Habari kaka Michuzi,
Nitakuwa si binadamu aliyekamilika kama sitakushukuru kwa kulifanyia kazi ombi langu. Nashukuru sana kwa msaada na ninaamini Inshallah Mungu atajibu maombi yangu. Nashukuru kuwa wengi waliojibu wameelewa situation niliyo nayo na nyingi ya comments zina nia ya kunisaidia.
Nashukuru sana pia wale waliochukua muda wao kuniandikia e-mail. Mungu awabariki sana kwa ushauri, busara na moyo mlionipa.
Ningependa tu kuomba samahani maana inaelekea labda kujieleza kwangu kidogo kumefanya watu wasielewe. Nimejieleza zaidi kuhusu status yangu kwa ajili nilidhani itakuwa vizuri kuwapa watu background yangu. Sikuwa na nia ya kuonyesha unyanyapaa.
Naomba mnisamehe sana kwa hilo.
Pili mimi sijamlaumu mtu kuwa ameniambukiza HIV la hasha. I made peace with myself muda mrefu uliopita and I know it's not healthy to dwell on blames. Kilichotokea kimetokea, I had the responsibility of making sure I am not infected, lakini sikufanya hivyo and I have no one to blame but myself.
Kuhusu kum-expose ex kwa kweli inaniwia vigumu. Hivi Tanzania kuna law yoyote kuhusu mtu anaeambukiza HIV kwa makusudi? Na hata kama ipo, si kuna sheria inasema uhuru wa kupima anao mtu akiamua hataki kupima huwezi kumlazimisha. Sasa hata nikisema nimu-expose ex-husband, si ana haki ya kukataa kupima au kuonyesha records zake? Then it will be my word against his, kwa kweli hiyo courage ya kulumbana nae sina.
Ninachoamini kila jambo mtu alitendalo duniani, jema au baya basi mwenyezi Mungu hulipa. Kwahiyo naamini na yeye malipo yake yapo. Kama hujapata tatizo nililo nalo ni vigumu sana kulielewa.
Nimejua kuwa nimeathirika miaka mitano na miezi kadhaa iliyopita. Niliolewa nikiwa na miaka miaka 27, na sasa nina miaka 35. Mume tumeachana nae miaka 3 iliyopita. nilijitahidi sana tuweze kuishi pamoja ili tusaidiane lakini ilishindikana. Ilikuwa ngumu sana. Na maamuzi yote niliyofanya, niliomba sana Mungu anipe njia iliyo sahihi.
Naamini maamuzi yote niliyoyachukua ilikuwa ni muongozo wa Mungu. Si kweli kwamba simjui Mungu. Na bila kuwa na imani na kumuomba sana sidhani kama ningekuwa hai leo. Mafundisho yanakataza kuidhulumu nafsi, ni mara nyingi mawazo hayo yalikuja kichwani, lakini nilipokumbuka makatazo ya Mungu, sikufanya hivyo.
Kwa hiyo wapendwa, Mungu ndie ngao yangu kuu katika maisha yangu kabla na baada ya kuathirika. Najitunza, nafanya mazoezi, nakula vizuri na ninatumia dawa. Kuhusu jinsi ya kuishi hilo ni my number one priority. Namuomba Mungu aniweke mpaka hata miaka 90.
Kutafuta mwenzi yaweza onekana kama ni upuuzi/uhuni/etc, lakini nimejitahidi sana, upweke unasumbua, unasumbua sana jamani. Nia hapa si ngono.
I need company, I need to feel loved, nahitaji mtu wa kunijali na wa kumwambia kila nililo nalo moyoni.
When all my friends are at their homes, and I am alone at home watching a movie, reading or just lazing around, pale ndio huwa naona upweke wa hali ya juu.
Labda tuko tofauti kuna wanaoweza kuishi na upweke lakini mie nimeshindwa. Na ndio maana nikapata courage ya kumuandikia kaka Michuzi apost ombi langu. Haukuwa uamuzi rahisi. Nina imani nitafanikiwa.
