Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimu wajumbe wa mkutano wa Halmshauri kuu ya CCM muda mfupi kabla ya kuendesha kikao hicho mjni dodoma leo.Wengine katika meza kuu ni Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume,Katibu mkuu wa CCM Yusuf Makamba na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi taifa akiwmo Waziri kiongozi wa Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha na Mzee John Samuel Malecela wakijiandaa kwa kikao mjini Dodoma
Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa Mzee Kingunge Ngombale Mwiru na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee David Cleopa Msuya wakijadiliana wakati wa Mkutano wa halmashauri kuu ya CCM taifa uliofanyika dodoma leo.
Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Nape Nnauye na Dr Emmanuel Nchimbi wakijadili jambo wakati wa kikao cha Halmashauri kuu ya CCM inayofanyika mjini dodoma leo


Namuona hapa 'Barua Pepe'akitoa cheko babu kubwa la kinafiki kwa mtu aliyemtimua uanachama.Kweli siasa ni mchezo mchafu.
ReplyDeletekweli wapemba wanajuana kwa vilemba
ReplyDeleteMichuzi picha nimezikubali sielewi nini kinaendelea dodoma
ReplyDeleteHiii ndio inatakiwa
TO ALL NALITOLELAS MIMI NI PETER NALITOLELA NAWATAFUTA NDUNGU ZANGU WALIOSOMA MZUMBE CHUO KIKUU....!MICHUZI NISAIDIE TAFADHALI.......
ReplyDeleteHata mimi ni Peter nalitolela nimemaliza mzumbe chuo kikuu last year tulikuwa na migomo ya kila mara lakini inshaalah tumemaliza. Hee michuzi kumbe kina Peter Nalitolela tupo wengi naona na mimi ninaishi Mbagala basi nimepata muda wa kuwasalimia kina Nalitolela wenzangu H.School nimemalizia St. Antony Mbagala najua watu wengi mtanikumbuka ingawa hatufahamiani lakini naomba wote nyie kina Nalitolela humu kwenye blogu tukutane inawezekana baba yetu ni muhuni kawachalaza mama zetu halafu katupa majina yanafanana mbaya zaidi katuweka katika mazingira ya kusoma Chuo kikuu kimoja Mzumbe sasa sijui ni uchawi ama ni nini? Mbona tunaanzakujuana leo na tumemalizia chuo kimoja? Mimi naona ni Uchawi...! halafu wote tulikuwa na akiri sana darasani!
Unafiki unapokubuhu unaleta kichekesho.
ReplyDeleteOnly in CCM you can be sacked and afford a smile like it aint shit.
Kila la kheri katika mpambano usio na kichwa wala miguu.
Huyo mmoja si tunaona wamemuangua uanachama? Au unaweza kuondolewa nusu na nusu uwe?
ReplyDeleteAHHHHHUUUUGHHH CCM
Chama bomba sana hiki.......toka usitoke .....
nimekubali S!S!eM wanajua kuweka mambo sawa!
ReplyDeletekwani magazeti yanavyochonga na jinsi hapo watu wanavyotabasamu waweza jua UkWELI wa mambo!
...!!
Zimwili likujualo kaka!!! yaani tungekuwa na vifua vya vioo sijui tungeona nini kwenye nyoyo zao!!
ReplyDeleteKweli siasa ni mchezo wa kinafiki!!
Wadau napenda kuuliza kama mtu anaongoza taasisi yenyewe wendawazimu!! yeye kama kiongozi atakuwa nani!!
Kazzy
mi naona siku wakikutana bush na osama usishangae wakapiga story na kucheka sana,siasa mchezo mchafu,wananch yetu macho
ReplyDeletesasa hapo wanapiga story gani?
ReplyDeleteAJENDA YAO KUBWA KATIKA KIKAO HICHO NI JINSI GANI WANAWEZA KUWALINDA NA KUWATETEA MAFISADI DHIDI YA WANANCHI.
ReplyDeleteAnonym: 9:08pm Kiongozi wa wendawazimu anaitwa MWEHU
ReplyDeleteSasa nyie ndugu zetu kina Nalitolela hili ndo wazo la busara, sasa kama mpo wengi kiukweli na hamjuani ni busara kutafutana na kutambulishana hasa wewe uliyeandika hii comment yako hapa, ndo unaonekana wewe ndo hutambuliki ukooni kiasi sq (x2)wako hakutambui na vile wewe unalugha mbofumbofu huwa patiner wako hapendelei, anaona kama unamchafua kila unapojaribu kufunua ubongo wako hapa. Ila hapa nimekusifu kidogo kwani nadhani ule ushauri niliokupatia kwenye post(comments) ya mr Blue akirejea marekani, hakuna anaelipia jina kodi TRA HIVYO NI HURIA MTU KUITWA JINA IKIWA SIKAMPUNI. naona unaufanyia kazi Big up kama kweli unatafuta nduguzo kila la kheri, ila taratibu maana nyie watoto wa nje huwa mnamakeke sana mnapotaka utambulisho kwenye familia na wanaotakiwa kukupokeeni pia huwa wanakuwa na mtihani na maneno kidogo hivyo. kila la kheri kwenye kikao chenu cha kutambulishana kina Nalitolela's msije mkoozeshana au kuoana ndugu wa baba mmoja kina aunt na mama zenu wakakosa pa kuweka nyuso zao.
ReplyDeleteHuwezi siasa usiingie wala usichangie jambo utabaki na aibu.
ReplyDeletehivyo vicheko ndo vinatakiwa sasa kwenye siasa.
Macho ya Nchimbi mmh!!
ReplyDeletesiii mchezo,,,ivi uyu Nape Nauye ni mtoto wa yule jamaa wa mwanzoni ivi??alikua waziri sijui nini??
ReplyDeleteheeee sarogate,,,siasa za inji hii
Kaka Michuzi Naomba Unitoe Utata Ukiwa Kama Mkuu wa Nanilii Najua Kabisa Utakua Ni Mwanachama Wa CCM Kwani Najua Huwezi Kua Mkuu Wa Nanilii Bila Kua CCM.Utata Nilio Nao Ni Hivi Ni Kwa Nini Vikao Vyote Na Hadi Hiki Hapa Rais Karume Hajawahi Kuonekana Akiwa Na Hio Shati Ya CCM? Hivi Ni Maamuzi Ya Mtu Kuvaa ?Walah Sijawahi Kuona Katika Vikao Vyote Karume Kavaa Jersey Ya CCM Au Mwenzetu Sio CCM Wanamlazimisha?? Ukinitupa Ok Ila Utakua Umenisoma
ReplyDeleteMmh huu 'Uhuru Maoni' huu, mtamu japo mchungu!Kweli kazi ipo hasa kwa wenye 'fikra za kigrafu'!Hebu cheki uchambuzi huu wa mwanablogu wa Kisauzi:
ReplyDeletehttp://pitsotsibs.blogspot.com/2008/09/zapiros-cartoon-strong-message-of.html
Hizo Picha mbili za mwisho USANII mtupu!!!! Hiyo ndio ile kitu tunayoiita "for public image"!!!
ReplyDelete