

MDAU UNAKARIBISHWA KUCHANGIA MAONI YAKO KWA JINSI UNAVYOMKUBUKA BABA WA TAIFA KATIKA KUADHIMISHA SIKU HII
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
NAMKUMBUKA PALE UWANJA WA MKENDO, MUSOMA, SIKU ALIPOWAKATAA HADHARANI WAGOMBEA WAWILI WA CCM , MAREHEMU MUNEMA & NA HATA MAREHEMU DR. MAGOTI KUTOKANA NA MIENENDO YAO ILIYOKUWA NA MASWALI KIBAO KWA WANANCHI WA MKOA WA MARA.
ReplyDeleteKWA NINI MPAKA LEO VIONGOZI WAKUU WA CCM WALIENDELEA KULAZIMISHA KUMSIMAMISHA MTU KAMA PETER ZACHARIA HUKO TARIME?
WANACCM WENZANGU SUNAMI LILILOTUANGUKIA TARIME LITATUKUMBA HATA MUSOMA MJINI KWA AJILI YA WATU KAMA MBUNGE MATHAYO NA MWENYEKITI OBETO.
TUSOME ALAMA ZA NYAKATI!!
Asante sana Michuzi kwa kutupa nafasi ya kueleza hisia zetu. Nami ninaungana na kila mpenda amani na mtukuza utu kumkumbuka Mwl JKN, mtu wa watu. JKN alipagania haki za binadamu wote bila ubaguzi wa rangi au dini, au kabila, ndani na nje ya Tanzania. Hulka yake hiyo ya utu ndio ilimsukuma hata kutaka kufanya majaribio ya siasa ya ujamaa na kujitegemea. Mimi ni msomi wa nondoz nyingi, na sina budi nikiri hapa kuwa kama isingekuwa siasa ya ujamaa wa mwalimu leo hii ningekuwa kijijini ninalima mihogo. siasa hiyi ilipigwa vita na mabepari na kwa hiyo haikuweza kutufikisha alipotaka, na hatimaye akaamsha mikono. Waliochukua mikoba yake leo hii hawana hata aibu wanaimba eti ubepari ndio njia ya kuleta maisha bora kwa kila mtanzania wakati hata watoto wa shule za dar wanakaa juu ya mawe au sakafuni wamerundikana zaidi ya mia katika darasa moja!!! hawa wanaandaliwa kuwa machinga, na mafisadi wanachukua vyao mapema. Nji pekee muafaka ya kumkumbuka JKN ni sote kujiunga kwa dhati na mapambano dhidi ya mafisadi.
ReplyDeleteOCT 14, naikumbuka siku zote, nilihuzunika baada ya kutangazwa kuwa Baba wa Taifa ametutoka.
ReplyDeleteNilikuwepo Uwanja wa Ndege mwili wake ulipowasili na nilibahatika kwenda Taifa kumuaga.Tunakukumbuka Baba.
Nakumbuka nilikuwa London England, nilisikia kwenye bbc radio.
ReplyDeletetutakukumbuka milele,Mafundisho yako,uliondoa ukabira Tanzania, ulipigana na rushwa! Amani uliyoianziasha tutajaribu kuimaintain ingawa hawa mafisadi wanatushinda.
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikua mtu wa watu amabae katika maisha yake yote alipigania kuboresha maisha ya walalahoi(wanyonge)alipinga UBEPARI NA UKABAILA vitu ambavyo sasa ndiyo sela ya nchi yetu UBEPARI + UKABAILA=UFISADI.Kila hotuba aliyokua akitoa ilikua inabeba ujumbe fulani katika jamii.Ikiwa ni kokosoa ,kutoa maelekezo,kuimiza n.k.Tofauti na hotuba za viongozi wetu wengi wa sasa ambazo mimi naziita SOGA au BLAH BLAH ambapo wanapinga UFISADI wakati wao WENYEWE ni MMAFISADI Wanapinga RUSHWA wakati wao ni WALARUSHWA WAKUBWA.ALIKUA KIONGOZI WA WATU AMABAE KILA HOTUBA YAKE ULIKUA UANAWEZA KUAPATA MAJIBU KWANINI LIMETOKEA HILI AU LILE?NINI KINACHOENDELE?NA NINI CHA KUFANYA? MWALIMU MUNGU AKULAZE MAHALA PEMA PEPONI FIKRA ZAKO,MATENDO YAKO YATADUMU MILELE.MUNGU IBARIKI TANZANIA
ReplyDeleteItakuwa jambo la ajabu kama mtu anazaliwa na kukaa tuu milele hapa duniani pasi kupitia hii sehemu ya maisha yetu ya KUFA kama viumbe hai. Hivyo Mwalimu ametimiza moja ya mambo ambayo kila mmoja atapitia kam avile kuzaliwa basi kuna KIFO vile vile.
ReplyDeleteHatuna budi kumshukuru Mungu kwa yote ambayo ametujaalia na la msingi zaidi katika nakala yangu hii ni sisi Watanzania kumpata mtu kama Mwalimu ambaye si kwamba alikuwa kiongozi wa kisiasa bali Mwalimu katika nyanja zote za maisha ya binaadamu. kama alivyo wahi kusema yeye mwenyewe katika moja ya hotuba zake "Sisi siyo malaika, tumefanya makosa... lakini la muhimu ni kuzingatia yale mema tuliyofanya na kuyaendeleza na siyo kila kukicha tunazingatia ama kuongela yale ya KIJINGA" ... Hakika hakuna manono ya busara ya kuyaenzi kama maneno haya ya Mwalimu. Tatizo letu bado tunawatu wengi tu ambao watadanganya na matepeli.