Asanteni sana wapendwa.
Mdau HIV+ve


Pole sana kwanza kwa jinsi unavyoandika inaonekana kichwani zipo na mtu kama wewe ilitakiwa kuwa hazina kubwa kwa taifa. Pia umenishtua usimuone mtu barabarani ukavamia maanake huwezi jua mtu ana matatizo gani. Nadhani kizazi hiki ukishapata mpenzi wako basi inabidi ni uaminifu tu. Inaonekana una peace, je ina maana kwamba wewe ndio ulipata ugonjwa kwanza?
ReplyDeleteKuhusu upweke kwa wengine wetu hilo ni jambo la kawaida. angalau labda TZ una ndugu, jamaa na marafiki. Can you imagine kuwa nchi za watu unalazimisha kutafuta hata mtu wa kuongea nae kiswahili?? Anyway dawa ya upweke ni ndugu, jamaa na marafiki. Social groups and activity mbalimbali kama sports, gym, movies
Na hope utapata mtu utakayoweza kushare life together. Kwa jinsi ulivyojieleza unaonekana uko mtu poa na Mungu akupe nguvu
Pole sana Dada yangu, I can imagine your situation. Hata mimi nina imani utafanikiwa, I wish you all the best!
ReplyDeleteMdau,
Gothenburg,
Sweden.
Umemalizia kwa signature,
ReplyDelete'Mdau HIV+ve' na hivyo kurudia kosa ulilokatazwa / uliloshauria na nafikiri ajiitaye Nyakatukule, la kujitambulisha kwa ugonjwa wakati unasifa nyingine nyingi za utu wako kama binadamu.
Nadhani naona sasa kuwa hii ni fiction au utunzi ili upate mawazo ya watu. Nami nashukuru kwa kutupa changamoto ya utunzi wako.
HEE WEWE MAMA USHAURI WANGU WOTE UMERUDI TENA...!
ReplyDeleteWEWE DADA SASA NAONA AKIRI INAANZA KUKURUKA NIMEKUPA USHAURI MZURI TENA WA BURE, ACHANA NA NGONO LAKINI BADO UNAENDELEA KUKUNWA NA HAMU YA KUJAMIIIANA INGAWA UNAJUA MADHARA YAKE NA YANLIYO KUPATA, UPWEKE UPWEKE HUONI KAMA UTAZIDIWA NA KUCHANGANYIKIWA ZAIDI PINDI HUYO MTU UTAKAYE BAHATISHA KUMPATA MKAFARIJIANA HALAFU SIKU TATU AMA WEEK AKAVUTA? HUONI KAMA UTARUDI TENA KWA MICHUZI KUANZISHA MIJADARA ISIYO NA KICHWA WALA MIGUU.BY THE WAY KUNA ZERUZERU MMOJA NI MSHKAJI WANGU YUPO NGARA KARAGWE HUKO ANA NGOMA ANAMIAKA 39 NI MTU POA HAJATAILI NA NI HANDSOME SANA TU UNATAKA NIKUPE NUMBER YAKE UONE KAMA MTAWEZANA?NI MKIMYA NA MPOLE SANA NA INASADIKIKA ANA KIGONGO KIKUBWA SIYO MCHEZO KAMA UTAPENDA JAMAA HACHOKI KUTOA DOZE ASUBUHI MPAKA USIKU WA MANANE YUPO TU.MADACTARI WAMEMWAMBIA ATAISHI ZAIDI YA MIAKA 10+. BASI POA NIJULISHE NDIMI NALITOLELA WA MUZUMBE CHUO KIKUU!
usikonde wala nini dada, Hukuomba kuwa hivyo, yote ni mipango ya Mungu, na wako wengi wenye matatizo kama wewe, wanaogopa tu hata kutafuta rafiki kama unavyofanya, wewe ni shujaa, na Mungu hamtupi mja wake, utafanikiwa. watajitokeza tu, wape mda, wanavuta courage kama uliyokuwa nayo. u r a strong woman, big up.
