JK akikabidhi hundi ya Shilingi milioni mia moja kwa Mwenyekiti wa chama cha kuweka na kukopa cha juhudi SACCOS cha Kyela, Bwana Akim Luvanda(wa kwanza kushoto anayepeana mkono na Rais) iliyotolewa kama mkopo kutoka benki ya NMB kwa kikundi hicho.Makabidhiano hayo yalifanyika katika Uwanja wa michezo wa Mwakangale jana.Wengine katika piacha ni Meneja wa NMB Tawi la Mbeya Bwana John Magigita(Wapili kushoto) na kulia pembeni ya Rais ni katibu wa SACCOS hiyo Bwana Godfrey Sanga
JK akiwahutubia mamia ya wakazi wa wilaya ya Kyela katika uwanja wa michezo wa Mwakangale,mjini Kyela jana mchana.
JK akisalimiana na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Ikimba iliyopo wilayani Kyela,Mkoani Mbeya, iliyojengwa kwa nguvu za wananchi.Rais yumo Mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi ya siku kumi kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo




JK akiwapungia watoto waliokuwa wakiogelea katika mto Songwe wakati alipolikagua Daraja la mto huko Kasumulu,wilayani Kyela, mkoani Mbeya jana
JK akisoma kitabu katika maktaba ya Taasisi ya Mango Tree,huko wilayani Kyela baada ya kufungua rasmi maktaba ya taasisi hiyo ambayo pia inatoa huduma za elimu na matibabu kwa watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu.Pembeni ya Rais ni Mkurugenzi wa Taasisi ya The Mango tree Orphan Support Programme Trust Bwana Andilile Sylvester Ibrahim
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania Dr.Marcelina Chijoriga akimwonesha JK maeneo mbalimbali katika jengo jipya la ofisi ya TRA lililojengwa na Mamlaka hiyo huko,Kasumulu,wilayani Kyela,mpakani mwa Tanzania na Malawi, muda mfupi baada ya Rais kufungua jengo hilo jana
Mzee Aidan Mwaisobwa akimpongeza JK baada ya sherehe za kijadi za kumtambua kama mmoja wa machifu wa kabila la Wanyakyusa zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Mwakangale,wilayani Kyela jana.Katikati ni Mama Salma Kikwete ambaye amefuatana na Rais katika ziara hiyo ya kikazi ya siku kumi ya mkoa wa Mbeya





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Naona mama Chijo kaweza kuudhibiti mwili sasa(Atakuwa anareport Gym) wakati nikiwa pale FCM-UDSM alikuwa amechana sana. Ila mama ni kichwa kizuri sana. Nafikri atakuwa facult dean pale FCM kwa sasa, wakati nipo pale alikuwa head Finance Dept.

    ReplyDelete
  2. HUYU NI RAISI WA CCM AU WA WATANZANIA? NILIONA AKIPOKELEWA NA GWARIDE LA JESHI LA CCM, HIVI POLISI WAMESHINDWA KAZI KIASI WANASAIDIWA NA JESHI LA CCM! WAPINZANI NAO WAKIUNDA VIKOSI VYAO MAGAZETI YASIPIGE KELELELE. SASA HIYO BENDERA YA CCM INAFANYA NINI HAPO? IWEJE ANATUMIA PESA ZA WANANCHI KWA ZIARA ZA KICHAMA?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...