He was true leader stand for his people and country. If almighty GOD he could make him return, I will be so gratefully. Now we realise that, it ia real "elder brothers looking for they are brothers, while younger brothers looking for DOLLERS". We can see how the country get mess since he died. MAy almighty GOD bless him always.
ReplyDeleteMichuzi,
ReplyDeleteWe might differ on our opinion on this, but I DO APPRECIATE your point of view, and I respect that,
How is NYERERE was simple in life?, then Barack Obama will be goddess if that the case, his granny still live in the house without electricity, his brother live on a modest house. Barack don't exploit his position to channel privileges to his family and friends, ie. education, offering them jobs, and others.
He should have earned thousands after finishing on the top university in the world(Havard) by joining wall street or being a corporate lawyer, and he decided to turn that down and decided to work as community organizer for less than 15K US dollars per year.
Going back to Nyerere Record, he ban his own citizens to own even a TV, he is anti technology, anti democrat, anti human rights, anti opposition, shrines made on his name, his philosophy and policy still affecting the inefficiency of the current leadership(DUMB LEADERSHIP, WELL ON EVERYTHING), lack of education, modernization, development programs and so forth.
CIVIL arguments are more than welcome, rebuke with facts and understanding.
I wonder what Nyerere would say about opposition. probably would have faced persecution, just being critical or disagree on anything for that matter.
By Mchangiaji
nilikuwa darasa la tano kule Arusha, tulikuwa tunatoka kunywa chai ya saa nne asubuhi, baada ya chai tukiwa tunaenda darasani baadhi ya wapitajia waliokuwa na redio ndio walituambia kuwa baba wa taifa amefariki.nafikiri Nyerere ndio marehemu wa kwanza kunitoa machozi.Mungu amulaze mahali pema peponi. we miss him alot
ReplyDeletenakumbuku nilienda uwanja wa taifa kutoa heshima na nilisimama kwenye mstari kuanzia saa sita mchana mapaka saa kumi na moja jioni ndipo nilipata fursa ya kutoa heshima zangu...na ilikuwa ni sahihi
ReplyDeleteWewe uliye onge kizungu umeongea vizuri sana ila kizungu chako kigumuu, ungoengea kiswahili ili watu wengi tuelewe maan sisi wengine ni victim za itikadi ya huyu baba waTaifa , hatuwezi ongea au hat andika sentensi nzima ya kizungu .
ReplyDeleteEti alikwua mtu simple ,jamani tusidanganya , mwenzetu alikua anapanda Cidiz kwenda kazini, ndege first class, Akikanyaga majuu huko ndio usiseme kwenye hizo Posh Apartments, watoto wanasoma nje , maisha wake yote aliyaweka vizuri kwa pensheni ya kumuwezesha aishi vizuri milele, halafu unaniambie eti simple?.
Kwanza kwanini alikua anajiita Mwalimu? kwani kujiita Raisi kunatatizo gani? kwani yeye hakuwa raisi , alikuw anataka kutudanganya nini kw akujiita mwalimu? au eyey alidharau kuwa ualimu sio kitu muhimu ndio maana akaamua kujiita mwalimu sababu ana dharau proffesional ya ualimu sababu ni ya hali ya chini, kwahiyo ana jita mwalimu kutuvunga eti yeye ni anajiona masikini? hapo ndio chanzo cha walimu manesi na wengine muhimu kudharaulika na kulipwa mishahara duni wakati ni muhimu sana kwenye jamii.
Uliza kw awanae mjua zile suti zake za kichina sijui zilikua na quality gani, hapo ndio mtajua kama kwlei alikuwa simple.
Janani mesikiliza hotuba ya Rais Nyereri, alisema"Kuna mtu alisema serikali yote kaiweka mikononi mwake " Nyerere akasema "Nikamkamata na kumweka ndani ,wakatuma watu amuombee nikasema hapana" , hapo nikakumbuka juzi juzi rais Kikwete aliposema kuwa yeye ni rais akitaka kutumia powers zake kwa hawa wana habari anaweza ila haoni ni haki , hapo nikasema huyu Nyerere alikuwa mkandamizaji na mpingaji haki za binadamu kwa kuhofia kuondoka madarakani, mbaka akaona hakuna jinsi ndio akatoka ili ku jifanya ana ng'atuka .
Ni wachache kama yeye walio katika kundi la kina Mandela, Mahatma Ganghi na Old Major (kwa waliosoma novel au kutazama filamu ya Animal Farm). Kwa bahati mbaya uzuri wa mtu huja zaidi pale unapolinganishwa na ubaya uliopo. If only we could turn the clock back. Kama alivyosema mwanablogu mmoja karibuni matukio ya karibuni katika masoko ya hisa duniani yanatukumbusha kauli yake moja kwamba "...ubepari ni unyama..." Na labda kweli ni unyama. More interestingly, aliwahi kuhoji iweje mtu aje akukope pesa akagombee ubunge au urais kwa ahadi kuwa akishinda "...atakulipa...atazipata wapi?". Pengine kwenye mshahara wake. Yes, kidogo kidogo.
