

Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Salaam Aleikhum wadau mimi nauliza Rais na Makamu wake wanapofutarisha watu hizi pesa huwa ni zao mfukoni au za Serikali hapo sielewi nisaidieni jamani maana mimi mwenyewe huwa najaribu kwa Familia na joto ya jiwe naliona je hawa wakubwa vipi?
ReplyDeleteSheikh Issa nbona lugha unaiharibu?
ReplyDeleteFutari= chakula cha kufungua swaumu
Futuru= kitendo cha kufungua swaumu
FUTURISHA = ni kitendo cha kuwafungulisha swaumu waliofunga na sio KUFUTARISHA
Ni kwa nini futari hailiwi mezani?Ndiyo,zamani jamii zetu zilikuwa hazina mambo ya meza na viti,pia msikitini HATUSWALII kwenye viti kama wakristo TUFANYAVYO.Sasa ni kwa nini futari nayo iliwe kwenye majavyi while we aint in the msikiti?Naomba mnisaidie
ReplyDeletesalaam,ndugu mbigiri hiyo tabia ya kula chini ni sunna kwa waisilamu na sio kama unavyofikiria labda ni umaskini au vipi nadhani utakuwa umenielewa.
ReplyDeleteraisi anapofuturisha wananchi, hutumia fedha zake mwenyewe, au fedha za serikali?
ReplyDeleteMbona hamuulizi mapambo ya krismas kwenye majengo ya serikali yanatoka wapi?Mnauliza futari tuu!!
ReplyDeleteFutari na futuru inategemea ulipo.
ReplyDeleteUnguja tunasema saa ya kufutari
Bara wanasema saa ya kufuturu
Lengo ni hilo hilo moja
Sisi tuna tungule
bara mna nyanya.
Ukija Unguja baada ya muda utazoea, na muunguja akienda bara baada ya muda keshazoea, kwahio Michuzi alivyoandika hakuna kosa lolote
najuwa sio umaskini,Nachouliza ni kwa nini suna haiwezi kuliwa mezani?
ReplyDeleteFungu la futari hiyo linatoka ofisi ya makamo wa raisi
ReplyDeleteUnguja kuna mfereji
Bara kuna bomba
Unguja kuna msingi
Bara kuna mtaro
Mmenifahamu hapo??
Mbigiri jifunze kwanza maana ya suna
ReplyDeletesuna = nikitu kilichopendekezwa lakini ukikosa haidhuru kupata thawabu,
suna= ukifanya hivyo ndio unaongezewa kidogo katika thawabu zako.
Kwahio futari inaweza kuliwa mezani na ukapata thawabu.
Suna siyo chakula wewe, suna ni mwenendo wa Mtume. Kwa hiyo wanafanya hivyo kwa sababu Mtume alifanya, lakini najuwa unafahamu wanaweza kuwa na fenicha kali zaidi ya zako, si umeona vyeo?
ReplyDeleteWengine wasiojisikia kufuata suna hupasha mezani si neno.
Na ukiweka mabenchi utarukuu na kusujudu vipi?
ndugu mbigiri bado nipo na wewe bega kwa bega,sunna ni jambo ambalo ukifanya unapata thawabu ukiwacha kufanya hupati thawabu wala dhambi you get me,kama vile kula kwa kutumia mkono, mtume wetu muhammad (saw) ametuhimiza wakati wa kula tutumie mkono kuliko kijiko, sababu moja kubwa unapotumia mkono unakifanya chakula kiharibike upesi kabla ya kufika tumboni.mpaka hapo utakuwa umenifahamu tosha japo kuwa umeuliza wewe lakini faida wamepata wengi,ramadhan kareem.
ReplyDeleteKama ukisema kiharibike upesi watu wanaweza wasielewe, basi Digestion. waende kusoma kamusi. Digestion inaanzia mkononi.
ReplyDeleteExperiment: pika cahkula tufanye maharage, kisha pakuwa kwenye bakuli mbili. Moja gusa maharage kwa vidole nyengine usiguse. Yaweke baada ya muda, maharage yaliyoguswa yataanza kutoa harufu ya kuchacha.
Kuna bacteria mkononi? ndio lakini hawana madhara ni kama wale wa chanjo. Wengine wamejaa mwilini lakini sio wa maradhi.