


. wengi wamekutwa na maafa kama haya kwa kujaribu kuiba nyaya za umeme ambazo inasemekana ni mali katika viwanda vya kufulia chuma.
Hi Michuzi,
Nimeona nikumuvuzishie hizi snepu za huyu jamaa aliyekuwa anapiga hodi kwenye nguzo ya umeme, na umeme nao umemkaribisha vilivyo…jamani haya mambo sio mchezo inabidi watu wawe makini na uhalifu wakijinga.
Mdau Love child
Astakafirllwah, nadhani wenzake waameona nini kimempata mwenziwao, hilo ni fundisho tosha, ahsante mdau chidi na balozi, ujumbe umefika. Hata kama amekufa nadhani siku nyingine hatarudia tena.
ReplyDeleteHAhahahaa huyu Oganigwe kafanya nini tena jamani wamemkamata na waya za umeme HAhahaahh Mwanawane @ Oga imekuwaje na msumeno wako tena kwakwakwak Juzi Rahaboy leo Oganigwe.
ReplyDeletemaisha bora kwa kila mtanzania kwikwikwi.........Bongo tambarare!!!!!!!kasi mpya,ari mpya na nguvu mpya tehetehetehe.....
ReplyDeleteKwa kweli inatia simanzi kumuona kijana sijui mzee kwenda kutafuta balaa la nishati ya umeme pale juu hivi hivi tunamuona!sasa sijui alikuwa na matatizo fulani ya akili au maradhi yeyote tu yaliyomnyima amani kunako nafsi yake na kupelekea kujiua kwenye huo umeme?
ReplyDeletekama alikuwa mwizi a.k.a mzee wa kazi pale ni ajali kazini kwake ila dah kama ndiyo hivi hata mimi kazi ya wizi naacha na ninaawaasa wenzangu tuache hiyo mambo ni noma mazee,tutafute kazi nyingine za kufanya!
Mungu amrehemu, may be itakua fundisho kwa wengine.
ReplyDeleteSitetei WIZI..
ReplyDeletelakini hii inaonyesha UKALI wa maisha kwa MTANZANIA...
wengine wanaVijisenti... wengine.....
Sijui ni ukali wa maisha,ulimbukeni au matatizo ya nini.Tendo linaloambatana na ajali iliyosababisha kifo hicho ni ngumu sana.Hivi ikatoke jamaa huyo akajua una vijisenti wakati wa uhai wake ingekuwaje???Mungu wangu.
ReplyDeleteMichuzi ,
ReplyDeleteThat picture is too graphical , it is utterly unprofessional to post it without a disclaimer.
Safi sana na hili liwe fundisho kwa nguchiro wengine wanaofikiria kuiba nyaya.
ReplyDeleteMaoni yangu yataonekana kama na roho mbaya lakini wakati mwingine inabidi kusema ukweli wa mambo. Huyo anajua kuwa hizo nyaya zina moto halafu anataka kuzikata kwa msumeno.
Mtu mpaka kuamua kuchukua uamuzi kama huu sio kwa kupenda maisha magumu na serekali zetu kama unavyojua hakuna welfare. Sisaport wizi wala ujambazi ni ubinadamu tu na pole kwa wafiwa
ReplyDeleteDuh!Inasikitisha!:-(
ReplyDeleteLakini inatukumbusha kuwa TANESCO bado ipo na Maisha Magumu yanaweza yakakushawishi uingie katika ujasiriamali hatari!
Naomba nitofautiane kidogo na some of the comments zinazofurahia kifo cha huyu kijana.Nawapa pole familia ya huyo kijana,nina hakika wanahuzunika kwani hawakumtuma kufanya hicho alichokuwa anataka kukifanya.
ReplyDeleteBack to the issue:Tatizo hapa ni ukosefu wa ajira+Elimu(Suala ambalo ni jukumu la serikali).Potelea mbali kujiweka 'at risk'huyo jamaa alikuwa hajui hata madhara ya kiuchumi kwa kukatika umeme kwa dakika 1 kama angefanikiwa kuung'oa huo waya.