ReplyDeleteNimejaaliwa kuona tawala tofauti za nchi yangu. Bado nasubiri kuuona utawala uliojali watu kama utawala wake. Na kusubiri nitasubiri kwa sababu maisha yanakwenda mbele...
Pamoja na kumbukumbu ya miaka tisa tangu alipotutoka Mwalimu,Michuzi hebu uwe unaandika vitu kwa jinsi vilivyotokea ili vijana walio na umri wa chini ya miaka kumi na tano kwa sasa wafahamu vizuri historia.
ReplyDeleteMwalimu hakufa ghafla bali aliumwa kwa muda,sasa nielewavyo mimi mtu anayekufa ghafla ni yule anayelala bila kuwa amesumbuliwa na maradhi ambayo yanafahamika yalimsababishia kulazwa hospitalini na asubuhi kuamka watu wanamkuta amekwishafariki dunia.
Ingawa Waswahili wanasema kuugua sio kufa laini Mwalimu hakufariki dunia ghafla.Unapindisha historia Michuzi.
I am Proud of Mwalimu JK. He is and will always remain my Hero.We miss you baba especially now when the Nation vividly witness few selfish people plundering the wealth of the Nation and accumulate for themselves. Your people are still in Poverty Mwalimu! There are the haves and have not Mwalimu!Now we have the MAFISADI who could openly admit that what they have taken is just VIJISENTI Mwalimu! The EPA you know there at BOT for sometime was no longer used to pay for foreign debts but rather for the few Tanzanians even the unregistered Companies! So sad Mwalimu! We also had a fake RICHMOND Company that by the support of the haves came to provide no electricity when we had crisis but rather to just take our money! OOooh! Mwalimu we have a lot to tell you!I dont know if this could make you sad! Just a day! before yesterday our lovely party lost the Tarime election! we ar sad but that is Democracy! Freedom to choose! But I want you to know that you should not fear the CCM loosing in Tarime! rather I want you to fear the violence and fights that occassion in the campaigns nowdays! Can you believe that Mwalimu? It happened in TARIME we are not sure on 2010?
ReplyDeleteRest in PEACE our Hero JULIUS Kambarage. AMEN
Kifo chake hakikua cha ghafla acha uzushi
ReplyDeleteUnakumbuka wimbo wa asabuhi mashuleni..."Ujamaa na kujitegemea ndio..." Yani ilikuwa technique ya ku-brain wash watu...kudadadeki!
ReplyDeleteAlifanya vizuri kupita kiasi katika mambo ya kuondoa ukabila. Ni mmoja wa viongozi wachache sana walioweza kuleta elimu bure/kwa bei nafuu sana kwa wananchi. For those we thank him.
Lakini kiuchumi alituangusha sana. Siasa ya ujamaa sana sana. Kuna comment nilitoa juzi michuzi akanibania. So i wont say much. Kiutawala/administrative pia. Aliwapa polisi na public bodies nguvu kupita kiasi ambazo wanatumia mpaka leo. Mfano mwingine tanesco, na ttcl walivyokuwa wanajifanya enzi wana-monopolies. The Executive branch Tanzania ina nguvu sana. Pamoja na post ya Rais. Nguvu zote hizo angejua angezi-dilute kabla ya kuachia ngazi. Matokeo yake ni mafisadi sasa wanakula raha badala ya kuleta maendeleo.
Michu plz usibane
mtoto
Kaka Michu naomba na mimi unipe fursa ya kutoa mawazo yangu japo pengine hayana sukari na utamu kama yalivyo ya wengine hapo juu.
ReplyDeleteJAMANI TUTAHADHARI TUSIJE TUKAFIKIA KUMUABUDU HUYU MAREHEMU.KUNA WATU WAMESHAANZA KUTUAMBIA KUWA ALIKUWA NABII, KESHO SIJUI KUWA HATOPANDISHWA DARAJA ZAIDI YA UNABII.NI KWELI ALIKUWA NA BAADHI YA SIFA NZURI(HAKUWA MWIZI KAMA BAADHI YA VIONGOZI WENGINE WA AFRIKA)LAKINI PIA ALIKUWA NA MAPUNGUFU MENGI.
NI YEYE ALIYEEIINGIZA NCHI KWENYE VITA NA UGANDA ILI AWEZE KUMRUDISHA MADARAKANI RAFIKI YAKE OBOTE.ALIFANIKIWA LAKINI SINA HAJA KUELEZEA MADHARA YA VITA VYA UGANDA KWA TZ, LAKINI NCHI ILIIANGAMIA NA ROHO NYINGI ZA WABONGO ZILIPOTEA.WALIORUDI VILEMA BILA MIKONO WALA MIGUU WALIAMBIWA''HATUNA CHA KUWAPA, CHA KUWAPA NI ASNTE''.
NI YEYE ALIYEKUWA HAVUMILII MTU AU CHOMBO CHO CHOTE KUHOJI MAWAZO AU FIKRA ZAKE. HAKURUHUSU WATU KUWA NA VYAMA VYENYE MAWAZO TOFAUTI NA YEYE. HAKURUHUSU CHOMBO CHO CHOTE CHA HABARI ZAIDI YA VYOMBO VYA CHAMA NA SERIKALI AMBAVYO KAZI YAKE KUU NI KUWAELEZA WANANCHI KILA SIKU MWALIMU KASEMA NINI NA KUIMBA NYIMBO ZA "MWALIMU ASIFIWE".