ReplyDeleteWadau (wa kwanza na pili)mliotangulia hapo juu nimependa maoni yetu.
ReplyDeleteKwa kuongezea tu, ni kuwa ukiendelea na utaratibu uliojiwekea sasa wa kuishi life to the full; kama kufanya mazoezi, kuhudhuria ibada etc iko siku tu utapata mtu makini wa kukupa company. Naelewa inaweza kuwa vigumu sana kuamini kwa sasa lakini kuna watu wenye busara, uelewa na upendo wa kweli kila mahali tulipo. Nina imani iko siku mmojawapo kati ya hawa wapendwa ataingia katika maisha yako.
Nakutakia Dada yetu kila la kheri katika mtihani unaopitia. Kikubwa cha kukushauri na nina imani unakifahamu au utakuwa umesha shauriwa tena na tena ni "usikate tamaa" ukiweza kushinda majaribu ya kutokukata tamaa kwa hakika maisha yako yatakuwa kamilifu zaidi na zaidi.
Soames,
UK.
Yaani huwa siandiki comments lakini huyu dada!. Nimependa sana maneno yako ya faraja na busara. Usiwe na wasi wasi nimesikia Dawa zinatoka karibuni lakini zitakuwa bei ghali mwanzoni. Usiwe na hofu na imagine mtu kuwa na tatizo hilo na pia na maneno matamu kama hayo. Siombei kuupata ugonjwa huu lakini kuna msemo usemao hujafa hujaumbika naheshimu hilo neno, nakumbukua nilisikia huo msemo zamani wakati nilikuwa central police jail kwa matatizo ya kusingiziwa na yalikuwa sio makosa yangu na nilikaa kwa usiku mmoja lakini nilifikiria mambo nengina kushukuru kila muda ulionao hiyo ilikuwa miaka 13 iliyopita. Naamimi dada yangu na huo ujasiri uliona utaishi miaka mingi sana kupita hawa wanaokusema na kunyanyapa. Huo ujasiri na matumaini uliyonayo ni treasure kubwa sana ambayo watu wengi wanakosa na kufa kabla ya siku zao. Umebarikiwa na mungu akubariki. Huku marekani nawajua watu wengi sana ambao wako +ve na wana afya nzuri na wanaujasiri kama wako na wameshaishi karibia miaka zaidi ya 20 na hivyo virusi na wananiambia kuwa wakienda kwa Doctor ndio kwanza wanakutwa undectatable. Mungu yupo amesikia vilio na sala nyingi kuhusu huu ugonjwa ambao unawapata watu wasio na haki.
ReplyDeletepole sasa dada.pamoja na dawa unazokula nakushauri utumie vidonge vinaitwa MARIANDINA.ni vizuri sana kwa ku boost immunity.huko bongo nasikia kuna mtu anavi import toka UK,jaribu kuvitafuta.nakutakia afya njema,be strong,be positive.
ReplyDeletepole mdada, Mungu atakusaidia, kwani ndie muweza
ReplyDeleteOhh pole sana dada yangu, hiyo ni sehemu ya maisha unapofikwa na tatizo inabidi uwe strong ili maisha yaendelee, pia uone huo ugonjwa kama marelia au cancer ambayo watu wanaishi nayo na wanaamani, Usiwe desparati kutafuta mtu ambaye atakuliwaza, muombe mungu sana sana amka usiku sali, nenda kwenye nyumba za ibada omba, fanya sana mazoezi utakuwa unachoka then unalala unapunguza mawazo, mpaka hapo ulipofikia unaonyesha unamatumaini, katika maombi yako mungu atakupa tuuu, amini maneno yangu kwani mungu ni mwema atakupa unayestahili na si mpita njia. Pole sana dada. Utapata tuu kazana na ibada.
