Michuzi na wadau wote wa libeneke...
Kwa siku ya pili leo, mtandao wako uupendao wa
hauko hewani kutokana na tatizo la Bandwidth, ikiwa na maana kwamba mtandao umezidiwa mzigo.
Kwikwi hii imetokana na Host wetu kushindwa kutoa Bandwidth inayoendana na ukubwa wa mtandao wenu.
Tatizo hili linatafutiwa ufumbuzi wa kudumu, hivyo tunawaomba radhi wasomaji weto wote katika kipindi hiki cha kutafuta suluhisho hilo ambalo litachukua siku mbili zaidi zijazo.
Tunajua mnaumia kiasi gani, lakini ni tatizo ambalo liko nje ya uwezo wetu sisi waendeshaji wa mtandao huu na tunasikitika sana.
Tunaomba uvumilivu wenu.
WEBMASTER

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. "Kwikwi hii imetokana na Host wetu kushindwa kutoa Bandwidth inayoendana na ukubwa wa mtandao wenu...." acheni kutuyeyusha, ukweli ni kwamba ukilipa pesa kidogo, utapata bandwidth ndogo na SIYO kwamba host ameshindwa kutoa bandwidth inayoendana na ukubwa wa mtandao wenu

    ReplyDelete
  2. Tusibanie hela jamani hiyo site ni kubwa sana na inafanya kazi kubwa sana sasa kwa nini msichukue hosting yenye maana???Mimi hapo siwezi kuwalaumu hosting ndio wenyewe tatizo kwanza wakati mnanunua hamkua kama hosting ipo ya ukubwa gani???Sasa mnasema kwamba tatizo lipo nje ya uwezo wenu cha muhimu hapo mupunguze mzigo tu basi maana mzigo umekuwa mwingi ndio maana host imejaa na yenyewe pia......kwa ushauri zaidi mnaweza kuhost kutoka www.bluehost.com hawa jamaa wanakupa badwidth bure utajaza kila kitu unachotaka sasa hao wanaokupangia ukubwa wa badwidth achana nao hawana mpango kabisa

    Pia siku zote ukishanunua host account hapo uliponunua wanakuwa hawajihusishi tena na wewe maana wakati unanunua ulishaangalia badwidth na ukajua ukubwa wake vipi na hiyo host ipo kwa hiyo ukisema walishindwa kukupa host inayoendana na website hapo nitakaa...Yangu ni hayo tu

    ReplyDelete
  3. Global waambieni wadau ukweli. Hivi ni kweli host ameshindwa kutoa bandwith ya kutosha kuendana na ukubwa wa mtandao wenu au mmenunua bandwith kidogo kwa either kubana matumizi au kwa kujua kuwa itatosha mahitaji yenu??
    Kwa mtandao wenu na uwingi wa vitu mlivyovisheheneza,mlitakiwa mnunue package ya UNLIMITED bandwith, na sio robo robo eti wakilog watu 20 ndio max, wa 21 hawezi mpaka mmoja atoke ndio apate room.

    Dakta

    ReplyDelete
  4. Jamani... Kweli tumewakosa sana...
    Please fanyeni mambo fasta ili tuendelee kublogika kama kawa... Mahadithi ya Shigongo tumeyakosa kishenzi yani...
    Fanyeni mambo fasta please...

    Jacky

    ReplyDelete
  5. Sawa. Nyie tumekueleweni.

    Na Globu yetu ya "UTAMU" ndo imekuwaje tene?

    Mbona nayo haipatikani?

    ReplyDelete
  6. Si mara ya kwanza hii kutokea ila last time nakumbuka mlisema tatizo hili halitatokea tena ,sasa kulikoni?
    MRISHO hebu fanya mambo faster unajua ERIC hafahamu tatizo hili akigundua atakasirika wewe yaani acha tu.

    ReplyDelete
  7. mnahitaji kuwaona Web Technologies wako haidery plaza floor ya kwanza, wanatoa UNLIMITED BANDWIDTH HOSTING kwa $100 kwa mwaka!. Wana host high traffic websites ikiwemo ya BBA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...