NI YEYE AMBAYE SIKU ZOTE ALIKUWA "MGOMBEA PEKEE" IWE NI KWENYE CHAMA AU URAISI.
NI YEYE AMBAYE ALIWADHALILISHA NA KUWAFEDHEHESHA WABONGO MBELE ZA WAGENI WOTE WALIOKUWA WAKIJA BONGO NA KUKUTA WATU WANAPANGA FOLENI ZA SUKARI,MICHELE,NA SABUNI ZA KUFULIA NA HATA SIGARA AU DAWA YA MSWAKI HUIPATI MPAKA KWA RUSHWA AU ULANGULIWE. NAJUA KUNA MAZURI ALIYOFANYA LAKINI SINA HAJA YA KUYATAJA KWA VILE KAZI HIYO INAFANYWA ASUBUHI,JIONI, NA USIKU NA HAO WANAOTWAMBIA KUWA NI NABII.
ahahahhahhaha rytbon monie bro.i love jkn bt his way woz baaaad ezzzzz.thanks u open tz eyez on dat,dey dont c a lot dey kinda material ppl and a;;.
ReplyDeleteHenda Ndugu michuzi utaibana maoni yangu kama maoni mingine ya nyuma japokuwa sijawahi kuchafua hali ya hewa wakati wowote.
ReplyDeleteMimi ni mmoja wapo wa Watanzania ambaye sijaona kitu chochote muhimu Nyerere alichokifanya kwa Watanzania. Tulinyimwa haki zetu kama binadamu kwa kuwa yeye alitawala Tanzania kama kijiji chake. Wale waliokula serikalini yake hawakufungwa ili walibadilishwa madaraka na kupelekwa kwingine kula zaidi walipokamatwa na wizi. Haki ya binadamu haijaheshimika chini ya uongozi wake na ni sababu muhimu ya kuifanya Tanzania iwe nyuma kimaendeleo kutokana na siasa yake ya umoja na kujitegemea.
Kama mfanyabiashara wakata wa uhai wake, niliona jinsi Watanzania walivyokua wanateseka kutafuta chakula na wanakijiji wengi walikufa njaa. Nilipewa gunia mbili tu za mchele na Ugawaji ili niwauzie wateja wangu kwa mwezi na kila kitu ilikuwa kwa resheni.
Watu wengi walipoteza maisha yao na kutiwa ndani bila sababu maalumu. wakati wa Sokoine, watu wengi walitiwa ndani kwa kuwa na video au vitu ambavyo serikali ya Nyerere ilipinga wananchi wawe navyo kama kuwa na dola za kimarekani au kuwa na uwezo wowote zaidi ya jirani zao. Kulikuwa na askari kanzu kila kona ya nchi kama ilivyokua huko Urusi wakati wa Lenin yapokuwa bila ya mateso mazito kwa wananchi. Wazazi wangu ni mmoja wapo wa Watanzania waliotiwa ndani kwa kuwa hodari katika shughuli zao za biashara bila ya kumwibia mtu. Sokoine aliona wata kama wazazi wangu kama ni mafisadi tu au wezi wa jamii ya ujamaa. Ardhi yao na mali yao ikataifishwa kwanza na Nyerere wakati wa uhuru halafu wakati wa Uhuru halafu tena wakati wa Aaadhimisho la Arusha, halafu tena wakati wa Sokoine. Sidhani mtu yoyote mwenye kuelewa jinsi watu walivyoteseka kiuchumi na kihaki wanaweza kusema Serikali ya Nyerere ya zaidi ya miaka 25 iliisaidia kuiendeleza Tanzania kiuchumi au ilileta maendeleo yoyote.
Aluta Kontinua.
Mchangiaji 9:57. The kihinglish you are using is not reacheable! Kwanini usitumie kiswahili yani umeharibu lugha vibaya sana.Sijasoma comment yako yote kwa sabababu umeniboa kuanzia mwanzo!!!!!!!!
ReplyDeleteNakubaliana na Mchangiaji. Nyerere in one way ndiyo ameleta huu ufisadi. Sababu mwaka 1995, ali-interfer na natural process ya uchaguzi ambayo ingeupa upinzani viti vingi bungeni na kuwa wenye nguvu kuliko sasa. MREMA ASINGESHINDA ILA UPINZANI UNGEKUWA STRONG.
ReplyDeleteKizuri hakuwa mwizi, ila kama binadamu alikuwa na makosa vile vile. Makosa yake hakuyafanya kwa nia mbaya, ndiyo maana TUNAMUENZI
Nakukumbuka daima kipenzi cha wengi Nyerere baba wa Taifa, RIP!
ReplyDeleteNiliumia sana niliposikia umetutoka,tutakutana siku ya mwisho, keep enjoying with those angels darling!
Anony 9:57,
ReplyDeleteYou are entitled to your opinion about our late father of nation. However, i vehemently differ with you on the aspects of your comparision. You need to remember that Obamas and Nyereres eras are different. And more importantly, you speak of relatives of Obama (out of topic) and forget that the US economic system is different from Tz. No leader in this world is 100% perfect but what we are looking here is to be dedicated to your people. Nyerere has proven that and he made some of those mistake out of love and determination to an equal society.
