juu benki ya lehman brothers na chini ni jezi za jamaa
Brother michuzi,
Hebu weka hii issue ndogo tu lakini imenifurahisha sana sana na hapa nilipo nagoja tu ije kuwa kweli.
Issue yenyewe ni kuwa naamini umesikia hali ngumu ya uchumi duniani kwa wakati huu makampuni mengi yamefilisika, na ni jana tu bank ya Lehman Brothers yenye makao yake makuu US imefilisika.
Sasa kuna taarifa za kuaminika kuwa sponsor wa manuare AIG wana connection au deal na Lehman Brothers, jambo ambalo huenda likasababisha manuare kupoteza sponsor wao au kusimamishwa kwa muda.
Kicheko changu ni kuwa huenda weekend hii manuare nao wakawa kama west ham kubandika viraka katika shati zao!
habari kamili bofya hapa
ha ha ha ha ha ha ha ha!
can you imagine kama ikiwa ni kwa kudumu wapenzi wao wote wenye shati zao mpya itabidi wabandike viraka!
ha ha ha ha ha ha ha ha ha!!!!!
Mdau Zenji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Mdau uliendika hiyo post unanichekesha!Do you really think if they go bankrupt manchester wont get sponsor ship the next minute!Sio Mlandege hii mzee,Haya mkuu mbaya wako akikuombea mabaya basi we mwombe mazuri!Mimi nakuombea mwenyezi mung akupe upeo

    William uk
    united for life

    ReplyDelete
  2. Sasa cha kufurahisha hapo nini?
    Upeo mdogo wa akili.
    Watu wanakosa ajira we unafikiria Manchester wanaweka viraka, hovyo kweli.
    Hujui hata kutofautisha 'issue' za kuwa 'serious' na masihara!

    ReplyDelete
  3. Kuna sponsors kibao na wako tayari kutoa zaidi ya AIG. Kufa kufaana

    ReplyDelete
  4. Nitawajibu wote walioweka comments zao mbili hapo juu. kwanza wewe wa pili ndio ambae huju issue za serious na masihara! hii issue imeletwa kwa mtani wa manuare. wewe ndio mwenye upeo mdogo wa akili. Na kwa nini nijali watu wafanyakazi wa city wanaopoteza ajira, watu wanakufa sehemu tele za dunia kila siku na wafanyakazi wa city never gave a damn. Tuulize tukueleze namna hawa jamaa wanavyo behave na isirafu wazifanyazo hapa city. they live like there is no tomorrow. Na dharau ndio usiseme!!!

    Mdau wa kwanza atleast imepata point yangu, najua kama united watapata sponsor mwengine na hata west ham watapata, joke yangu ilikuwa ni kuziba sponsor kwa muda na ndio maana nikasema huenda weekend hii mtabandika viraka; kwa vile sio rahisi ku drop sponsor mmoja na kupata wa pili papo hapo.

    Mengine nyote wawili nawaambieni grow up!!!! Joke is a joke!!!!

    ReplyDelete
  5. NAOMBA NIMREKEBISHE MTOA HABARI AIG NI INSURER KILICHOFANYIKA NI KWAMBA BAADA YA HAO BROTHERS KUTANGAZA KUFILISIKA,AIG WAMETOA BILLIONI 20 KUKAVA ANY DEFFICIENCY AMBAYO INVESTORS WANGEINCUR,UNAJUA BANK ZA WENZETU ZINAKUWA NA BIMA INCASE MAMBO KAMA HAYA YAKITOKEA,KWA HIYO JAMAA ALITAKIWA AELEWE KINACHOENDELEA KABLA YA KUKURUPUKA

    ReplyDelete
  6. ananymous wa septer 16 8:47 aloandika kwa herufi za kupiga kelele, naona huo ushauri uliompa aloleta hii topic nawe ungelifuata hayo hayo, kwani alochosema yeye ni pia soma website tele utaona kinachoelezwa.

    Watoaji mawazo wa kwanza na wa pili ni wapi mleta maoni alopowacheka walokosa ajira? alichokichekea ni man utd kuwa huenda wakajikuta hawan sponsor kwa kipindi (japo kidogo), pia washabiki wao watajikuta wana shati zisizofanana na timu yao, yaani out of date shirts!

    ReplyDelete
  7. msikose sponsor nyie nani bwana mbona west ham wamecheza juzi wameshonea jezi... nyi vipi si mmezikia XL chini ground ndege airuki oh credit crunch soo nyie pigeni trip tu mwishoe huko itakuw akama zim currency. Wapi tuaend ajamani kama nauli sh. 500 Damn pounds 500 mshahara wa mtu hapa UK kwa week

    ReplyDelete
  8. akina GT,KISHOKA,ICADON,PUNDIT na STEVE D wamekamua sana kuhusus hili kule kwa siku zote aka JAMIIFORUMS

    http://www.jamiiforums.com/habari-hoja-mchanganyiko/17999-lehman-brothers-your-predictions.html

    asante michu kwa kutuletea hii

    ReplyDelete
  9. punguzeni chuki west ham sio man utd. haraaaa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...