Serikali/dola inawafahamu wanunuzi na wahujumu wa uchumi,lazima iwe serious.Na nyaya za TTCL,hata kama 'haziui'kuna watu wanazihujumu kwa sana.Kuna siku nilienda kuomba TTCL wakanifungie simu ya mezani'landline' nje kidogo ya jiji la Dar nikaambiwa huko walishaacha tangu 2004 kuna wizi wa nyaya!Unaweza kuona tatizo lilivyo.Thanks to TTCL Wireless Fixed Terminal-At least.
Balozi wa Zain,samahani kuna comment nimeituma na kuzungumzia Tanzania lakini baadae nilirudia kusoma maelezo vizuri nikagundua hakuna sehemu inayosema hilo tukio ni la wapi na nchi gani.Samahani kama itakuwa imeleta usumbufu.
ReplyDeletebrother michu please please ondow picha ya mwisho inasikitisha sana sana, please ondowa na usiseme haiwezekani. please brother michuzi wafikirie pia jamaa wa marehemu kuona ndugu yao namna hii sio vizuri
ReplyDeletesiamini kuwa mtu analeta comments za kucheka au kukebehi ilhali juu ya habari hii, ilhali ni issue ya kusikitisha, mtu amepoteza maisha yake, ok humjui lakini sio uungwana kuanza kucheka au kukejeli. kweli alokuwa anajaribu kufanya sio zuri na wafikirie ndugu na jamaa zake, pia jiulize ni shida ya kiasi gani aliyokuwa nayo kiasi kuwa ahatarishe maisha yake ili kujipatia visenti vya haraka?
ReplyDeleteKaka Michu mbona huku malizia picha zingine za jinsi jamaa alivyoungua ki sawia mpaka sehemu sehemu ya nonihi???...
ReplyDeleteMarehemu hawasemwi vibaya, lakini hawa watu wa aina hii wanatutesa mno watumiaji wa umeme (kila mtu lazima anavutia kwake), mtaani kwetu walitusindikiza mwezi mzima bila umeme kwa sababu ya kuiba nyaya hizi....Kwa sisi ambao kwa njia moja ama nyingine tumepata kuwa wahanga wa kazi zao, tuna imani itaendelea kuwa fundisho kwa watu wengine wa 'professional' hii...
ReplyDeleteMichuzi ,
ReplyDeleteThis is not something to lough about, let me put it bluntly IT IS NOT FUN !
I am wondering why didn't you ask for viewers discretion. To call it ajali kazini is pathetic and below the belt, mind you we rae talking about human life that that has been lost .
Hii inaonesha jinsi ubinadamu umekwisha, Mtu ata kama alikuwa mwizi na amefariki wakati akiiba sio wote mcheke na kuona kifo kama kitu cha kawaida.
ReplyDeleteNi jambo la kusikitisha sana kuona watu wakicheka na kudharau kuhusu kifo cha huyu ndugu. Inasikitisha sana na inaonesha wote mlio cheka na kudharau hamna kabisa ubinadamu.
Poleni ndugu na Marafiki wa Marehemu.
NaWaKiLiShA.
Wezi wa nyaya za umeme na nafuta ya transfoma wanakera sana hasa eneo linalokumbwa na mkasa. Kufa kwake hakufurahishi ila iwe ni fundisho kwa wale wote wenye akili size ya mosqiuto, wafanye kazi na sio kukalia kuiba na kupata hela za chap chap. Nakumbuka mtaani kwetu wezi walliba mafuta ya transfoma, tulikaa miezi mitatu bila umeme, ni giza tupu, uwezo wa jenereta hatuna, tunawasha mishumaa na chemli kwa kwenda mbele, achilia mbali swala la kunyoosha nguo uende kazini. Ni taabu maisha mabaya sana hayo, hakuna tv, radio mpaka mkanunue za betri, taabu ya nini.