He was accepted by majority (not all which was the case for Jesus)and he wanted perfect people to lead this country. If Nyerere was alive you wont see the trend of friends, musicians, redio presenters and other related groups rulling this country. I like Obama but people like you need to visualise generally and not to a particur issue. He was the man and every scholar and international figure will tell you that. Be open HE WAS A MAN and i wish he was alive for more few years to advise what to do with Richmonds, Kiwiras, Nnauyes and EPAS. Who can dare do that? Hands UP! HE WAS A GREAT MAN NO DOUBT.
BY Mchangiaji hueleweki unataka kusema nini? nakushangaa unaposema elimu hamna! unakumbuka NYERERE alitoka lini madarakani? ni more than twenty years ago, kama unakumbuka before that elimu ilikuwaje, au umezaliwa juzi unasoma propaganda za watu, hivi unjuwa kuwa elimu ilikuwa bure toka vidudu hadi mwisho wa madarasa, na hiyo ilitupatia wasomi wote wa Tanzania wewe unaowajuwa, bila yeye tusingekuwa nao, pia unatakiwa kutofautisha nyakati, Nyerere alitawala wakati nchi yetu ni changa na masikini kuliko sasa, pata la taifa lilikuwa dogo sana kufanya mambo yanayofanyika sasa lakini nia na mawazo alikuwa nayo, eti alikataza TV na technologia, hivi wewe unaushahidi wa kusema nyerere alikataza TV! alikuwa na priorities wakati akifanya vitu vyake, ulitaka ajenge TV station wakati watanzania walikuwa hawajuwi kusoma wala kuandika! hata hivyo hakukuwa na market ya hiyo TV ni nani alikuwa na uwezo wa kununua TV hiyo miaka ya 60 na 70, hata hivyo unafahamu historia TV ilianza lini? hata huku Ulaya hiyo miaka ya 60 TV haikuwa hata na miaka zaidi ya 30. NYEYERE he was a great thinker hamna mfano hata sijuwi kama tutaja mpata mtu kama huyu tena, nakumbuka alipoenda USA aliitikisa USA watu walikanyagana to Airport hadi alikofikia na walikufa kwa kukanyagana, na walisema alipashwa kuwa rais wa nchi iliyoendelea ka USA na alizaliwa kwa bahati mbaya Africa, pata vitabu vyake na hutuba zake na utajuwa that he was brainy and the man of the people.
ReplyDeletePole sana Mchangiaji tunashukuru Mungu hatukupata kiongozi kama wewe.TV kwa watu wasio na shule haisaidii chochote jua utamaduni wetu ungepata dosari kuwa na TV programm za wenzetu jamii ingejifunza ya watu bora tulipoanza kunzisha ya kwetu kwa kujua jamii yetu inamipaka.Maendeleo alileta Nyerere ni makubwa sana hakuna kiongozi alifikia hapo.Leo tunaongea lugha moja ikiwa ni nchi pekee Africa tunazungumza kwa lugha moja ikituunganisha kuwa ndugu upendo tulionao Watanzania ni mfano kwa Mataifa mengine zaidi nilitegemea wachangiaji kuchukua nafasi kumuenzi Baba wa taifa kwa kudumisha umoja wetu na mbinu za kuwahukumu Mafisadi kwa maendeleo ya Taifa kwa ujumla Tudumishe Umoja wetu kwa kutumia akili na nguvu tulizonazo na ni jukumu la viongozi wote kufanya hilo.Mungu Ibariki Tanzania
ReplyDelete"if you live everyday like it's your final day, someday it will most certainly be right.
ReplyDelete... life is limited, don't waste it living someone else's life! .. BY STEVE JOBS
I have lived Nyerere Era, and I definitely don't want to go back, I have queue for hours just for Yanga bovu to feed myself and my family, I have resonated on entangled/encapsulated/broken/brainwashed education system that has been endured by foolish leaders,(dont know how to lead), they certainly they have high hope for our country, but they don't know how, we are all suffering from that era, I am suffering from that era.
I certainly dont deny that, Nyerere has the interest at hearts for our country and citizen, but he was simply spoiled dictator, who extinguish any fikra from any corners whithin even on his own party, he SURERLY GETS HIS WAY BACK THEN, He was such a BULLY! That can be a right word to describe him.
I do believe we are on transition period, a period of healing, a period of young and intellectual individuals who can do a lot for this country, a period of high hope, a period of understanding others and not just myself and finally a period of reversing and unbutton the previous obscurity.
FINALLY STAY HUNGRY STAY FOOLISH. Seek knowledge!
By Mchangiaji
I second mchangiaji's comments.
ReplyDeleteTatizo ni binadamu ni wasahaulifu. Wewe kuwa na kitu chochote mpaka ukaombe kibali unadhani raha. baiskeli ikipata pancha kununua tairi mpya mpaka uonyeshe kuwa una baisket...tehehehe. One needs to write a book so that we dont forget.
Tulipopata uhuru tulikuwa sawa na nchi kama Singapore, etc katika maendeleo. Sasa leo ni wapi na wapi jamani? Uchina yenyewe aliyoipenda sana na kuiga kila kitu hadi kaunda suti, iliacha mfumo wake zamani miaka ya themanini. Mpaka leo katika Katiba yetu tunajiita nchi ya kijamaa. His policies were a total and complete failure.