ReplyDeletePole sana dada,rafiki wa kweli ambaye anakufariji wakati wote katika shida na raha ni mmoja tu yaani yesu kristu.Mjue yeye binafsi haijalishi upo katika hali gani."Anasema njoni enyi musumbukao na kuelemewa na mizigo mizito ya dhambi nami nitawapumzisha".Kumbuka miaka 2000 iliyopita pale msalabani alitubebea kila udhaifu likiwemo na magonjwa yote.Mpe maisha yako sasa ili uone mabadiliko katika maisha yako kwani yeye tu peke yake atakayekusamehe dhambi,atakupa uzima wa milele,atakuponya magonjwa yote likiwemo ukimwi,atakupa mahitaji yake yote,ataandika sheria zake zote moyoni mwako,atakupa roho wake mtakatifu ambaye atakufundisha yote na kukukumbusha yale yote ambayo yesu ameyaacha kwetu.Lisilowezekana kwa mwanadamu mungu anafanya.Tunaokolewa kwa imani na zawadi zote hizi zina kuja kwako ukiwa tayari kupokea fanya sasa hivi mungu anakupenda kuliko wewe unavyodhani.CHUKUA BIBLIA YAKO FUNUA WARUMI 10:9, Hapa haijalishi upo katika dini gani,dhehebu au kanisa gani dada.Mungu akutangulie katika yote
ReplyDeleteNi mimi
Tuwasiliane kwa ushauri zaidi
bqwerty@yahoo.com
Mpendwa,
ReplyDeletePole sana dada lakini nina imani kuwa utashinda tu. Kutokana na maelezo yako inaonyesha kuwa wewe ni mtoto wa Mungu kwani unamtanguliza kwa kila kitu na Yeye hatokutupa ukimtumainia na naamini imani yako itakufanikisha yote unayoyaomba hasa huyo mwenza ambaye atakuliwaza. Mpendwa katika Bwana, mimi nakuombea kwa Mungu najua pia kuna wapendwa wengine ambao watakuwa wamesoma kwenye blog hii wanakuombea pia. Unaonyesha kuwa wewe ni jasiri na umekubali kosa lako na kukubali hali uliyo nayo.
Nitazidi kukuweka katika maombi ili Mungu akujaalie ndoto yako iwe kweli ya kumpata mwenzio wa kuweza kuishi nae ambaye pia mtaweza kuwa na maelewano mazuri. Ubarikiwe na Bwana.
Dada usiumie moyo na jinsi baadhi yetu tulivyo kupokea lazima uelewe kuwa sisi kama binadamu tupo ktk mapokeo tofauti kila mtu anuwezo wake wa kupokea matukio ndio maana ukiangalia comments kuna waliokupa pole,waliokupokea kidini nk.mm nakushauri kama bado ujiunge na vyama kama vya Shidefa+ maana nina uhakika huko utapata wenza na ata ndoa maana tumeshuhudia mfano ndoa ya Ndugu.Kaaya huko.
ReplyDeleteusahuri wangu
ReplyDeletewewe hauna tofauti na mtu yeyote yule, na usijiwekee kuwa mpaka aliyeadhirika tu ndiye utaweza kuishi nae
bali hata mzima mwenye kuona mbele. kwani bora uwe na mpenzi utakaejuwa ameadhilika na ukawa nae mnatumia kinga kuliko kuwa na mpenzi ambae ukazania mzima na kumbe kaadhirika ukamwamini.
watu wakujuwa hilo najuwa ni wachache waliojariwa ila wapo usijari. amini utampata tena jipende zaidi ya hapo awali.
mimi ni mwanamke na pia siko nchini ila ningependa nikuone tuongee mengi ila wapi niko nje ya nchi. mimi ndiye yule nimetoa maoni yakuwashangaa wanaokwambia umrudie mungu kana kwamba uliwaambia umemkana.
Nalitolela it seems something wrong with you! Since niliposoma maoni yako kuhusu Mugabe kwamba unampenda kuliko Baba yako! Nilishangaa sana! Sio lazima ufungue mdomo wako kama huna cha kusema, kwa maoni yako ya sasa hivi inaonekana kama unamsanifu kiaina huyu Dada, sio vizuri ndugu yangu, hujafa hujaumbika, sijui kama wewe mwenyewe umepima.
