombea kwa mwenyenzi Mungu.

    Wewe al Musoma kama husomi kila siku humu basi usikurupuke tu nakulaumu...Follow up na past topic utaelewa what happened to this guy

    ReplyDelete
  10. kaka athuman mm naamini mungu anakupenda sana tena anampango na maisha yako hivyo sisi tunakuombea uzima upone. Mungu bni mwema sana.

    wishing you quick recovery bother Athuman. kuwa na imani utapona

    ReplyDelete
  11. Pole sana kaka,you will be ohk.we lav u

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...