The question is how do u measure success? Kwangu mimi the difference between what we achieved compare to what we lost...is too huge to call a success.
mtoto
NAKUBALIANA NA USHAURI WA KUTUNGWA VITABU VINAYOTUKUMBUSHA TULIKOTOKA PAMOJA NA KUELEZA MAZURI NA MA MABAYA YA MWALIMU.BINADAMU TUNASAHAU HARAKA SANA. LEO MARA TUMESHASAHAU DHIKI NA ADHABU ZA KUISHI CHINI YA UDIKTETA WA CHAMA KIMOJA AMBACHO CHINI YA UONGOZI WA MWALIMU KILIWAFANYA WATU WENYE NIA YA KUJENGA NCHI YETU KIUCHUMI NA KIBIASHARA (PRIVATE INVESTORS) MAADUI WAO WAKUBWA NA KUWAITA MAJINA MABAYA MABAYA KAMA VILE KUPE,WANYONYAJI,MAKABAILA,VITIMBAKWIRI,MABWANYENYE N.K
ReplyDeleteMATOKEO YAKE NCHI ILIKUFA NA IKAWA NI WAKUBWA TU WALIOWEZA KUPATA CHAKULA,NGUO NA MAHITAJI YAO MENGINE BILA YA KUPANGA MAFOLENI NA KUHANGAIKA KUTOKA DUKA HADI DUKA.
MWALIMU ALIKABIDHIWA NCHI IKIWA SAWA NA NCHI NYINGI DUNIANI KIUCHUMI NA ALIACHIA MADARAKA NCHI IKIWA YA PILI KUTOKA YA MWISHO DUNIANI KWA UMASIKINI.NI SAWA NA MTU ALIYEKABIDHIWA GARI JIPYA AKALIELEKEZA KWENYE NJIA MBOVU MPAKA LIKAKWAMA KWENYE MATOPE KISHA AKATOKA NA KUMPISHA DEREVA MWENGINE.HATA UTENDAJI WA MAWIZARA SERIKALINI ULIKUFA BAADA YA KUFUNGULIWA MATAWI YA CHAMA KATIKA KILA WIZARA, IDARA NA MASHIRIKA YA UMMA NA WENYEVITI WA CHAMA WAKAWA NA KAULI KUBWA HATA KULIKO WAKUU WA HIZO TAASISI. HATA KUPATA HICHO CHEO AU DHAMANA ILITEGEMEA ZAIDI NGUVU ZA SAUTI YAKO UNAPOSEMA "KIDUMU".
kumbe wengi mnakumbuka ujinga uliondelea enzi zile. Enzi za "marufuku". Watu wakanyimwa kupanda maua mpaka katikati ya mji walipanda maharage na mahindi...tehehe. Alafu hakuna kutumia magari jumapili. Alafu watu watumie farasi...hehehehe. Kweli ze comedy ingekuwepo enzi hizo wangekuwa na material za kutosha. Sema uhuru nao haukuwepo.
ReplyDeleteNyie Watanzania mnaokumbuka maumivu wakati wa Mwalimu mnasahau hata wamerekani na wachina walipitia vipindi kama hivyo. Eti Tanzania ilikua kama Singapore, waulizeni Zimbabwe na Kenya maana ya upepari. Na hata hali hii ya kibenki sasa hamuioni? Yes alikuwa dikteta, na ndio viongozi tunaotaka sasa sio wapulizaji. Ndio maana Rwanda na Uganda zinawapita kwenye ukuaji wa uchumi....wengi wetu ni wavivu na mnahitaji mwanajeshi awabadilishe uswahili wenu. Mwalimu aliwajali na ugali wa njano uliliwa sana Afrika sio Tz tu. Tufanye kzai kwa bidii kuonyesha alikosea basi...Ndio njia pekee ya kumuenzi na sio kukaa vijiweni
ReplyDeleteKama kiongozi akikosea bila kuiba, basi ni bora maana amekuonesha kuwa kupita njia hiyo kuna matatizo. Vilevile wanaofuata ndo wanapata mwanga na namna ya kwenda vizuri kutokana na makosa ya yule wa kwanza. Alikuwa na mawazo, ambayo yalikuwa hayakubaliki na wakubwa wa dunia. Kuiita mipango yake ni "total failure" si kumtendea haki kwani unakuwa umesahau factors nyingine zilizofanya mipango yake ishindikane, ambayo si yeye tu duniani yalimkuta, kuna wengine pia. Tunamsifu kwa kuwa na degree kubwa ya uadilifu tukilinganisha na viongozi wa sasa, kuwa na mipango, uwezo wa kukemea, kuona yaliyo mbele, uongozi nk vitu ambavyo waliomfuatia madarakani hawana zaidi ya wizi tu.
ReplyDeleteTusome vizuri mifumo ya siasa iliyokuwepo duniani, tutapata majawabu mazuri ambayo sidhani kama yanalingana na haya majibu ya moja kwa moja tunayoyatoa kuwa "he was a total failure". Alikuwa na dira, alijua alikokua anaelekea. Kwa makosa aliyokuwa ameyafanya, ilihitaji watu wengine kuyarekebisha, sio ku abondan yooooote ya Mwalimu.
Ninamkumbuka sana na naamini mawazo yake mengi yanahitajika sana kuendelea kutumiwa ili kulikwamua taifa hili kutoka kwenye huu ujinga uliokithiri. Maana utajiri tunao kinachotusumbua sasa ni ujinga.
Nawasilisha.
Wa Milimani (Serengeti of Flowers)
Wa Milimani...unataka kusema policy yake ya Ujamaa haikuwa "a total failure". Niliandika comment kuhusu ujamaa sema michu alibibania. Lkn ngojea niseme kwa kifupi kwa nini ujamaa hautakaa ufanye kazi:
ReplyDelete1. Binadamu ni mnyama mwenye fikra za kibinafsi.