ReplyDeletePole saana dada. Subira ndiyo silaha nzuri katka kila jambo.
ReplyDeleteLa muhimu: usipomfichua x wako basi ataendelea kufagia watu kuelekea kaburini. Okoa watu hao.
Japo unaamini malipo kwa Mungu kwa kila mtenda, pia ujue kuamrisha mema na kukataza mabaya imeamuriwa.
Kataza uuwaji huu. Jipe subiara, upige moyo konde, uwe jasiri, ujuwe utaliendeaje. Pata hata ushauri, nahisi watu wana fikra na hekima.
Unyanyapaa ni bora kuliko mauaji!!!
pole sana dada yangu ndio maisha Mungu anapanga na kupangua .sali sana na kumuomba Mungu akuwezeshe na kukulinda.Huyo mdau kwa jina la Nalitolela sidhani kama ana akili zote , na kama anazo basi alishakuwa taahira hapo zamani .kwa sababu mtu mwenye akili timamu hawezi kuongea mambo ya kishamba kama aliyosema yeye.yangemkuta angejua how it feels ukiwa na tatizo kama hilo .Mimi namshauri huyo mdau kama alikosa acha kufanya angeenda hata chooni akae apoteze muda wake kuliko kukaa na kuongea uchafu.
ReplyDeleteDada yangu usijali utampata mtu na mtaelewana sana , Mungu yupo na wewe .
Waonee huruma hao...inasikitisha kuonyesha kuwa miaka zaidi ya 25 lakini watu hawajui hata huu ugonjwa .....baadoo kabisa....Tanzania ...tunahitaji elimu ya huu ugonjwa sio utani
ReplyDeleteJipe moyo utashinda achana na hawa sio kosa lao ni kosa la knowledge yao
huye anayesema usiseme au usimalize na kuweka HIV+ ni mshamba....kwani hapa anaomba kazi anaomba na kutafuta mtu kwenye relationship ...na hata huku nilipo kwenye magazeti nilipo kuna ukurasa wa magay/ lasbian na waathirika na wote wanajitaja.
Hivyo kutumia sijui cheo chake kwa wakati huu si sawa......
You are in my prayers my dear
NALITOLELA huyu wa MUZUMBE UNIVERSITY/MZUMBE UNIVERSITY anaonekana hazimo hata kuandika Mzumbe, HAWEZI HUKO CHUO KIKUU ANASOMA NI? KUKARIRI VITABU TU! ANATUTIA AIBU WASOMI WANZAKE. Dada you semees brilliant, and you have something upstairs, achana na NALITOLELA chizi. muombe mungu na utaishi maisha marefu, kwani sote kama tumejitahidi sana ni miaka 100 tutakufa hamna atakaye ishi milele.
ReplyDeleteNALITOLELA you seem to have a more serious disease in your brain than HIVA WHICH THE LADY HAS AQUARED. since you think you are immune to any heartaching problem.but mind you that when you open your mind you let people see what is in your mind.iguess you are stilla young boy whose being in MZUMBE university has alured his mind and can see the world as asimple thing tu just say the word and is done.
ReplyDeletewords are dangerous than even a bomb!because once said you can't grab it back into your mouth!HOW CAN YOU FEEL IF YOU GET MARRIED AND YOU GET A CHILD,ALL OF A SUDDEN YOU FIND THAT YOUR CHILD IS INVALID FOR LIFE e.g has downs syndeome!!anyway you don't know what tomorrow holds for you!but i advice go check your HIV status in this week,ok?