ReplyDeleteMuda umefika wadanganyika kufanya kazi, nenedeni vijijini mkalime, fanyeni kazi za ufundi, mtaiba mpaka lini, mna mtaji wa kuiba maisha yenu yote? Hii hata wizi wa simu, unarudisha sana maendeleo.
Muda ulishafika wa watu kuwa creative, mambo ya kuomba omba hayachangamshi akili, kukaa vijiweni na kusubiria kuiba hakusaidii jamani. Watanzania tufumbuke macho,tafuta riziki yako kihalali, jenga nchi yako na sio kuporomosha.
Ni ugumu wa maisha na uizi ni uizi tu. Siajabu hiyo si mara yake ya kwanza na ilikua bahati yake mbaya. kwani majambazi wanaouliwa kila siku lakini wengine tunawaona bado wanaendeleza uizi wao.
ReplyDeletekwa wanaofanya hivi hapa hata hawaoni hii kabisa.
Mnakumbuka ule winbo ulikuwa unasema "ahangaikaye, usiku umefika, watoto waniuliza, baba yuko wapi, na mimi nawajibu, baba yupo kazi, kumbe sio ukweli, bado anatafuta kazi, bado nahangaika"
MAISHA MAGUMU, HATA UKITUMIA BONGO KICHWANI HUFANIKIWI SIKU HIZI BONGO
Kama watu wanaweza kumchoma moto mwizi kuku au kibaka, bila huruma kuna haja gani ya kumuonea huruma huyu jamaa mpinga maendeleo. Hii itakuwa si mara yake ya kwanza ujua za mwizi ni arobaini nafikiri timing ilikuwa mbovu na msumeno ukaguza waya 11KV ambao huandama strong magnetic field. Hii si mara ya kwanza kama miaka mitatu iliyopita nilishuhudia mwingine pale maeneo ya TAZARA nae alijikaanga na 11KV(11,000 Volts). TANESCO wakamwacha mpaka saa tano asubuhi ili watu wajifunze.
ReplyDeleteUnajua hii ignorant itatumaliza, Wenyewe TANESCO wana kitengo maalum cha High Voltage Ambao hufanya kazi wakiwa wamevaa SUIT Special kwenye High Voltage kama umeme ukiwa haujazimwa. Sasa huyu marehemu masikini alikuwa na ujasiri gani.
Tumuombee mungu amlaze panastahili na liwe fundisho kwa vibaka japo ni wepesi kusahau.
Tunasema 'safi sana' ili na wengine wapate fundisho. Safi sana! Lakini najaribu kulinganisha umeme uliomuua huyu jamaa na ule 'umeme' wanaouita 'miwaya' kama watu husema safi sana, na wengine wapate fundisho.
ReplyDeleteHahaha... safi sana! Real?
Tunasikitika sana huyu amekufa akitaka kuiba waya za umeme...ila tunajichukulia sheria kwa kupiga vibaka mpaka kuua mitaani..sasa ubinadamu uko wapi?
ReplyDeleteshukrani brother michuzi kwa kuondowa picha ya mwisho kama nilivyokuomba. hongera sana kwa kusikiliza maoni ya wapenzi wa blog yako.
ReplyDeleteWatanzania wana safari ndefu sana ya kujikwamua kiuchumi. Porojo zote za maisha bora kwa kila mtanzania zimeishia kwenye nyaya za umeme. Tumsamehe
ReplyDeletekweli watanzania tuna safari ndefu ya kupambana na umasikini. Porojo zote za maisha bora kwa kila mtanzania yameishia kwenye nyaya za umeme. Tumsamehe
ReplyDeleteKama mnahasira na haya maoni basi mkatolee hizo hasira bwana safari. Yeye ndiye aliyeahidi maisha bora(kwa wachache) EPA watu wamekula hela na bado wapo mtaani. Sijawahi kuona maishani mwangu eti mwizi akiishaiba halafu anarudisha alichoiba halafu ndio basi. Hakuna kesi, hakuna kwenda segerea. Mkawatolee hasira watu walioiba pesa za EPA si mnawajua na bado wapo mtaani.
ReplyDelete