2. Ujamaa unategemea personal sacrifice to the good of the country
3. Viumbe hai vinavyofuata mfumo wa ujamaa kwa mfano mchwa na nyuki...unapozaliwa katika society huna chance yeyote ya kubadilika - kwa mfano nyuki mfanyakazi hawezi kuwa malkia. Wakati sisi binadamu tuna huo uwezo.
4. Sisi tunafanana na wanyama wengine waishio katika system ya survival of the fittest na sio survival of the colony.
It comes to the conclusion that Ujamaa is actually against our own nature as animals. Sasa sijui Mwalimu (kwa heshima zake zote) alifuataje system kama hii. Ujamaa siku zote yahitaji oppression kufanya kazi...cheki China at the moment. Huwezi kukusoa kitu chochote.
Kwa watu mnaotoa mfano wa uchumi wa dunia sasa ivi, mnategemea nini wakati unapoacha system bila regulations?! Kuweka regulations kuzui ujinga kama huu uliotokea sio kana kwamba ni socialist...its necessary katika society. There is no perfect system...but capitalism goes well with our nature. All it needs is a few regulations kuzuia waonevu.
Feel free kupinga.
Alafu the fall of Zimbabwe sio kwa sababu ya capitalism. Uchinjaji Kenya sio sababu ya capitalism. Tofautisha siasi na hali ya uchumi.
Unaweza kunipa mfano wa mawazo ya JKN yawezayo kutumiwa wakati huu?
mtoto
Anony 10.19, Nafikiri mjadala wa ujamaa na upepari ulishakufa na kwa sasa ni ngumu kuelezea tabia zake kutokana na mabadiliko. Je Uchina ni wajamaa? Je Japani ni mapebari? Kinachotofautisha mifumo siku hizi ni upo wapi kimaendeleo na teknologia. Ndio maana tuna nchi za kaskazini na Kusini.
ReplyDeleteKuhusu machafuko kwenye taasisi za kifedha, nafikiri sheria ngumu sio dawa peke yake. Zaweza kusababisha kudumaa kwa uchumi na biashara kidogo. Ni fomula tu inayojaribiwa na Bw. Godon Brown na hatujui kama itafanikiwa.
Kilichotokea Kenya au Zimbabwe sio upebari tu ila maslahi ya wachache (Mugabes, Kibakis na Odingas) na ndio jibu kwako kwamba hawafanani na JKN. Ni kukosa fadhila kudhani kwamba hakuna hata moja jema ametenda kwa hii nchi. Siwezi kutaja ila aliamini kwamba ili tuendelee unahitaji kuondoa ujinga, umaskini na maradhi. Ndio maana mimi na wewe tunawasiliana sasa. Ninachosema ni kwamba hoja si mifumo bali ni kujitoa kwa watu wako na lengo liwe zuri.
Nawasilisha
Mtoto una hoja nzuri sana. ujamaa na ubepari ni dhana tunazozijenga tu kijamii na kuzabatiza hivyo. Lakini ukweli binadamu tuna hulka zote mbili "ujamaa na unyama". Mfano wa mawazo ya JKN yawezayo kutumiwa wakati huu ni kutoa elimu bora "bure" kwa watoto wote kutoka chekechea hadi sekondari (kama ambayo mimi nilipewa na siasa za JKN) ambayo ndio utaratibu huo unaofuatwa na Marekani, kinara wa 'unyama'. Kumbuka nimesema elimu bora na si bora elimu. Kwa hiyo unaona tunachopaswa kufanya ni kuchukua vitu vinavyofaa kutoka kila sehemu, ikiwa ni pamoja na hizo regulation unazosema. Marekani walikuwa wanazipinga lakini sasa wanalazimika kuzifikiria ikiwa ni pamoja kufanya utaifishaji-nusu wa mabenki!! JKN yeye alitaifisha kikamilifu!!!! Katika baadhi ya miji na wilaya za Marekani leo hii karne ya 21 kuna huduma kama vile za usafiri na umeme, maji, nk zinazoendeshwa na kutolewa na kampuni za umma kama ilivyokuwa wakati wa JKN. Ninafikiri umenipata!!!
ReplyDeleteAsanteni kwa comments
ReplyDeleteNadhani kuna comment zangu za juu nilizo-appreciate idea yake ya elimu bure. Lakini ukumbuke kuwa kitu chochote unachofanywa bure au kinachotolewa na state kwa bei nafuu kwa ajili ya umma huwa cha low quality. Hapa tunaingia katika argument ya public goods and private goods. Moja ya majukumu ya serikali ni kuhakikisha utoaji wa public goods kwa wananchi. Vitu kama umeme, ulinzi, maji, elimu. Serikali inaangalia kitu gani hasa wananchi wanahitaji na kinatolewa as a public service. Kwa iyo kama a state govt itaona usafiri ni shida...basi itatoa usafiri. Hiyo sio kusema kuwa wewe ni mbepari na wewe ni mjamaa. Hayo ni majukumu ya serikali.