HUYU DADA AMEZIDI ETI UPWEKE? NAAMINI AKIMPATA HUYO ZERUZERU NI BINAMU YANGU ANAPENDA KAVU NA CIRCUMSITION FREE NA KIGONGO 6FEET ATAMFAA SANA HUYU BINTI, WALA SIMSANIFU NASAIDIA KUTATUA HII ISSUE MIMI NGOMA NIMEPIMA PALE TMJ MAMBO NI POA TOKA HITO SIKU MPINI WANGU NIKILALA NAIVISHA SOKSI SIAMINI MTU LABDA NIPATE KWA NJIA YA MIUJIZA NABADIRI SOKSI KILA MARA HATA KAMA NIKIWA NA NYAPU SIMNYONYI NA NIKIPIGA BASI UJUE MIPIRA MINNE IKO KWENYE MPINI NIMEVISHA,LOH! UPWEKE KWA KWELI SIUWEZI. SASA DADA HUYO ZERUZERU NUMBER YAKE NI 0754 234 153 ATAFURAHI SANA UKIMPATA KWA HIYO NUMBER! NALITOLELA WA MUZUMBE
ReplyDeleteMtu unayojihita NALITOLELA,pole! Ninachotaka kukufahamisha hii Blog ya jamii ya kuelimishana,kusaidiana.Wewe umeiingilia,umedandia tu,Nyie mnayo blog yetu ya matusi mnatukanana nyie, wazazi, wenu,familia zenu na koozenu zote.Blogi ya Wasomi Matahahira,Watu wenye husuda,Malimbukeni wa maisha,wanakuranika,wanahizaya.Blogi yenu sitaki kuitaja jina,sisubutu kwani nikiitamka,natamani nisikie MLIO WA PARAPANDA!DUNIA ICHUKULIWE MBALINI.
ReplyDeleteNalitolela unatafuta sifa. Hapa si mahali pake. Afu huna akili, yani zero, sifuri hamna kitu. Mzumbe ndio nini? Michuzi hebu angalia uhalali wa huyu mtu, kwani inawezekana kabisa ana nia ya kumchafulia jina mtu halisi. Mfano, mi nikijisajili kama Michuzi, utakuwa na kidhibiti gani kuwa si mimi. Huyu jamaa anakera. Hata kama tuna uhuru wa kuongea, si hivi.
ReplyDeleteDu!we Nalitolela mbona MBAGALA SEC(St Anthony)hukuwa hivo hiyo roho ngumu umeitoa wapi?Ina maana wewe hutokuja kuzaa maishani?huyo huyo utakayezaa naye hata mkipima kabla, watu wanaweza kukupigia vilevile na kama ndo umekuwa hivo sikuiz pole kwakweli.
ReplyDeleteKUNA MAPUNGUFU YAMEJIONYEHSA KWAKWELI LABDA KAMA UNAFANYA UTANI!
ndugu wadau, huyu mtu anayejiita Nalitolela wa "Muzumbe" university nimeona mara kadhaa akipost upuuzi hapa nikamua kum-ignore tu.
ReplyDeleteIla naona sasa amezidi na baadhi ya watu wanapotoka na kudhania pengine ni mimi (e.g. mdau wa September 07, 2008 6:05 PM). I always post comments hapa using my blogger account, unlike huyu jamaa mwingine, so you should be able to tell it's not me. And this other person always has some serious spelling mistakes iwe kwa Kiswahili au Kiingereza.
Anyways, I just want to make it known kuwa sio mimi, na wala sio mtu yeyote niliye related naye maana hakuna ndugu yangu yeyote aliyesoma Mzumbe U.
Nashawishika kuongea kutokana na maoni ya mtu anaejiita Nalitolela, mimi hisia zangu nilijua alikuwa anataka kuumiza hisia za wengine humu au aonekane wa tofauti na watu wamzogome kwa kulitajataja jina lake hapa, Kwani naamini kila moyo wa nyama una hisia za huruma na uchungu unapoosikia mwengine amepata tatizo ambalo si zuri, sasa yeye alipoanza kushabikia na KUTOVUKA utovu wa adabu humu nikamsamehe na kumuweka kwenye kundi la jumuia fulani ya watovu wa adabu wasio na huruma, nikahisi hata akienda msibani huyu huendea umbea na kusanifu tu, sio kwenda kufariji au kutoa heshima zake, kwani anaonekana si muungwana kuna msemo unasema limjazalo mtu ndilo limtokalo.
