Mkongwe Pembe Rashid aka DJ Zee akifanya vitu vyake
Wadau pembezoni mwa mto Sagami. Wa kwanza kulia (full jeans) ni Makamu mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Nchini Japani,Mh. Andrew Hussein Kapinga
Kina dada nao walihudhuria kwa wingi
Nyama choma zilikuwapo kwa wingu tu, watu walikula weeeee mpaka wakasaza
Mwakilishi wa kikosi cha mizinga (kulia) na mdau wa manzese crew (shoto) nao walikuwepo
JUMUIYA YA WATANZANIA JAPANI WAFANYA BBQ ILI KUHAMASISHA WATANZANIA WANAOISHI JAPANI KUJUINGA NA JUMUIYA

Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani (TANZANITE SOCIETY), Jana Jioni walifanya BBQ ya nguvu katika kampeni yao ya kuwahamasisha watanzania wanaoishi nchini Japani kujiandikisha na Jumuiya.

Shughuli hiyo ya “nyama choma” iliyofanyika pembezoni mwa mto Sagami, huko mkoani KANAGAWA ilihudhuriwa na viongozi wote wa juu wa Jumuiya. Muziki wa nguvu wa DJ Zee ulisindikiza shughuli hiyo.

Watanzania kadhaa waliohudhuria, ambao sio Wanajumuiya waliahidi kujiunga na Jumuiya haraka iwezekanavyo.

Uongozi wa Jumuiya unapenda kuchukuwa fursa hii kuwaomba watanzania wote wanaoishi nchini Japani ambao bado hawajajiunga na Jumuiya kufanya hivyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Poa Tumeshikia Kiunyonge weka matokeo ya Chadema kuishinda CCM tarime

    ReplyDelete
  2. bei ya gari hiyo ikiwa mpya kweli mtanzania wa kawaida anaweza kupata kwa kipata chake tu au ndio ufisadi wenyewe huo?basi yetu macho wewe mithupu na mafisadi wako hao

    ReplyDelete
  3. Braza Michu ingawa wote tunajua wewe ni CCM damu na umeonjoy sana hela za mafisadi BUT pleeeeeeeeeeease tuletee hata mabreaking news ya Tarime kuwa CHADEMA wameshinda basi

    CHADEMA oyeee

    haha usichukie mtani

    ReplyDelete
  4. Muuza gari naomba uweke bei mambo ya makubaliano ndio nini? Tupe kianzio basi

    ReplyDelete
  5. Wadada wanne ndio wanaitwa wakina dada walikua kibao?

    ReplyDelete
  6. WATU HATA WAKIWA WANNE, TUTAAMBIWA "MTU KIBAO". JIKO LENYEWE CHA MTOTO, MUZIKI USISEME. MI NILIDHANI HUKO KUNAKOTAMBA KWA ELECTRONICS TUNGEONA MUZIKI WA NGUVU? MUZIKI KAMA TUNAPIGISHA DISCO UWANJA WA FISI...LETS GO WITH TIME BOB

    ReplyDelete
  7. Ni wanga tu pekee ambao wanakutana huku wamesimama namna hii juu ya mawe. Kikao muhimu mngekuja hata viti vya mkunjo? Unakitoa kwenye gari kunjua na ukimaliza kikao unakikunja unakirudisha. Au ndio kujifanya mko fit kama wajepu?

    ReplyDelete
  8. dah noma kijiko chenyewe ovyo watu wenyewe kweli 4 kwa 4 au walikuwa wanafanya ....bbq noma japan kweli mmechoka jaman?

    ReplyDelete
  9. Man you aint no Gangster so puts yours hands down and act like respectable African

    ReplyDelete
  10. ni noma!

    is this for real? someone stop this joke please.
    hawa ni washikaji tu walikuwa wanajichomea mishikaki yao na sio jumiya nzima!
    na kuna majiko murua ya BBQ ( Charbroil) yako kwenye sale maana summer imekwisha hapo Machida Costco.......for anyone who wants a real BBQ thing!

    ReplyDelete
  11. MIMI MDAU NIKO JAPAN. NAOMBA CONTACT ZA MWENYEKITI AU MWANACHAMA YEYOTE TAFADHALI.

    ReplyDelete
  12. Tupac & Natedog the last pic

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...