Kumbukumbu ya baba yetu kipenzi
Maabadi Ramadhan.


Imepita miaka 20 tangu ulipoiaga dunia ingawa kwenye kumbukumbu zetu bado inasikika kama ni jana tu, kwani upendo, busara na ucheshi wako kwetu havitasaulika kamwe.

Tunataraji re-union siku moja sote tutakapoitwa mbele ya haki.
Mwenyezi Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi,
Amina.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Dah! Huyo ni Maabadi yupi?. Ni yule aliyekuwa anaishi Chmbagerni Flats Tanga miaka ya 1976/78. Hebu ndugu yetu uliyeleta hiyo picha na wengine kama wewe muwe mnatoa details za ziada watu kuweza kumtambua mtu. Hasa ukitilia maanani mtu aliyefariki miaka 20 ilyopita wasomaji wengi wa sasa si rahisi kumtambua kwa sura, kwani wengi walikuwa bado wananyonya au kindergaten, unless kama alikuwa ni mtu mwenye jina kuu linalotambulika kirahisi katika jamii. Na imani kama ni yule aliyekuwa Chumbageni NHC Flats(High Cost) Tanga tu wachache tunaosoma blog hii tunaoweza kumkumbuka. Mwenye enzi mungu aiweke roho yake mahala pema pepeoni- Ameen

    ReplyDelete
  2. Mdau hapo juu Kumbukumbu haitaji detail nyingi hasa ukizingatia Marehemu amefariki Miaka 20 iliyopita, ni kutia majonzi familia kama wataweka kila detail kwenye kumbukumbu.

    Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi.

    Mjusi

    ReplyDelete
  3. Hujakosea kaka ndiye mwenyewe. Samahani kama kuna mapungufu ya maelezo na mimi ndiye first born wake.

    ReplyDelete
  4. Mungu aibariki familia yenu na kumjazia marehemu rehema.

    ReplyDelete
  5. Mwenyezi Mungu azidi kumuangazia mwanga wa Milele na tumuombee baba yetu,mbarikiwe wana familia.
    tx.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...