ReplyDeleteDADA MUATHIRIKA JIPE MOYO, naamini mungu yupo atakuwezesha na atakushindia, Pia nafarijika kuona unaujasiri mkuu juu ya hali yako hiyo na ujasiri umeonesha pale ulipoona unahitaji kusonga mbele bila kukata tamaa na hali uliyonayo. hiyo ni nzuri na itakuzidishia umri kwani huna unyonge na mawazo ya kukata tamaa ndani yako ambayo yangeweza kukudhoofisha, MUNGU AKUPE HAJA YA MOYO WAKO
nafikiri baadhi yetu tunashindwa kumuelewa huyu dada kwa maana baadhi yetu tunaposikia anatafuta mwenziwe moja kwa moja tumeshafikiria ngono nilivyosoma maelezo yake nimeona kama ni mtu mwenye busara sana kwa maana hiyo hata kama atapata mwenziwe nafikiri itakuwa kwa ajili ya upweke alionao na hata ikifikia huko(ngono)nafikiri huyu dada atachukua tahadhari zote mimi namuelewa sana mtu aliyezoea kuishi na mume halafu sasa yuke peke yake halafu na matatizo kama hayo hata hivyo mtu jasiri sana huyu dada kwa hivyo naomba tuendelee kumpa moyo azidi kupata nguvu
ReplyDeletemr michuzi
ReplyDeletetafadhali kwa hisani ya wastaarabu wa hii blog yako,,,"MTOE UYU MTU APA NALITOLELE SIJUI!!UCTUME POST ZAKE APA ZINACHEFUA AFU ANATAKA MISIFA TU"
apa sio mahali pake,,analugha chafu sana hii blog sio ya ivi,,ata km mtoa mada hii anatoa changamoto bt sio ivi anthr guy aandika mitusi apa
alaaaaa
anony wa 1:55 na 9;32 mngetuelewesha vizuri hasa mnamaanisha nalitolela yupi? maana mwenyewe wa kweli naona kajieleza hapo juu kuwa kuna mtu anamchafulia jina humu.
ReplyDeleteMi nilishaanza kuhisi maana Peter mwenyewe namfahamu na siku zote comment zake humu huwa ni za busara na kujiheshimu, hivyo nilishangaa kuona kacomment utumbo katika post fulanifulani
Dada ningependa kukupongeza kwa kupata nguvu ya kuongelea magumu ya moyo kama hayo, kwani mara nyingi watu hawataki kuongelea swala la ukimwi esp kama ni HIV+ve, bila kujua kwamba kwa kufanya hivyo inaraise awareness, inspires the actions and challenge the fear kwenye society na sorrounding HIV/AIDS.
ReplyDeleteNingependa kukushauri dada usijali hizo comments za watu kama huyo hapo anayejiita Nalitolela kwani ni unkind and hurtful comments mwombe Mungu atakufariji.
Jaribu kutembelea website inayoitwa http://www.tht.org.uk/howwecanhelpyou/livingwithhiv/positivelifestories/ na kama upo UK ungeenda kuwaona wanasaidia vitu vingi mojawapo ni kukukutanisha na watu.
Mama Henrick
Birmingham
Michuzi, siku hizi post zangu hutumi kwa nini?
ReplyDeletenaomba kurudia tena. dada umeathirika hapa duniani na hilo jambo moja wenzio wameathirika na jambo jingine, huo ndio ubinadamu. Usije ukachukulia kama hiyo infection ndio sababu ya kuwa tegemezi, au kutegemea kupewa fadhila ya mapenzi au vinginevyo.
Wewe ni mtu kama sisi tu. Shida upweke ndio jadi yetu. Hasa ukikaribia 40's hata kama una mpenzi, kwa hiyo ishi tu kama wengine. Kwani hujui wasichana wasio na wapenzi/waume hapo ulipo?
Cha kufanya jishirikishe na makundi ya watu makusudi, kama kwaya, vikundi vya kusaidiana mtaani, kacheze na watoto yatima vikundi ya kujitolea, vya kukimbia nk. utapata faraja na marafiki wengi tu, sio kwa kuwa uko positive ndio eti upweke unazidi, sikubaliani na hilo, upweke tunao wote tunapojitenga kwa sababu yoyote ingine.