Tatizo linatokea pale unapoingiza siasi katika utoaji wa huduma hizi. Na hapo ndipo Mwalimu alikosea sana. Sisi binadamu ni washindani...na ndo maana nasema ubepari unafit na nature yetu. Mfano mzuri ni jinsi polisi ilivyodorora. Uanzishwaji wa makampuni binafsi ya ulinzi kwa wingi ni sababu ya kudorora kwa public service ya usalama wa raia. Sasa hizi zinaleta ushindani kidogo katika kutoa usalama bora wa "properties" (sio watu). Nadhani sasa traffic police section nayo ibinafsishwe...hehehe. Labda itapunguza rushwa za njiani ambazo wananikaba nazo kila siku nikirudi nyumbani....hehehe.
I understand kuna challenges nyingi sana Mwalimu ali-face wakati wa Uhuru lakini some mistakes were very obvious. Anon wa October 16, 2008 5:45 PM, sijakubaliana nawe kwenye mambo ya ubepari na ujamaa. Hii bado ni mifumo iliyo hai mpaka leo. Swali ni 'to what extent do you fall into either category?' Wachina wao katika mfumo wao wa uchumi si wajamaa tena. Siasi kwao ndo imebaki ya kijamaa. Very restrictive. Mimi kusema kweli nisingependa kuishi sehemu nabaniwa hata kutoa opinion yangu kuhusu vitu. Umuhimu wa kuishi unakuwa nini hasa?
Pia nakubaliana na wewe kwa kusema kuwa Mwalimu hakuwa mbinafsi. Hapa nampa 90%. Lakini alipenda madaraka sana...na ndio hicho tunalipia sasa ivi kwa kuwa na hawa mafisadi. In other words mafisadi are a result of the ideology and the system of govt Mwalimu aliotengeneza.
Umesema alimtaja ujinga kuwa adui wa taifa. Sasa ngojea nikuulize swali moja: Mwalimu hakutumia ujinga wa wengi kututawala ki-dikteta?
mtoto
Mtoto,
ReplyDeleteNahisi tunahitaji mifano kutofautisha mifumo ya kimaendeleo. Leo UK wamefanya utaifishaji wa mabenki binafsi (hii ni moja ya sifa za wajamaa) lakini ukiwaita Uk wajamaa watakushangaa. Kuhusu JKN, hakuna anayebisha alikuwa na mapungufu yake. Hata viongozi wa dini wanayo mapungufu siku hizi. Kitu ambacho nataka kukipandikiza kwako ni kwamba mengi ya mapungufu ya huyu mzee yalitokana na nia njema (good faith) kwa walalahoi. Alitaka tuishi kwa usawa na yeye alikuwa mfano wa kilalahoi. Nakubai alikuwa "dikteta" lakini na nakaribisha hoja, ndio aina ya watu tunaowataka kuibadilisha hii nchi. Kwa nia njema kabisa. Nani anapenda tume au rushwa halafu unasingizia kuogopa sheria kuwashughulikia wahusika? Kagame aliruhusu viboko kwa trafiki na makonda kwa rushwa na uzembe (pamoja na vifungo) na tizama Rwanda ilipo. Lakini pia mwisho wa yote, tunafanya nini kama wananchi wa kawaida? Tubadilike na kuwa mifano ya kuchukia mabaya na tuonyeshe mifano kwa wengine wa chini yetu.
Sawa alifanya machache mazuri...but common...he wasnt such a great leader as people like to believe! Watu tumesahau ujinga wake mwingi tu. Swali: Kulikuwa na wasomi wangapi Tanzania mpaka kumchagua nanihii mwenye elimu ya darasa la nane sijui kuwa makamu wa rais. Hii ni miaka ya 80s. Kama sio kupenda madaraka hiyo ni nini? Watu wanasema mwalimu hakupenda kujilimbikizia...kuna siku hata moja kweli mwalimu angeweza kukaa asiwe na chakula hata kidogo. Hapo kwake kuna siku hata moja tanesco walishafanya mgao?...common be serious. He was no where close to be treated as a normal citizen. Alipewa zawadi ngapi na serikali na watu binafsi jamani? Kwa nini flani flani alitunguliwa ddm?
ReplyDeleteHis ideas were great on paper lakini wapi zingefanya kazi?!
Alafu i think na wewe umeingia katika wimbi la kusikiliza habari na kuzitoa bila kuchambua. Maana ya ujamaa ni total state control of all means of production. Wewe leo UK ukitaka kuanzisha banki yako in the midst of this economic turmoil...watakukataza? HAPANA. That is free market. Hapo juu nilisema kuwa kazi ya serikali ni kuhakikisha utoaji wa public goods. Sasa kama serikali ya uingereza/marekani wameona kuwa sasa mabanki yanadorora yakaamua kuyasimamia...that is part of their duty as a government. Uhuru wa kibepari upo pale pale.
Tanzania ulikuwa huwezi kuanzisha kitu chochote. Badala ya kujenga shule...unaenda kutaifisha za ma-sista, nk. Kwa nini?...hehehe. Shule nzuri sana zikafa hivyo hivyo. Fikra duni hizo. Na mpaka sasa ivi hizi agencies kama TRA wanauwezo mkubwa sana wa kufunga biashara. Uliza Kilimanjaro walifanya nini? Ua uchumi kabisa wa mkoa. Na yote hii imetokana na policies na mafunzo waliojifunza kutoka kwa Mwalimu. Aliwapa too much power.
Na kwa anayesema Mwalimu hakupenda madaraka...nani alimchagua Mkapa 1995?...hehehehe. be serious mate! Dont just sit and praise...question it!