JK akimfariji Maureen Mwanawasa mke wa Rais wa Zambia Marehemu Levy Mwanawasa wakati wa Mazishi ya kiongozi huyo yaliyofanyika jijini Lusaka jana.
JK akiwafariji watoto wa Marehemu Dr. Levy Mwanawasa wakati wa mazishi ya Rais huyo wa Zambia yaliyofanyika katika viwanja vya embassy Park jijini Lusaka
JK akimfariji Patrick Mwanawasa mtoto wa kwanza wa kiume wa Rais wa Zambia Marehemu Dr. Levy Mwanawasa,wakati wa mazishi ya kiongozi huyo yaliyofanyika jijini Lusaka
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, JK, na Mama Salma Kikwete wakiongozwa na askari wa jeshi la Zambia kuweka shada la Maua katika kaburi la Rais wa Zambia marehemu Levy Mwanawasa,mjini Lusaka jana.

JK na Mama Salma Kikwete wakitoa heshima katika kaburi la Rais wa Zambia Marehemu Levy Mwanawasa mara baada ya kuweka shada la maua katika kaburi hilo eneo la Embassy Park jijini Lusaka
Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa wakienda kuweka shada la maua katika kaburi la marehemu Dr.Levy Mwanawasa
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole Rais wa kwanza wa Zambia Dr.Keneth Kaunda wakati wa mazishi ya Rais wa Zambia Marehemu Dr. Levy Mwanawasa,yaliyofanyika jijini Lusaka Zambia jana.Rais Kikwete amerejea jijini Dar es Salaam jana jioni
Askari wa jeshi la Zambia wakiwa wamebeba jeneza la Rais Wa Zambia Dr.Levy Mwanawasa tayari kwa mazishi yaliyofanyika katika viwanja vya Embassy Park, jijini Lusaka, Zambia jana.
Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Zambia Dr.Levy Mwanawasa muda mfupi kabla ya kushushwa kaburini jijini Lusaka Zambia jana wakati wa Mazishi ya kiongozi huyo za taifa la Zambia
Mjane wa aliyekuwa Rais wa Zambia Maureen Mwanawasa akiwa katika majonzi wakati wa mazishi ya mumewe
Mjane wa aliyekuwa Rais wa Zambia Mama Maureen Mwanawasa akiwaongoza wanae kuweka shada la maua katika kaburi la Marehemu Dr.Levy Patrick Mwanawasa
Mjane wa aliyekuwa Rais wa Zambia,Mama Maureen Mwanawasa akiwaongoza wanae kwenda kuweka shada la maua katika kaburi la baba yao Marehemu Dr.Levy Patrick Mwanawasa aliyezikwa jana jijini Lusaka Zambia.
Rais wa Kwanza wa Zambia Dr. Kenneth Kaunda na Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa wakati wa Mazishi ya Rais wa Zambia Dr.Levy Mwanawasa. picha zote ni kwa mujibu wa mdau Freddy Maro wa Ikulu aliyeshuhudia mazishi hayo

This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteTangulia Mwanawasa, nenda Mwananwasa...kamwambie mwalimu huku kumeharibika, TZ mafisadi kibao, viongozi wa afrika wanang'ang'ania madarakani mpaka wanamwaga damu ya wasio na hatia.
ReplyDeleteWadau ehe! Mama Salma mlimsema hashauriwi kuhusu kivazi, sasa huyo anaemshauri sasa ivi anachemsha...Bi Mkubwa kavaa suruali tena yupo kwenye mfungo wa ramadhani (wadau msitafsiri vibaya kusema ndani ya ramadhani) ila nazungumzia maadili ya mwanamke wa kiislam esp kwenye msiba.....Bi Mkubwa kivazi hakijatulia.
TUSEME NINI BWANA!! HATUNA LA KUSEMA BALI TUNASHUKURU. NI WEWE ULIYETOA NA NI WEWE ULIYETWAA.
ReplyDeleteHAKIKA DUNIANI SI KWETU
jamani big up to mama Kikwete, nathani amepunguza uzito na anaoneka presentable sasa, aendelee hivyo hivyo mambo ya madhahabu kilo tatu sidhani kama ni hadhi yake, aendelee kuvaa hivyo hata kama kitenge lakini sio na mabling meengiiii!
ReplyDeleteRIP Levy Mwanawasa. Watoto wadogo bado jamani.
ReplyDeleteHeshima yako kaka,naitwa Joel,mdau toka a town,nakupa saluti kutokana na blogu yako makini inayoelimisha jamii..Nimefungua blogu yangu hivi majuzi,ambayo ni chikoma.blogspot.com ,naomba uiweke hewani ili wanajamii waitambue.Ahsante
ReplyDeleteMungu amlaze marehemu mahali pema peponi na aibariki nchi ya Zambia iweze kupata kiongozi mwingine jasiri na mchapa kazi asiye na makuu
ReplyDeleteni Njia wote tunapitia,Pumzika salama.Mh our presida anatabasamu sana hata kwenye kutoa pole?Ni sawali nauliza wadau,sioni huzuni usoni mwa Mr hon presida wetu.Ni bora sasa awe siriasi kama Mkapa at least huwez jua furaha wala huzuni
ReplyDeletehe he, nyie vipi mwenzenu kasmile anatongoza. kwani nyie inawausu nini. apa duniani ukiondoka unawaachia wenzio ujue. Na uyo anaezungumzia suruali ya mke wa rais, we kwani mke wako kavaa nini. Bongo si tumeamua kuiga watu wa magaribi sasa! angalia wenzetu. gauni la mama mjane linatisha.
ReplyDelete