Kaka Michuzi, nakupongeza sana kwa kupost comments zote hizi, kwani binadamu waweze kujua kuwa kuna watu hata ukiwapa kila kitu wanacho hitaji, bado wanaupungufu wa ustaarabu, busara na hekima tena huu ni ugonjwa mkubwa kuliko HIV, hawa kama Nalitolela wanaitesa sana jamii tena ujificha kwa ngozi ya sungura kumbe ndani ni nyoka. Dada Nakupongeza kwa busara zako MUNGU NI MWEMA KILA JAMBO ANASIKIA UMWOMBAPO, usiwe na wasiwasi ukiona majibu yamechelewa jua bado MUNGU yuko kwenye maandalizi mpe MUNGU nafasi na utafanikiwa sanaaa!!!.
ReplyDeletesiwakwazi waisalamu au dhehebu lingine ila natumia nafasi hii kwani wote twajua mungu yupo.. DADA NAKUTAKIA MAISHA MEMA mistari yangu ni kumbuka Yeremia 17:14, 1Wathesalonike 5:17,18 Zaburi 34:4, na mathayo &:11.6-9
KAKA MICHUZI NAONA HUYU NALITOLELA NI HUYO EX HUSBAND WAKE - TUMIA SAIKOLOGY, ROHO INAMUUMA. watu wenye Tabia hizi wanapenda kutesa familia zao na hawapendi waone mnapoachana unaishi maisha ya raha. SHETANI ANAMSUMBUA.
DADA hongeraaaa
Nalitolela wa Muzumbe naomba nikueleweshe HIV pamoja na kutumia kinga lakini unaweza kuipata kwa njia zifuatazo:
ReplyDeleteUmepata ajali ya kuhitaji upasuaji
Umepata sickle cell
Umepigwa-Radio/chemotheraphy kutibu saratani
unaupungufu wa platelates
listi ni ndefu, ila utahitaji upate matibabu na kuongezewa damu ndio njia ya kwanza kuokoa maisha yako Nalitolela wa Muzumbe, hapo ndipo utakapo jifunza kuto kuwanya- nyapa watu wenye matatizo mbali mbali, na matatizo hayo yasikupate ukiwa sehemu yenye huduma hafifu za kisasa ku-screen damu utakayo.
Mdau
Mwonambali
ndugu wadau,
ReplyDeletewala msijisumbue kumjibu "Nalitolela wa Muzumbe" (a.k.a fake Nalitolela).
I am sure he (whoever he is) was not serious on these comments. It is clear he was writting all this nonsense to create an impression that it was me and hence make me look stupid/cruel, etc (for whatever reasons). As you can tell from his comments on other poosts found here:
1. mdau asaka wa ubani (http://issamichuzi.blogspot.com/2008/09/mdau-asaka-wa-ubani.html)
2.shukrani na kunradhi za mdau HIV+ev (http://issamichuzi.blogspot.com/2008/09/shukrani-na-kunradhi-za-mdau-hivev.html)
3.Mdau HIV+ve atafuta mwenzi (http://issamichuzi.blogspot.com/2008/09/mdau-hivve-atafuta-mwenzi.html)
4.mugabe atoa pole
(http://issamichuzi.blogspot.com/2008/09/mugabe-atoa-pole.html)
5. £500m dream team (http://issamichuzi.blogspot.com/2008/09/500m-dream-team.html)
I doubt even a person of sub-normal intelligence would seriously write such stuff.
Hivyo kumjibu/kumshauri/kumwelewesha ni kupoteza muda wenu na kutimiza azma yake. Pia inafanya jina langu liendelee kuhusishwa na upuuzi
Mdau, kuna sheria ya ukimwi ya mwaka 2007 kwa watu wanaoambukiza makusudi. Ni iwapo mtu atashitakiwa atapimwa kwa lazima bil a consent. Fika TACAIDS au police utoe taarifa
ReplyDelete