Wana FC BONGO Helsinki Tuna furaha kubwa ya kuwaalika wote mnaopata ujumbe huu, kwamba siku ya jumamosi tarehe 11.10.2008 kuanzia saa mbili usiku katika Ukumbi wa RAUHAN ASEMA Helsinki tutasherehekea rasmi ushindi wetu wa kunyakua kombe la HELSINKI PREVENTION CUP.

Vinywaji, nyama choma na Disco la nguvu litakuwepo hapo.

Mwaliko rasmi uende kwa wana KILIMANJARO wa Stockholm na wana TAS wa Tampere pamoja na kwa mkuu wa wilaya ya nanihii maana tumesikia atakuwa anga hizi hivi karibuni katika vekesheni.

Hakyanani tena tunawaahidi ndugu zetu hawa kuwa siku hiyo watakula nyama choma mpaka washindwe wao na sio vibawa vya kuku au pilau bila nyama.
Madijei maarufu wa kibongo akina EZZA, RUMMY,EDO na ALIKO watakuwepo hapo kumwaga vitu vyao, wasanii wa Bongo flava akina MAD ICE, OCG na TONY LUV watakuwepo pia kutumbuiza katika tafrija hiyo...
Kila anaepata ujumbe huu anaombwa amjulishe mweziwe. Msije kusema ooooh hamkusema mapema. Habari ndiyo hiyo mapemaaaaaaaaa....

Pichani hapo wana FC BONGO wakikaa mkao wa nanihii wakisubiri kombe lao baada ya kuwabamiza Nigeria bao mbili katika fainali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Asante kwa mwaliko, tutawasilisha kama kawa tuje kufurahi kwa pamoja.

    ReplyDelete
  2. Jumamosi ni tarehe 12 na sio 11
    Nilitaka tu kurekebisha manake kuna watu wangeweza kuja kesho Ijumaa
    Ahsante

    ReplyDelete
  3. Jumamosi sio tarehe 12 wala 11. Ni tarehe 13

    ReplyDelete
  4. Jumamosi ni tarehe 13.Unaweza kudai kusahihisha kumbe swaumu.Bongo hamna lolote kiboko yenu Kilimanjaro Stars ya Sweden.

    ReplyDelete
  5. Jumamosi tarehe 11 ya october sio mwezi huu, hebu someni vizuri.

    ReplyDelete
  6. I hope mtachinja Ng'ombe. Si ndio nyie wapenda nyama au nimekosea? Hilo pilau tunataka nyama kila mkono mtu akipiga anatoka nayo.

    Tunataka tuje tuone mfano wa pilao la nyama niaje?

    ReplyDelete
  7. Mkuu wa wilaya ya nanihii kama atakuwepo hapa helsinki wakati huo itabidi tumtayarishie extra ishuz.

    ReplyDelete
  8. Na watu wa tampere wanavyopenda nyama choma watakuja mapemaaa kabla ya saa mbili wawahi kufaidi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...