msanii mashuhuri wa uganda jose chameleone (juu shoto akiwa na mama sweya wa tbl na msanii mr nice mwezi aprili 2006) inasemekana amevunjika miguu yote miwili baada ya kuanguka toka ghorofa ya tatu ya hoteli moja kubwa ya kitalii a-taun mwishoni mwa wiki. habari za uhakika toka kampala zinasema chameleone, ambaye alikuwa bongo kwa ziara ya maonesho, hivi sasa amelazwa hospitali jijini humo kwa matibabu.
uhakika wa nini kilimsibu msanii huyo bado unatafutwa lakini habari za awali zinadatisha kwamba alikuwa ameamka kitandani kwake na kuelekea kwa kutembea huku akiwa ndotoni (sleep walking, nadhani kwa kiinglishi) kwenye balkoni ya chumba chake na kula mwereka. globu ya jamii inafuatilia habari hii na itatoa taarifa kamili mara zitapopatikana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. This is very sad news.I hope no one has attempted to finish him in our lovely Country.God forbid, we love him. we would still like to hear more new nice tracks from him. Get well soon Jose Chameleone
    Mdau,Cardiff

    ReplyDelete
  2. Pole sana Chameleone...i hope no one is trying to finish him as commented previously for sure...

    Ila kama alinyweshwa machimpumu yakamzidi nguvu ndo hapo chacha... atapona mtu wa kazi

    ReplyDelete
  3. Sio mkono wa mtu walisahau kumwambia bangi ya bongo kali sana. Kaka yangu alikua anajifunza kuvuta hii kitu alipokua kijana siku hiyo tulimwona anakimbia uchi nguo zote kavua baba alivyoitwa akakimbizwa hospital wakizania ni malaria. Kupelekwa hospital hamna malaria. Siku hiyo ndio ilikua mwanzo na mwisho wake wa kujaribu hiyo kitu.


    Mimi hapo nadhani either alikua high au anaugonjwa hawautambua wa akili

    ReplyDelete
  4. pole Chamilioni, mimi bado nakumbukaonesho lako la Ht,TX, U r the best, pona haraka urudi kazini love yo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...